Mkasa wa maisha yangu

Mkasa wa maisha yangu

Status
Not open for further replies.
Kutapeliwa katika hali ya kumsaidia mtu....kuna baraka kwa mwenyezi mungu...
 
Nina imani baada ya wadau kuhakiki hicho ulichoandika tutajitoa kwa kidogo tulicho nacho kuhakikisha una piga shule kadri ya ukomo wa kichwa chako
 
nilitaka kuingia kichwakichwa nimsaidie bora nimesoma comment zenu zimenifumbua macho
kumbe ndo zake anatapel kupitia mitandao heee ameshafumwa hajui kuwa hapa ni jf imara
Huyu Mbaga Michael ni tapeli aliwahi kuomba mchango wa kumtibia babake kule facebook 2011, alidai kalazwa bugando hutu.
 
Njaa kali

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Habari ndg, WanaJF

Kabla ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa mema mengi aliyotenda juu yangu sina budi kumwambia ahsante kwa upendo wako kwangu.

KUZALIWA
Nimazaliwa mwaka 1991 katika kijiji cha Chamhunda wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza katika familia ya Mzee Michael Chilato nikiwa mtoto wa mwisho kwa mama yetu kati ya wake watatu wa baba yetu.


Mama yangu alikwisha kutengana na baba yangu tangu mwaka 1996 nikiwa bado mtoto[5] ambapo mzee alioa mke mwingine hivyo nimelelewa na mama wa kambo mpaka kukua kwangu.

SHULE

Nilianza shule mwaka 2001, nikiwa darasa la tano mjomba wangu alikuja kutusalimia nyumbani na akaniomba niende kwake nikasomee huko, alimweleza baba na hakukataliwa hivyo safari ikapangwa ya kuelekea mkoani Shinyanga tayari kwa masomo huku kwa mjomba.

Maisha yaliendelea kama kawaida hatimae mwaka 2007 nilihitimu masomo yangu ya elimu ya msingi, nilirudi nyumbani kusalimia pia nikisubiri matokeo kama nitafanikiwa kuendelea na elimu ya sekondari au laah?
Matokeo yakatoka nilichaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari Pandagichiza iliyoko wilaya ya Shinyanga [V] Niliandaliwa mahitaji ya shule ingawa yooote hayakutimia.

Hivyo nilikuwa nasumbuliwa sana shule nalienda hivyo hivyo mpaka nikamaliza kidato cha 1

Hivyo nilirudi nyumbani kwa ajili ya kufuata ada ya mwaka uliofuata pamoja na madeni ya mwaka uliopita kwa kipindi kile wengi wetu hatukuwa tunamiliki simu hivyo mawasiliano na watu wa nyumbani hayakuwepo, hivyo hata nauli alinikopesha mwl ili nitakaporudi nimrudishie, niliondoka na kurudi nyumbani.

Ilipofika januari nilitakiwa kurudi shule lakini jambo la kushangaza na ambalo mpaka leo siamini nikikumbuka, Baba yangu alikataa kunisomesha katakata akidai nikamwambie mama yangu anisomeshe maana hata yeye ni mzazi wangu anapaswa kunisomesha, anatamka hayo akitambua fika kuwa mama yangu hana kipato chochote cha kuweza kunisomesha. Hivyo ndoto zangu za kuendelea na shule zikaishia hapo.

Nilipenda na napenda sana kusoma hivyo ikanibidi nitoke nyumbani niende mjini kutafuta kazi, nilibahatika kupata kazi ya bar nilifanya pale kwa mwaka mmoja nikiwa kama counter. Niliacha kazi kuendelea kufuatilia swala langu la shule huko mkoani Shinyanga baada ya kupata viela kidogo cha kusikitisha nilipofika shuleni sikuruhusiwa kuendelea na masomo kwa sababu mimi si mwanafunzu tena kwani nimekwisha kufutwa kwa sababu ya kutohudhuria shule kwa miezi mitatu mfululizo bila taarifa yoyote, niliumia sana nimeacha kazi kwenda shule nimefika shule siruhusiwi kusoma.

