Mambo 6 ambayo Yanga SC imeizidi Simba SC

kalisheshe

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
1,873
3,492
Huwa sifurahii kuona mafanikio ya Yanga kitu kilichofanya nisiwe naangalia michezo Yao.
Kama bahati mbaya Jana nilikaa peke yangu mbele ya luninga kuangalia mechi ingawa niliumia ila hiki ndio nilichokiona Kwa yanga.

1. Uongozi mzuri unaowapa hamasa wachezaji na benchi la ufundi ndio umeifikisha hapa yanga.

2. Wachezaji wa yanga wanajituma, wakipoteza mpira haraka wanapambana kuutafuta na kuurejesha kwenye himaya Yao.

3. Yanga wamefanya usajiri wa maana sana, sifikirii na sidhani kama Kuna kiongozi aliyechukua 10% Ili amlete mchezaji

4. Pacome zouzou ni mtu, Simba SC walifika mapema Ivory coast na wakashindwa kumsajiri ( poor leadership).

5. Morali ya timu Iko juu sana, timu inapambama kupata inachokitafuta na ndani ya muda mfupi inakipata, tofauti kabisa na Simba ambayo inacheza bila kujua inatafuta nini ( rejea mechi ya juzi na Asec)

6. Wachezaji wanacheza kitimu na yeyote akionekana hayuko mchezoni anapumzishwa nje ( tofauti na timu yangu ambayo mkalimani saidoo hachezi kitimu na anamaliza dakika zote 90 ).

Mnyonge mnyongeni Yanga SC Iko moto sana.
 
Sitacomment chochote mpaka uje hata kusalimia hapa..
Screenshot_2024-02-25-06-30-14-803_com.android.chrome.jpg
 
Uko sahihi ila mpira wa Jana inaonekana yanga waliuhifadhi mahali Kisha wakauleta Jana
Mkuu kubali tu kuwa yanga Wana kikosi bora mno sio kwamba mpira wa jana tu ndo unadhihirisha uwezo wao,tangu msimu umeanza wako vyema
 
Huwa sifurahii kuona mafanikio ya Yanga kitu kilichofanya nisiwe naangalia michezo Yao.
Kama bahati mbaya Jana nilikaa peke yangu mbele ya luninga kuangalia mechi ingawa niliumia ila hiki ndio nilichokiona Kwa yanga.

1. Uongozi mzuri unaowapa hamasa wachezaji na benchi la ufundi ndio umeifikisha hapa yanga.

2. Wachezaji wa yanga wanajituma, wakipoteza mpira haraka wanapambana kuutafuta na kuurejesha kwenye himaya Yao.

3. Yanga wamefanya usajiri wa maana sana, sifikirii na sidhani kama Kuna kiongozi aliyechukua 10% Ili amlete mchezaji

4. Pacome zouzou ni mtu, Simba SC walifika mapema Ivory coast na wakashindwa kumsajiri ( poor leadership).

5. Morali ya timu Iko juu sana, timu inapambama kupata inachokitafuta na ndani ya muda mfupi inakipata, tofauti kabisa na Simba ambayo inacheza bila kujua inatafuta nini ( rejea mechi ya juzi na Asec)

6. Wachezaji wanacheza kitimu na yeyote akionekana hayuko mchezoni anapumzishwa nje ( tofauti na timu yangu ambayo mkalimani saidoo hachezi kitimu na anamaliza dakika zote 90 ).

Mnyonge mnyongeni Yanga SC Iko moto sana.
acha kutumia r kwenye l sio kusajiri ni kusajili
 
Kosa mnalofanya wengi wenu ni kulinganisha Yanga na vikundi vya kihuni.
 
1. Majini ,
2. Akili
3. Wao wapo kimaslahi
5. Wachezaji wao wanajua ukizingua unasepa
6. Siri

Simba
1. Wapo kama washiriki
2. Wao waganga wao wamebuma wanashikwa shikwa
3.hawatolewi wala hawagombezwi wakifanya vitu labda kocha
4. Wapo tu nyota zao zipo yanga
5. Hawana majini makali
6. Wakishafika uwanjani akili inahama inaenda yanga na juhudi yote ndio maana ukitoka yanga unakuwa hujijui unatumika kimajini
 
  • Quality players
  • Quality coach
  • Quality scouting team
  • Quality training environment ( Avic town)
  • Quality digital team
*

Benchika huenda ni kocha mzuri...lakini bado ni kama anashindwa kutengeneza team ya ufundi.
Labda USM ALGIERS walikuwa team kubwa.

Simba inahitaji kufanya ovehaul transformation ..izalishe kizazi kichanga chenye mchanganyiko wa skills..
 
Huwa sifurahii kuona mafanikio ya Yanga kitu kilichofanya nisiwe naangalia michezo Yao.
Kama bahati mbaya Jana nilikaa peke yangu mbele ya luninga kuangalia mechi ingawa niliumia ila hiki ndio nilichokiona Kwa yanga.

1. Uongozi mzuri unaowapa hamasa wachezaji na benchi la ufundi ndio umeifikisha hapa yanga.

2. Wachezaji wa yanga wanajituma, wakipoteza mpira haraka wanapambana kuutafuta na kuurejesha kwenye himaya Yao.

3. Yanga wamefanya usajiri wa maana sana, sifikirii na sidhani kama Kuna kiongozi aliyechukua 10% Ili amlete mchezaji

4. Pacome zouzou ni mtu, Simba SC walifika mapema Ivory coast na wakashindwa kumsajiri ( poor leadership).

5. Morali ya timu Iko juu sana, timu inapambama kupata inachokitafuta na ndani ya muda mfupi inakipata, tofauti kabisa na Simba ambayo inacheza bila kujua inatafuta nini ( rejea mechi ya juzi na Asec)

6. Wachezaji wanacheza kitimu na yeyote akionekana hayuko mchezoni anapumzishwa nje ( tofauti na timu yangu ambayo mkalimani saidoo hachezi kitimu na anamaliza dakika zote 90 ).

Mnyonge mnyongeni Yanga SC Iko moto sana.
Hizo story namba nne mnapangwa na viongozi wenu eti kila mchezaji mzuri wa Yanga,Simba alifika mapema mara Zengeli mlifika mapema,mara Aucho, mara sijui Pacome nk.Kubalini hamna jicho la kuwaona wachezaji.Yanga ya Hersi ikimtaka mtu inaweka mzigo haijiulizi na Sajili za Pacome, Yao Yao,Max na Ki zilikuwa kimya kimya, ila Ki Azam peke yake ndio walikuwa wanatuvurugia.

Mna maskauti mmewasajili ilivyo isha ligi msimu uliopita,still mnasajili wachezaji wa hovyo na ukitizama hata hao maskauti hawa shirikishwi kwenye usajili.
 
Back
Top Bottom