Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Duh! ama kweli bado kuna watu wana mawazo ya mwaka 47!!!! Eti wabongo ni wivu na jazba tu!!! Labda ulinufaika kwa namna moja au nyingine na ufisadi wa fisadi Mkapa ndiyo maana unamkingia kifua kwa nguvu zote na hutaki kuona ushahidi chungu nzima uuliokuwepo dhidi ya fisadi Mkapa. Hakuna atakayeshut up, wewe ni nani katika Tanzania mpaka utuamrishe umma wa Watanzania tu shut up!!! Watu wengine bwana!!!! wanapenda kujipa madaraka wasiyokuwa nayo!!! Hajatwambia JK tushut up sembuse wewe!!!!.

Katika nchi yenye utawala bora hakuna yeyote yule ambaye anastahili kuwa juu ya sheria. Kama kafanya madhambi ambayo yameliingizia hasara Taifa kubwa basi ushahidi ukusanywe dhidi yake na kisha kufikishwa kwa pilato na akionekana ana hatia basi asote lupango kwa miaka mingi tu na kufilisiwa pia afilisiwe. Hili litarudisha imani ya Watanzania katika serikali yao. Mwambie fisadi hana pakutorokea maana za mwizi ni arobaini.

Bubu usiwe na jazba, I mean ushaidi unao wewe mfukoni. Subiri mpaka hapa utakapokuwa ushahidi wa kimahakama wa kuweza kumweka hatiani. Zingine zote unaongea ni porojo kama porojo zingine zozote mitaani. Ninaposema shut-up nina maana hii. Siyo usiseme. Hapana. Ila as long as ushahidi wako unao mfukoni na haujawa table kwa Feleshi kama unafaa kumtia hatiani, wewe tu.. Kuongea ruksa. Kila mtu anaweza ongea bila kikomo.

Ndiyo hivyo tu bwana bubu. Hata kama hutaki.
 
Mwanjelwa,
Yote uliyoaandika kuhusu JK ni mapungufu ya uongozi wake..Kama vile Nyerere na Ujamaa.. Lakini Mkapa katuibia makusudi nje ya mfumo wa kiuchimi ama kisiasa akijua hatuwezi kumfanya kitu kwa sababu sisi ma Mbumbumbu na yeye ni rais...
Na kwa sababu hiyo kuna kiola haki ya kumfikisha mahakamani tena basi ana bahati sana kayafanya haya Tanzania ingekuwa Liberia yangemkuta ya Samuel Doe!..
 
Hata wewe kesho naweza kukutuhumu kwa chochote kile kama nikiwa informed wrongly! Tuhuma haithibitishi kuwa una makosa. Mpaka itapotolewa hukumu kuwa unayo. Kwa hiyo hata kushitaki mtu siyo kwamba ana makosa. Mpaka mahakama iseme anayo. Hapa ndipo tunapishana na wengi humu. Wamekomaa sana kuwa Mkapa ana makosa. Sheria inasemaje? Mpaka hapo sheria itakapokuwa ready kuthibitisha kuwa una makosa ndiyo mtu unaweza kuhemka kama jamaa hapo juu alivyokuja juu! Hakuna sababu ya BP. Tuongee tu kama waongeaji wengine na tusiwe na uhakika kama vile tunapuliza saxaphone humu kila mtu asikilize.

Hizi tuhuma tuhuma. Mara nyingi tuhuma ndizo zinafanya watu wanapigana mishare bila sababu mitaani.
 
Mwanjelwa,
Sheria ya mahakamani haihusiani na ukweli uliopo, wewe umetumia tuhuma kuvuta hoja yako lakini unashindwa kutazama upande wa pili.
Sasa nakuuliza ikiwa wewe umeshuhudia mimi nikua kwa makusidi kabisa aidha kuingia benki na kuua watu utasema mimi sio muuaji hadi pale sheria itakapo toa uamuzi!.Hata huko mahakamani wewe kama shahidi utaulizwa nani aliyeua! Je, unamwona hapa mahakamani!..unaweza kum point out... na kadhalika.

Mkuu wangu hapa JF sio mahakama ndogo isipokuwa ni kijiwe cha wananchi wanaojadili yale yaliyoajiri maadam facts zipo huko mahakamani ni process tu ya haki kutumika badala ya kila mtu kuchukua sheria mkononi..Ni utaratibu uliokubalika kuweza kusimamisha rule of law lakini haina maana kila lisemwalo nje ya mahakama ni tuhuma.
 
Bubu usiwe na jazba, I mean ushaidi unao wewe mfukoni. Subiri mpaka hapa utakapokuwa ushahidi wa kimahakama wa kuweza kumweka hatiani. Zingine zote unaongea ni porojo kama porojo zingine zozote mitaani. Ninaposema shut-up nina maana hii. Siyo usiseme. Hapana. Ila as long as ushahidi wako unao mfukoni na haujawa table kwa Feleshi kama unafaa kumtia hatiani, wewe tu.. Kuongea ruksa. Kila mtu anaweza ongea bila kikomo.

Ndiyo hivyo tu bwana bubu. Hata kama hutaki.

Kwa taarifa yako mimi sina jazba yoyote ile ila napenda kuona haki inatendeka dhidi ya mafisadi wote akiwamo Mkapa kwa kujipatia utajiri Mkubwa kwa njia za haramu kupitia wavuja jasho wa Tanzania. Mkapa miaka michache iliyopita hakuwa na utajiri aliokuwa nao sasa hivi huu ni utajiri alioupata kwa njia za haramu na pia kuna ushahidi wa kutosha kwamba alipojiuzia Kiwira yeye na Yona walifanya hivyo kwa kutumia nyadhifa zao na njia za haramu. Mkapa kahusika kwa karibu mno na kashfa ya ununuzi wa Rada pamoja na Chenge na Mramba, ununuzi wa ndege ya Rais, magari ya jeshi na helicopters. Amelitia hasara Taifa la Watanzania ya $200 millioni kwa uamuzi wake wa kuuza nyumba za serikali.

Hakuna Mtanzania yeyote yule ambaye ana wivu dhidi ya Mkapa. Wote tunafahamu fika kwamba Tanzania hatuna tabaka mbili au zaidi mbele ya sheria. Unapotenda maovu basi kuna kila sababu ya wewe kuchunguzwa dhidi ya tuhuma za maovu yako, na kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yako basi bila kujali wadhifa wako inabidi upelekwe kwa pilato ukajitetee.

Na kwa taarifa yako kashfa dhidi ya Mkapa si porojo za mitaani. Ukiona swala linazungumziwa na wanasiasa waliopita na waliopo madarakani pamoja na wanasheria wanaoheshimika katika jamii ya Tanzania karibu kila siku iendayo kwa Mungu, basi ujue hizo si porojo tena maana hata Spika ameshasema swala hili ataliruhusu lijadiliwe bungeni. Sikumbuki ni lini ilikuwa mara ya mwisho kwa porojo za mitaani kujadiliwa bungeni.

Mwambie Mkapa za Mwizi arobaini, na za kwake zimewadia. Na sheria ni msumeno kama alidhani ataiba kwa kutumia wadhifa wake na kuachwa huru akipeta uraiani basi mwambie yeye ARIE TU!
 
Mwanjelwa,
Sheria ya mahakamani haihusiani na ukweli uliopo, wewe umetumia tuhuma kuvuta hoja yako lakini unashindwa kutazama upande wa pili.
Sasa nakuuliza ikiwa wewe umeshuhudia mimi nikua kwa makusidi kabisa aidha kuingia benki na kuua watu utasema mimi sio muuaji hadi pale sheria itakapo toa uamuzi!.
Mkuu wangu hapa JF sio mahakama ndogo isipokuwa ni kijiwe cha wananchi wanaojadili yale yaliyoajiri maadam facts zipo huko mahakamani ni process tu ya haki kutumika badala ya kila mtu kuchukua sheria mkononi..Ni utaratibu uliokubalika kuweza kusimamisha rule of law lakini haina maana kila lisemwalo nje ya mahakama ni tuhuma.

