Mbunge Minza Mjika Ahoji Mkakati wa Serikali wa Kujenga Vituo vya Afya kwenye Kata za Mkoa wa Simiyu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

Mbunge Minza Mjika Ahoji Mkakati wa Serikali wa Kujenga Vituo vya Afya kwenye Kata za Mkoa wa Simiyu

Katika kipindi cha miaka mitatu ya fedha 2021/22, 2022/23 na 2023/24 serikali imejenga jumla ya vituo vya afya 466 vilivyogharimu shilingi bilioni 718.1 katika maeneo ya kimkakati kote nchini ambapo mkoa wa Simiyu jumla ya vituo vya afya nane (8) vimejengwa katika kata za kimkakati kwa gharama ya shilingi bilioni nne (4)

Hayo yamesemwa, Alhamisi Februari 15.2024 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Dkt. Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum mkoa wa Simiyu Minza Mjika aliyehoji mkakati wa serikali wa kujenga vituo vya afya kwenye kata za pembezoni mwa mkoa huo

"Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika kata za kimkakati kote nchini zikiwemo kata zilizopo katika Halmashauri zote za mkoa wa Simiyu" -Dkt. Dugange.
 

Attachments

  • GGYLpaKWgAAZ9Ow.jpg
    GGYLpaKWgAAZ9Ow.jpg
    441.4 KB · Views: 1
  • sddefaultmkoi.jpg
    sddefaultmkoi.jpg
    45.2 KB · Views: 1
  • GGYDVI_XMAEEcWk.jpg
    GGYDVI_XMAEEcWk.jpg
    385.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom