Mkapa: Yote yanayosemwa juu yangu namuachia Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa: Yote yanayosemwa juu yangu namuachia Mungu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Nov 19, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

  Rais mstaafu Benjamin Mkapa, amesema yote yanayosemwa juu yake, anamwachia Mungu.

  Alitoa kauli hiyo jana jioni, kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa taasisi yake jijini Dar es Salaam.

  Kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, kufungua mkutano wa siku mbili wa Mkapa Foundation, taasisi inayojihusisha na Ukimwi, Mkapa alisema kuwa anamfahamu vizuri Makamu wa Rais kwa siku nyingi na kwamba wamewahi kufanya kazi pamoja.

  Alisema lakini yeye (Mkapa) katika siku za karibuni, hajawahi kusemwa kwa mazuri wala kusifiwa lakini yote anamwachia Mungu.

  Baada ya kusema hayo, alimkaribisha Dk. Shein kufungua mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam bila kusoma hotuba yake, ambayo baadaye waligawiwa waandishi wa habari.

  Mkapa amekuwa akituhumiwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya bila kufuata taratibu na kwa bei ya kutupa.

  Inadaiwa kuwa alishirikiana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali yake, Daniel Yona, kujimilikisha mgodi huo kwa Sh. milioni 700 badala ya thamani yake halisi ya Shilingi bilioni nne.

  Hata hivyo, licha ya kujimilikisha kwa gharama ndogo, pia inadaiwa kuwa waliishia kulipa Sh. milioni 70 tu.

  Chanzo: IPP Media Web
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  Mungu anamjua leo....????????????????
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  atoke hapa! Angefanya kazi yake mambo mengine wala yasingefika hapa. Anataka tumsifie kwa uwanja wa mpira?
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ana mengi ya kusifiwa si uwanja wa mpira tuuu...

  Makosa pia kiuongozi anayoo ila mfumo huchochea kwa kiasi kikubwa kuyafanyaa..Anayakubali makosa ila ajadiliwe kwa haki pia.

  Ulikuwa ni uongozi wa pamoja ambao mafanikio ya awamu yake yametumika sana kuhalalisha awamu iliyopooo...

  Kumjadili Mkapa bado hakuisadiii jamii zaidi ya kunufaisha waliopo kuendeleaa kuwepo madarakani..Hata kampeni za kumchafua ni mikakati kwa masilahi binafsi.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwani dogo hilo?
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Lingekuwa ni jambo la maana sana kama mkuu Mkapa angesema anaiachia mahakama, kuliko kumwachia Mungu. Au wanaomsingizia angeiachia mahakama iwashughulikie, much better kama angewafikisha kunakostahili, happo Mungu angetuonesha wazi zaidi nani ni nani. Nadhani hata Mungu anayemzungumzia hapendi wanafiki. Isn't it Ben?
   
 7. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  mh! Shemeji? come home plz.
   
 8. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwi kwi kwi tehe teh teh............
   
 9. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Ila katika kipindi chake Tanzania imebadilika kiuchumi...HILO HALINA UBISHI.Uchumi na science pamoja na technology vimekua.
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Duh! Mkuu I can tell you are a CCM supporter. I am also a fan of CCM although the party has irritated me after all the current scandals. Lakini ushabiki pembeni wewe una fikiri kweli uwanja wa mpira ni big deal? Kwa hiyo mtu awe raisi miaka kumi kwako utaona uraisi wake ulikuwa na mafanikio kwa uwanja mmoja wa mpira? You can't be serious mkuu na sidhani uwanja wa mpira una justify ujinga mwingine ulio fanyika chini ya uongozi wake.
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Uchumi maybe but science and technology? Are you for real mkuu?
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Endelea na mapumziko yako BM. Uliyoyafanya watu wa kawaida tunayaangalia kwa macho ya makengeza. Ni kweli ni Mungu peke yake atakayeweza kuamuai vema ukamwachia yeye ambaye atapima kwa urari unaolingana
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Du shemeji tena? Mkuu Ben na admire sana kazi aliyofanya Ben. No doubt ni kiongozi bora aliyewahi kutokea kwenye "modern" Tanzania. Kuna kila evidence ya kufanya vizuri kwenye karibu kila litu alichofanya wakati wa urais wake, lakini hii haina maana tukae kimya kwa kitendo chake cha kututosa kwenye mdomo wa Simba, am sure alikuwa anajua wazi kabisa kuwa nchi inachukuliwa na kina nani na inakwenda kwa kina nani, hakuonesha effort yoyote ya kutusaidia.

