Mke wangu kapata kazi Mkoani!

Mke wangu kapata kazi Mkoani!

Out of all the wishez, i wish you good bruhv!

Take it from me kama mkeo hakika unampenda usimuache akaenda huko Bukoba. Kama dhiki pambaneni nayo tu mkiwa pamoja Mungu atafanya wepesi ila usikubali utengano na mkeo sababu ya kazi.

Nakuhakikishia in 6 months time toka aondoke hakutakuwa na ndoa tena. Probability ya hilo kutokea ni 89%!
Hizo 11% nawaachia walimwengu...
 
Huyo kwa haraka haraka ataishi nje ya mkoa kwa miaka kibao.

Kama ni muislamu we mruhusu tu aende ongeza mke wa pili,,, kama ni ile dini nyingine wanafata sheria za viongozi badala ya maandiko yaliyoruhusu kuongeza mke basi vumilia usingo ama utafte mahusiano nje ya ndoa tajatifu.
😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Mwanamke anajichunga mwenyewe,mwache aende,hiyo ni mipango ya MUNGU kumpima kama ni mwaminifu kwako akiwa mbali,kubali aende sasa na wewe ufanye kama kipimo juu ya mapenzi yenu
Hakunaga hio, mwanamke yeyote akienda ugenini lazma wakware wamtafune. Anakuwa hana ujanja atakaza mwanzo ila akishaanza kuyazoea mazingira wahuni wataweka kama kawaida. Usimuwekee mdhamana mwanamke utashangaa.
 
Kama mchongo ni wa pesa ndefu bhas na ww hamia nae huko kisha utatafuta mchongo huko[emoji28]
 
Through hii post kuna mengi sana ya kujifunza, Kikubwa tuwapendeni wake zetu tusiache wakakaa mbali na sie. 😊😊
 
Mtoto wa miaka mingapi??
Je bado ananyonya??
Tuanzie hapo kama upo serious nijibu
 
Mwache aende ila hakikisha UNA EMERGENCY RESPONSE PLAN.
 
Angalia kama unaweza kuulipa huo mshahara anaoupata mwisho wa mwezi, basi mwache akae tu.

Ila kama huwezi na unaona umuhimu wa hio kazi unauona,

let her go to work...

Halafu kama wasiwasi wako ni kuchapiwa, kumbuka hata hapo ulipo bado kuna nafasi ya kuchapiwa.

kama tatizo ni distance, angalia namna ya kuhamia BK kule mkaishi kwa kula ndizi na senene.

mwisho kabisa,
mkeo akienda huko atachukua.miezi 6 tu akirudi atakua analoanisha godoro balaa😂😂😂
Vyakula vya wahaya vinatengeneza maji mengi sana mwilini
Acha utani basi nautoto mwenzako anawaza mtoto wake kuwa mbali na mama hata nayeye anamchepuko sio wife tu .
So kama wewe unawaza mapenzi koma
 
Ananyonya
Hawezi kuripoti kazini nakuomba japo miezi miwili aweke sawa mambo yake kumuhusu mtoto aende na mama huko aliko ajiriwa na huko amtafute msichana wakazi akae naye asubuhi hadi ijioni . Akisharudi huyo dada anarudi kwao au kwake .

Au aende na ndugu yake wakike kama anaye au ndugu yako wakike kama unaye akae na mtoto kwa kipindi yupo kazini mpaka mtoto atakapoachishwa nyonyo.

Au kama hujaajiriwa basi nenda naye kaa huko hadi apate msichana wakazi mwaminifu halafu ndio urudi.
 
Mruhusu ila kila siku ahsubuhi uwe unamtumia wimbo wa Sheta na Mavocco "Usilete UKIMWI NYUMBANI" utanishukuru.
 
Mi sijaoa ila maisha ya sasa hivi sio kama ya zamani

Ukaribu wa familia huwa ni mzuri na unamjenga mtoto kwenye makuzi meama mnapokua nae wote karibu

Na ishu ya kuchepuka ukikaa na mke wako wewe mwenyewe vishawishi ni vidogo sana zaidi ya mkiwa mbali anaweza kutana na mtu huko mwisho mkavunja ndoa ukapoteza familia wanawake ni watu rahisi kuwashawishi hasa akiwa insecure

Ushauri wangu kazi zipo tu nyingi mwambie atafute kazi mkoa ambao upo maana matangazo ya kazi huwa kuna sharti la eneo la kufanyia kazi

Jali mahusiano ya familia kwanza hasa mtoto vitu vingine kama pesa mnaweza tafuta zikapatikana tu kwa eneo mliopo
 
Mke wako alafu anadaiwa na ndugu?? Walikuazima walikuozesha? Msiruhusu watu waingilie ndoa zenu jamani
Ndoa ni mkataba wa hiari unaowaunganisha mume na mke.Katika mkataba huo mara nyingi kukutokea dispute mwathirika mkubwa ni mke hivyo ni muhimu mke akafuata ushauri wa ndugu ili kuweza kuwa na kipato chake cha ziada kitakachompatia uwezo wa kuisaidia familia yake,ndugu na akiba ya baadae endapo ataachika.Nb;kuoa binti wa MTU haina maana umpangie kila jambo ambalo halina tija.

Ushauri wangu kwa ndugu yetu "hakuna ndoa iliyodumu kwa wanandoa kuishi mbali kwa kipindi kirefu"

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Habarini wana jamvi!

Ebhana wife kapata kazi Mkoa wa Kagera na kazi ni nzuri, amekaa muda mrefu bila kazi takriban 5 yrs. Lakini kwa sasa ana mtoto mdogo, binafsi si kwamba sipendi akafanye kazi ila naona kama ni mbali sana na nyumbani, Kagera to Dsm ni parefu mno.

Naomba maoni yenu aende ama atulie tu, kwa sasa ni mama wa nyumbani na yuko desperate kweli kupata kazi.

Funguka Mdau, Hapa matusi si pahala pake.
Atulie Hapo mungaliane.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom