Huu Uzi ufutwe, hauna msaada wowote kwa muomba ushauri Wala kwa jamii. Umejaa mawazo potofu na ya kubomoa jamii na familia kuliko kujenga. Zaidi sana, watu wanatoa mawazo mepesi kwa mambo mazito, wanashusha hadhi na utukufu wa ndoa kwa kulinganisha na umalaya na tamaa za kimwili. Watu wanajitoa ufahamu mradi waonekane tu wanaongea Ila ukweli wanaujua na kuuficha makusudi, wengine hawajui lolote kuhusu ndoa na maisha ya familia lkn ndio wanaojitokeza kuwa washauri wakubwa wa ndoa. Wengine maisha hayo yalishawashinda, hukai kwa mke Wala mume hata kwa mwezi mmoja kwa tabia zako mbaya, Leo hii unataka kutoa ushauri jinsi ya mwenzako atakavyodumu kwenye ndoa milele. Na sisi wanandoa tupunguze mitandao tunajianika sana hadi kwa mashetani, namna ya kuishi na kutatua changamoto zetu itokee ndani ya ndoa yenyewe, kutafuta suluhu ya matatizo ya ndoa nje ya ndoa ni "kutoka nje ya ndoa" kitu ambacho ni dhambi kubwa katika ndoa. Tatizo la kijana kutafuta mke mitandaoni, kuchumbia mitandaoni, mahari kwa mtandao, ndoa kwa mitandao, mtoto akizaliwa wa kwanza kujua ni mtandao, chakula Cha mke mtandao ndo unaambiwa ni kizuri au kibaya, hizi ndoa za mitandaoni kila kitu mitandao Mimi nilivyofundishwa mafundisho ya ndoa na katekista wangu "ni ndoa batili tangu mwanzo" hivyo hata zikivunjika ni sawa na "hazikuwahi kuwepo".