Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 356
- 704
Mwaka 2002 ni mwaka ambao kwa familia hakuwa mwaka mzuri, familia ilipata uzuni ya ghafla kila mmoja aliumia kwa wakati wake
Baba yangu aliumia sana kwa sababu katika watoto wa familia dada yangu alikuwa ni mtoto pekee wa baba yangu na kwa kweli kwa darasani akili zake ziliwashinda kaka zetu wote.
Familia nzima tulikuwa tuna imani juu ya dada yetu kwamba ndiye atakuuwa engineer wa kwanza katika familia
Dada yangu alikuwa anasoma mchepuo wa sanyansi nakumbuka kipindi hicho nilikuwa mdogo lakini nilijua dada yangu alikuwa ni kipanga kweli kweli
Wadada walikuwa hawakatiki nyumbani kwa ajili ya kupata mafundisho kutoka kwa sister, hivyo tulikuwa na imana naye sana ya yeye kuwa msomi wa kwanza wa familia kwenda chuo kikuu
Matokeo ya kumalizs kidato cha sita yalitoka na dada yangu hakufanikiwa kufanya vizuri hivyo kukosa nafasi ya kwenda chuo kikuu.
Kipindi kile ukikosa kwenda chuo kikuu hakuna option na kama familia hakuna uchumi mzuri mtoto anakwenda kusoma diploma ya ualimu na maisha yanaendelea
Baada ya matokeo yale mama yangu akaniambia nisije kusoma sanyasi, wakati anasema mimi nilikuwa kidato cha kwanza hata sijaju nikimaliza shule nitachagua sanaa au sanyasi sikuwaza sana juu ya maneno yake kwa kuwa nilikuwa ni mtoto wa mwisho nilijua alisema na mimi.
Nikiwa kidato cha pili nilianza kuonyesha uwezo katika masomo ya sanyansi binafsi nilikuwa najua ninauwezo katika masomo ya sanyansi hasa hesabu lakini sikujua ni kwa kiwango cha kusoma sanyansi
Siku moja mara baada ya kufanya mtia wa mock wa kidato cha pili katika wilaya , matokeo yalitoka na mara baada ya matokeo kutoka shuleni kwetu tulikuwa na mikondo 4 ya kidato cha pili mimi nilikuwa mkondo A.
Matokeo yalipotoka baadhi ya marafiki zangu wakaanza kunipongeza kwamba mwalimu wangu wa hesabu amenisifia sana katika madarasa yao kiasi watu waka wanataka kunijua huyu ni nani.
Matokeo ya kidato cha pili yalikuwa kama muujiza kwangu , kwa sababu sikuwa mtu ambaye nilikuwa nafahamika katika chochote kuhusu elimu
Matokeo yale somo la hesabu niliongoza sio shuleni tu ni wilaya nzima nilikuwa mtu wa kwanza.
Haikuwa rahisi mimi mwenyewe siku amini matokeo yangu kwa kweli ule mtihani nilipata maswali yote hadi msahishaji akanipunguzia maksi 2 kutokana na kutokuweka desimal 2 katika majibu
Mara baada ya matokeo yale nilianza kuongeza bidii nilijua sasa nitakuwa naangaliwa kwa jicho la tofauti
Kweli bidii yangu ilinisaidie katika somo la hesabu sikuwai kukosa top 3 , maana darasani kulikuwa na vipanga wawili ambao niliweza kuwaotea kwenye mock lakini baadae tukawa tunapishana tu marks 2 au 3.
Kidato cha tatu ndio kidato ambacho nilifanya vizuri sana katika matokeo yale niliweza kuingia top3 katika masomo yote nikiongoza masomo ya hesabu na kemia
Kidato cha nne, niliendelea kuweka bidii katika masomo sana tu , kipindi cha kuchagua masomo kikafika
Nikiwa kidato cha nne nilikuwa karibu sana na kaka yangu maana ndiye aliyekuwa anisupport ata pesa za kwenda tuition vitabu nk
Nilimshirikisha maamuzi yangu ya kusoma sayansi akanikubaria , changamoto ilikuwa kwa bi mkuwa.
Sio kwamba mama hakupenda tusome sayansi hapana ni kwa sababu jinsi dada yangu yalivyomkuta hakutaka namimi nipate kile kilichomkuta dada yangu
Kaka na dada yangu wote walinikubaria kusoma sayansi na mama pia ingawa hakuniamini sana kama nitafanya vizuri ukizingatia historia yangu kielimu haikuwa nzuri kama ya dada yangu.
Uchaguzi wa shule , kuchagua shule ya kusoma A Level nilitamani kusoma shule za bodi maana nimesoma shule za day muda wote, lakini namshukuru kaka yangu alinishauri kwamba muda wangu wa kusoma Alevel ni mfupi sana kama mwaka na nusu hivi, akanishauri kwenda shule za bodi inawezakuwa nzuri ila mazingira unaweza kwenda shule mazingira yakakukataa na mwisho alinishauri shuleni sio kwenda kupata uzoefu wa maisha ni kwenda kutafuta hatiama ya kesho yangu hivyo nichagua vizuri
Namashukuru Mungu niliweza kusoma sayansi katika shule aliyosoma dada yangu kwa kweli nilimwona Mungu katika masomo yangu ya Alevel
Wazazi ni vizuri kutushauri lakini pia tuangalie uwezo wa watoto wetu
Inawezekana mama aliona kusoma masoma ya sanaa ni rahisi lakini sio kwa wote
Ni bora mtoto kusoma kile ambacho anakiweza kuliko kile unachomchagulia
Sio kwamba kumchagulia mtoto masomo ya kusoma ni vibaya ila ni muhimu kuangalia uwezo wake na kumshauri pia.
Wazazi wengi wanatamani watoto kusoma kile alichosomea lakini sio muhimu wote tukasoma kitu kimoja maana Mungu kaweka kitu kwa kila mtu