Aliyeozesha mwanafunzi kwa ng'ombe 15 azitema

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
154
Reaction score
153
MKUU wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Dkt. Vincent Anney ameongoza juhudi zilizofanikiwa kuvunja ndoa ya kimila iliyokuwa imefungwa kati ya Mahene Kulwa na mwanafunzi aliyekuwa amechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka huu, baada ya kubainika kuwa aliolewa kwa mahari ya ng'ombe 15.

Tukio hilo lilitokea Julai 19, 2026 katika Kijiji cha Mwamashindike, Kata ya Budekwa, Wilaya ya Maswa. Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa amechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Nyalanja, Wilaya ya Meatu, na alitarajiwa kuanza masomo mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza leo Julai 23, 2026, Dkt Anney amesema vyombo vya ulinzi na usalama, hususan Jeshi la Polisi, vilifanikiwa kumkamata Mahene Kulwa pamoja na baba mzazi wa binti huyo, Shilinde Ntegwa, dada yake Felister Kulwa na washenga waliodaiwa kushiriki kufanikisha ndoa hiyo.

Akieleza , Mahene amesema kabla ya kufunga ndoa alimuuliza binti huyo kama alikuwa amemaliza shule, na alijibiwa kuwa hana uhakika wa kuendelea na masomo.

"Nilipokutana naye aliniambia amemaliza shule na hana uhakika kama atafaulu na kuendelea na masomo. Nikawashirikisha wazazi wangu, wakakutana na baba wa binti na wakakubaliana mahari ya ng'ombe 15 ndipo tukafanya harusi ya kimila," amesema.

Ameongeza kuwa siku ya harusi binti huyo alikuwa hajisikii vizuri, hivyo dada yake, Felister Kulwa, alivaa mavazi ya harusi na kukaa nafasi ya bibi harusi ili kuficha utambulisho wa mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake, baba wa binti, Shilinde Ntegwa, amekiri kumuozesha mtoto wake kwa madai kuwa hakuwa na nia ya kuendelea na elimu ya Kidato cha Tano.

"Nilimuuliza kuhusu shule, akasema hataki kuendelea na masomo. Lakini kwa sasa ni lazima aende shule," amesema.

Hata hivyo, baada ya kuhojiwa na Dkt Anney mwanafunzi huyo amesema yuko tayari kuendelea na masomo ikiwa atapatiwa nafasi hiyo.

Dkt Anney amesema Serikali itahakikisha mwanafunzi huyo anarudi shuleni ili aendelee kutimiza ndoto zake za elimu.

Aidha, amewataka wazazi wilayani Maswa kuachana na mila na desturi zinazowakatisha wasichana masomo kwa kuwaelimisha kuwa elimu ndiyo msingi wa maendeleo yao na ya taifa.

"Inashangaza kuona walijua ni mwanafunzi, wakaamua kumweka dada yake avae mavazi ya harusi ili watu wasitambue. Nalishukuru Jeshi la Polisi kwa kushiriki operesheni hiyo na kuwakamata wote waliohusika," amesema.

Mwisho.
 
Shehe Mwaipopo alitangaza hadharani ana kikundi cha mauwaji lakini hajakamatwa kwa kosa la ugaidi badala yake ameenda kukamatwa mhadhiri wa UDOM
 
Moja ya kitu mbacho naionaga serikali yetu imefeli ni hapo inakuwaje mutu alazimishwe kenda shule na kata akiendelea anaishia kuwa jobless mtu kashackukua option yake aache akifanye anchoona sahihi kwake au ukisoma ndo ndo unaonekana mtu sana
Acha ujinga mjomba
 
MKUU wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Dkt. Vincent Anney ameongoza juhudi zilizofanikiwa kuvunja ndoa ya kimila iliyokuwa imefungwa kati ya Mahene Kulwa na mwanafunzi aliyekuwa amechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka huu, baada ya kubainika kuwa aliolewa kwa mahari ya ng'ombe 15.

Tukio hilo lilitokea Julai 19, 2026 katika Kijiji cha Mwamashindike, Kata ya Budekwa, Wilaya ya Maswa. Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa amechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Nyalanja, Wilaya ya Meatu, na alitarajiwa kuanza masomo mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza leo Julai 23, 2026, Dkt Anney amesema vyombo vya ulinzi na usalama, hususan Jeshi la Polisi, vilifanikiwa kumkamata Mahene Kulwa pamoja na baba mzazi wa binti huyo, Shilinde Ntegwa, dada yake Felister Kulwa na washenga waliodaiwa kushiriki kufanikisha ndoa hiyo.

Akieleza , Mahene amesema kabla ya kufunga ndoa alimuuliza binti huyo kama alikuwa amemaliza shule, na alijibiwa kuwa hana uhakika wa kuendelea na masomo.

"Nilipokutana naye aliniambia amemaliza shule na hana uhakika kama atafaulu na kuendelea na masomo. Nikawashirikisha wazazi wangu, wakakutana na baba wa binti na wakakubaliana mahari ya ng'ombe 15 ndipo tukafanya harusi ya kimila," amesema.

