Mkasa wa maisha yangu

Mkasa wa maisha yangu

Status
Not open for further replies.
Mkuu umeona lakini maisha yake yanavyotia simanzi.

Mkuu P. Majaribu, naomba nikushauri kidogo, siku nyingine unajua habari ya mtu hapa jukwaani, na ana nia mbaya kama kutapeli. Tafadhali iweke wazi kuliko kufumba mafumbo, kama ulivyofanya kwa huyu.
Ungeweka wazi tu kuwa jamaa ana A to Z, inasaidia kuokoa muda, pia watu wasitapeliwe.
Sasa wewe umezunguka sana, mtu kaweka picha zake ndio unaanza kufunguka kidogo si vizuri. Ndio maana baadhi ya wadau hapa walikuona kama hutaki tu asaidiwe.
Jaribu kuwa muwazi kwenye jambo la kujenga km hili.
 
Last edited by a moderator:
Kama ni shule mwanangu komaa, km yupo wakuthibitisha, kuhusu anayoyasema bwana mdogo basi tuweni tayari kumuunga mkono, jamani kijana hajaomba chakula ameomba elimu ili siku nyingine asiombe pesa.

Mungu atakupigania mwanangu Mbaga

Ndugu msisite kumsaidia, kama kadanganya hukumu ni juu yake.
 
Mtoto mdogo anapangilia maneno na kuandika kwa hekma kiasi hiki? ..kweli katoto haka? Si kwweli. Naungana na wanaomtilia shaka!.. hata hivyo mi siwaamini sana watu wanoomba msaada kwa watu wasiowajua...wengi ni matapeli mnaopenda kutapeliwa enndeleeni.


Haaaa Haaaa wengine IQ zao Zipo juu mkuu
 
Mbaga Michael Hakuna aliyekataa kukusaidia, tumejitokeza humu tupo ready kukupa msaada.
Ni Vizuri ukadhibitisha haya
1. wewe ni Mbaga Michael wa facebook
2.ulitangaza nia kugombea ubunge?
3.sasa hivi dodoma unakaa kwa nani?
4.ni msaada wa sh ngapi unaokidhi hitaji la ada?
5.usajili kwa watahiniwa binafsi kwa mwaka huu si umeshafungwa? au unataka kujisajili kwa mwakani?
6.je unadhani kuna kitu kingine unahitaji kusaidiwa mbali na ada?

Eleza vizuri usaidiwe jamii ya Jf ni kubwa. Together We Can.

Io hoja ya ubunge.nna wasiwasi nayo maana kwa Sasa Ana miaka 23....Je Huo ubunge aligombea akiwa na miaka mingapi???
 
Last edited by a moderator:
kama ni kweli basi mm ntakuwa tayari kukusaidia endapo ntapata uthibitisho wa ukweli kuhusu hili humu jf
 
Mkuu P. Majaribu, naomba nikushauri kidogo, siku nyingine unajua habari ya mtu hapa jukwaani, na ana nia mbaya kama kutapeli. Tafadhali iweke wazi kuliko kufumba mafumbo, kama ulivyofanya kwa huyu.
Ungeweka wazi tu kuwa jamaa ana A to Z, inasaidia kuokoa muda, pia watu wasitapeliwe.
Sasa wewe umezunguka sana, mtu kaweka picha zake ndio unaanza kufunguka kidogo si vizuri. Ndio maana baadhi ya wadau hapa walikuona kama hutaki tu asaidiwe.
Jaribu kuwa muwazi kwenye jambo la kujenga km hili.

Nimetumia njia shirikishi ili watu wengi wathibitishe zaidi,isije ikaonekana Kama ninamsingizia huyo dogo.
 
Last edited by a moderator:
Io hoja ya ubunge.nna wasiwasi nayo maana kwa Sasa Ana miaka 23....Je Huo ubunge aligombea akiwa na miaka mingapi???

