Mke wa Dk. Slaa awa kivutio mkutanoni

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
Mke wa Dk. Slaa awa kivutio mkutanoni

Na Burhani Yakub

MBUNGE wa Jimbo la Karatu kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa na mkewe Rose Kamili, ambaye ni diwani wa Kata ya Basotu wilayani Hanang kwa tiketi ya CCM, ni wapinzani wa kisiasa, lakini wanashirikiana katika kufichua ufisadi kama ilivyodhihirika mwishoni mwa wiki.

Akiiwakilisha asasi isiyo ya kiserikali ya Pingo inayofanya kazi zake chini ya programu ya PETS katika mkutano wa wadau wa maendeleo wa Pact, mke huyo wa katibu wa Chadema alisisimua wengi alipoeleza jinsi alivyofichua kiasi cha Sh119.8 milioni ambacho hakikutumika kukarabati vituo saba vya afya wilayani Hanang.

Alisema wakati wakitekeleza jukumu walilopewa wajumbe wa asasi ya Pingo kuchunguza matumizi ya ruzuku ya serikali zinazopelekwa katika halmshauri ya Wilaya ya Hanang, uongozi uliwapa nyaraka zenye taarifa za kughushi.

Diwani huyo alisema mbali ya kutoa taarifa ya kughushi, uongozi huo wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang ulimtuma afisa maendeleo ya jamii kupeleleza kinachofanyika wakati wa kuchunguza matumizi ya fedha za serikali ili kutafuta njia za kuficha ukweli.

“Baada ya kugundua hilo, nilitumia nafasi yangu ya udiwani kwenda halmashauri kuomba taarifa za matumizi ya fedha, lakini hata mimi nilinyimwa ndipo nikaenda nyumbani kupekua mafaili ya vikao vya Full Council tukagundua kumbe walitupa taarifa feki,” alisema Rose.

Alisema baada ya kufanya uchunguzi ikabainika kuwa katika mwaka wa fedha wa 2005/2006 Halmashauri ya Wilaya ya Hanang ilipokea kiasi cha Sh119,880,000 kwa ajili ya ukarabati wa vituo saba vya afya ambavyo hadi walipokuwa wakichunguza mwanzoni Mei 2008 zilikuwa hazijatumika.

Alivitaja vituo ambavyo havikukarabatiwa licha ya halmashauri kuchukua fedha zake kuwa ni Masakta, Bassodesh, Endasak, Gidahababieq, Sirop, Dawr na kituo cha afya cha Katesh.

Baada ya kuchachamaa, mwaka huu halmashauri ilitoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa vituo hivyo. Haijulikani sababu za kuziweka fedha hizo kwa kipindi cha miaka miwili bila kuzitumia.

Diwani huyo machachari alisema licha ya halmashauri kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivyo vya afya, Pingo imebaini kuwa kiasi cha Sh55,128,000 bado hazijaingizwa kwenye akaunti husika na haifahamiki zimepelekwa wapi na kwa sababu zipi.

"Hili ni jambo ambalo naahidi kulifanyia kazi kwani hatuwezi kukubali kuona wananchi wanacheleweshewa maendeleo kwa makusudi," alisema.

Baada ya kutoa taarifa hiyo ukumbi ulilipuka kelele za shangwe huku wale wanaofahamu uhusiano wake na Dk. Slaa wakijiuliza ni vipi wakaweza kuwa kitu kimoja wakati wanatofautiana kiitikadi.

"Mimi siipendi kabisa Chadema na kwenye eneo langu la udiwani nahakikisha wafuasi wa CCM hawarubuniwi kuhama. Lakini nipo pamoja na Dk. Slaa katika suala zima analofanya la kufichua mafisadi," alisema Kamili.

"Mume wangu ni mzalendo mwenye uchungu na nchi yake."

Mkutano huo ulioandaliwa na Pets kwa kushirikiana na Pact Tanzania na Shirika la Misaada la Marekani (Usaid) na mfuko wa rais wa Marekani wa Millenium Challenge ulifayika kwa siku mbili na kushiriki wajumbe wa asasi mbalimbali kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani

source: mwananchi
 
Kwa ujumla hawa jamaa (Rose na Wilbroad) ni wasanii, wanawachezea akili wairaqw huko Karatu, na hakika wamefanikiwa! Huyu mama anatudanganya "anachukia" CHADEMA, chama ambacho mumewe ni Katibu Mkuu. Hapohapo tunafahamu kuwa huyo Dr Slaa aligombea ubunge kupitia CCM mwaka 1995 wakamwondoa "kimizengwe" licha ya kuwa alishinda kwenye kura za maoni, na ndiyo sababu pekee iliyomfanya akimbilie CHADEMA. Nadhani hata ile kadi ya CCM bado Wilbroad anayo. Nawasifu hawa jamaa kwa maigizo, hakika wamebobea!
 
