Mkapa: Yote yanayosemwa juu yangu namuachia Mungu

Ishu sio kusamehewa ishu ni kuwa haki iko wapi tukishamsamehe mabilioni ya EPA yatapatikanaje?, Import support, mashirika ya umma yaliyouzwa kama njugu?, na mengineyo mengi
 
Kapwani,

Nini maana ya Demokrasia kama hatutaweza kuleta mabadiliko kwa kutumia Ballot boxes? Nchi zote nilizotolea mfano hapo juu zinatumia hayo masanduku ya Kura na zimeweza kuleta mabadiliko tunayoyaona leo.

Je, mnataka tulete mabadiliko kwa njia gani mnayoona nyie ni muafaka? Mnataka watu waende msituni wapindue nchi? Au mnataka kichaa mmoja wa JWTZ akachukue Ikulu kwa nguvu??? Ndichoi mnachotaka kweli??

Tatizo la Wa-tz hamtaki kutumia demokrasia kujiandikisha na kupiga kura ili mchague chama au mtu mnayeona anafaa!!Mfano halisi ni ichaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Oktoba. Matokeo yake CCM wamejiandikisha na ndo waliochukua uongozi!!!

Kazi yetu ni kulalamika tu kwenye vijiwe vya gahawa.Lakini inapofikia mahali kuwa watu walete mabadiliko kwa kutumia haki yao ya kikatiba unakuta wanaingia mitini. Katika nchi hii ni sehemu chache sana zenye mwamko wa kuleta mabadiliko.Sehemu kama Karatu kwa kina Wilbroad Slaa, Kigoma, Tarime na maeneo mengine yanayoongozwa na vyama vya siasa mbali ya CCM.

Ni sanduku la kura peke yake na si mtutu wa bunduki!Hiyo ndiyo njia pekee ya kuleta mabadiliko kwa Watanzania. Nje ya hapo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.
 
atoke hapa! Angefanya kazi yake mambo mengine wala yasingefika hapa. Anataka tumsifie kwa uwanja wa mpira?

Pamoja na hayo 'mambo mengine' Mkapa ni KIONGOZI, kuliko huyu tuliyenaye sasa.

Nadhani TZ tuna tatizo kubwa la kuandaa na kupata viongozi bora; ninahofu zaidi kuhusu kiongozi ajaye baada ya JK, tutamwona JK ni bora zaidi kuliko atayemrithi.

Mungu atausaidie
 
Its pity kati ya yote mema aliyo yafanya Mkapa watu wameona uwanja mpya wa taifa tu!

Huu ni upofu usio yumkinika lakini si shangai hilo kwani hao wanaodai hayo wapo Detroit kwenye comfort zone zao.

Wataonaje barabara za viwango vya lami, vituo vya afya, maboresho ya maslahi serikalini (zamani watu walikimbia kufanya kazi serikalini siku hizi kila mtu anataka) maboresho ya vitendea kazi serikalini magari, samani nk. Miradi mikubwa ya kama daraja la Mkapa, mradi wa maji kutoka ziwa Victoria Shinyanga, uchumi kuimarika. Inflation to go down to single digit, mipango ya MMES, TASAF, MKUKUTA, MKURABITA nk if you know them.

Na mengine kadhaa wa kadhaa lakini ma pundit wa JF wameona uwanja wa taifa tu loo shame on you! Mkapa atabaki kuwa miongoni if not onlgoingy the best President taifa letu limepata kuwa nae.

Masatu

Faida zilizotokana na daraja la Mkapa,mradi wa Maji Ziwa Victoria kule Shinyanga,MMES,TASAF,MKUKUTA,MKURABITA n.k is just 0.0000001%ukilinganisha na hasara ambayo Mkapa ameisababishia nchi hii.