Ameongeza kuwa siku ya harusi binti huyo alikuwa hajisikii vizuri, hivyo dada yake, Felister Kulwa, alivaa mavazi ya harusi na kukaa nafasi ya bibi harusi ili kuficha utambulisho wa mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake, baba wa binti, Shilinde Ntegwa, amekiri kumuozesha mtoto wake kwa madai kuwa hakuwa na nia ya kuendelea na elimu ya Kidato cha Tano.

"Nilimuuliza kuhusu shule, akasema hataki kuendelea na masomo. Lakini kwa sasa ni lazima aende shule," amesema.

Hata hivyo, baada ya kuhojiwa na Dkt Anney mwanafunzi huyo amesema yuko tayari kuendelea na masomo ikiwa atapatiwa nafasi hiyo.

Dkt Anney amesema Serikali itahakikisha mwanafunzi huyo anarudi shuleni ili aendelee kutimiza ndoto zake za elimu.

Aidha, amewataka wazazi wilayani Maswa kuachana na mila na desturi zinazowakatisha wasichana masomo kwa kuwaelimisha kuwa elimu ndiyo msingi wa maendeleo yao na ya taifa.

"Inashangaza kuona walijua ni mwanafunzi, wakaamua kumweka dada yake avae mavazi ya harusi ili watu wasitambue. Nalishukuru Jeshi la Polisi kwa kushiriki operesheni hiyo na kuwakamata wote waliohusika," amesema.

Mwisho.
Tamaa
 
sijaelewa, wanamkamata muoaji kwa kosa gani? she is 19, kwani umri unaoruhusiwa kisheria kuolewa/kuoa tanzagiza ni kuanzia miaka mingapi? nielewavyo ni 18, kama amevuka 18 siyo mtoto tena na wala hahitaji ruhusa ya mtu kuoa/olewa ....
 
MKUU wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Dkt. Vincent Anney ameongoza juhudi zilizofanikiwa kuvunja ndoa ya kimila iliyokuwa imefungwa kati ya Mahene Kulwa na mwanafunzi aliyekuwa amechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka huu, baada ya kubainika kuwa aliolewa kwa mahari ya ng'ombe 15.

Tukio hilo lilitokea Julai 19, 2026 katika Kijiji cha Mwamashindike, Kata ya Budekwa, Wilaya ya Maswa. Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa amechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Nyalanja, Wilaya ya Meatu, na alitarajiwa kuanza masomo mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza leo Julai 23, 2026, Dkt Anney amesema vyombo vya ulinzi na usalama, hususan Jeshi la Polisi, vilifanikiwa kumkamata Mahene Kulwa pamoja na baba mzazi wa binti huyo, Shilinde Ntegwa, dada yake Felister Kulwa na washenga waliodaiwa kushiriki kufanikisha ndoa hiyo.

Akieleza , Mahene amesema kabla ya kufunga ndoa alimuuliza binti huyo kama alikuwa amemaliza shule, na alijibiwa kuwa hana uhakika wa kuendelea na masomo.

"Nilipokutana naye aliniambia amemaliza shule na hana uhakika kama atafaulu na kuendelea na masomo. Nikawashirikisha wazazi wangu, wakakutana na baba wa binti na wakakubaliana mahari ya ng'ombe 15 ndipo tukafanya harusi ya kimila," amesema.

Ameongeza kuwa siku ya harusi binti huyo alikuwa hajisikii vizuri, hivyo dada yake, Felister Kulwa, alivaa mavazi ya harusi na kukaa nafasi ya bibi harusi ili kuficha utambulisho wa mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake, baba wa binti, Shilinde Ntegwa, amekiri kumuozesha mtoto wake kwa madai kuwa hakuwa na nia ya kuendelea na elimu ya Kidato cha Tano.

"Nilimuuliza kuhusu shule, akasema hataki kuendelea na masomo. Lakini kwa sasa ni lazima aende shule," amesema.

Hata hivyo, baada ya kuhojiwa na Dkt Anney mwanafunzi huyo amesema yuko tayari kuendelea na masomo ikiwa atapatiwa nafasi hiyo.

Dkt Anney amesema Serikali itahakikisha mwanafunzi huyo anarudi shuleni ili aendelee kutimiza ndoto zake za elimu.

Aidha, amewataka wazazi wilayani Maswa kuachana na mila na desturi zinazowakatisha wasichana masomo kwa kuwaelimisha kuwa elimu ndiyo msingi wa maendeleo yao na ya taifa.

"Inashangaza kuona walijua ni mwanafunzi, wakaamua kumweka dada yake avae mavazi ya harusi ili watu wasitambue. Nalishukuru Jeshi la Polisi kwa kushiriki operesheni hiyo na kuwakamata wote waliohusika," amesema.

Mwisho.
Bila kuwafunga hao waoaji na waozeshaji wa kisukuma hawatoacha hiyo tabia
 
Back
Top Bottom