Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 975
- 47
Mke wa Dk. Slaa awa kivutio mkutanoni
Na Burhani Yakub
MBUNGE wa Jimbo la Karatu kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa na mkewe Rose Kamili, ambaye ni diwani wa Kata ya Basotu wilayani Hanang kwa tiketi ya CCM, ni wapinzani wa kisiasa, lakini wanashirikiana katika kufichua ufisadi kama ilivyodhihirika mwishoni mwa wiki.
Akiiwakilisha asasi isiyo ya kiserikali ya Pingo inayofanya kazi zake chini ya programu ya PETS katika mkutano wa wadau wa maendeleo wa Pact, mke huyo wa katibu wa Chadema alisisimua wengi alipoeleza jinsi alivyofichua kiasi cha Sh119.8 milioni ambacho hakikutumika kukarabati vituo saba vya afya wilayani Hanang.
Alisema wakati wakitekeleza jukumu walilopewa wajumbe wa asasi ya Pingo kuchunguza matumizi ya ruzuku ya serikali zinazopelekwa katika halmshauri ya Wilaya ya Hanang, uongozi uliwapa nyaraka zenye taarifa za kughushi.
Diwani huyo alisema mbali ya kutoa taarifa ya kughushi, uongozi huo wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang ulimtuma afisa maendeleo ya jamii kupeleleza kinachofanyika wakati wa kuchunguza matumizi ya fedha za serikali ili kutafuta njia za kuficha ukweli.
Baada ya kugundua hilo, nilitumia nafasi yangu ya udiwani kwenda halmashauri kuomba taarifa za matumizi ya fedha, lakini hata mimi nilinyimwa ndipo nikaenda nyumbani kupekua mafaili ya vikao vya Full Council tukagundua kumbe walitupa taarifa feki, alisema Rose.
Alisema baada ya kufanya uchunguzi ikabainika kuwa katika mwaka wa fedha wa 2005/2006 Halmashauri ya Wilaya ya Hanang ilipokea kiasi cha Sh119,880,000 kwa ajili ya ukarabati wa vituo saba vya afya ambavyo hadi walipokuwa wakichunguza mwanzoni Mei 2008 zilikuwa hazijatumika.
Alivitaja vituo ambavyo havikukarabatiwa licha ya halmashauri kuchukua fedha zake kuwa ni Masakta, Bassodesh, Endasak, Gidahababieq, Sirop, Dawr na kituo cha afya cha Katesh.
Baada ya kuchachamaa, mwaka huu halmashauri ilitoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa vituo hivyo. Haijulikani sababu za kuziweka fedha hizo kwa kipindi cha miaka miwili bila kuzitumia.
Diwani huyo machachari alisema licha ya halmashauri kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivyo vya afya, Pingo imebaini kuwa kiasi cha Sh55,128,000 bado hazijaingizwa kwenye akaunti husika na haifahamiki zimepelekwa wapi na kwa sababu zipi.
"Hili ni jambo ambalo naahidi kulifanyia kazi kwani hatuwezi kukubali kuona wananchi wanacheleweshewa maendeleo kwa makusudi," alisema.
Baada ya kutoa taarifa hiyo ukumbi ulilipuka kelele za shangwe huku wale wanaofahamu uhusiano wake na Dk. Slaa wakijiuliza ni vipi wakaweza kuwa kitu kimoja wakati wanatofautiana kiitikadi.
"Mimi siipendi kabisa Chadema na kwenye eneo langu la udiwani nahakikisha wafuasi wa CCM hawarubuniwi kuhama. Lakini nipo pamoja na Dk. Slaa katika suala zima analofanya la kufichua mafisadi," alisema Kamili.
"Mume wangu ni mzalendo mwenye uchungu na nchi yake."
Mkutano huo ulioandaliwa na Pets kwa kushirikiana na Pact Tanzania na Shirika la Misaada la Marekani (Usaid) na mfuko wa rais wa Marekani wa Millenium Challenge ulifayika kwa siku mbili na kushiriki wajumbe wa asasi mbalimbali kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani
source: mwananchi