Mke wa mtu sumu: Msela nondo anapigania uhai wake Bugando

Jocasta

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
474
588
Amefanyiwa operation ya kwanza kichwani wiki iliyopita na jana alifanyiwa operation ya pili, inauma na inaumiza sana kijana mdogo sana ambaye hata miaka 20 hajafikisha. Jamani mke wa mtu sumu.

Iko hivi, jamaa alipopata taarifa ya kwamba "msela nondo" anatoka kimapenzi na mke wake alimtafuta na kumuonya na alimtamkia kabisa ya kwamba usipoacha siku nikikufumania ntakumaliza,"msela nondo"alikataa katakata.

Siku ya siku ikafika, mida ya jioni jamaaa akamuaga mkewe ya kwamba anaenda kuangalia mifugo huko bondeni inakochungwa, ambapo kama kawaida ilitegemewa angelala huko. hawakujua kuwa siku hiyo ilikuwa mtego.

Mkewe bila hiyana akamtaarifu "msela nondo" kuwa jamaa hatakuwepo usiku hivyo aje, ni kweli "msela nondo" akatinga na moja kwa moja wakaanza mchezo.

Muda si mrefu mwenye mke akatinga(walikuwa wanamuita boya), kugonga mlango ukaitika moja kwa moja chumbani, uso kwa uso na "msela nondo". Katika hali ya kujitetea apate nafasi ya kuchomoka "msela nondo" akamchoma kisu tumboni jamaa mwenye mke(kosa Lingine kubwa alilofanya).

Mwenye mke akashika kiti na kumpiga nacho "msela nondo" kichwani, "msela nondo" akazima. Mwenye mke akaanza kutumia panga kumkata kata "msela nondo" kila sehemu mwilini, hasa kichwani ambako alikata panga za kutosha.

Mpaka alipohisi ya kuwa amemmaliza kabisa, akambeba juu juu na kumpeleka kwao, bahati yake.

Tumuombee msela nondo apone, huenda akapata nafasi ya kujifunza. Narudia kusema mke wa mtu sumu, inauma sana tena sana, naamini akipona hatarudia alichokifanya.
 
Amefanyiwa operation ya kwanza kichwani wiki iliyopita na Jana alifanyiwa operation ya pili,inauma na inaumiza Sana kijana mdogo Sana Ambaye hata miaka 20 hajafikisha Jamani mke wa mtu sumu

Huyo sio mke, apewe jina stahiki

UFUNUO 2:19-23
19 Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;
23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
 
Amefanyiwa operation ya kwanza kichwani wiki iliyopita na Jana alifanyiwa operation ya pili,inauma na inaumiza Sana kijana mdogo Sana Ambaye hata miaka 20 hajafikisha Jamani mke wa mtu sumu

Iko hivi,jamaaa alipopata taarifa ya kwamba "msela nondo" anatoka kimapenzi na mke wake alimtafuta na kumuonya na alimtamkia kabisa ya kwamba usipoacha siku nikikufumania ntakumaliza,"Msela nondo"alikataaa katakata

Siku ya siku ikafika,mida ya jioni jamaaa akamuaga mkewe ya kwamba anaenda kuangalia mifugo huko bondeni inakochungwa ambapo Kama kawaida ilitegemewa Angelala huko,hawakujua kuwa siku hiyo ilikuwa mtego

Mkewe bila hiyana akamtaarifu "Msela nondo"kuwa jamaa hatakuwepo usiku hivyo aje, Ni kweli "Msela nondo" akatinga na moja kwa moja wakaanza mchezo

Muda si mrefu mwenye mke akatinga(walikuwa wanamuita boya),kugonga mlango ukaitika moja kwa moja chumbani, uso kwa uso na "Msela nondo"katika Hali ya kujitetea apate nafasi ya kuchomoka "Msela nondo"akamchoma kisu tumboni jamaa mwenye mke (kosa Lingine kubwa alilofanya)

Mwenye mke akashika kiti na kumpiga nacho "Msela nondo"kichwani, Msela nondo akazima,Mwenye mke akaanza kutumia panga kumkata kata "Msela nondo"kila sehemu mwilini,hasa kichwani ambako alikata panga za kutosha,

Mpaka alipohisi ya kuwa amemumaliza kabisa,akambeba juu juu,na kumpeleka kwao"Bahati yake

Tumuombee Msela nondo apone Huenda akapata nafasi ya kujifunza,NARUDIA KUSEMA MKE WA MTU SUMU,INAUMA SANA TENA SANA,NAAMINI AKIPONA HATARUDIA ALICHOKIFANYA.
Noma sana jana tumezika mtu uku kwetu kijijin kisa Mke wa mtu
 
Mwanaume Wa Kweli unaanzaje Kula Mke Wa mtu..?
Wakati Wanawake Kibao wanatafuta Waume..?
Wanawake Wamejazana huko kwa Manabii wapo kibao waombewe Waolewe....Wewe unaenda kula mke wa Mtu.?
Kwanza kuna mmoja hapo juu amecomment ni Kinyaa..kweli hiyo tabia ni kinyaa.
 
Mwanaume Wa Kweli unaanzaje Kula Mke Wa mtu..?
Wakati Wanawake Kibao wanatafuta Waume..?
Wanawake Wamejazana huko kwa Manabii wapo kibao waombewe Waolewe....Wewe unaenda kula mke wa Mtu.?
Kwanza kuna mmoja hapo juu amecomment ni Kinyaa..kweli hiyo tabia ni kinyaa.

Mithali 6:32​

Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
 
Back
Top Bottom