Niliamua kurudi shule maana sina mtu yoyote wa kunisaidia mjomba wangu nae alikwisha kuhama na kuhamia mkoani Tabora

Maisha yalibadilika na kuwa magumu sana sina kazi nitaishije bila kazi, nilihamua kutafuta tena kazi nilibahatika kukutana na bw. mmoja hivi ambae aliniunganisha na jamaa yake Arusha ana bar hivyo nikafanye kazi huko, nilipata hivyo nikatakiwa kwenda Arusha kutafuta hela tena, nilifanya pia kwa mwaka ka na nusu hivi nikarudi Mwanza kutafuta shule ili niweze kuendelea niliende nje ya mji ambako nilidhani ningaliweza hata kuuziwa jina lakini ilishindikana.

katika pitapita katika mitandao ya kijamii nilikutana na bw. mmoja hivi ambae tulijenga urafiki na hatimae nilimweleza history ya maisha yangu huyo bw anaka Dodoma na anafanya kazi huko ya kufundisha aliniambia njoo huku ninaweza kukusaidia nilifunga safari mpaka dodoma nimkiwa mwenye furaha isiyo na kifani ya kuona malengo yangu yanakenda kutimia narudi darasani tena, ilikuwa ni 2012 juni kwa vile muda ulikuwa umeenda nilianza shule mwaka uliofuata nikiwa kama private candidate [QT] ambayo unasoma miaka miwili kisha unafanya mtihani wakidato cha nne.


Nilifurahi sana nilisoma kwa bidii sana na uchungu mwingi kwa misukosuko niliyokutana nayo, mwezi wa kumi na moja mwaka jana tulifanya necta kwa ajili ya kupata usajili wa kitado cha nne mwaka unaofuata, nilifaulu hivyo nilitakiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu lakini cha kusikitisha na maajabu kwangu huyu mdhamini wangu baada ya kuoa ameniambia ameshindwa kuendelea kunisomesha maana mzigo umekuwa mkubwa nae pia anatakiwa kwenda kusoma hivyo niangalie naman nyingine ya kujisaidia.

WANAJF
mimi ni mdogo wako, mwanao, rafiki yako, jamaa yako n.k nakuombeni msaada wenu wa hali na mali niweze kumaliza elimu yangu hii ya kuungaunga nimalize hta hicho kidato cha nne mpaka sasa toka mwaka jana nifanye mtihani sijarudi shule, nisaidie chochote kile nifanikishe malengo yangu, natanguliza shukrani zangu za dhati kabisa kwenu kwa wale mtakaosoma na kuguswa na jambo hili.


Ahsante Mungu

Kwa mawasiliano 0769782386 au 0716863406


Mungu na awabariki sana

Mtu hana school fees ana simu mbili?

Ukiona ji-habari reeefu ujuwe ni utapeli. Mwenye shida ya ukweli haombi msaada mtandaoni.

Mwenye kutaka msaada kweli huwa hana wakati wa kutunga kisa cha maisha yake!

Wana JF jichungeni, huu ni utapeli hakuna zaidi. Msiseme watu wazima hatuja-wa-tanabahisha.
 
Nenda shule. Weka taratibu zote sawa pesa tunakutolea. Ila pesa zote zitatumwa kwa mkuu wa shule.
 
hacha uvivu wa kufikiri,simu nikitu kisichoepukika unaweza lala njaa ili ununue simu...
 

Mtu hana school fees ana simu mbili?

Ukiona ji-habari reeefu ujuwe ni utapeli. Mwenye shida ya ukweli haombi msaada mtandaoni.

Mwenye kutaka msaada kweli huwa hana wakati wa kutunga kisa cha maisha yake!

Wana JF jichungeni, huu ni utapeli hakuna zaidi. Msiseme watu wazima hatuja-wa-tanabahisha.

huyo ni tapeli......
 
Utapeli in action. Huyu jamaa alifungua akaunti hii inaonyesha kwa ajili ya hii misheni .Hili msiwe na doubt akafanya na verification kabisa. Kuna statement anasema yupo Dom toka 2012 na hajaenda Mwanza. Kuna mawili hapa. Aidha huyu dogo account yake imekuwa hacked baada ya kusahau ku log out kwenye internet Cafe au yeye mwenyewe ndo tapeli.
 
Mr [MENTION=101135]@Michael Mbaga watu wanasema wanakufaham na ulishawahi kutapeli huko mwanza sasa wawekee picha yako hapa kuthibitisha kuwa sio wewe na wanakufananisha. Weka kapicha pliiiizzz. Pia weka namba ya mkuu wa kituo unachotarajia kufanyia mtihani tuwasiliane nae kwa uthibitisho zaidi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom