Waratibu wa huduma ndogo za fedha nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana na BoT

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Na Eva Valerian na Asia Singano

Waratibu wa huduma ndogo za fedha nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ili kuboresha huduma za fedha na kuleta maendeleo ya kiuchumi hapa nchini.

Hayo yalisemwa na Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro, wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa waratibu wa Biashara ya Huduma ndogo za Fedha na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, jijini Dodoma.
PIC 1.jpg

Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo kwa waratibu wa Biashara ya Huduma ndogo za Fedha na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, yaliyofanyika jijini Dodoma, Wizara ya Fedha katika ukumbi wa Kambarage.
PIC 2.jpg

Mtaalamu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Grace Samweli akitoa mada kuhusu mfumo wa Usajili na Usimamizi wa Vikundi vya Kijamii vya Huduma Ndogo za Fedha Pamoja na Wahamasishaji wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha; unavyofanya kazi, ili kuwajengea uelewa dhidi ya mfumo huo na kuwarahisishia kazi waratibu hao wanaporudi kwenye vituo vyao vya kazi.
PIC 3.jpg

Baadhi ya Waratibu wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, wakifuatilia mafunzo ya namna bora ya utoaji huduma ndogo za fedha, yaliyofanyika jijini Dodoma, Wizara ya Fedha katika Ukumbi wa Kambarage.
PIC 4.jpg

Picha ya Pamoja na baadhi ya Waratibu wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, waliohudhuria mafunzo ya namna bora ya utoaji huduma ndogo za fedha, yaliyofanyika jijini Dodoma, Wizara ya Fedha katika Ukumbi wa Kambarage.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
 
Back
Top Bottom