Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

kpis6.jpg

Credit: Mjengwa blog
 
...ningekuwa JK na kwa sababu haya mambo ni mageni na uswahili umetujaa ningekula deal na Mkapa kwamba acha awe prosecuted then akiwa guilty nitampatia pardon lakini tayari itakuwa lesson learned kwenye demokrasi yetu na itasaidia kuonyesha mafisadi no one above the law
 
Mkapa ana dossier ya madhambi ya Mtandao iliyotayarishwa na Phillip Mangula. Kama Kikwete anashindwa kumshughulikia basi naamini hiyo ndiyo sababu kuu.

Hivi Sumaye vipi jamani? Nilitegemea huyu ndiyo atakuwa mtu wa kwanza kushughulikiwa na JK.
 
It's friday dude....whatchu got goin' on...?

'Am dry on liquor dawg, can't shop wont shop! worst still gat ma head spinnin from a m*fo colds... uuuuuuuuuuuwii, holy sh... help me!! Dawg, the 'hitch hikin Cheech&Chong concentrate' wont work either 🙁

SteveD.
 
Mwacheni mzee BWM apumzike kwa amani.

Kasema kastaafu siasa, nyie mnataka nini?

Kasema hatojibu masuala ya kisiasa, sasa?

Kama alivyosema JK, muacheni apumzike. Nauliza ni nani aliye msafi kati yenu awezaye kumrushia MKapa jiwe?!

What? tumuache "Mzee" apumzike? kwa kipi? Apumzike kwa kui squander BOT? Hivi ile debt relief tuliyopewa na Sweden, Norway, US,na nchi nyingine imefanya kazi gani? kwa nini wananchi hatupewi facts? au ndio imeongeza mishahara ya hawa "walala heri"?
Yes mimi sio msafi lakini sijaiba mabilioni ya fedha za wananchi. BM aliaminiwa na wananchi na akapewa dhamana na kwa sababu ya hiyo dhamana lazima awe responsible. FD unakumbuka ule usemi unaosema "To whom much is give, much is expected"? Alipewa dhamana ya kuliongoza taifa na sio kujaza mifuko yake na accounts zake. Mkapa kama CEO na sisi waka stakeholders tuna haki ya kumuuliza juu ya strategies zake na profits na losses za kampuni yetu.. kwa sababu tuna hisa. So haachwi mtu hapa.
 
Nkapa amekuwa kama Yuda wa Iskarioti? aliyemuuza YESU kwa Vipande 32 vya Fedha,Lakini Yuda baadae alilia kwa aibu na kutupa hizo Shekheli 32 hope na Nkapa atafanya Hivyo.
Na hao wabunge especially wa sehemu ambazo Madini hayo yanatoka wao wamepewa Ice Cream na kuwaacha watu wao waachwe na ndege ya Lowasa. Hususana Mara/Mwanza/Shinyanga/Tabora/Bila kusahau Mererani.
Sasa Ice Cream ikiisha yayuka ndipo watakapo elewa Kosa walilofanya.
Wenzao wataendelea kuruka na Ndege wao wataishia kuomba lifti au kupanda Biskeli
 
Mwacheni mzee BWM apumzike kwa amani.

Kasema kastaafu siasa, nyie mnataka nini?

Kasema hatojibu masuala ya kisiasa, sasa?

Kama alivyosema JK, muacheni apumzike. Nauliza ni nani aliye msafi kati yenu awezaye kumrushia MKapa jiwe?!

Tangu lini kujibu Tuhuma za Wizi Ubadhirifu na Ufisadi imekuwa Siasa?

Yule aliyeuliza na kutoa dhubutu na kusema asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe hakuwa akihalalisha uovu alikuwa kionyesha jinsi jamii ilivyotoa hukumu kwa kuzingatia jinsia ya mkosaji kuliko kosa lenyewe. Alihukumiwa mwanamke tu mwanaume aliachwa.

Hapo sioni ni vipi sisi Watanzania tutashindwa kumrushia mawe MH Mkapa.
Ni kweli Viongozi wenzie hawawezi kurusha hata donge la pamba kwani Mawazo yao na matendo yao ni sawa.

MH Mkapa, Tuhuma za Ufisadi siyo Siasa ni kosa la Jinai.
 
Sasa jamani, hivi kweli huyu ndiye rais wetu mstaafu tutakayeendelea kumlipa hadi mwisho wa maisha yake? Yaani akishastaafu tu anasema mabovu yangu yote msinisakame tena? Yaani anasema kuwa ni haki kwa wanasiasa kufanya mambo aliyofanya ila wakishastaafu basi game over?

Sasa itatusaidia nini kuendela kumlipa kama hata yeye mwenyewe hata hatambui nafasi yake katika jamii yetu ?

Mr Clean Huyo

Mimi naona amnaonesha mfano mzuri, kwamba amestaafu siasa na sasa anashughulikia masuala ya kijamii kama hilo la afya za wananchi. Hao wanaomtuhumu waende mahakamani. Wanashindwa nini? Maana hata akijitetea mbele ya waandishi wa habari wanaomtuhumu bado hawataamini kuwa alichokisema ni sawa. Mzee Mkapa kula pini hivyo hivyo, ulishastaafu, achana na malumbano yasiyo na msingi. Tulia, ule pensheni yako. Mwenye wivu ajinyonge, na yule mwenye suala la msingi la kulalamikiwa aende mahakamani au kwenye vyombo vingine stahili. Watu mnakalia majungu tu. Ovyoo!
 
Wewe mwongopee tu nduguyo; hivi sasa atakula pini hivyo hivyo sawa...ila pini hizo hazitoisha...atazidi kusokomezewa na tutaona kama tumbo lake halitapasuka kwa shibe haramu...na kibaya zaidi pini hizo zitabadilika na kuwa misumari si punde!! Wengi wapo walioingizwa mkenge na wenye ushauri kama wako. Cha mtemakuni hakitabiriki ila hukiona.

SteveD.
 
Mkapa up for 6.5bn/- leadership prize

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

A spokesman for Mo Ibrahim said the ’long list’ of candidates in no particular order includes Mathieu Kerekou (Benin), Azali Assoumani (Comoros), Domitien Ndayizeye (Burundi), Henrique Rosa (Guinea Bissau), Maaouya Ould Sid’Ahmed Taya (Mauritania), Joaquim Chissano (Mozambique) and Sam Nujoma (Namibia).

Others also in the running for the prize are Benjamin Mkapa (Tanzania), Abass Bonfoh (Togo), Gnassingbe Eyadema (Togo), Bakili Muluzi (Malawi), France-Albert Rene (Seychelles) and Abdiqassim Salad Hassan (Somalia).

Hapo Mkapa anachuana na Chissano na Nujoma. Wengine wasindikizaji.
 
Mimi naona amnaonesha mfano mzuri, kwamba amestaafu siasa na sasa anashughulikia masuala ya kijamii kama hilo la afya za wananchi. Hao wanaomtuhumu waende mahakamani. Wanashindwa nini? Maana hata akijitetea mbele ya waandishi wa habari wanaomtuhumu bado hawataamini kuwa alichokisema ni sawa. Mzee Mkapa kula pini hivyo hivyo, ulishastaafu, achana na malumbano yasiyo na msingi. Tulia, ule pensheni yako. Mwenye wivu ajinyonge, na yule mwenye suala la msingi la kulalamikiwa aende mahakamani au kwenye vyombo vingine stahili. Watu mnakalia majungu tu. Ovyoo!

Ninavyokufahamu Kithuku ni mtu makini sana katika hoja. Ila hapa umefunika funika....ushabiki au unazi umezidi hoja. Tuhuma nzito namna hii, inakuwaje tena malumbano yasiyo na msingi? Mwishoni umefunga kazi kabisa....majungu. Ama kweli ukistaajabu ya Musa...
 