Hebu nipe faida za MMES wa kwetu. Kwangu mimi sioni faida yeyote baali hasara tupu.MMES inashughulika na shule za Sekondari. Kila mtu anajuwa kuwa Shule za Sekondari hazina waalimu,hazina nyumba za waalimu, hazina madawati,hazina vitabu vya kiada, mishahara ni mibovu kila siku waalimu wanatishia kugoma!!!

TASAF ni mradi wa mama Anna Mkapa hauna tija yeyote.
MKUKUTA na MKURABITA ni maneno ya kisanii ya kuwachanganya Wadanganyika tu wala hayana any positive results. Ati sijui Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania! Uchumi upi umekuzwa na Umasikini upi uliopunguzwa??? Just show me anywhere in Tz kama kuna kitu kama hicho???Hizo zilikuwa propaganda za Mkapa za kufanyia ufisadi.

Njoo kwenye MKURABITA(Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania). Rasilimali zipi na wanyonge wapi wanazungumziwa kwenye mpango huu fake? Kama Rasilimali zote za Taifa yakiwemo madini umewapa Wageni au Wawekezaji kama wanavyoitwa na huyu Mwananchi ndo anakuwa kibarua kwa hawa Wageni, Do you think that your MKURABITA will work???Never on earth, hakuna kitu kama hicho.

Remember hivi karibuni balozi wa South Africa aliyekuwa anamaliza muda wake alizungumza kitu ambacho ni challenge kwa Mkapa,Kiwete na CCM yao. Kwamba Afrika Kusini wanachofanya ni opposite ya kile CCM wanafanya. SA wanachofanya ni kuwa-empower au kuwawezesha wazawa kwanza ili waweze kumiliki Rasilimali za Taifa kabla ya kumfikilia mgeni.

Mkapa ndiye alikuwa kinara wa sera hizi potofu. Alifika mahali akawatukana Watanzania kuwa sisi ni WAVIVU WA KUFIKIRI WALA HATUKOPESHEKI! Nenda Barclays Bank ukaombe mkopo kama utapewa ki ulaini kama atakavyopewa Mwekezaji.Sasa hivi nchi imejaa wawekezaji uchwara kila kona wengine wanauza mpaka karanga,mapazia,vifaa fake vya electronics n.k sijui wazawa mtafanya biashara gani!

Masatu mimi siko Ulaya wala Marekani niko hapa hapa Bongo kwa hiyo huwezi kuni-fool kwa namna yoyote I know each and everything happening in this Bongo land.
 
Kwani dogo hilo?

Ni kubwa kiasi chake lakini usisahau amefanya machache mazuri na mengi mabaya, Sidhani kama kuna Rais ambaye amejinyakulia utajiri mkubwa kwa njia zisizo halali kama yeye. Nchi kaiuza mpaka kamaliza kila kitu, mikataba mibovu yote kaingia yeye, halafu unatetea eti dogo hilo? Nyie ndio wanafiki wenyewe. Asimame na kipaza sauti atuombe radhi watanzania kwa kuiuza nchi yetu ndio amgeukie Mungu. Hana lolote nafikiri dhamira yake inamsuta. Hivi ndo tunavyoviita viini macho.
 
Inatia moyo sana kuona kwamba kuna Watanzania kama wewe ambao siku zote huuweka ukweli mbele badala ya kutaka kusifia vile ambavyo havistahili kusifia hata siku moja. Ahsante sana.
 
Masatu mimi siko Ulaya wala Marekani niko hapa hapa Bongo kwa hiyo huwezi kuni-fool kwa namna yoyote I know each and everything happening in this Bongo land.

Ndiyo zao hizo Makoye2009, wakishaona unawashinda hoja basi watakwambia una chuki binafsi na Mkapa, alikunyima cheo na blah blah blah nyingine chungu nzima badala ya kukwambia una mapenzi ya kweli na nchi yetu au watakwambia uko nje ya nchi hujui chochote kinachoendelea Tanzania pamoja na kuwa kuna mtandao, simu na watu wana ndugu wa karibu, jamaa na marafiki ambao wanazungumza nao ili kujua nini kinachojiri Tanzania. Na wakati mwingine Watanzania walio nje wanaweza kuwa wanayajua mengi kuliko wale walio nchini.