Whats your point? Kwamba its not possible Mrs Slaa kuichukia Chadema?

Schwazeneger( sijui hio spelling ni sawa?) ni Republican na mkewe ni democrat wa nguvu,aliyejitokeza wazi kuwa anam support Obama.sasa na hayo ni maigizo?
Kama huyu mama anachukia Chadema kweli ni kwamba mume wake anajua,na haihusiani na uhusiano wao
 
Wewe nimekusikia. Na wengine mnasemaje?
 
Behind any Husband Mpinga Fisadiz there is a Wife Mpinga Fisadiz!
 
Wewe nimekusikia. Na wengine mnasemaje?

Na suala hapa siyo kwamba kama Mke wa Slaa anachukia CHADEMA ama la ila suala hapa ni kwamba wote kwa njia moja ama nyingine wanapingana na Fisadiz!
Chuki zao za kisiasa hazisaidii ili mradi tunawajua wezi na wazalendo!
 
Kwa ujumla hawa jamaa (Rose na Wilbroad) ni wasanii, wanawachezea akili wairaqw huko Karatu, na hakika wamefanikiwa! Huyu mama anatudanganya "anachukia" CHADEMA, chama ambacho mumewe ni Katibu Mkuu. Hapohapo tunafahamu kuwa huyo Dr Slaa aligombea ubunge kupitia CCM mwaka 1995 wakamwondoa "kimizengwe" licha ya kuwa alishinda kwenye kura za maoni, na ndiyo sababu pekee iliyomfanya akimbilie CHADEMA. Nadhani hata ile kadi ya CCM bado Wilbroad anayo. Nawasifu hawa jamaa kwa maigizo, hakika wamebobea!

tatizo tanzania tunachukulia siasa kama uadui!!! tusiwe kama kingunge tuwe na mtizamo mpana. maslahi ya taifa kwanza chama baadae
 
Nakubaliana na aliyesema kwamba hawa ni wasanii, kwa kuwa tu siasa ni sanaa na ukiitumia vyema hii sanaa kwa nia njema na kwa maslahi ya Taifa, sanaa ya siasa haina ubaya.

Mfano, Dk. Slaa alifanya sanaa ya siasa kutoa ile hoja yake bungeni na kuiwasilisha kwa wanananchi katika mkutano wa hadhara baada ya kuona inacheleweshwa na mambo yanazidi kuharibika na matokeo yake, Jk naye akafanya sanaa yake wakawapa wakaguzi wa nje kwa akaunti moja tu ya EPA wakague tena kwa mwaka 2005/2006 tu, bila kujali EPA ilianza zamani na wengi walichota karibu chaguzi zote tokea 1995. Halafu wakafanya sanaa nyingine kwa kuunda Timu ya kina Mwanyika, ambayo nayo baadaye wakaifanyia sanaa nyingine kuiongezea muda, sasa CCM wanafanya sanaa nyingine kumpongeza JK kwa sanaa aliyoifanya katika hotuba yake bungeni kwamba fedha za EPA zitapelekwa kwenye kilimo na watakaoshindwa kurudisha hadi Oktoba 31 watafikishwa mahakamani, ikiwa na maana watakaolipa wamepona!!! Tunasubiri sanaa nyingine.

Kama Dk. Slaa alifanya sanaa baada ya kutoswa na CCM akaingia Chadema, matunda yake tumeyaona na wengine waige kufanya hiyo sanaa, wahame CCM waingie upinzani na huko wafanya kazi ya kutetea wananchi na si matumbo yao, hapo tutaipongeza hiyo sanaa.
 
Mke wa Dk. Slaa .......
"Mimi siipendi kabisa Chadema na kwenye eneo langu la udiwani nahakikisha wafuasi wa CCM hawarubuniwi kuhama. Lakini nipo pamoja na Dk. Slaa katika suala zima analofanya la kufichua mafisadi," alisema Kamili.