Mkapa, kwanza kabisa Watanzania tunapenda kukufahamisha Tanzania hakuna kipengele chochote katika sheria za nchi yetu kinachosema kwamba kiongozi aliyestaafu hatakiwi kujibu tuhuma nzito dhidi yake mara anapostaafu. Hakuna nchi yeyote hapa duniani yenye kipengele kama hicho. Ipo mifano mingi tu ya viongozi waliostaafu na kutakiwa kujibu tuhuma ziliwakabili kwa yale waliyofanya walipokuwa madarakani. Mfano wa hivi karibuni ni wa aliyekuwa Rais wa Zambia Mr. Chiluba.

Tuhuma tunazotaka uzijibu ni kama zifuatazo.

1. Inasemekana ulikuwa unafanya biashara ulipokuwa Rais wa Tanzania. Je, uliamua kufanya biashara kutokana na mshahara na marupurupu madogo uliyokuwa ukiyapata kama Rais? Hukujua kama maadili ya uongozi kama Rais wa Tanzania hayakuruhusu kufanya biashara ukiwa Ikulu? Biashara uliyokuwa unafanya ilikuwa ni ya kitu gani? Biashara hiyo ulifanya ndani au nje ya nchi? Biashara hiyo ulifanya na makampuni gani au kama ni watu binafsi ni akina nani? Je, unadhani wadhifa wako kama rais wa Tanzania ulikusaidia kwa namna moja au nyingine katika biashara hiyo/hizo?

2.Ulipokuwa madarakani Mama Anne Mkapa katika moja ya ziara zake Marekani alipewa mabilioni ya pesa na Bill Gates ili kusaidia katika mapambano dhidi ya ukimwi katika nchi yetu. Pesa hizo alipewa kama First Lady wa Tanzania na sio kama Mama Mkapa. Kwanza kabisa tungependa kujua pesa hizo zilikuwa ni kiasi gami? Na kiasi gani kimeshatumika mpaka sasa hivi? Na kama kuna salio liko wapi na ni yupi anayestahili kufuatilia ili kujua pesa hizo zinatumika katika minajili aliyokusudia Bill gates?

3.Katika ununuzi wa Rada, ambao ulipingwa na Watanzania wengi kwa kuwa bei yake ilikuwa ni kubwa mno hasa ukitilia hali ya halisi ya Tanzania kama nchi maskini, wakala katika ununuzi wa rada hiyo mwenye asili ya kihindi aliyechaguliwa na wewe alilipwa $12,000,000. Hizi ni pesa nyingi sana. Watanzania tungependa kujua kama na wewe ulipata mgao katika pesa hizo alizolipwa huyo wakala. Pia wakala huyo huyo alihusika katika ununuzi wa ndege ya Rais, helicopters na magari ya jeshi. Tungependa kujua ni taratibu gani zilizofuatwa katika kumteua wakala huyo na waliohusika katika uteuzi huo. Je, na wewe ulihusika katika uteuzi huo?

4.Ulihusika katika kusaini mikataba ya uchimbaji wa dhahabu na makampuni mbali mbali na kuamua kuifanya mikataba hiyo iwe siri kwa wabunge na hata Watanzania ambao ndio wamiliki wa rasilimali hizo. Kwanini uliamua details za mikataba hiyo iwe siri kwa Watanzania? Kwa faida ya nani?

5.Kuna tuhuma kwamba katika kutafuta mgombea wa CCM kwa ajili ya uchaguzi wa 2005 rushwa ilitawala sana. Wewe kama Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania hukuliona hili la rushwa na kwanini ulilifumbia macho?

6. Watanzania pia tumesikia kwamba wewe na Yona ndio wamiliki wa Kiwira Coal Mining. Tungependa kujua taratibu zilizotumika katika kuwa wamiliki wa KCM. Mlilipa kiasi gani ili kupata umiliki huo wa KCM na mlimlipa nani? Ni nani aliyepanga bei hiyo ya KCM?

7. Ulihusika katika uamuzi wa kuziuza nyumba za serikali. Watanzania wangependa kujua kama na wewe ulinunua nyumba yoyote ya serikali. Kama ulinunua (z)ipo wapi na ulilipa kiasi gani katika ununuzi huo?

8. Kampuni ya shemeji yako Simu 2000 ndiyo ilihusika katika kuwaleta Net Group ili kuiendesha TANESCO. Kama utakumbuka uamuzi huo ulipingwa sana na Watanzania walio wengi wakiwemo viongoz na wafanyakazi wa TANESCO. Je, Simu 2000 walilipwa kiasi gani kwa kuwa wakala wa kuwaleta Net Group Solutions? Na taratibu zipi zilizotumika katika kuichagua Simu 2000 kama wakala?

7. Pia simu 2000 katika mazingira ya kutatanisha ilipewa tenda ya kusimamia uuzwaji wa Asetts zote za TTCL. Je ni taratibu zipi zilizotumika katika kuwapa Simu 2000 tenda hiyo ukitilia maanani kwamba walikuwa hawana uzoefu wowote wa kusimamia uuzaji wa Assets?

8. Pia kuna tuhuma kuwa wewe na aliyewahi kuwa Waziri wa madini A. Kigoda mna mgodi wenu wa dhahabu chini ya kampuni yenu ya WAZAWA. Je, mlilipa kiasi gani kununua mgodi huu? Na kama mlilipa ni nani aliyepanga bei hiyo? Kama hamkulipa, je mnalipa mrahaba wowote kwa serikali ya Tanzania na ni kiasi gani?

Watanzania tunasubiri kwa hamu kuu kusikia majibu yako kuhusiana na tuhuma hizi nzito dhidi yako
 
Quote: Mtanzania
Mkapa up for 6.5bn/- leadership prize

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

A spokesman for Mo Ibrahim said the 'long list' of candidates in no particular order includes Mathieu Kerekou (Benin), Azali Assoumani (Comoros), Domitien Ndayizeye (Burundi), Henrique Rosa (Guinea Bissau), Maaouya Ould Sid'Ahmed Taya (Mauritania), Joaquim Chissano (Mozambique) and Sam Nujoma (Namibia).

Others also in the running for the prize are Benjamin Mkapa (Tanzania), Abass Bonfoh (Togo), Gnassingbe Eyadema (Togo), Bakili Muluzi (Malawi), France-Albert Rene (Seychelles) and Abdiqassim Salad Hassan (Somalia).

Hapo Mkapa anachuana na Chissano na Nujoma. Wengine wasindikizaji.

Katika dunia ya leo hakuna jambo la ajabu, lakini UJUE WEWE AMBAYE UMENUFAIKA NA KEKI ILIYONONA NA HUYO BEN, hata kama akipata ni sawa na majambazi wanaopora na kwenda baa kujichana kwa bia, kiti moto juu ya stuli za baa, lakini VIJANA WA MWEMA wakicharuka na kuzimwaga risasi kama walivyofanya kule HAI na kuua WAKENYA 14, kila kitu hugeuka kuwa kichungu. Nakwambia ZAWADI MKAPA HASTAHILI NA KAMA NI HAKI HAPATI, ANAYESTAHILI NI CHISANO ILA AKIPATA (Kwani wanaotoa ni binadamu kama wewe) AJUE DHAMIRA ITAMSUTA KWAMBA HASTAHILI KATA CHEMBE KWANI SASA WATANZANIA WAMEKWISHA KUMFAHAMU NA KUPITIA KWAO DUNIA IMEMFAHAMU NA KUWAFAHAMU WATU KAMA WEWE, AMBAO MUNA MACHO LAKINI MUMEVAA MIWANI ZA MBAO, MUNA MASIKIO LAKINI YAMETIWA PAMBA ZA .....
 
8. Kampuni ya shemeji yako Simu 2000 ndiyo ilihusika katika kuwaleta Net Group ili kuiendesha TANESCO. Kama utakumbuka uamuzi huo ulipingwa sana na Watanzania walio wengi wakiwemo viongoz na wafanyakazi wa TANESCO. Je, Simu 2000 walilipwa kiasi gani kwa kuwa wakala wa kuwaleta Net Group Solutions? Na taratibu zipi zilizotumika katika kuichagua Simu 2000 kama wakala?

7. Pia simu 2000 katika mazingira ya kutatanisha ilipewa tenda ya kusimamia uuzwaji wa Asetts zote za TTCL. Je ni taratibu zipi zilizotumika katika kuwapa Simu 2000 tenda hiyo ukitilia maanani kwamba walikuwa hawana uzoefu wowote wa kusimamia uuzaji wa Assets?

Bubu Ataka Kusema, nakupongeza kwa stail yako nzuri ya "KUMTENDEA HAKI" Mkapa, maana umeweka maswali anayoweza kujibu bila shaka yoyote na hayahusiani na "siasa" anazozisema, kwamba ameshastaafu. Anatakiwa kujibu tuhuma zinazomkabili na si SIASA.

Ama baada ya pongezi, naomba kufanya masahihisho muhimu.

1-Kwanza kabisa kwa kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba Simu2000 Limited si kampuni binafsi na si kampuni ya shemeji yake Mkapa. SImu2000 ni kampuni ya serikali iliyoundwa kusimamia mali na madeni ya TTCL baada ya ubinafsishaji. Mkapa alimteua mtoto wa mke wake aitwaye Peter Maro, kijana mdogo kabisa kuongoza shirika hilo. Kuna tuhuma za Mkapa kujibu kwamba je, ni kweli yeye na mkewe wameuziwa na huyo mtoto wa Anna Mkapa (wa nje) nyumba kibao nchi nzima na kwa Dar es Salaam nyingi ziko maeneo nyeti, anatakiwa kujibu kama ni kweli ama la.

2- Pili ni kweli kampuni ya shemeji yake Mkapa ndio iliyoileta Net Group kampuni hiyo inaitwa Wace Technology, ambayo shemeji yake Mkapa aitwaye Joe Maro, anayefanya kazi BoT anaimiliki pamoja na rafiki yake wa BoT aitwaye Maganga. Mkapa alilazimisha Net Group kuingia Tanesco kwa kutumia FFU.

3.Suala la Simu2000 kuwa na uzoefu ama la, halina maana, hapa ni kama Peter Maro ana uwezo ama la si chombo kwa ujumla wake, maana tunaambiwa kijana anazurura tu kazi zinaendeshwa na watu wengine na yeye anachofanya ni kutoa maelekezo pale anapopata maelekezo kutoka katika familia, yaani 'baba' na mama. Inawezekana hata baba yake mzazi, ambaye wana JF munaweza kutusaidia.
 
Ahsante sana kwa masahihisho yako na pia kwa kuongeza tuhuma nyingine ambazo Mkapa anastahili kujibu kuhusiana na kuuziwa nyumba nyingi yeye na mkewe katika sehemu mbali mbali Tanzania. Once again, thank you.
 
Labda tusubiri akishapokea tuzo aje ajibu mapigo ya wananchi, hakuna haraka pole pole tu,

Heshima mbele wakuu kwa kuendelea kumkumbusha kuwa wananchi hatujalala!
 