Huyu Mkapa aliyekuwa mjuaji kusema sana alipokuwa madarakani, leo hii kaamua kuwa bubu hataki kabisa kuzungumzia madudu mbali mbali yaliyofanywa na yeye na yale yalitokea akiwa madarakani. Aliyoyafanya alidhani yatabaki kuwa siri sasa yameanikwa hadharani anakimbia kivuli chake.

Angekuwa msafi basi angekuwa wa kwanza kuomba iundwe tume ya kuchunguza madudu yake mbali mbali ikiwemo kufanya biashara akiwa Ikulu, ununuzi wa rada, ndege ya Rais ambayo leo hii iko juu ya mawe pale DIA, helicopters na magari ya jeshi ambapo wakala alikuwa ni yule yule Vithalani aliyejipatia $12 milioni na kugawana na mafisadi mbali mbali ndani ya Serikali.
 
Tusimshirikishe Mungu kwa vitu vya ajabu, binadamu ni binadamu na Mungu kama alivyosema tumwache aitwe Mungu, Mkapa? Mhh..!!!
 
Ni mungu yupi huyo anayemuachia, huyu wa Israel au wa Nangulukulu!
 
Ni kubwa kiasi chake lakini usisahau amefanya machache mazuri na mengi mabaya, Sidhani kama kuna Rais ambaye amejinyakulia utajiri mkubwa kwa njia zisizo halali kama yeye. Nchi kaiuza mpaka kamaliza kila kitu, mikataba mibovu yote kaingia yeye, halafu unatetea eti dogo hilo? Nyie ndio wanafiki wenyewe. Asimame na kipaza sauti atuombe radhi watanzania kwa kuiuza nchi yetu ndio amgeukie Mungu. Hana lolote nafikiri dhamira yake inamsuta. Hivi ndo tunavyoviita viini macho.
Unajua maana ya unafiki ama unapayuka tu?
 
- One of this days wananchi wa taifa hili tutakuja kugundua exactly what was nafasi ya Mkapa, katika historia ya taifa hili kiuongozi na hasa maadili. Mwalimu was a leader ingawa alikuwa na mapungufu kwenye technicalities za what to do na uchumi, pamoja na sheria lakini bado he was a greatest leader kwa maana ya kwamba aliweza kuishi kwa kufuata maneno yake mwenyewe mbele ya wananchi wake, matendo yake hayakutofautiana hata kwa an inch na tabia zake na hasa maisha yake binafsi kama rais na binadam, hiyo ni skill muhimu sana kwa kiongozi wa watu wowote wale, iwe dini au siasa.

- Baada ya kugundua makosa yake katika uchaguzi wa Mwinyi, Mwalimu aliamua kufanya marekebisho kwa kutegemea Mkapa, angelirudisha taifa kwenye maadili yake aliyoyaweka akiwa kiongozi, Mwalimu alijua kwamba technically kuna ambayo hayawezekaniki kwa mfano ya uchumi, lakini aliamini kwamba with nidhamu ya uongozi mengine yote yatakuwa contained na kueleweka na wanachi, kwa sababu pamoja na hali mbaya ya uchumi wa dunia bado viongozi wanaoongoza wakiweza kuishi maisha yanayokaribiana na wananchi, wananchi hawatakuwa kinyongo nao, wataelewa kama tulivyokuwa tukielewa under Mwalimu, kwamba sawa hali ni mbaya duniani na maisha yetu wananchi na ya viongozi hayapitani sana kwa hiyo we are in a good shape as a nation.