Hiyo ya ubunge nayo alitaka kutapeli.Huyu ni nguli katika mambo ya utapeli.
 
habari ndg, wanajf

kabla ya yote napenda kumshukuru mungu kwa mema mengi aliyotenda juu yangu sina budi kumwambia ahsante kwa upendo wako kwangu.

Kuzaliwa
nimazaliwa mwaka 1991 katika kijiji cha chamhunda wilayani ukerewe mkoa wa mwanza katika familia ya mzee michael chilato nikiwa mtoto wa mwisho kwa mama yetu kati ya wake watatu wa baba yetu.


Mama yangu alikwisha kutengana na baba yangu tangu mwaka 1996 nikiwa bado mtoto[5] ambapo mzee alioa mke mwingine hivyo nimelelewa na mama wa kambo mpaka kukua kwangu.

Shule

nilianza shule mwaka 2001, nikiwa darasa la tano mjomba wangu alikuja kutusalimia nyumbani na akaniomba niende kwake nikasomee huko, alimweleza baba na hakukataliwa hivyo safari ikapangwa ya kuelekea mkoani shinyanga tayari kwa masomo huku kwa mjomba.

Maisha yaliendelea kama kawaida hatimae mwaka 2007 nilihitimu masomo yangu ya elimu ya msingi, nilirudi nyumbani kusalimia pia nikisubiri matokeo kama nitafanikiwa kuendelea na elimu ya sekondari au laah?
Matokeo yakatoka nilichaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari pandagichiza iliyoko wilaya ya shinyanga [v] niliandaliwa mahitaji ya shule ingawa yooote hayakutimia.

Hivyo nilikuwa nasumbuliwa sana shule nalienda hivyo hivyo mpaka nikamaliza kidato cha 1

hivyo nilirudi nyumbani kwa ajili ya kufuata ada ya mwaka uliofuata pamoja na madeni ya mwaka uliopita kwa kipindi kile wengi wetu hatukuwa tunamiliki simu hivyo mawasiliano na watu wa nyumbani hayakuwepo, hivyo hata nauli alinikopesha mwl ili nitakaporudi nimrudishie, niliondoka na kurudi nyumbani.

Ilipofika januari nilitakiwa kurudi shule lakini jambo la kushangaza na ambalo mpaka leo siamini nikikumbuka, baba yangu alikataa kunisomesha katakata akidai nikamwambie mama yangu anisomeshe maana hata yeye ni mzazi wangu anapaswa kunisomesha, anatamka hayo akitambua fika kuwa mama yangu hana kipato chochote cha kuweza kunisomesha. Hivyo ndoto zangu za kuendelea na shule zikaishia hapo.

Nilipenda na napenda sana kusoma hivyo ikanibidi nitoke nyumbani niende mjini kutafuta kazi, nilibahatika kupata kazi ya bar nilifanya pale kwa mwaka mmoja nikiwa kama counter. Niliacha kazi kuendelea kufuatilia swala langu la shule huko mkoani shinyanga baada ya kupata viela kidogo cha kusikitisha nilipofika shuleni sikuruhusiwa kuendelea na masomo kwa sababu mimi si mwanafunzu tena kwani nimekwisha kufutwa kwa sababu ya kutohudhuria shule kwa miezi mitatu mfululizo bila taarifa yoyote, niliumia sana nimeacha kazi kwenda shule nimefika shule siruhusiwi kusoma.

Niliamua kurudi shule maana sina mtu yoyote wa kunisaidia mjomba wangu nae alikwisha kuhama na kuhamia mkoani tabora

maisha yalibadilika na kuwa magumu sana sina kazi nitaishije bila kazi, nilihamua kutafuta tena kazi nilibahatika kukutana na bw. Mmoja hivi ambae aliniunganisha na jamaa yake arusha ana bar hivyo nikafanye kazi huko, nilipata hivyo nikatakiwa kwenda arusha kutafuta hela tena, nilifanya pia kwa mwaka ka na nusu hivi nikarudi mwanza kutafuta shule ili niweze kuendelea niliende nje ya mji ambako nilidhani ningaliweza hata kuuziwa jina lakini ilishindikana.

