Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Kinachozungumzwa hapa ni kuwa viongozi wa nchi, hawapaswi kujihusisha na biashara. Wana JF, kamwe hawasemi Baregu na Jenerali ni watu safi. Hata kama Baregu na Jenerali wangelikuwemo kwenye serikali na wakati huo huo wanafanya biashara wangepewa vidonge vyao. Hoja ya msingi hapa ni kwamba unapokuwa kiongozi mwenye dhamana kubwa ya kuliongoza taifa hupaswi kujiingiza katika mambo ya biashara. At one time, the conflict of interest would be inevitable. Huwezi kutumikia mabwana wawili na kuwatimizia haja zao kwa wakati mmoja!

Mkuu Mwanamalundi,

Heshima mbele, Salute na sasa you made my day saaa ya kulala nitakuona kesho, I mean hii ndio tunaita,

Where We Dare Kumkoma Nyani Mchana Kweupe Kwa Mwendo Wa Mdundo!


Mkuu FMES, heshima mbele mkuu. Wakati umefika sasa watu kupewa vidonge vyao. Wakimeza, wakitema shauri yao.
 
Mkuu Masatu,

Ni ndugu mmoja huko nyuma niliyekuwa ninamjibu aliyemfananisha Clinton na Mkapa, nikasema na ninarudia kuwa ni kweli wanafanana sana waliyoyafanya, meaning maovu kwa mataifa yao, lakini ya Clinton yanavumilika, kuliko ya huyo mwingine,

Anyway, heshima mbele na good debate, keep it up na msimamo imara wa kusimamia hoja, au unachokiamini, maana tunawahatiji sana hapa JF, wenye misimamo kama yako!

ES,
Mkulu umesikika loud & clear kanyaga twende.......


Mkandara,
Sawa mkuu unajua ktk maisha watu wote ambao hutumia kamusi huwa ndio wenye upeo mdogo kwani kamusi hutumika tu pale unaposhindwa kuelewa maana.
Neno FISADI tunalitumia kila siku ktk maisha yetu hata kama kamusi haipo ndio maana nikasema hata mtoto mdogo asojua kusoma anafahamu maana ya nenoi hili. Ukiwa hujui kusoma ina maana bado unaweza kutoa tafsiri ya neno hili bila kamusi.

Now ur talking! kwa hiyo wenye kutumia kamusi (nikiwemo) ndio tuna upeo finyu eeeh... hapa neno upeo finyu haiwi tusi la nguoni!

Pili, sikuipata tafsiri ya neno hili ktk Taarabu ila nimekupeleka wewe upate kujua matumizi ya neno hili.. kwa sababu ulidai ushahidi.. sasa huo ushahidi niutoe wapi?..ndio maana nikasema hapa nilipo siwezi hata kutoa ushahidi wa jinsia yako kwani hili sii jambo naloweza kuwa nalo mkononi na wala haihusiani kabisa na hoja. Kisha mjomba maana ya neno na matumizi ya neno ni vitu viwili tofauti!.. ijue lugha yako.
Kiswahili lugha nyepesi sana isipokuwa tunaweza kujichanganya sisi wenyewe. Fisadi ni character inayotokana na neno la kiarabu Fasad... na kweli ina maana nyingi lakini maana zote zinahusu mtu mbaya mharibifu na kamwe haiwezi kuhusiana na Kutongoza unless mwandishi alikuwa akizungumzia kuhadi kuwa ni fisadi nayo pia bado haileti matumizi mazuri ya neno hili.
Nimemaliza...

Swadakta! kwa hiyo uliponipeleka ktk ule wimbo fisadi kiwembe ulikuwa unataka kueleza matumizi ya neno fisadi, hapa nakubaliana na wewe kabisa! lets extend the line of reasoning kidogo hivi ukiambiwa fulani ni kiwembe sana nadhani moja ya maana hapa ni kuwa huyo mtu ni hatari kwa totoz au sio, if thats the case tuje kwenye matumizi ya neno fisadi kiwembe. Mwana fasihi anawasilisha ujumbe kupitia mipasho kuwa kuna huyu fisadi kiwembe ni mtu hatari. Kwa msingi huo basi huna haja ya kwenda mbali ili kunasibisha neno fisadi na kutongoza!

Upo hapo?
 
Usiwe na wasiwasi mkuu nachukua maneno yako mwenyewe kama ulivyosema kuwa hapa JF hakuna kutishana ila tunataka issue na kumkomalia nyani giledi!. Ikiwa hilo neno sio tusi nakuomba ulipokee kama ulivyolipamba!