- Lakini the minute alipoingia tu huyu Mkapa akaanza taratibu kum-betray Mwalimu, na hatimaye sisi wananchi wote wa hili taifa, kwa mara ya kwanza tukaaanza kujionea masikini wamejaa mabara barani hasa kwenye traffic lights, unafikiri kwa nini wale masikini wanafanya vile ni kwa sababu wanajua kuwa wenye njaaa ni wao tu sio wananchi wote, na ndio maana walianzia pale Salender Bridge, maana walijua pale ndio mahali pa kuwaomba hela viongozi wetu wanapokuwa njiani kwenda kazini ni lazima wapitie pale ndio ikasambaa kila kona sasa ya jiji.

- Uongozi bora ni pamoja na wewe unayeongoza kua kioo kwa unaowaongoza, Mkapa amepoteza a very important opportunity ya kulirudisha hili taifa kwenye nidhamu ya uongozi, kama huamini tizama uongozi aliotuachia, huu utamsuta mpaka anaingia kaburini hata aseme nini kujaribu kujitakasa huu uongozi wa sasa ni yeye aliyetuletea, tatizo letu Tanzania sio anything ila ni viongozi wabovu tu! na Mkapa bares 100% responsibility for it! na hasa this national misery we are in sasa hivi!

Respect.

FMEs!
 
-
Uongozi bora ni pamoja na wewe unayeongoza kua kioo kwa unaowaongoza, Mkapa amepoteza a very important opportunity ya kulirudisha hili taifa kwenye nidhamu ya uongozi, kama huamini tizama uongozi aliotuachia, huu utamsuta mpaka anaingia kaburini hata aseme nini kujaribu kujitakasa huu uongozi wa sasa ni yeye aliyetuletea, tatizo letu Tanzania sio anything ila ni viongozi wabovu tu! na Mkapa bares 100% responsibility for it! na hasa this national misery we are in sasa hivi!

Respect.

FMEs!
Hapa Mkapa anahusika vipi? weka sawa....
 
- One of this days wananchi wa taifa hili tutakuja kugundua exactly what was nafasi ya Mkapa, katika historia ya taifa hili kiuongozi na hasa maadili. Mwalimu was a leader ingawa alikuwa na mapungufu kwenye technicalities za what to do na uchumi, pamoja na sheria lakini bado he was a greatest leader kwa maana ya kwamba aliweza kuishi kwa kufuata maneno yake mwenyewe mbele ya wananchi wake, matendo yake hayakutofautiana hata kwa an inch na tabia zake na hasa maisha yake binafsi kama rais na binadam, hiyo ni skill muhimu sana kwa kiongozi wa watu wowote wale, iwe dini au siasa.

- Baada ya kugundua makosa yake katika uchaguzi wa Mwinyi, Mwalimu aliamua kufanya marekebisho kwa kutegemea Mkapa, angelirudisha taifa kwenye maadili yake aliyoyaweka akiwa kiongozi, Mwalimu alijua kwamba technically kuna ambayo hayawezekaniki kwa mfano ya uchumi, lakini aliamini kwamba with nidhamu ya uongozi mengine yote yatakuwa contained na kueleweka na wanachi, kwa sababu pamoja na hali mbaya ya uchumi wa dunia bado viongozi wanaoongoza wakiweza kuishi maisha yanayokaribiana na wananchi, wananchi hawatakuwa kinyongo nao, wataelewa kama tulivyokuwa tukielewa under Mwalimu, kwamba sawa hali ni mbaya duniani na maisha yetu wananchi na ya viongozi hayapitani sana kwa hiyo we are in a good shape as a nation.

- Lakini the minute alipoingia tu huyu Mkapa akaanza taratibu kum-betray Mwalimu, na hatimaye sisi wananchi wote wa hili taifa, kwa mara ya kwanza tukaaanza kujionea masikini wamejaa mabara barani hasa kwenye traffic lights, unafikiri kwa nini wale masikini wanafanya vile ni kwa sababu wanajua kuwa wenye njaaa ni wao tu sio wananchi wote, na ndio maana walianzia pale Salender Bridge, maana walijua pale ndio mahali pa kuwaomba hela viongozi wetu wanapokuwa njiani kwenda kazini ni lazima wapitie pale ndio ikasambaa kila kona sasa ya jiji.

- Uongozi bora ni pamoja na wewe unayeongoza kua kioo kwa unaowaongoza, Mkapa amepoteza a very important opportunity ya kulirudisha hili taifa kwenye nidhamu ya uongozi, kama huamini tizama uongozi aliotuachia, huu utamsuta mpaka anaingia kaburini hata aseme nini kujaribu kujitakasa huu uongozi wa sasa ni yeye aliyetuletea, tatizo letu Tanzania sio anything ila ni viongozi wabovu tu! na Mkapa bares 100% responsibility for it! na hasa this national misery we are in sasa hivi!

Respect.

FMEs!

Ahsante sana Mkuu kwa maneno yaliyojaa hekima na busara chungu nzima. Siku zote nitakuheshimu sana kwa kutoficha ukweli kwamba wewe ni mwanachama wa CCM lakini michango yako hapa jukwaani siku zote huweka mbele maslahi ya nchi yetu badala ya yale ya chama au Viongozi mufilisi ambao matendo yao na mahubiri yao hayaendani kabisa. Ni miongoni mwa wanaJF ambao nawaheshimu sana hapa jukwaani pamoja na kuwa siku zote hatuwezi kukubaliana kila kitu.

Mkapa hakumuachia Mungu pale alipotutukana Watanzania eti tuna wivu wa kike tunapomuona mtu ana mali na uchache wake, lakini inapokuja kwenye madudu yake hataki kuongelea kabisa nini kilichojiri hadi akaweza kupata utajiri mkubwa katika miaka 10 aliyokuwa madarakani au kwanini halipi mkopo wa shilingi bilioni 7 aliochukua toka NSSF na madudu yake chungu nzima na alihusika vipi na madudu hayo kama vile ununuzi wa rada n.k.

Kama kweli anataka heshima toka kwa Watanzania walio wengi basi auanike hadharani ukweli wote au awe mstari wa mbele kuomba iundwe tume ichunguze madudu mbali mbali yaliyofanywa na yeye kama kiongozi na yale yaliyojiri alipokuwa madarakani ambayo mpaka hii leo bado yanapigiwa kelele na Watanzania walio wengi. Vinginevyo ataendelea kuonekana ni fisadi aliyejaa uroho wa utajiri wa haraka haraka na aliyetumia cheo chake kujitajirisha yeye, familia yake, ndugu, jamaa na marafiki.
 
Mkitupa sisi CUF ridhaa ya kuongoza Mkapa ni mfungwa mtarajiwa.

Mchagueni Lipumba ,then mtaona kazi yake .
 
Ndugu Mkapa:

Njoo kwetu uibe kuku tu na baadaye uone kama utapewa nafasi ya kumwachia Mungu.
 
*ASEMA HAWEZI KUZUIA WATU KUSIKIA, LAKINI ANAWEZA KUZUIA MDOMO WAKE

Nora Damian na Exuper Kachenje

RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa amesema kuwa hana wasiwasi kuwa anazo sifa za uongozi na ndizo zilimfanya afanikiwe katika kipindi cha miaka 10 ya utawala wake.

Mkapa alitoa kauli hiyo jana alipozungumza katika mkutano wa pili wa wadau wa taasisi yake ya mapambano ya Ukimwi, Benjamin Mkapa HIV/AIDS, Foundation, ikiwa siku moja tangu aliposema tuhuma zote zinazomkabili anamshukuru Mungu.

"Yote nayapokea na kumshukuru Mungu," Mkapa alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari alipozungumza wakati akimkaribisha makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein kufungua mkutano huo juzi katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mkapa alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali kutoka kwa mmoja wa washiriki wa mkutano huo, Nicholas Kingazi ambaye ni Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ya Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana aliyemuuliza rais huyo mstaafu wa awamu ya tatu iwapo anazo sifa za uongozi.

