Mkasa wa Yanga kuchapana bakora na kuvunja timu baada ya kupigwa 4-1 na Simba, Mwaka 1994

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,722
45,129
Tukiwa tunaeleka derby ya kariakoo hapo kesho, sio mbaya tukakumbusha baadhi ya vituko, mikasa na visa vilivyowahi kutokea huko nyuma. Leo tuikumbuke mechi iliyowafanya Yanga (Gongowazi) kuchapa bakora na kupelekea kufukuza karibia wachezaji wake.

July 2, 1994 katika dimba la Uhuru, Dar Es Salaam. Kulifanyika mchezo kati ya Simba dhidi ya Yanga.

Ikumbukwe, Yanga alikuwa bingwa mtetezi wa Kombe la Klabu bingwa Afrika Mashariki (Sasa Kagame Cup)
walitwaa kombe hilo nchini Uganda mwaka mmoja uliopita. Yanga alikuwa na kikosi kizuri sana. Lakini pia katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Yanga aliifunga Simba 2-0. Hivyo Simba waliingia kama underdog.

Kuelekea mechi ya derby, Yanga wakaanza kuvutana wenyewe kwa wenyewe. Kulikuwa na Yanga asili chini ya Marehemu Mzee Mengi na matajiri akina Gulamali na Yanga kampuni chini ya mwenyekiti Mpondela.

Katika maandalizi ya mechi hiyo, Timu ya Yanga ikatekwa na kundi la Yanga asili na kufichwa Kibaha mkoani Pwani. Hali iliyompelekea aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Augustine Liyatonga Mrema kutoa tamko Wachezaji warejeshwe Dar Es Salaam. Kweli siku ya 3 wakarejeshwa.

July 2, ikafika, uwanja ukiwa umefurika, mechi ikapigwa, mapema tu kipindi cha kwanza Costantine Kimanda na George Magere Masatu wanazifungia timu zao na kufanya matokeo kuwa 1-1 wakati wa mapumziko.

Kipindi cha pili, kukatokea mauaji ya sharubela, Mnyama mkubwa mwituni, Simba Sc akaonyesha ukubwa wake, wakaisasambua Yanga bila hiyana.

Magoli ya Athumani China, Madaraka Selemani na Dua Said yakaizamisha Yanga jumla ya 4-1.
Mashabiki wa Yanga wakakasirika, wakatoka mapema uwanjani moja kwa moja mpaka klabuni Jangwani.

Kulikuwa na tuhuma za wachezaji wa Yanga kuhujumu mechi hiyo, basi hapo ndipo Yanga walipotembezeana bakora mpaka kuitana gongowazi. Yaani mwenye fimbo, gongo, mti angeweza kuitumia kama silaha ili kuadhibu waliohujumu iwe kiongozi, mwanachama au mchezaji.

Baada ya kipigo hiko, Yanga aliwafukuza karibia wachezaji 18 wa kikosi cha kwanza na kubakiza wachezaji nane tu akiwemo beki nguli Costantine Kimanda (aliyepo Ubeleshi kwasasa)

Baadhi ya wachezaji, waliofukuzwa ambao walikuwa mastaa ni pamoja na Said Mwamba Kizota, Steven Nemes, Edibily Jonas Lunyamila nk.

Yanga wakapandisha wachezaji wa kikosi B ili kuziba nafasi za waliofukuzwa, baadhi ya waliopandishwa ni pamoja na Anwar Awadh, Maalim Saleh, Nonda Shaban Papii.
9BC53EE0-1C9B-4440-939D-9067EFCF584B.jpeg
 
54AEE3CA-5D14-40E0-8D5F-1DDF2F8C6A49.jpeg

Waliosimama kutoka kushoto; Salum Kabunda "Ninja", Costantine Kimanda, Steven Nemes, Kenny Mkapa na Selemani Mkati.

Waliochumamaa kutoka kushoto ni; Nico Bambaga, Sekilojo Chambua, Edibily Jonas Lunyamila, James Tungaraza "Bolizozo" na Said Mwamba Kizota.

Hiki ndio kikosi kilicholamba 4-1 na kuamsha ghadhabu kubwa mitaa ya Twiga na Jangwani.
 
