Najiandaa kumhalalisha mchepuko kuwa mke kisha nimtimulie mbali mke ananikosea adhabu sana

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,524
Habari wakuu, kama mada inavyosomeka hapo juu,

Mimi ni kijana miaka 34 sasa nimeoa nina watoto wawili, Mwaka 2021 nilikutana na huu mchepuko katika harakati za utaftaji na tukaanzisha mahusiano. Sikuwahi kuona Bwana ake tangu nafahamiana nae pamoja kwamba kwake nilikuwa napafaham vizuri na nilikuwa naenda mara kwa mara katika harakati zangu, ila aliwahi kuniambia Bwana ake yupo Dsm katika utaftaji na sikutaka kuchimbua zaidi maana haikuwa inanihusu kiivo,

Tumeendelea na huyu mchepuko kwa mda sikumoja ndo kanifungukia kuwa yey na bwana ake hawako vzuri kwa kuwa jamaa ake analazimisha waende dsm na yeye hataki kwan Dsm wamekaa almost miaka 5 bila mafanikio yoyote wanaishia kupanga chumba kimoja huku wakiwa na watoto wakubwa, inafkia mda watoto wanarudishwa mkoani kukaa kwa wazazi huku wao wakikaa Dsm bila mafanikio, kwa hiyo ndio chanzo cha wao kushindana na jamaa na dem ndo kaamua kurud zake mkoani ili apambane na mishemishe zingine hata kilimo kuliko kukaa dsm bila lolote la maana,

Kiufupi alinismulia hilo kwa ufupi sana na sikutaka stori zaidi maisha yakaendelea, ila kufikia mwaka jana mahusiano yakawa deep sana kias kwamba ikafkia hatua nikahisi kama yule Bi dada kuna kitu alikuwa anakosa maishani mwake maana kwa kiasi alichokua ananiganda haikuwa kawaida, ile hali namimi wife ndo hivo hasomeki so tukawa kama wote tunaliwazana flani ivi.

Tukaendelea na mahusiano ila kuna kipindi akaniambia mme wake amerudi nyumbani so nikawa sihitaji tena mawasiliano nae, maana nikaona inaweza kuniletea shida na istoshe huwa napita sana mitaa ya hom kwao kutokana na mishe mishe zangu,

Ila kwa mawasiliano ya mara chache chache sana niliokuwa nikifanya nae alikuwa analalamika sana kuhusiana na jamaa ake anavyomfanyia, ikafkia wakati mimi ndo nikawa mshauri wake mkuu wa kumtaka avumilie maana alikuwa anadai anataka kuondoka atafte maisha kwngine, Inasemekana jamaa alikuwa anataka kupitia mtoto wa mke wake yaani kabla ya ndoa huyu mchepuko alikuwa na mtoto na jamaa anataka kuzagamua mtoto wa mke wake,
Mwanzo sikutake serious nilijua ni maneno ya mkosaji tu ila baadae ikawa serious, hadi yule bibie akaamua kuondoka kwa jamaa, na akaniambia amepata kazi town ambapo ndio maskani bahati nzuri alipata mwenyeji jirani na maskani kwangu kabisa ni mtaa wa pili toka ninavoishi, NB sikuhusika kuratibu hilo ila ilitokea automatic akawa jirani,

Hapa mizagamuano ikawa Daily akitoka kazini nampitia nampeleka kwa mwenyeji wake ukaribu ukazidi mara 2 zaidi ya mwanzo, alikuwa anafanya kazi ya mgahawa sehem, ila tukaendelea nikampa wazo la kupanga chumba, ili ahame kwa watu alipokuwa anakaa, na nikampa kiasi cha pesa kidg na yy akaongezea alichokuwa amepata akapanga chumba, hapa relation ikazidi kukua, ila hapa kuna vitu nikaanza kuvinotice kwa huyu mwanamke tofauti kabisa na wife, kwanza ni mpambanaji sana, pili ni mzuri sana katika budget, tatu ana upendo wa dhati kwangu,

Tumeenda akaniambia anataka kufungua mgahawa wake mwenyewe mwanzo sikuamini maana nilishawahi kumpa wife wazo la kufungua magahawa alishindwa kabisa hata kunipa budget na istoshe vyumba vya biashara ninavyo yaani flem za biashara ninazo ila wife biashara hataki kabisa hata nikimfungulia biashara anasusa kufungua mwisho wa siku naajili watu wengine ikishindkana nafunga kabisa kiufupi wife ni mwanamke flani asiyependa kujishughulisha na alinizoesha hivyo nishamzoea hata simshirikishi lolote kuhusu biashara maana sio mtu wa kufikilia kuzalisha yey ni mtumiaji tu.

Tumeenda baadae akasema hataki tena kwenda kazn kwan boss wake anamtumikisha vibaya na kumsema nikamwambia atulie hom nitamhudumia hadi titakapo pata planeB, Sasa nikapata dharula ya kusafiri nikamwachia 100k laki moja ya matumizi kwa mda wa wiki 2 nitakazotumia kukaa ninapoenda, ila cha kushangaza nilivyorudi nilikuta kanunua vitu kidg na kaomba kiflem flani kafungua kamgahawa anapika pika chai, kwa kweli nilivyorud nilikuwa suprised sana, ilikuwa aibu kidg kulingana na aina ya biashara aliyofungua maana mtaji ulikuwa kidg sana hamna hata kiti wala kikombe, ikabidi nimnunulie chupa ya chai na viti kidg na vitu vingine vidogo, vidogo.