Katika pitapita katika mitandao ya kijamii nilikutana na bw. Mmoja hivi ambae tulijenga urafiki na hatimae nilimweleza history ya maisha yangu huyo bw anaka dodoma na anafanya kazi huko ya kufundisha aliniambia njoo huku ninaweza kukusaidia nilifunga safari mpaka dodoma nimkiwa mwenye furaha isiyo na kifani ya kuona malengo yangu yanakenda kutimia narudi darasani tena, ilikuwa ni 2012 juni kwa vile muda ulikuwa umeenda nilianza shule mwaka uliofuata nikiwa kama private candidate [qt] ambayo unasoma miaka miwili kisha unafanya mtihani wakidato cha nne.


Nilifurahi sana nilisoma kwa bidii sana na uchungu mwingi kwa misukosuko niliyokutana nayo, mwezi wa kumi na moja mwaka jana tulifanya necta kwa ajili ya kupata usajili wa kitado cha nne mwaka unaofuata, nilifaulu hivyo nilitakiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu lakini cha kusikitisha na maajabu kwangu huyu mdhamini wangu baada ya kuoa ameniambia ameshindwa kuendelea kunisomesha maana mzigo umekuwa mkubwa nae pia anatakiwa kwenda kusoma hivyo niangalie naman nyingine ya kujisaidia.

Wanajf
mimi ni mdogo wako, mwanao, rafiki yako, jamaa yako n.k nakuombeni msaada wenu wa hali na mali niweze kumaliza elimu yangu hii ya kuungaunga nimalize hta hicho kidato cha nne mpaka sasa toka mwaka jana nifanye mtihani sijarudi shule, nisaidie chochote kile nifanikishe malengo yangu, natanguliza shukrani zangu za dhati kabisa kwenu kwa wale mtakaosoma na kuguswa na jambo hili.


Ahsante mungu

kwa mawasiliano 0769782386 au 0716863406

mungu na awabariki sana

nitumie account number za necta nitakulipia
 
JF dodoma mmeshindwa kuthibitisha au n ukweli kuwa jamaa n tapel?
Ila nmefuatilia nmegundua jamaa n mhitaji halisi, hvo natoa wito tumchangie kwa kupitia shule anayosoma, ki msingi Jf dodoma wangetusaidia kumpata mkuu wa shule ili tuwasilishe michango kwake,
Ushaur kama hutaki kuchangia acha hulazimishwi!
 
Mtoto mdogo anapangilia maneno na kuandika kwa hekma kiasi hiki? ..kweli katoto haka? Si kwweli. Naungana na wanaomtilia shaka!.. hata hivyo mi siwaamini sana watu wanoomba msaada kwa watu wasiowajua...wengi ni matapeli mnaopenda kutapeliwa enndeleeni.

Kumbuka kazaliwa 1991,kuomba msaada amalizie elimu ya O level haimaanishi ni mtoto,najua unajua hesabu so utakuwa ushakalkuleti umri wake
 
ILA mimi nina kinyongo na baadhi ya watu hapa JF mwanzoni nilijua sote ni ndugu ndo mna huwa hata kama mtu una tatizo unakuja hapa unashauriwa na hatimaye unasolve tatizo
HILI JAMBO lililomkuta DOGO na wengine kuanza kuandika yao si mageni na yalinikuta binasfi na nilijuta kama itatokea siku yoyote nikwame sehemu iwe safarini au kibinadamu nije kuelezea hapa eti watasaidia wapo wenye mioyo yao lakini kuna viatu pia.IMAGIN umejielezea sana na upo katikati ya shida unaomba msaada mtu anaanza kukujudge mwandiko kwa nini kwenye r umeweka l utakuwa mwongo wewe.....AISEEEE! This if Jf of now DAYS! FULL OF WONDERS AND HEARTLESS PEOPLE!

kweli dunia ina mambo manake ww unamuamini huyu dogo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom