Zee la shamba
Member
- Oct 17, 2007
- 55
- 7
kama aliweza kuuza mashirika ya umma chama kitamshinda kuuza?
This Guy is a businesman.
This Guy is a businesman.
kama aliweza kuuza mashirika ya umma chama kitamshinda kuuza?
This Guy is a businesman.
19.10.2007 0123 EAT
Mkapa ang'aka
*Akataa kuzungumzia tuhuma anazoelekezewa
*Asisitiza kuwa hivi sasa ni muda wa maendeleo
*Asema alikwishastaafu masuala ya siasa nchini
Na Benedict Kaguo, RCT
RAIS mstaafu, Bw. Benjamin Mkapa, amekwepa kuzungumza na waandishi wa habari kwa kusisitiza kuwa huu sasa si wakati wa siasa, bali anaangalia zaidi masuala ya kimaendeleo na kusema alishastaafu siasa.
Bw. Mkapa alitoa kauli hiyo kwenye hoteli ya Kunduchi, Dar es Salaam jana, alikokuwa kufungua mkutano wa mwaka wa taasisi yake ya Mkapa Fellow Programme, unaojadili mafanikio yaliyofikiwa na Mfuko huo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Waandishi wengi wa habari waliokuwapo eneo hilo, walionekana kuwa na shauku ya kutaka kupata maoni ya kiongozi huyo ambaye amekuwa akituhumiwa kuvunja kanuni za maadili wakati akiwa Ikulu.
Akionekana kufahamu shauku hiyo, Rais mstaafu Mkapa alitoa kauli hiyo wakati akihitimisha hotuba yake na alipomaliza, alisisitiza kuwa hakuwa tayari kuzungumzia masuala ya siasa.
"Tuko hapa kujadili mafanikio yaliyofikiwa na Mfuko wa Benjamin Mkapa, tangu kuanzishwa kwake Julai mwaka jana, ambapo tumejikita zaidi kutoa elimu na dawa kwa wananchi waishio maeneo ya vijijini kukabiliana na UKIMWI na si masuala ya kisiasa," alisema Bw. Mkapa.
Hata hivyo wakati akitoka ukumbini, waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari walisimama mbele yake, ili kumuuliza maswali kadhaa, lakini kiongozi huyo alionesha ishara ya kuomba apishwe apite na kwamba hakuwa tayari kuzungumza.
Juzi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bw. Joseph Butiku, ambaye ni mmoja wa watu waliokuwa karibu na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, alizungumza na vyombo vya habari na kushauri kuwa ni vyema Rais mstaafu Mkapa akajitokeza na kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake kuliko kuzinyamazia.
Kitendo cha Bw. Mkapa kukwepa kuzungumza na wanahabari jana kwa kusisitiza kuwa huu si muda wa siasa kwake, kinaweza kufasiriwa kuwa mwendelezo wa kiongozi huyo kupuuzia tuhuma zinazoelekezwa kwake.
Akizungumza awali kuhusu taasisi hiyo, Bw. Mkapa alisema imeanzishwa ili kuona Watanzania wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI, hususan waishio vijijini, wanapatiwa huduma sawa za matibabu ingawa alisema kuna upungufu mkubwa wa wataalamu wa afya katika maeneo hayo.
Alisema kupitia programu hiyo, walifanikiwa kuwa na wataalamu 99 ambapo 69 kati yao, wako katika wilaya 23 na wanatarajia kupeleka watumishi 30 zaidi katika wilaya 10 ifikapo Novemba 10 mwaka huu.
Programu hiyo imelenga kuendeleza juhudi zinazofanywa na Serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
Alisema, mfuko huo peke yake hauwezi kukabiliana na changamoto zilizopo na hivyo kwa kushirikiana na Serikali na Asasi Zisizo za Serikali, mafanikio yanaweza kupatikana.
Aliwasihi wadau wa maendeleo, kutoa nafasi za ubunifu kwa kadri watakavyoweza katika utekelezaji wa programu hiyo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Deo Mtasiwa, alisema lengo la programu hiyo mbali ya kutoa mafunzo, pia ni kuajiri na kuwapeleka wataalamu kazini, kwa lengo la kusaidia jamii.
"Ninawaomba tushirikiane na kuzuia kuingiliana katika kazi moja, ili tuweze kutumia fedha na wataalamu katika kushughulikia janga hili nchini," alisema.
Alisema lengo la programu hiyo ni kutoa mafunzo, kuajiri na kupeleka wataalamu kazini kwa ajili ya kutoa huduma za kitabibu nchini.
Aliongeza kuwa programu hiyo inafadhiliwa na Serikali ya Norwei na kwa sehemu ndogo kutoka katika Mfuko wa Misaada wa Bill Clinton.
Huyu Dawa yake ni Dola kuchukua hatua, kwa kumuweka katika One of the Safe Houses, wakati taratibu zingine zinafuatwa kumfungulia mashtaka katika mahakama kuu kwa uhujumu uchumi au , bunge ku-lift immunity yake kama ipo then kumfungulia mashtaka katika mahakama kuu kwa makosa ya kuhujumu uchumi
Zee la shamba,Huyu Bwana Mkubwa ni Jeuri na Jeuri yake inaongezeka baada ya JK kusema kuwa hawezi kuwachunguza viongozi wastaafu kwani kufanya hivyo kunawafanya viongozi wengi kutaka kubadili katiba ya Nchi ili waendelee kutawala kwa kuogopa kushtakiwa.
Sasa kama mtu kafanya madudu wakati wa utawala wake kwanini asishtakiwe?
Sitaki kuamini kwamba JK naye alijua kuwa atafanya madudu ndio maana akamuwekea kinga Ben. kuhofia naye baadae wembe ambao angeutumia kunyolea Ben ungekuja kumnyoa yeye Pia.
Kulindana kumezidi cha msingi ni wananchi kuungana kwa pamoja na kuwatimulia mbali hawa mafisadi.
"It ain't over till it's over"
Mwacheni mzee BWM apumzike kwa amani.
Kasema kastaafu siasa, nyie mnataka nini?
Kasema hatojibu masuala ya kisiasa, sasa?
Kama alivyosema JK, muacheni apumzike. Nauliza ni nani aliye msafi kati yenu awezaye kumrushia MKapa jiwe?!
Mwacheni mzee BWM apumzike kwa amani.
Kasema kastaafu siasa, nyie mnataka nini?
Kasema hatojibu masuala ya kisiasa, sasa?
Kama alivyosema JK, muacheni apumzike. Nauliza ni nani aliye msafi kati yenu awezaye kumrushia MKapa jiwe?!
Mwacheni mzee BWM apumzike kwa amani.
Kasema kastaafu siasa, nyie mnataka nini?
Kasema hatojibu masuala ya kisiasa, sasa?
Kama alivyosema JK, muacheni apumzike. Nauliza ni nani aliye msafi kati yenu awezaye kumrushia MKapa jiwe?!
Oooh, by the way Kichuguu, nili 'kumiss' kichizi mzee wangu wa busara. Nashukuru Mungu kuwa umerudi tena jamvini na ninakutakia kila kheri na baraka katika familia yako ili usipotee tena 🙂
SteveD.