Akaanza rasmi biashara ya mama ntilie, ila kila nikienda nakuta mabadiliko kuna vitu kanunua mara mda kidogo nikakuta kamtafta mdada msaidizi na anamlipa, mda kidogo kanunua bati mwenyewe kapanua eneo na biashara imechangamka sana,

Tumeenda hata chumba nilichompangishia kodi anajilipia na vitu anajinunulia, ajabu kila nikifika unakuta amenunulia vitu mara nguo, mara zawadi hii mara hii yaani huwezi amini kwa mda mfupi huyu mwanamke amenibadlilisha sana hadi wife anashangaa, yaani napendeza hata mwili kwa wenye kumbukumbu nilishawahi kuanzisha uzi hapa wa namna ya kufanya nipate mwili ila nimeumuka gafla nimekuwa kibonge kila nikipita watu wananishangaa kwa kweli jinsi nilivyobadilika kwa huyu mwanamke, nitaweza picha hapo chini.

Kubwa na lililonileta hapa, ni kwamba kuna siku kimaskhara tu aliniambia mme wngu nataman nikuone unaendesha Gari kwa sasa kutumia hii bodaboda nitakupoteza mapema, kwa kuwa kigari changu kiliroga nikawa natumia boda, sasa juzi napita pita mtandaoni kwa dalali maarufu muuza magari nikakuta jamaa kapost ka Premio anauza Mil 12. Nikamuonesha kiutani akaniambia mme wangu nunua hii,nikamwambia sina pesa akasema kama ukiwa na 8mil hiyo 4 nitakuazmia sehem, nikajua utani ila nashangaa jioni kweli ananipigia sim ananiambia twende tukaone ile gari, kufika akatoa 4m kanikabidhi na mimi nimaongezea hiyo mil8 na tukaondoka na ndinga,

Hakika huyu mwanamke kafungua ukrasa mpya katika maisha yangu, na sikuwahi kufikiria kama kuna wanawake wapambanaji kama huyu mwanamke, ila cha kusikitisha ameishi na jamaa miaka 6 jamaa hakuwahi kumtolea mahari na alimzalisha watoto 4.

Kiumri huu mchepuko umenipita kama 4 years hivi, na ana watoto 4 aliozaa na jamaa na 1 huyo binti ambae jamaa alitaka kuzagamua, ila kimuonekano huwezi kudhania kama anawatoto 5, japokuwa alipokuja town alikuwa anaonekana kama mzee wa miaka 80 alivyokuwa kachoka kachakaa na kadhoofu, huwa ananishukuru hadi analia akikumbuka alivyokuja na alivyo kwa sasa ila nikifkiria kiundani sioni mchango wangu mkubwa kwake binafsi naona nilichompa ni kidg sana ila amekikuza na sasa anajipambania mwenyewe ila anatangaza kwa kila mtu kuwa mimi ndio niliemuokoa na kumpa hope mpya ya maisha, Ila jamaa anapiga simu analia anaomba msamaha kila siku na dem kampiga blcklist na hataki kabisa story yoyote inayomhusu mwamba kiasi kwamba hata mimi nikimgusia jamaa katika story zetu naona kabisa anatoka kwenye mood, kiufupi sijajua jamaa nikipi alimfanyia huyu mwanamke zaidi, ila huyu mwanamke hataki hata kuskia jina lake mwamba.

Hapa nimekuja hapa jukwaani kuuliza wazee wenzangu kuwa huu mchepuko niurasmishe kabisa kuwa wife material au niuache tuishi hivihivi?

20230526_160013.jpg
 
Wewe ushawekwa mtu kati.Huyo single maza anaye SUPPLIER wake pembeni.
Milioni 4???? Mhhhhhhhhhh!!!!!!
Braza shtuka!!! Halaf ni single maza mwenye watoto wawili? Mzee unakitafuta kifo kwa nguvu sana ..shauri yakoo.
Huyo endelea tu kummega kisela hapa na pale maisha yaende..ngoja ufukuze mkeo halaf uchukue mke wa mtu mpambanaji uone mtakavyo pambana humo ndani!!!

Mwanamke mzuri akiwa nje..Akitia maguu ndani baba umekwishaaaaa!!!.

Kazi kwako
 
Wewe ushawekwa mtu kati.Huyo single maza anaye SUPPLIER wake pembeni.
Milioni 4???? Mhhhhhhhhhh!!!!!!
Braza shtuka!!! Halaf ni single maza mwenye watoto wawili? Mzee unakitafuta kifo kwa nguvu sana ..shauri yakoo.
Huyo endelea tu kummega kisela hapa na pale maisha yaende..ngoja ufukuze mkeo halaf uchukue mke wa mtu mpambanaji uone mtakavyo pambana humo ndani!!!

Mwanamke mzuri akiwa nje..Akitia maguu ndani baba umekwishaaaaa!!!.

Kazi kwako
Mmmh ahsante mkuu haya ndio maoni tunatafta hapa
 
Wewe ushawekwa mtu kati.Huyo single maza anaye SUPPLIER wake pembeni.
Milioni 4???? Mhhhhhhhhhh!!!!!!
Braza shtuka!!! Halaf ni single maza mwenye watoto wawili? Mzee unakitafuta kifo kwa nguvu sana ..shauri yakoo.
Huyo endelea tu kummega kisela hapa na pale maisha yaende..ngoja ufukuze mkeo halaf uchukue mke wa mtu mpambanaji uone mtakavyo pambana humo ndani!!!

Mwanamke mzuri akiwa nje..Akitia maguu ndani baba umekwishaaaaa!!!.

Kazi kwako
Umeona eh,!
 
Back
Top Bottom