Sasa huu ndio uongo ulizidi kifani maanake sijui kama ndugu yangu Nsesi ulikuwa mjenzi..Kufikia kusema ati 2005 mabati yalikuwa bei hiyo. Hivi unaweza kunambia ongezeko la gharama ya Ujenzi kwa mwananchi wakati wa Mkapa hadi JK ukilinganisha na ule wa Mwinyi kuingia Mkapa. Kumbuka tu Mwinyi aliondoka Dollar 1 ikiwa Tsh 500, nailifkia Tsh 1000 within 6 years, na aliondoka tayari tumegonga 1100. Sasa nambie mwananchi mkulima ambaye mazao yake yameshuka bei atalipa kiasi gani cha Tsh kwa mali ile ile aliyokuwa akinunua wakati wa Mwinyi.Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, pamoja na kuibuliwa kwa uchafu wakati wa utawala wake ukweli unabaki pale pale mengi mazuri.
Wakati anaondoka madarakani bundle moja ya bati tulinunua 87,000/= lakini ilipofioka January 2008 ilishafika 280,000/=, nauli za daladala zilisimama kwa miaka yake yote ya utawala katika 100/=; haya ndiyo mambo sisi watu wa kawaida tunayoyaangalia;
Wakati wa Mkapa tulikuwa tuki budget, leo hii haiwezekani, tumebaki kuishi kwa matumaini tu.
Sio sahihi kabisa kumbeza mzee huyu kwamba hajafanya kitu, hapana amefanya makubwa kuliko hayo mabaya.
Kwanza mikataba ya madini ilianzia kwake, tuwe wakweli, IPTL nani alikuwa waziri wa madini na nishati na nani alikuwa rais!!!!
Mwacheni mzee wa watu apumzike.
Wakati wa Mkapa tulikuwa tuki budget kitu gani? maanake nakumbuka hadi anaondoka serikali inadaiwa fedha za walimu na wafanyakazi kibao wa halmashauri za wilaya na mikoa. hautuna shule Zahanati, maji, Umeme, Usafiri reli ya kati mwisho Dodoma..ATC chini ya SA imekwisha, Tanesco hoi bin taaban karibu kabisa kutaifishwa. Bandarini ndio hapasemeki Mombasa took over, tunapigwa VAT za asilimia za ajabu, exemption kwa matajiri na vigogo yaani hata haisemeki. hata uwekezaji ktk hisa ulikuwa ktk sigara na bia tu.. hakuna hata kitu kimoja kilichokuwa kikipanda ktk soko letu zaidi ya dhahabu ambayo hatukuwa na hisa hata moja. Kazi kubwa alikuwa nayo JK ni kujaribu hata kurekebisha moja na ameshindwa hivyo utawala wake wote umeonekana bure kwa sababu ya Mkapa.
Mradi wa IPTL ulianzishwa wakati wa Mwinyi lakini mkataba ulipita wakati wa Mkapa. soma report inayohusu IPTL utaelewa kilichofanyika.