Najua watu wengi mnataka Mkapa ajibu tuhuma na ameshawaambia kuwa hatajibu. Nadhani amejibu kwa busara sana, swali je angeamua kuwa kama Ditto na kuwaambia fisadi mama zenu mngefanya nini?
Kwa mawazo yangu ni vigumu sana kwa nchi kama bongo kuendelea, mara nyingi watu wanajaribu kutafuta ufumbuzi wa mambo bila hata kujua njia za kutatua jambo hilo.
Watu walifuta miiko ya uongozi na kuruhusu viongozi kufanya biashara au kuwa na kipato zaidi ya kimoja watu mnaliacha swala hilo kana kwamba rais anazuiwa kufanya biashara. Kwa miiko ipi ya uongozi? Nadhani kuna watu wanaona nafuu Mbowe angekuwa rais, je akiwa rais hizo biashara anazofanya toka amezaliwa aziache? Je, ni sheria ipi itakayomzuia asichanganye urais na biashara? Mimi sina tatizo na rais kufanya biashara lakini lazima kuwe na miiko mbayo haitasabaisha hali ngumu ya wananchi wengine. Nampongeza sana Dr. Slaa kwa "list of shame" kwani kabla ya kuandika ali-define vigezo vya ufisadi alivyotumia.
Tukiangalia katiba yetu ambayo watu wachache sana wanaipigia kelele. Ibara ya 37-(1) inasema kwamba mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na halazimiki kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote....malalamiko ya wananchi au kelele za mtu yeyote hazimweki hatiani. Upo hapo. Kali zaidi ni pale atakapofanya makosa kama rais hata akistaafu huwezi kumshtaki soma katiba ibara ya 46-(1)(2)(3)...itakuwa marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuachia madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa katiba hii... What does this means? Ukimshtaki rais umevyunja katiba ya jamhuri ya muungani na unastahili mvua...
Huko nyuma nilielezea swala la rushwa, hivyo vyombo vya kupambana na rushwa vilianzishwa toka mwaka 1974 na rushwa haiishi wala kupungua hakuna mtu hata mmoja anayeshtuka kuwa tunatumia wrong approach.. hata adhabu ya rushwa iwe kunyongwa, rushwa haitaisha kwa sababu sababu za kuchukua rushwa zipo..nitarudi kwenye hili swala la rushwa huko mbeleni. Kama mmepitia leo kule kwa michuzi kuna kijana nadhani wamemtoa roho kwa sababu ya kuiba simu, hivi hawa vibaka hawajui kuwa ukikamatwa cha moto utakiona? Mbona bado wanaiba?
Turudi kwenye ufisadi, hata Mkapa akijibu hizo hoja then what? Nadhani kwa kipindi hiki tumeshajifunza mengi tunatakiwa tupiganie mabadiliko ambayo yanawezekana kwanza kama katiba, miiko ya uongozi n.k Kama hawataki kubadilisha kwa njia za amani serikali ni yetu kwa nini tusiichukue hata kwa mawe?
Kuna mambo mengi sana ya ajabu ajabu kwenye katiba, Bunge linaweza kumuundia Tume Rais aliyopo madarakani na kumuondoa lakini haijasema kitu chochote kuhusu rais alioondoka madarakani na hao PCCB hawana meno ya kumuuma Mkapa wanapiga tu kelele.
 
Kama mtu aliyewahi kushika madaraka makubwa kabisa nchini, Mkapa ataendelea kuwa kiongozi wa Watanzania hadi mwisho, atake asitake. Hivyo, bado anawajibika kuitekeleza sera yake ya ukweli na uwazi.

Heshima mbele tuendelee kumpigia paka kengele!
 
Mimi nashindwa kabisa kuelewa sisi Wadanganyika tutaweza vipi kupima mambo kwa mzani na sio kutunga hoja!..
Hao wanaotaka wananchi wamshtaki Mkapa mahakamani.. watuambie ni kifungu gani cha sheria wanachokitumia wao! maanake tumeisha ambiwa Rais Jk amekataa kufanya hivyo, vitengo vya kuzuia rushwa haviwezi kumfikisha kutokana na sheria inayomlinda.
Yet kuna watu bado mnasisitiza kuwa ni jukumu la wananchi kumfungulia mashtaka Mkapa mahakamani!... HOW?
Hivi tunaongea lugha moja ama!..
 
sam
I totally support you, we need a permanent solution which is to change the status quo of our constitution.
 
Back
Top Bottom