Pili, neno Kiwembe, hapana mjomba Kiwembe tazama tena kamusi itakupa jibu... na kama ktk mipasho kiwembe maana yake ni mtu anayeharibu akikata kama wembe ndivyo ilivyotumika... hilo la totoz ni kiswahili cha bara ama kimepitwa na wakati kama vile tulivyokuwa tukisema chai ya rangi!.
 
Usiwe na wasiwasi mkuu nachukua maneno yako mwenyewe kama ulivyosema kuwa hapa JF hakuna kutishana ila tunataka issue na kumkomalia nyani giledi!. Ikiwa hilo neno sio tusi nakuomba ulipokee kama ulivyolipamba!

Pili, neno Kiwembe, hapana mjomba Kiwembe tazama tena kamusi itakupa jibu... na kama ktk mipasho kiwembe maana yake ni mtu anayeharibu akikata kama wembe ndivyo ilivyotumika... hilo la totoz ni kiswahili cha bara ama kimepitwa na wakati kama vile tulivyokuwa tukisema chai ya rangi!.

Good finally bingwa wa kiswahili umeona kuwa upeo mdogo sio tusi.

Kiwembe kufafanisha na kiswahili cha bara au kilichopitwa na wakati si sahihi actually hiko ndio kiswahili cha sasa na ukiongea na wazee wa zamani utawaacha patupu.
 
Duh! ama kweli mzee wangu mbishi... hivi unaamini kabisa kuwa kiwembe kimetumika ktk wimbo huo kama mtu wa totoz?..
Mshikaji mwenzako nafunga kati ya 50 kiumri na nimekitumia kiswahili hicho nikiwa shule ya msingi!.. ushahidi gani zaidi unataka!
Hata hivyo kulingana na madai yako, tafsiri ya kiwembe haisemi hivyo ktk kamusi sasa mbona wabishana na wataalam wa kiswahili?.. Anyway nakuacha dogo, mshindi wewe turudi kwa Mkapa!... Field marshal ES anakusubiri kwa hamu.
 
Nyani Ngabu,
Hapa kijiweni hoja zangu ni za Umri mtupu hakuna darasa kwa hiyo unaweza fahamu kwamba Kuishi kwingi ni kuona mengi!
 
Duh! ama kweli mzee wangu mbishi... hivi unaamini kabisa kuwa kiwembe kimetumika ktk wimbo huo kama mtu wa totoz?..
Mshikaji mwenzako nafunga kati ya 50 kiumri na nimekitumia kiswahili hicho nikiwa shule ya msingi!.. ushahidi gani zaidi unataka!
Hata hivyo kulingana na madai yako, tafsiri ya kiwembe haisemi hivyo ktk kamusi sasa mbona wabishana na wataalam wa kiswahili?.. Anyway nakuacha dogo, mshindi wewe turudi kwa Mkapa!... Field marshal ES anakusubiri kwa hamu.

Bob, si umesema una tafsiri neno kiwembe kwa matumizi yake na sio kwa maana yake, kwa muktadha huo na ndio tafsiri ya totoz inapokuja kwa matumizi ya neno kiwembe.. kwa mfano wewe ulisema hivi;

Pili, neno Kiwembe, hapana mjomba Kiwembe tazama tena kamusi itakupa jibu... na kama ktk mipasho kiwembe maana yake ni mtu anayeharibu akikata kama wembe ndivyo ilivyotumika... hilo la totoz ni kiswahili cha bara ama kimepitwa na wakati kama vile tulivyokuwa tukisema chai ya rangi!.

Kwa msingi huo basi mimi ninae tegemea kamusi nikuta maana ya kiwembe kwa mujibu wa kamusi ni hii;

Kiwembe (nn) Kifaa kidogo cha madini chenye umbo bapa na makali pande zote mbili kinachotumika kunyolea.

Haya sasa niambie hiyo maana yako ya kuharibu umeitoa wapi?

Takriban sote hapa tumepitia shule ya msingi na kiswahili likiwa ni moja ya masomo.

Suala hapa sio ubishi, bali ni kuelimishana tu.
 
Masatu:
Shukrani kwa kuja hapa na kamusi, hii imesaidia wengi kutoa tongotongo zao katika lugha yetu nzuri ya kiswahili..Ingawa wengine wameendelea kubisha tu, japo ukweli wanahufahamu.
 
