_Flames
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 2,927
- 3,925
Ni katika hali ya story za kuhusu masuala yanayohusu mazingira tunayoishi, Hapa namaanisha kuhusu usafi na mengineyo na Mimi ni single boy hivyo sina wa kusimamia masuala hayo zaidi ya mimi mwenyewe ndipo tukajikuta tunazungumzia masuala ya mahusiano na ndipo mwanadada huyu akaenda direct kwenye topic ya wivu.
Kuhusu wivu akaanza kumkandia mumewe kwamba ana wivu wa Kimbatu (wivu wa kijinga) kwani hajiamini hata kidogo na wala hamuamini yeye mwenyewe... Picha linaanza jamaa anamkagulia simu kila wakati, Imefika hatua jamaa ame-divert simu yake kwamba kabla simu au message yoyote haijafika kwa mwanadada huyu basi inapita kwanza kwa jamaa, Mwanadada anaongea kwa uchungu sana kuonesha hali hiyo kwamba inamkwaza sana na kumfanya ahisi kama anaishi gerezani, Anasema kila simu itakayopigwa au message kuingia akiwa na jamaa yake ndani basi ni lazima aulizwe "Nani huyo..." kwa sauti yenye tempa😁, Muda wote huo nilimsikiliza kisha kumuuluza "Lakini Happy kama wewe ni muaminifu kwake basi kwanini ukwazike yeye kujihakikishia?" Mwanadada yule hakuridhia majibu yangu bali aliendelea kuelezea tu jinsi gani anavyokereka na mwenendo wa jamaa
Mwanadada amefunguka mengi sana ila wakati anataka kuelekea kwenye kuongea madhaifu ya jamaa kitandani mimi nikamkatisha kwa kujipokelesha simu ya uwongo na kweli na kumuacha kwenye mataa mwanadada yule huku nisichangie neno lolote wala kumpondea jamaa. Ama kweli mimi na wana ni dam dam.
Mwisho: Wakuu acheni kukagua simu za wanawake zenu kiasi wakajua mnawafuatilia, Hiyo ni ishara kwamba hujiamini na hilo ni jambo ambalo linakushusha thamani kwa mwanamke ndani ya dk 0, Kingine jinsi unavyoonesha udhaifu wa kumpenda mwanamke na kuwa na wivu wa hali ya juu ndipo unapompa hamasa ya yeye kutaka ku-teste the new test.