Hivyo pekee ndivyo vitu vya kudumu ambavyo Wadanganyika watamkumbuka..Duh basi inamaana kumbe mze mkapa hakufanya jambo lolite kwa wananchi wake!
Hivyo pekee ndivyo vitu vya kudumu ambavyo Wadanganyika watamkumbuka..Duh basi inamaana kumbe mze mkapa hakufanya jambo lolite kwa wananchi wake!
Jamani wakuu kuna useme wa wahenga unasema myonge mnyogeni lakini haki yake mpeni,Mh.Rais wa awamu ya tatu amefanya mengi mazuri na ya kuleta tija na maemdeleo kwa wanachi na taifa letu la tanzania kwa ujumla.
Tabia ya sisi viumbe binandamu tunaangalia sana upande mmoja wa maisha ya mwanandamu hasa upande mbaya,na ubaya unaenea haraka kuliko wema hii ndiyo hulka ya wanadamu tangu enzi hizo.
mimi binafsi pamoja na mambo yote yanayoemwa kuhsu rais mstaafu wa awamu ya tatu bado nakubali utendaji kazi wake uliyotukuka kwa maslahi ya nchi yetu changa ya Tanzania
Peru. Nixon asingepata pardon na kujiuzulu alikuwa anaelekea lupango. At least huko rule of law reigns.Niambie nchi iliyowahi kumfunga rais wake wa zamani, wote wamejaribu kuwapeleka mahakamani na hamna hata aliewahi kutolewa hukum...in short though law inasema no one is above the law, hawa watu wapo na kinga kubwa...hata wakipelekwa kesi zao haziishi, au ataishia kuchukua assylum.
tukimfungulia tunamfungulia kwa kosa gani na katika sheria ipi?, je makosa hayo yapo katika criminal law ya Tanzania.
Semenya,
Upo dunia gani mkuu
Yaani huyajui makosa ya Mkapa yanayostahili kumfungulia mashtaka? Kwani kuna makosa ambayo hayapo katika criminal law ya Tanzania!?
Mkapa amefanya mema mengi kuliko haya mabaya yanayobeba vichwa vya habari kila leo.Mi cyo mwana ccm ila huyu jamaa hata akigombea kesho nitampa kura yangu hakuna mwingine ndani ccm ninayeweza kumpigia kura yangu.

Baadhi ya Watanzania ndivyo walivyo!!! Unakumbuka kauli ya "Hata majani tutakula lakini rada lazima inunuliwe" habari yote kuja kuanikwa hadharani kumbe ile rada thamani yake ilikuwa ni $28 millioni tu $12 miilioni fedha za walipa kodi mafisadi wameingia nazo mitini. Huyo huyo Vithalani ndiye aliyekuwa wakala wa ununuzi wa ndege ya Rais na helicopters za jeshi hapo lazima kutakuwa na ufisadi ambao hatujaujua lakini iko siku tutakuja kuufahamu.
Siku za mwisho za Mkapa ndiyo papa fisadi Rostam alichota $40 miilioni si ajabu hapa pia Mkapa alihusika kwa namna moja au nyingine. Kakopa shilingi bilioni 7 toka NSSF na hadi hii leo hajarudisha hata senti tano. Huyu alikuwa anazimezea mate nyumba fulani za Serikali akaja na mpango wake wa kuzitapeli nyumba za Serikali kwa kuziuza kwa mawaziri na makatibu wakuu kwa bei poa kabisa. Kufuatilia hili Serikali imeingia hasara ya $200 millioni kwa kuwaweka maofisa wake mahotelini kwa ukosefu wa nyumba. Huyu huyu Mkapa ndiye aliyesaini mikataba ya uchimbaji madini ambayo Tanzania tunapata 3% tu huku wageni wakichukua 97% Wabunge walipokuja juu kama sikosei 2003 au 2004 kutaka kuiona mikataba ile ya madini akawafuata Dodoma na sijui kama aliwatisha au aliwaambia nini maana baada ya kikao kile kelele za Wabunge wa CCM kutaka kuiona mikataba ile na kuijadili Bungeni zikapotea kabisa.
Aliiba Kiwira na kututukana Watanzania kwamba tuna wivu wa kike tukimuona mtu ana vijisenti vyake tu basi tunadhani ni mwizi (kumbe mara nyingi huwa hatukosei). Pamoja na kumlipa mshahara na marupurupu makubwa, hakutosheka akaamua kufanya biashara akiwa Ikulu hadi hii leo hataki kusema alikuwa anafanya biashara gani na alifanya nani. Yote haya huyaoni kama ni kasoro kubwa kwa kiongozi wa nchi ambaye ameaminiwa na Wananchi wake na kumpa madaraka ya kuwaongoza eti unadai akigombea tena utampa KULA (kura) YAKO!!! Kweli Watanzania ndivyo walivyo!!! Wacha nchi yetu igeuzwe kichwa cha mwendawazimu miaka nenda miaka rudi!
Mkuu lazima tukubali kuwa hakuna aliyemtumilifu kwa 100% kuna mambo ambayo nakubaliana na wewe na yapo ambayo nitapingana na wewe na kumuona Mkapa ni kiongozi kwangu mimi binfsi.
Suala la madini ni kweli na ndo kwanza tulikuwa tunaingia kwenye hii biashara lakini mbona hata waliokuja mbele yake wamesaini mikataba fake? Mfano mzuri ni Karamagi au haya unayasahau? Wao baada ya kuona mapungufu ilibidi warekebishe na si kuturudisha nyuma tena.
Na kuna mengine kama Rada, ndege na mgodi ni tamaa tu za waliokuwa nyuma yake kutaka kujilimbikizia mali kwa fedha za walipa kodi cyo kwamba Mkapa ndo aliyepanga na kumaliza haya mambo huenda na yeye kuna mengine alipotoshwa na hawa walafi wachache.
Kafanya mengi mazuri kama kuiweka nchi angalau vizuri kidogo kiuchumi ikiwa ni pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei n.k kajenga sana barabara achilia mbali uwanja wa burudani...

Mvina
Ukimlinganisha Mkapa na mwungwana wa sasa, Mkapa hakamatiki. Lakini kwa vipimo vya kizalendo alivyoviacha Baba wa Taifa, basi Mkapa si lolote kama asemavyo Bubu.
Ubora wa uongozi ni relative. Kwa hali hiyo tusimlinganishe Mkapa na viongozi wachovu kama JK.