Masatu,
Hivi mjomba kiswahili kinapanda ama?... samahani lakini.
Nimesema maana ya neno Kiwembe haikubadilika kuwa mtu wa totoz kama ulivyodai ila ni maana ile ile ambayo ipo ktk kamusi ambayo kulingana na makali ya wembe ndivyo fiasadi anavyoweza kuharibu uhusiano wa jamii fulani. Huu wembe hauwezi kukata ikiwa haujatumika ktk kufanya hivyo na ndio maana wakatanguliza neno Fisadi Kiwembe, kwa hiyo kiwembe hiki kimetumika ktk Ufisadi.
Kwa hiyo jaribu kuelewa kwanza matumizi ya neno ktk sentesi ili upate kuifahamu maana halisi ya neno kama ilivyotumika.
Na kumbuka kwamba ubishi huu unatokana na neno hili kutumika ktk kuwaita viongozi waliohujumu uchumi wetu kuwa ni Mafisadi kwa hiyo usije toka nje kwa kulundika maana mia moja kutafsiri Fisadi. Nikisema leo unachemsha, kisha wewe ukaanza kutafuta kamusi na kutafsiri matumizi ya neno hili ktk kamusi, kisha ukajitazama mwili wako kama una maji yanayochemka mjomba tutakesha. Nikisema kaa kitako haina maana nimesema kaa la moto, kaa mdudu wa majini ama utafute hiki kitako ni kitu gani. ndio maana nazidi kusema kiswahili ni lugha yetu haina haja kabisa ya kutazama kamusi kupata maana na matumizi ya neno fulani.
Nitakupa mfano mwingine naweza kabisa kusema hawa viongozi wetu ni Makafiri nikiwa na maana hawamuogopi Mungu. sasa ukianza kutazama kamusi kutafuta maana ya kafir bila kujali matumizi yake utakuja ambiwa vitu tofauti kabisa na pengine unaweza ku draw conclution kuwa nimesema Viongozi wetu wote sio Waislaam..
Kifupi utanisamehe mjomba, nachoona hapa ni vioja vitupu yaani unazidi kutoka nje kabisa ya somo hili. Neno lolote lile hutazamwa maana yake ktk matumizi yake iwe ktk lugha yoyote ile. Neno la kiingereza LIVE linaweza kuwa latamkwa Laivu ama livu inategemea na matumizi ya neno hili na maana yake pia hutegemea pia matumizi yake. Ukitazama maana ktk kamusi bila kujali matumizi yake mjomba utakuwa wazidi kupotea.
 
Mkuu hapa naona una lazimisha hoja kwa kuleta mifano isiyo muafaka. Kiswahili cha kumwambia mtu kachemsha sio kiswahili fasaha unachukua maneno ya mitaani na kusukumia hoja zako. Hii ni sawa na kusema mchezaji fulani mbaya sana akiwa karibu na goli kwa kiswahili cha mitaani hapo mbaya imekuwa badala ya mahiri! sasa mkuu turudi ktk hoja ya msingi tusupelekane kusiko husika.

Narejea kusisitiza kuwa neno fisadi kama lilivyo tafsiri na wataalam ndio usahihi, hizo maana unazoleta wewe ni za kimataani na ndio maana unapata taabu kuelewa.

Nadhani kiswahili kimekuwa taabu kwako sasa....
 
Sawa wewe endelea na tafsiri yako ambayo haikubaliani na matumizi ya Fisadi ktk kuwataja hawa viongozi wachafu na wahujumu uchumi. Na nadhani hapo upo peke yako Tanzania nzima... wewe mjuzi wa lugha..
Sisi tunaamini kuwa hawa viongozi ni MAFISADI kwa maana yetu sasa kama wewe utaendelea kufikiria kuwa tunasema wao ni malaya na watongozaji endelea kufikiria hivyo na kamusi yako.
Hata mifano unashindwa kuelewa inatumika vipi yaani unachotazama wewe ni kiini macho cha lugha. Mbona usizungumzie LIVE ama KAA si yote lughha safi ya kamusi?. Sikukupa neno moja nimeweka mengi upate picha acha kufahamu lakini ndio badooo..
 
Sawa wewe endelea na tafsiri yako ambayo haikubaliani na matumizi ya Fisadi ktk kuwataja hawa viongozi wachafu na wahujumu uchumi. Na nadhani hapo upo peke yako Tanzania nzima... wewe mjuzi wa lugha..
Sisi tunaamini kuwa hawa viongozi ni MAFISADI kwa maana yetu sasa kama wewe utaendelea kufikiria kuwa tunasema wao ni malaya na watongozaji endelea kufikiria hivyo na kamusi yako.
Hata mifano unashindwa kuelewa inatumika vipi yaani unachotazama wewe ni kiini macho cha lugha. Mbona usizungumzie LIVE ama KAA si yote lughha safi ya kamusi?. Sikukupa neno moja nimeweka mengi upate picha acha kufahamu lakini ndio badooo..

Mkuu Mkandara, sasa unapotosha ili kulazimisha hoja yako. Nilipo nukuu kamusi kuelezea maana ya neno Fisadi ilikuwa dhahiri kabisa kuwa neno fisadi lina maana nyingi. Sasa naona umechokuza tongoza kwa makusudi ili kupotosha. Sasa basi kwa faida yako na wengine naiweka tena tafsiri ya Fisadi kulingana na kamusi;

Fisadi nm (ma-) mtu mbaya; mtongozaji, mharibifu, mpotevu, mwasharati kv Guberi.

Sasa hizo maana nyingine mtu mbaya, mharibifu, mpotevu hukuziona bali umeng'ang'ania mtongozaji ili kulazimisha hoja yako yako sio?

Je vipi ile tafsiri yako kwa mujibu wa mipasho umeiacha tena...
 
Hitler ndiye aliyekuwa responsible kwa vita kuu ya pili dunia na ndiye angekuwa wa kwanza kunyongwa,kama asingejiua.Sasa wanakamata watu wa chini tu wanaukula elfu kumi, rushwa itaisha lini tanzania?Nasema watu wa juu kama mkapa et al washugulikiwe kwanza kama sivyo PCB ivunjwe.Haina maana.Viongozi ndio wanapaswa kuonyesha mfano!
 
Kuna mawili, ama JK amshitaki Mkapa na kumuondoa EL ama aendelee kuwabeba watu hawa na kuendelea kuiponza serikali yake na yeye mwenyewe washindwe kutoautishwa nao. Njia pekee ya kurudisha heshima yake kwa umma wa Tanzania ni kwa JK kutekeleza hayo hapo juu kuhusu MKapa na EL
 
Gazeti la mwanahalisi tarehe 17.10.2007

Mwandishi: Saed Kubenea.

Imefahamika kwamba hadi mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) na Rais wa Awamu ya tatu Benjamini Mkapa alingatuka Juni 2006, alikuwa ameshindwa kuongoza chama na tayari alikuwa amekibinafsisha kwa matajiri.

habari zilizolifikia Mwanahalisi wiki hii zinasema kushindwa huko kwa Mkapa na ubinafsishaji huo wa CCM kwa matajiri ulikuwa unajulikana kwa wajumbe wote wa Kamati kuu na Halmashauri kuu (NEC) ya chama hicho.

Udhaifu wa Mkapa ktk kukiongoza chama hicho unadaiwa kuanza zamani baada ya kukamata chama hicho mwaka 1996.

Habari zinasema udhaifu huo ulizidi kujibainisha wazi katika mkutano mkuu wa CCM wa mwaka 2002. na kipindi cha kuelekea mchakato wa uteuzi wa mgombea urais kwa kiteti ya chama hicho mei mwaka 2005.

Ktk baru yake ya kurasa 14, ya tarehe 10 Aug 2005 yenye kumbukumbu Na. MNF/AD/37 aliyombwandikia Mkapa na nakala yake kusambazwa kwa wajumbe wa kamati kuu ccm na wenyeviti wote wa mikoa wa ccm katibu mtendaji wa mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF) Joseph Butiku anasema pamoja na mambo mengine " CCM sasa imeanza safari ya kuelekea kwenye kifo chake. imekumbatia jambo ovu, Rushwa, ambayo imeua viongozi wazuri wengi. Vyama vya siasa na serikali makini duniani.

CCM imeanza kushindwa kusema na kutetea haki na ukweli. Imeanza kuvumilia na kutetea ubaguzi. Imeanza kuwa CCM ya viongozi wafanyabiashara wasioonyesha nia thabiti ya kujali maadili ya chama chetu na taifa letu" alisema Batiku.

Hili ni tatizo la mwenyekiti maana yeye ndiye mwenye dhamana ya kutoa na huruhusu matumizi ya ushahidi usiokusanywa na vyombo vya taifa vilivyoteuliwa kufanya kazi hiyo.

Butiku anasema sasa wana CCM wengi na wananchi wengine wanao wasiwasi na nchi kununuliwa na wenye fedha kupita viongozi wa CCM.

Anauliza "Hivi kuna ushahidi fedha nyingi zinazotumika ktk uchaguzi huu zinatoka wapi? Ni za nani? Hao wanaozitoa wanayo malengo gani kwa Tanzania na Watanzanai?
 
Tuliwashauri Mwanahalisi Wawe Na Tovuti Au Blogu Yao Ndio Njia Rahisi Zaidi Je Kwa Wale Walio Nje Ya Nchi ?
 
Waungwana nilitabiri kuwa mzee JB anayo mengi dhidi ya Mkapa lakini ni wazi 2005 presidency run imeleta walemavu wengi ktk jamii yetu,tuwe na subira juu ya yote ipo siku Mzee JB atashuka kizimbani kuwapa waungwana ufafanuzi.

What is next waungwana?
 
Back
Top Bottom