Makonda azuru kaburi la Benjamin Mkapa

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda amezuru kaburi la Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamin William Mkapa Kijijini kwao Lupaso Mkoani Mtwara.

Mwenezi Makonda aliyesitisha ziara yake Mkoa wa Ruvuma na Mtwara kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ameshiriki pia kwenye sala maalum ya kumuombea kheri na pumziko jema Mkapa.

Akiongea na Wanafamilia wa Mkapa, Mwenezi Makonda amesisitiza kuhusu uadilifu, mapenzi mema kwa Nchi yake na uchapakazi wa Hayati Mkapa kama miongoni mwa tunu muhimu alizokuwa nazo.

Credit - AyoTv
 
Back
Top Bottom