biologically, the more unapoongezeka umri, the more nguvu ya kufanya ngono inapungua. watu kuanzia miaka 45 and above, 50 huko, sayansi inasema hata usimamaji wa maumbile ni dhaifu kuliko wa vijana wa miaka ya 20s. kipimo chake wanasema ni mkojo wa kawaida, ukikojoa ukarusha mbaliiii izo ni enzi za ujana ndio urijani wenyewe, ukiona unalowesha suruali mkojo haufiki mbali ndio hivyo umeshaanza kuzeeka. worse enough, sijui kama kweli, inasemakana wanawake wakifika menopous (miaka 50 hadi 55 hapo) wanakuwa na hamu kupita maelezo wakati baba ndio imeshakuwa jioni. akienda kwa kakijana maombile yake yanasimama mno na anapata anachotafuta, ndio maana wamama wengi wanalea viserengeti boys.
wasichojua ni kwamba, hii miili tunayoringia ni mabua tu, ni takataka tu. ni Kweli Mungu ametubariki na miili hiii na tunapaswa kumshukuru na kuitunza, ila tujue ni udongo tu. leo nilitembelea hospitali ya Banjamin Mkapa, kuna jamaa anaumwa yupo icu. nimefika pale nikavua viatu nikaingia kumwangalia, nimekuta vitanda kadhaa vya watu pale kila mtu anahangaika kwa nafasi yake peke yake peke yake. miili yao haina msaada wowote, hawaongei, wanapumulia mashine. nikakumbuka kwamba hao pia wanatamani wangekuwa wazima ili waishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu.
tunamshukuru Mungu ametuumba na miili yenye afya, binafsi namshukuru Mungu, ni rijani haswa though nipo kwenye early 40s. kuna wakati hadi waifu anaomba tuweke tu ratiba kwasababu akifanya mchezo naweza fululiza jumatatu hadi jumapili. hilo kwangu ni jambo la kumshukuru Mungu kwaababu najua wapo wanaoenda hadi kwa waganga wa kienyeji wapate nguvu za kiume lakini mimi Mungu amenipa bure. kwa umri huu bado nikiamka asubuhi kitu kipo juuuu kama nilivyokuwa kwenye 20s.
pamoja na hayo, tuishi tukijua kwamba pamojana utamu wa ngono ulivyo, Mungu hajatuumba ili tufanye uzinzi, bora ukose hata kitu kizuri sana lakini usimkosee Mungu. bora usifanye ngono hata miaka 10 au hata maisha yako yote kama ngono hiyo itakufanya uukose ufalme wa mbinguni.
Biblia inasema, kama jicho lako ndio huwa linakukosesha, likate litupe bora ubaki kipofu anayeingia mbinguni kuliko kuwa na mamcho yako mawili ukaingia motoni. unaweza kuwa na kitu fulani kizuri, chene faida, kinachokusaidia, unachofurahia n.k lakini kama hicho kitu kinafanya umkosee Mungu bora uachane nacho ili umpate Mungu kuliko kuingia motoni na icho unachokifurahia. simaanini kwasababu unafurahia ngono ung'ofoe viongo unavyofanyia ngoni, la hasha, ila bora uukose utamu wa ngono, bora ukose pesa, bora ukose mwanamke, bora ukose mtoto, bora ukose chochote kila kama kukipata icho kitu kutakutenga na Mungu wako.
Mungu anatupenda sana, anatujali, anatulinda, ameshikilia pumzi zetu, na hata unapoenda kuzini huwa ni yeye ameshikilia pumzi yako, anakuona, tunapaswa kuona aibu kwasababu jicho la Mungu linaona kila mahali hakuna pa kujificha. bora uogope Mungu, usiogope mwanadamu, usiogope ukimwi, usiogope chochote, ogopa Mungu anayeweza kuua mwili na roho na kukutupa moto wa milele.
jueni leo enyi nyote msomao hapa ya kwamba, wazinzi wote, waasherati, wachawi, wafiraji, waabudu sanamu na wote wanaofanya yale yanayofanana na hayo, hawataurithi ufalme wa mbingu/Mungu. Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana, mwiteni maadamu yu karibu, mtu mwovu na aache njia yake mbaya na mtu asiye haki aache mawazo yake, na amrudia Mungu wake naye atamrehemu, arejee kwa Mungu naye atamsamehe kabisa. usisubiri uwekwe ICU ndio uanze kutafuta uso wa Mungu, unaweza usimpate kwasababu mazingira yanaweza yasiruhusu, pengine hata uwezo wa kuinua ulimi useme Mungu nisamehe hautakuwa nao. kuna jamaa juzi alikuwa kwenye shughuli zake za kila siku, amepata ajali, yupo icu, hata hajitambui, nafasi ya kutubu hana kwasababu alishtukizwa, usifikiri shetani anatamani kukupatia nafasi ya kumrudia Mungu katika maisha yako, okoka leo, wala usisite. Haleluya to the Lamb of God!