Kingazi aliuliza " ..Umezungumzia sifa tisa za uongozi, je katika miaka kumi ya uongozi wako sifa hizi unazo?."

Katika jibu lake Mkapa alisema, "..Naogopa kuongea bila kuweka rekodi, lakini juu ya suala hilo sina shaka kwamba ninazo na ndiyo maana uongozi wangu ulikuwa wa mafanikio."

Aliongeza: " Huwezi kufanya usichokijua, lazima ujue wapi pa kuanzia, nini ufanye leo, nini usifanye, kipi kipaumbele na nini kisubiri. Ukiwa na hayo unaweza kuonyesha unazo sifa za uongozi."

Baada ya kutoa majibu hayo umati wa wajumbe uliokuwepo ukumbini ulimshangilia Mkapa kwa kumpigia makofi.

Awali katika hotuba yake Mkapa alitaja sifa tisa za kiongozi bora akimnukuu mwandishi maarufu wa vitabu wa Marekani Lee Iacoca katika kitabu chake kiitwacho (Where have all leaders gone), Viongozi wamekwenda wapi?.

Akinukuu kitabu hicho Mkapa alisema," Maisha juhudi za pamoja, hakuna anayefika mbali akiwa peke yake. Nimepata baraka kutoka kundi maalumu, kubwa na teule la watu walioniunga mkono, kunitia moyo na kunikosoa. Hayo ni mambo muhimu kwa kiongozi kufanikiwa. Tambua kundi hilo na uwe nalo."

Aidha Mkapa alisema kuwa hawezi kuzuia masikio ya watu kusikia, lakini anaweza kuzuia mdomo wake kuzungumza.

"Kuna msemo wa kiafrika unaosema, huwezi kuzuia masikio yako kusikia bali kuuzuia mdomo wako kuzungumza. Ndiyo siwezi kuzuia masikio yenu kusikia, lakini naweza kuziba mdomo wangu nisizungumze."

Baadhi ya sifa hizo tisa alizozitaja Mkapa ni pamoja na uwezo wa kuwasiliana, nguvu na uwezo wa kutanzua mema na mabaya, ujasiri, ushawishi kwa unaowaongoza.

Alisema sifa hizo anastahili kuwa nazo kiongozi yeyote hata kiongozi wa sekta ya afya kama taasisi yake ya Benjamin Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF) ili kuliletea taifa maendeleo pamoja na kuwashirikisha anaowaongoza.

"Kiongozi lazima aweze kujua nini kifanyike leo, nini kisifanyike, kipi kipaumbele na nini kisubiri. Huwezi kufanya kitu usichojua 'prioritise'," alisema Mkapa.

Alisema kwa kufanya hivyo kiongozi ataweza kuwa na nguvu ya kuamua, kujenga imani na heshima, kujitolea na ushirikiano miongoni mwa viongozi, wafanyakazi, wafadhili, marafiki na jamii kwa jumla.

Aliongeza kuwa kiongozi huyo lazima pia aweze kujenga mahusiano mema ya kijamii pamoja na watendaji wengine na kutambua na kuuthamini mchango wa wengine.

Akizungumzia swali lake kwa rais mstaafu, Kingazi alisema kuwa aliuliza ili kujua iwapo kipindi cha uongozi wa awamu ya tatu yeye Mkapa na viongozi wengine wakiwemo mawaziri,wakuu wa mikoa na wa wilaya walikuwa na sifa hizo zilizotajwa.

"..Nafasi ya kujipima anayo, Mkapa hana sifa hizo zote, ila amejitahidi. Kwa mtazamo wangu si rahisi kuwa nazo sifa hizo zote, anaweza kuwa nazo tano kati ya tisa alizotaja," alisema Kingazi na kuongeza:

"Mimi pia ni kiongozi na sifikishi sifa hizo, huwezi kuzifikia bila ya 'support' (Kusaidiwa) na unaowaongoza."