"Mume wangu ni mzalendo mwenye uchungu na nchi yake."

source: mwananchi

Kwa ujumla hawa jamaa (Rose na Wilbroad) ni wasanii, wanawachezea akili wairaqw huko Karatu, na hakika wamefanikiwa! Huyu mama anatudanganya "anachukia" CHADEMA, chama ambacho mumewe ni Katibu Mkuu. Hapohapo tunafahamu kuwa huyo Dr Slaa aligombea ubunge kupitia CCM mwaka 1995 wakamwondoa "kimizengwe" licha ya kuwa alishinda kwenye kura za maoni, na ndiyo sababu pekee iliyomfanya akimbilie CHADEMA. Nadhani hata ile kadi ya CCM bado Wilbroad anayo. Nawasifu hawa jamaa kwa maigizo, hakika wamebobea!

Dr. Slaa yumo humu mtandaoni kwa hiyo anaweza kutueleza kama aliwahi kugombea uongozi ndani ya CCM au la. Kama aliwahi, basi inaelekea kwao siasa ni ajira na sio kuwa wanashabikia tofauti za kiitikadi kati ya CCM na CHADEMA. Popote watakapopata ajira ndio watakapopigia kelele wanayoyapigania. Kama kelele zao ni za danganya toto, basi hilo ndio la kudadisi.
 
Nakubaliana na aliyesema kwamba hawa ni wasanii, kwa kuwa tu siasa ni sanaa na ukiitumia vyema hii sanaa kwa nia njema na kwa maslahi ya Taifa, sanaa ya siasa haina ubaya.

Mfano, Dk. Slaa alifanya sanaa ya siasa kutoa ile hoja yake bungeni na kuiwasilisha kwa wanananchi katika mkutano wa hadhara baada ya kuona inacheleweshwa na mambo yanazidi kuharibika na matokeo yake, Jk naye akafanya sanaa yake wakawapa wakaguzi wa nje kwa akaunti moja tu ya EPA wakague tena kwa mwaka 2005/2006 tu, bila kujali EPA ilianza zamani na wengi walichota karibu chaguzi zote tokea 1995. Halafu wakafanya sanaa nyingine kwa kuunda Timu ya kina Mwanyika, ambayo nayo baadaye wakaifanyia sanaa nyingine kuiongezea muda, sasa CCM wanafanya sanaa nyingine kumpongeza JK kwa sanaa aliyoifanya katika hotuba yake bungeni kwamba fedha za EPA zitapelekwa kwenye kilimo na watakaoshindwa kurudisha hadi Oktoba 31 watafikishwa mahakamani, ikiwa na maana watakaolipa wamepona!!! Tunasubiri sanaa nyingine.

Kama Dk. Slaa alifanya sanaa baada ya kutoswa na CCM akaingia Chadema, matunda yake tumeyaona na wengine waige kufanya hiyo sanaa, wahame CCM waingie upinzani na huko wafanya kazi ya kutetea wananchi na si matumbo yao, hapo tutaipongeza hiyo sanaa.

Nafurahi kwamba mkuu nawe pia umeona hili, hakuna kitu kama commitment kwa itikadi wanayodai kufuata katika vyama vyao, ni wajanja hawana tofauti na wacheza ngoma ambao wanaongeza manjonjo ya unenguzi kwa kufuata kelele za washangiliaji! JK, Slaa na mkewe, wote wasanii tu!
 
Mke wa Dk. Slaa awa kivutio mkutanoni

Na Burhani Yakub

MBUNGE wa Jimbo la Karatu kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa na mkewe Rose Kamili,

Baada ya kutoa taarifa hiyo ukumbi ulilipuka kelele za shangwe huku wale wanaofahamu uhusiano wake na Dk. Slaa wakijiuliza ni vipi wakaweza kuwa kitu kimoja wakati wanatofautiana kiitikadi.

"Mimi siipendi kabisa Chadema na kwenye eneo langu la udiwani nahakikisha wafuasi wa CCM hawarubuniwi kuhama. Lakini nipo pamoja na Dk. Slaa katika suala zima analofanya la kufichua mafisadi," alisema Kamili.

"Mume wangu ni mzalendo mwenye uchungu na nchi yake."

source: mwananchi

Mkuu, Burhani Yakub, wa MWANANCHI,

Mpe ujiko mama bila kuanza aya ya kwanza na reference to her husband.

Dr. Slaa na CHADEMA sio the subject of the story. Huwezi kuanza story hivyo. Hata kama sio nia yenu, it smacks of male chauvinism and crummy journalism. Na mimi sikwenda hata darasa moja la Uandishi, kwa nini nyinyi wahariri hamuoni hivyo vitu?

(Granted that Mama nae is shooting her self in the foot by converting her 15 minutes of fame into "my husband" story. Wanawake na nyinyi jikomboeni. Mama Slaa ungekataa kuongelea mume ningekuhusudu ile mbaya. Unge stick kwenye CCM, ufisadi, na Udiwani. Kwishne.)
 