  Even worse alitudanganya kuwa atahakikisha kuwa tunapata rais mzuri, look at what he has done to us.
   
 14. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #14
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  kuna mazuri mkapa kafanya, makosa ni sehemuya uongozi.

  hebu niambien huyu tulie nae nini cha maana kinaonekana amefanya?!
  hata yeye akitoka mtaponda tu. wengine humu hata mambo ya familia zenu yanawashinda kazi kunyooshea vidole wengine.
  hata msemeje mkapa ndo kafanya mengi mazuri na nchi imepata heshima.

  kimya!!!
   
 15. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Barabara zimetengenezwa sana pia wakati wake. Kwenye swala la globalisation, kila nchi ya Africa linaitafuna. Hii kitu ukienda nchi yoyote ile Africa lazma wazungu wamewaingiza kingi. Ukitaka kuji isolate nao wanakuchapa bakora ya mbali, just ask Zimbabwe u gonna get the clue. Tukumbuke IMF, worldbank na WTO wamezishika wao we can never run away from them. namaanisha hatuwezi ishi bila uwezekaji maana naona malalamiko ya BM mengi yanaelekea kuwaleta wawezekaji.
   
 16. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  nafsi inamuuma sana, reputation zero kabisa, akimwangalia mwenzie SHAIN alikaa nae kama makamu na sasa yupo na Mkwere lakini hana kashfa hata kidogo,
   
 17. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Makosa ni sehemu ya binadamu yoyote. Lakini pia lazima tuangalie hayo makosa yalikua yapi. Kuna makosa yanaweza kuwa excused lakini kuna makosa mtu lazima ahojiwe na ajieleze vizuri.

  Mkuu Kikwete anasemwa hata sasa hivi na akiondoka nae lazima wananchi watafanya review ya uongozi wake. Hapa ana jadiliwa Mkapa na siyo Kikwete. Ni sawa sawa na mwanafunzi afeli mtihani halafu uanze kuonyoosha kidole kuwa mbona mwingine nae alifeli.

  Uraisi siyo kuongoza familia. Mambo ya familia yana husu familia husika tu na haya athiri watu wengine. Uraisi ni uongozi wa nchi nzima na una tuathiri wote kwa hiyo lazima tujadili.

  Scrutiny is part of public service. Being a public servant means having accountability and taking responsibility.
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  mtu mbishi hata akiwekwa kwenye chupa bado ananyoosha kidole!!
   
 19. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama isingekuwa tamaa (bila shaka kutokana na kuwa na washauri wabovu), huyu jamaa alifanya mambo mazuri mengi kwa maendeleo ya nchi. Mpaka sasa sielewi kwa nini alikubali kununuliwa na makaburu walioitwaa NBC yetu. Sijui ilikuwaje pia akapata kichaa cha kutumia vibaya madaraka yake na kununua Kiwira. Ukiondoa dosari hizo na kiburi chake cha Kimachinga, alifanya vizuri.
   
 20. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #20
  Nov 19, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wakuu kuna useme wa wahenga unasema myonge mnyogeni lakini haki yake mpeni,Mh.Rais wa awamu ya tatu amefanya mengi mazuri na ya kuleta tija na maemdeleo kwa wanachi na taifa letu la tanzania kwa ujumla.

  Tabia ya sisi viumbe binandamu tunaangalia sana upande mmoja wa maisha ya mwanandamu hasa upande mbaya,na ubaya unaenea haraka kuliko wema hii ndiyo hulka ya wanadamu tangu enzi hizo.

  mimi binafsi pamoja na mambo yote yanayoemwa kuhsu rais mstaafu wa awamu ya tatu bado nakubali utendaji kazi wake uliyotukuka kwa maslahi ya nchi yetu changa ya Tanzania
   
Loading...