Mke wangu anawasifu wanaume waliojenga nyumba

Mke wangu anawasifu wanaume waliojenga nyumba

Kilawo

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2016
Posts
2,008
Reaction score
3,633
Mimi nimeoa miaka 6 iliyopita tuna mtoto mmoja na tunaishi nyumba ya kupanga lakini mke wangu anawasifu Sana wanaume waliojenga nyumba zao.

Wanajukwaa, mliwezaje kujenga kwa biashara ndogo ndogo, kama ninazofanya mimi? Maana kiwanja kipo tatizo lipo kupata pesa ya kuanzisha ujenzi, nyie muliwezaje kujenga ?
 
Kujenga hakuhitaji fedha nyingi, kunahitaji nia ya dhati ya kumuliki mjengo, mimi nikiwa na kiwanja silali nyumba ya kupanga badala yake nafanya hivi
1. Nasafisha kiwanja
2. Nanunua bati used
3. Najenga banda la mabati na choo cha pipa nahamia kwangu chap
4.Nikishindwa hayo hapo juu nanunua carpet za 10k mbili najenga hema nahamia mengine ntajua cha kufanya mbele kwa mbele
 
Kujenga hakuhitaji fedha nyingi, kunahitaji nia ya dhati ya kumuliki mjengo, mimi nikiwa na kiwanja silali nyumba ya kupanga badala yake nafanya hivi
1. Nasafisha kiwanja
2. Nanunua bati used
3. Najenga banda la mabati na choo cha pipa nahamia kwangu chap
4.Nikishindwa hayo hapo juu nanunua carpet za 10k mbili najenga hema nahamia mengine ntajua cha kufanya mbele kwa mbele
Huko wala si kuhamia kwako, huko ni kukimbia Masimango mkuu
 
Anza kununua matofali kidogo kidogo kwa kiasi cha pesa unachomudu, yakitosheleza utaanza kujenga taratibu
Tofali anunue awamu 3 tu, ya kwanza tofali 300, ya pili 300, ya tatu 300. Jumla 900k acheki saruji. Moja inajenga tofali 60-70. Fundi ujenzi tofali moja amjengee kwa 400. Mengine atakuw anaongeza kidogo kidogo
 
Mimi nimeoa miaka 6 iliopita tuna mtoto mmoja na tunaishi nyumba ya kupanga lakini mke wangu anawasifu Sana wanaume waliojenga nyumba zao wanajukwaa mliwezaje kujenga Kwa biashara ndogo ndogo, kama ninazofanya Mimi maana kiwanja kipo tatizo lipo kupata pesa ya kuanzisha ujenzi Nyie muliwezaje kujenga ?
Huyo mwanamke anafanya nini kufanikisha nyie kujenga nyumba.
Kama anakupa pressure kwa kukulinganisha na wanaume wengine piga chini now kwa usalama wako.
Comparison haitaisha kwenye maisha yenu hata siku mkipata nyumba yenu still atakucompare na wanaume wenye magari. Utakuwa kwenye constant comparison ya mke wako for the rest of your life.
Set boundaries mpe mipango yako ya kupata nyumba. Kama anaiona hawezi mfungulie mlango asepe.
 
Huyo anakupa changamoto ili ujenge japo uwasilishaji wake sio mzuri....
Nikupe hongera sana kwa kumiliki kiwanja kwani hiyo ni hatua kubwa sana
Ushauri wangu; Ungetafuta duka kubwa la vifaa vya ujenzi pamoja na matofali kama lipo
Au kiwanda cha matofali uanze kuwekeza kidogo kidogo

Mfano: matofali ya inchi tano; unaweza kuuliziwa shs 1000
Hivyo unachofanya unakuwa na daftari kwenye kiwanda cha matofali; Kila ukipata hela hata shs 10,000 unampatia na una andika ambapo hapo ni matofali 10. Ndani miezi sita unaweza kuta umemaliza matofali 1000 ambapo yanatosha kwa kuanzia.

Una anza kuwekeza mabati; ndani ya miezi sita unaweza kuta umekamilisha mabati pengine 50 ya meta tatu. Una anza mbao, ndani ya miezi sita sita unaweza kuta umemaliza
Una malizia cement na hela ya fundi

Hapo ikiisha miaka 3 unaweza kuta unasimamisha nyumba chap kama fisadi hadi watu wanashangaa kumbe umekusanya polepole....
 
Huyo anakupa changamoto ili ujenge
Hongera sana kwa kumiliki kiwanja kwani hiyo ni hatua kubwa sana
Ushauri wangu; Ungetafuta duka kubwa la vifaa vya ujenzi pamoja na matofali kama lipo
Au kiwanda cha matofali uanze kuwekeza kidogo kidogo
Mfano: matofali ya inchi tano; unaweza kuuliziwa shs 1000
Hivyo unachofanya unakuwa na daftari kwenye kiwanda cha matofali; Kila ukipata hela hata shs 10,000 unampatia na una andika ambapo hapo ni matofali 10. Ndani miezi sita unaweza kuta umemaliza matofali 10,000
Una anza kuwekeza mabati; ndani ya miezi sita unaweza kuta umekamilisha mabati pengine 50 ya meta tatu
Una anza mbao, ndani ya miezi sita sita unaweza kuta umemaliza
Una anza cement
hapo ikiisha miaka 3 unaweza kuta unasimamisha nyumba chap kama fisadi hadi watu wanashangaa kumbe umekusanya polepole....
Changamoto ya huyo mwanamke ni negative kwa jamaa. Huwezi kuwasifia wanaume wengine. Yeye aeleze hitaji lake kwa mume wake bila kuingiza watu wengine. Assume jamaa akianza naye kusifia wanawake wengine?
 
Back
Top Bottom