Mkuu, Burhani Yakub, wa MWANANCHI,

Mpe ujiko mama bila kuanza aya ya kwanza na reference to her husband.

Dr. Slaa na CHADEMA sio the subject of the story. Huwezi kuanza story hivyo. Hata kama sio nia yenu, it smacks of male chauvinism and crummy journalism.

Na mimi sikwenda hata darasa moja la Uandishi, kwa nini nyinyi wahariri hamuoni hivyo vitu?

Ndio maana nikasema huyu mama na mumewe ni wasanii tu, wanacheza maigizo hapa. Huyu mwandishi Burhani Yakub has (probably unknowingly) just jumped into the duo's bandwagon!
 
Kama Dk. Slaa alifanya sanaa baada ya kutoswa na CCM akaingia Chadema, matunda yake tumeyaona na wengine waige kufanya hiyo sanaa, wahame CCM waingie upinzani na huko wafanya kazi ya kutetea wananchi na si matumbo yao, hapo tutaipongeza hiyo sanaa.

Huu wa mama Slaa kupingana na mumewe itakuwa ni usanii kama ni kweli Dr.Slaa alihama CCM baada ya kukosa uongozi, hata kama ilikuwa ni "kimizengwe". Kwa hiyo hii inaweza kuelezea kwa nini Dr. Slaa ameamua kuwa mtu wa kukubali tu ya m'kiti wake, Mbowe, bila kupinga, hata kama yana ubovu, ili asije akapoteza tena ajira aliyo nayo hivi sasa.
 
Ndio maana nikasema huyu mama na mumewe ni wasanii tu, wanacheza maigizo hapa. Huyu mwandishi Burhani Yakub has (probably unknowingly) just jumped into the duo's bandwagon!

Ha ha aaa aaa

That's a little too brutal, Kithuku, noma!

Kwa hiyo Mama alikuwa anampigia mumewe debe?

It's plausible to look at it that way. You got a point there. But, all in all, mi naamini mambo anayoyapigia kelele Dr. Slaa anamaanisha kutoka moyoni.

Na namsifu mkewe kwa kutokumfuata mumewe huko CHADEMA.

Lakini hiyo dynamic duo yao, labda kweli inaweza kuwa na mushkeli, in terms of authenticity of their differences.
 
Investigation ya dokta Masau vipi?
 
Kwa ujumla hawa jamaa (Rose na Wilbroad) ni wasanii, wanawachezea akili wairaqw huko Karatu, na hakika wamefanikiwa! Huyu mama anatudanganya "anachukia" CHADEMA, chama ambacho mumewe ni Katibu Mkuu. Hapohapo tunafahamu kuwa huyo Dr Slaa aligombea ubunge kupitia CCM mwaka 1995 wakamwondoa "kimizengwe" licha ya kuwa alishinda kwenye kura za maoni, na ndiyo sababu pekee iliyomfanya akimbilie CHADEMA. Nadhani hata ile kadi ya CCM bado Wilbroad anayo. Nawasifu hawa jamaa kwa maigizo, hakika wamebobea!

Nadhani Kithuku suala hapa siyo usanii kama ulivyosema.Mantiki hapa ya thread iliyotolewa ni kuwasilisha ukweli uliopo kwa wanasiasa hawa wawili.

Kwa mtizamo wangu Dr Slaa na Mkewe wanawasilisha maana halisi ya uanasiasa.Siasa ni kutofautiana kiitikadi bila kuathiri mtizamo sawa wa kulijenga taifa.Hakuna usanii wowote katika utumishi wa hawa wanasiasa.Pengine usanii huo waweza kuonekana kwa yule anayetizama harakati nzuri kwa jicho la siasa potofu
 
Mkuu, Burhani Yakub, wa MWANANCHI,

Mpe ujiko mama bila kuanza aya ya kwanza na reference to her husband.

Dr. Slaa na CHADEMA sio the subject of the story. Huwezi kuanza story hivyo. Hata kama sio nia yenu, it smacks of male chauvinism and crummy journalism.

Na mimi sikwenda hata darasa moja la Uandishi, kwa nini nyinyi wahariri hamuoni hivyo vitu?

(Granted that Mama nae is shooting her self in the foot by converting her 15 minutes of fame into "my husband" story. Wanawake na nyinyi jikomboeni. Mama Slaa ungekataa kuongelea mume ningekuhusudu ile mbaya. Unge stick kwenye CCM, ufisadi, na Udiwani. Kwishne.)

Mkuu Kuhani,
Nafikiri isingewezekana kwa huyu mama kuandikwa gazetini kama asingekuwa ni mke wa mtu maarufu kama Dr. Slaa. Ndio maana heading ikabidi iwe kama ilivyo. Kwa maana nyingine ni kuwa mwandishi naye ameshangaa kuoana hawa wawili wakiwa wanapigania mambo yanayofanana lakini wakiwa na itikadi tofauti.

Hata hivyo, mkuu Kithuku baada ya kuangalia historia zao, ndio akawaona kuwa ni wasanii tu kitu ambacho inawezekana ikawa hivyo.
 
Siasa adilifu ni njia ya kupata ruhusa/ridhaa ya wananchi kutoa huduma kwa namna unayopenda au unayodhani utafaidisha wananchi na wewe pia.

ni sanaa, ni kipaji, ni utaalamu, ni imani nk.
LAkini kwa kuwa ni njia ya kutufikisha tunakotaka kwenda, then waacheni wawe wanasiasa wa chama chochote, mradi lengo ni kuhakikisha bajeti yetu inatumiwa kama ilivyopangwa. Isichotewe kwenye mifuko mingine.
Kama wanataka kuila, waombe hela ya kula wasisingizie hospitali halafu wakaila hiyo hela.
 
Dr. Slaa yumo humu mtandaoni kwa hiyo anaweza kutueleza kama aliwahi kugombea uongozi ndani ya CCM au la.

Mh. Dr. Slaa, niajuavyo ni kweli aliwahi kugombea ubunge kupitia CCM, kamati kuu kwenye kuchuja majina wajumbe wengi walitaka Dr. Slaa apewe hiyo nafasi kwa sababu CCM wana kamati ya kutathmini hali ya jimbo ambapo hufanya utafiti wa hali ya juu sana kwamba nani anayekubalika katika lile jimbo, na hii huwa ni kazi ya makamu wa mwenyekiti wa CCM.

Mapendekezo yao kwa kamati kuu ya CCM, ilikuwa ni DR. Slaa ndiye anayekubalika katika lile jimbo, la Karatu. Kati ya majina ya wagombea kulikuwa na jina la rafiki wa karibu wa mwenyekiti wa CCM then, Mkapa, kama sikosei alikuwa ni Quaresi, kikao kilimalizika na hayo makubaliano kuwa DR. Slaa ndiye apewe ile nafasi kwa tiketi ya CCM, lakini Mkapa akaamua kutumia ubabe wake na kumpitisha rafiki yake over chaguo la wananchi wa Karatu na kamati kuu ya CCM, DR. Slaa,

Ndipo DR. Slaa akaamua kugombea ubunge kwa kupitia Chadema na akashinda ushindi wa kishindo, tena sio mara moja so far na hajawahi since then kurudi CCM, na amekuwa nyota njema kwa taifa kwa sababu ya kuweza kuwafichua mafisadi wengi kutoka chama chake cha zamani CCM, ni majuzi tu hapa niliona baadhi mambers wakimtaka Nape kuhamia Upinzani, baada ya kuamini kuwa ameonewa kule CCM,

Sasa naomba kuuliza what is this topic all about, maana so far sijaelewa vizuri?Kwamba mke wa Dr. slaa ni lazima naye awe na siasa za upinzani au? Hiyo inapswa kuwa ni sheria au maneno ya mtaaani tu ambayo hapa JF tunayakataa sana!
 
Mkuu Kuhani,
Nafikiri isingewezekana kwa huyu mama kuandikwa gazetini kama asingekuwa ni mke wa mtu maarufu kama Dr. Slaa. Ndio maana heading ikabidi iwe kama ilivyo. Kwa maana nyingine ni kuwa mwandishi naye ameshangaa kuoana hawa wawili wakiwa wanapigania mambo yanayofanana lakini wakiwa na itikadi tofauti.

Hata hivyo, mkuu Kithuku baada ya kuangalia historia zao, ndio akawaona kuwa ni wasanii tu kitu ambacho inawezekana ikawa hivyo.

Nimekuelewa vizuri sana kwa nini huyu Mama akapata media coverage in the first place. The heading is perfect. The problem is how he opens up the story: "MBUNGE wa Jimbo la Karatu kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa na mkewe Rose Kamili..." Angesema "Mke wa Mbunge wa CHADEMA..." ingekuwa poa.

Back to a bigger issue. Nilikubaliana na Kithuku kwamba Mama alipoanza kumpigia debe Baba unaweza kusema plausibly kwamba ilikuwa ni aina ya usanii.
 
Back
Top Bottom