Nonda shaaban alikuwa wa kawaida Sana ajabu akaenda kucheza Ulaya akiacha wachezaji waliomzidi vipaji
 
Mleta mada tunaomba utukumbushe na ya mwaka 1968 na 1969 ilikuwaje maanake vijana wa humu jukwaani hata baba, zao walikuwa hawajazaliwa. Itakuwa vizuri sana ukitusimulia na ya zama hizo.
 
Hii stori Huwa napenda kuitoa pia Ili kuwananga Makolo wasijisifie sana kuifunga Yanga goli nyingi Huwa lazima Kuna Mgogoro Jangwani.

Mwaka 2012 Simba waliifunga Yanga magoli 5 - 0.

Jangwani kulikuwa na mgogoro mkubwa sana na siku moja kabla ya mechi Mimi binafsi niliona Mzee Akilimali alikuwa akiongea ITV taarifa ya habari na akavua kofia akaweka juu ya Meza akasema kwa hasira kali kesho Derby ya Kariakoo tutajua nani mkubwa Yanga! Mzee Akilimali aliilaani timu. Akawin!!

Hebu Simba tufungeni Tena goli 5 tuhamie timu yenu mbovu!!

Kesho ni kichapo tu Simba lazima wakae kimya mji utulie na tutapata penati kupitia Moloko ambae atalazimisha mara nyingi kuingia kwenye penati box ya Simba na uchochoro Onyango atamuangusha!

Musonda ndie atatutoa kimasomaso atafunga goli 2.

Mayele atapiga goli 1.

Mudathir must play at his best ni kivuruge tunaemtegemea kesho.

Mauya acheze second half yote kukaba Simba watapambana sana kurudisha goli 3 tutakazowapiga kipindi Cha kwanza!!
 
Naona mtoa mada analeta story za Yanga asili vs Yanga Kampuni kwa lengo la kujipa moyo kuhusu mechi ya kesho.

Kwa bahati mbaya sana amesahau ya kwamba Yanga itakayocheza kesho, ni Bingwa mtetezi! Ni Yanga iliyokamilika kila idara! Ni Yanga yenye morali ya hali ya juu ya ushindi (mpaka muda huu imepoteza mchezo mmoja tu kwenye ligi)! Na ni Yanga yenye umoja kuanzia kwa mashabiki, wanachama, wachezaji, benchi la ufundi, na viongozi.

Kiufupi ni kwamba Yanga itacheza mchezo wa kesho huku ikiwa haina kabisa presha kama ilivyo kwa simba, ambayo ina michezo mingi migumu mbele yake; na wakati huo huo ikiwa haina kikosi kipana cha wachezaji.
 
Naona mtoa mada analeta story za Yanga asili vs Yanga Kampuni kwa lengo la kujipa moyo kuhusu mechi ya kesho.

Kwa bahati mbaya sana amesahau ya kwamba Yanga itakayocheza kesho, ni Bingwa mtetezi! Ni Yanga iliyokamilika kila idara! Ni Yanga yenye morali ya hali ya juu ya ushindi (mpaka muda huu imepoteza mchezo mmoja tu kwenye ligi)! Na ni Yanga yenye umoja kuanzia kwa mashabiki, wanachama, wachezaji, benchi la ufundi, na viongozi.

Kiufupi ni kwamba Yanga itacheza mchezo wa kesho huku ikiwa haina kabisa presha kama ilivyo kwa simba, ambayo ina michezo mingi migumu mbele yake; na wakati huo huo ikiwa haina kikosi kipana cha wachezaji.
Kwa mujibu wa mtoa mada hata yanga iliyokula 4 ilikuwa bingwa mtetezi. Ila yanga akipigika kwa Simba anapigwa kweli kweli
 
Kwa mujibu wa mtoa mada hata yanga iliyokula 4 ilikuwa bingwa mtetezi. Ila yanga akipigika kwa Simba anapigwa kweli kweli
Hizo ni zilipendwa! Kwa Yanga hii ya sasa, simba ikijitahidi sana basi ni sare. Na huu ndiyo ukweli mchungu.
 
Nonda shaaban alikuwa wa kawaida Sana ajabu akaenda kucheza Ulaya akiacha wachezaji waliomzidi vipaji
Alikua anajua kufunga,niliiona ule msimu alipokua mfungaji Bora Ligue 1,enzi hizo mwenye udambwi ndiyo mchezaji,nonda hakuwa na mengi
 
Back
Top Bottom