Akizungumzia taasisi yake Mkapa alisema mafanikio ya BMAF yasingekuwepo bila ushirikiano wa serikali ambapo alimshukuru Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dk Ali Mohamed Shein na serikali kwa jumla kwa ushirikiano na taasisi hiyo.

Kuhusu afya Mkapa alisema sekta hiyo ni moja ya sekta kipaumbele za taifa pamoja na elimu na miundombinu huku akisema serikali imekuwa ikitenga asilimia 11 ya bajeti yake kila mwaka kwa miaka mitatu iliyopita ikiwa na lengo la kufikia azimio la Abuja lililoagiza sekta hiyo itengewe asilimia 15 ya bajeti kwa nchi za Afrika.

Kuhusu uchumi Mkapa alisema Tanzania imekumbana na msukosuko wa uchumi kama ilivyo kwa nchi nyingine hali iliyofanya uchumi kudorora hasa kuporomoka kwa sekta ya utalii na kupungua misaada ya wahisani.

Alisema kama nchi nyingine zinazoendelea Tanzania imekumbana na matatizo ya kifedha, rasilimali watu, ufundi na vifaa mbalimbali ambavyo ni muhimu kwa maendeleo.

Mkapa alisema pamoja na hali hiyo uchumi wa Tanzania umekua kwa asilimia 7.4 katika mwaka 2008 ikilinganishwa na mwaka 2007 ambapo aliongeza kuwa ongezeko la asilimia tano linatarajiwa kwa mwaka 2009 huku ikitarajiwa kuwa mwaka 2012 utakua kwa asilimia 7.5.
 
Mkapa amefanya mema mengi kuliko haya mabaya yanayobeba vichwa vya habari kila leo.Mi cyo mwana ccm ila huyu jamaa hata akigombea kesho nitampa kura yangu hakuna mwingine ndani ccm ninayeweza kumpigia kura yangu.
Mvina,
Unafahamu kuwa RAISI wa Nchi yoyote ile ni MWAJIRIWA? na Mwajiriwa akimuibia Muajiri wake nini kinatokeaa? Ni kupoteza Kazi na kwenda Mahakamani. Hata kama wizi huo utagundulika baada ya kustaafu, madhali ushahidi upo Mwajiri ana HAKI ya kufungua KESI. MUNGU hahusiki kabisa na Biashara hiyo. Kwanza Mungu alishatoa Amri zake kuna moja inasema USIIBE na nyingine inasema USIUE na Mkapa ameshavunja zote Hizo. je Adhabu za Mungu Alizoyakinisha zitolewe kwa makosa hayo hapa Duniani MKAPA anazijua?? Au anajipeleka kwa Mungu kirahisi akidhani Mungu hamuoni au hajui aliyoyafanya?? (Amuone kwanza Mchungaji wa Kanisa lake apate ushauri) Kwa kifupi tulimwajiri Mkapa, tukamlipa Vizuri tu, Tukampa marupurupu kibao, USAFRI, KULALA, KULA, KUNYWA, KUNYA yeya na Familia yake BUREEEEEE! Na Walinzi tukamuwekea na Ahadi ya kumlipa kwa kipindi cha maisha yake kilichobakia. Yote hayo ni kwa ahadi na KIAPO kuwa ataenda mema kwa MUJIBU wa kazi yake ilivyotakiwawa.Mkapa hawadai WATANZANIA hajalalamika hata siku moja kuwa kati ya miaka kumi aliyokuwa RAIS kuna mwezi hakupata MSHAHARA wake, hivyo akajifidia kwa kutuibia na kutuuzia mali zetu OVYO tu. Kwa mema yawe mengi au machache kiasi gani Tulishalipana nae. Na MABAYA yawe mengi au machahe kiasi gani TUNAMDAI ni juu yetu ni WAJIBU wetu KUULIZA, KUKEMEA, KUPIGA MAYOWE, kama wanavyodai wengine MPAKA KIJULIKANE.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom