Mkuu Field Marshall ES;
Heshima mbele; Kwa hili la Mh. Mkapa naomba nitofautiane na wewe na Niwe kwenye kambi yakina Gembe etc!!! Kama nilivyosema Katiba haijazuia afunguliwe kesi akiwa amefanya kosa kama yeye binafsi.
Hoja yangu imejikita kwenye Utengamano wa Taifa!
Nchi hii ambayo inasifika kwa utulivu... (yes, nimesema utulivu sijasema amani) ni miongoni mwa nchi ambazo ziko vulnerable sana na mambo fulani fulani... hivyo amani kupotea haraka sana sio jambo la ajabu hapa Tanzania. mifano ya vulnerabilities nyingi za nchi yetu ni issue ya Dini, Siasa etc. Wakati mambo kama Ukabila na Usehemu mtu anapotoka hayana nguvu ya kuporomosha taifa... isipokuwa tu... sehemu kama unaongelea Unguja na Pemba
Mifano ya Mataifa yaliyopata misukosuko kwa kumshitaki Rais mstaafu ni Zambia... etc.
Best Practices:
Majirani zetu walikuwa na uhalali mkubwa sana wa Kumshitaki Mh. Daniel Arap Moi, ambaye alikuwa na kashfa nzito sana tena sana... lakini hawakufanya hivyo kwa ajili ya mstakabali wa Taifa lao.
Kumshitaki Mh. Rais Mstaafu Mkapa... sio jambo rahisi, kumbuka wanadamu wana mioyo... na kumbuka Jamii yetu... inaweza kugeuzwa kimawazo kirahisi sana huenda kuliko jamii nyingi sana... rejea uchaguzi wa 2005(Imani waliyokuwa nayo Wananchi juu ya Mh. Kikwete); 1995(Imani waliyokuwa nayo wananchi juu ya Mzee wa Kiraracha);
Ikumbukwe kwamba Mh. Mkapa alikuwa na Record nzuri ya utendaji... ikumbukwe pia Marais hawa wawili wanatoka Dini tofauti, ikumbukwe akitokea Mchungaji au Sheikh... akapandikiza kwamba hili linafanyika kwa chuki... ya dini, waaumini wataitikia AMEN/AMIN. hapatakalika hapa nchini kwetu.
Mwisho tujadili namna ya kumfanya mtanzania afanye kazi angalau 4hours a day, ili ajitosheleze kwa chakula na aweze kuwa taxable... ana eventually awezekuwa pensionable.
Mwisho:
Ni jambo lililo wazi kwamba at least mlioko hapa kwenye jamvi hili mna uelewa mzuri zaidi kuliko waheshimiwa wengine ambao hata kompyuta hawajawahiiona... of course wapo wachache wazuri zaidi, sasa kama sisi tunataka kutoana macho,,, pamoja na kwamba hatuonani je... kwa watu mitaani itakuwa je? Matusi yaliyoandikwa already hapa kuhusu hili suala... maneno kama mpuuzi,etc... ni miongoni mwa viashiria kwamba hili si jambo rahisi.
Mungu Mbariki Mkapa apumzike vyema Rais Wetu Mstaafu!
Mungu Ibariki Tanzania.