Yes! hata kama nikikuua na watu kibao wanaona hapo!. Siwezi kwenda moja kwa moja kwa bwana nyonga nyonga. Ni Mpaka mahakama iseme kuwa nina hatia. Naweza kushinda kesi mahakamani!. Imetokea mara nyingi sana bwana Mkandara.
Lakini pia JF sidhani ni kijiwe cha namna hiyo?. Mimi najua ni kijiwe cha facts na deep analysis kwa watu wanafuatilia vitu vya vina na siyo kwa feeling, tena kwa magazeti au mitaani. Nina amani na hii siku zote hivyo.
 
Kwa taarifa yako mimi sina jazba yoyote ile ila napenda kuona haki inatendeka dhidi ya mafisadi wote akiwamo Mkapa kwa kujipatia utajiri Mkubwa kwa njia za haramu kupitia wavuja jasho wa Tanzania. Mkapa miaka michache iliyopita hakuwa na utajiri aliokuwa nao sasa hivi huu ni utajiri alioupata kwa njia za haramu na pia kuna ushahidi wa kutosha kwamba alipojiuzia Kiwira yeye na Yona walifanya hivyo kwa kutumia nyadhifa zao na njia za haramu. Mkapa kahusika kwa karibu mno na kashfa ya ununuzi wa Rada pamoja na Chenge na Mramba, ununuzi wa ndege ya Rais, magari ya jeshi na helicopters. Amelitia hasara Taifa la Watanzania ya $200 millioni kwa uamuzi wake wa kuuza nyumba za serikali.

Hakuna Mtanzania yeyote yule ambaye ana wivu dhidi ya Mkapa. Wote tunafahamu fika kwamba Tanzania hatuna tabaka mbili au zaidi mbele ya sheria. Unapotenda maovu basi kuna kila sababu ya wewe kuchunguzwa dhidi ya tuhuma za maovu yako, na kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yako basi bila kujali wadhifa wako inabidi upelekwe kwa pilato ukajitetee.

Na kwa taarifa yako kashfa dhidi ya Mkapa si porojo za mitaani. Ukiona swala linazungumziwa na wanasiasa waliopita na waliopo madarakani pamoja na wanasheria wanaoheshimika katika jamii ya Tanzania karibu kila siku iendayo kwa Mungu, basi ujue hizo si porojo tena. Mwambie Mkapa za Mwizi arobaini, na za kwake zimewadia. Na sheria ni msumeno kama alidhani ataiba kwa kutumia wadhifa wake na kuachwa huru akipeta uraiani basi mwambie yeye ARIE TU!

hahahahahahah! Kazi kweli kweli kama unategemea ear says za wanasiasa na wanasheria ndugu yangu. Inatakiwa personal analysis na indepth follow-up kwa hivi vitu. Makini ya hali ya juu sana.
Ok. Ngoja nikuache hapo.
 
Mkuu utakuwa unakosea sana kuhusu suala la muheshimiwa kufanya biashara akiwa Ikulu. Yule bwana hakuchaguliwa kwenda ikulu kuwa CEO wa biashara zake binafsi; biashara aliyotakiwa kwenda kufanya pale ni kuwapatia faida wale waliompeleka ambao ni wananchi. Kama alikuwa na haja sana ya kuwa mjasirimali, basi angeendelea tu na biashara zake bila ya kuja kwetu sisi kutaka kura.
Hatukumuweka pale kama BWM, alikuwa pale kama Rais wa jamhuri ya Muungano wa tanzania, na kama ukipitia katiba ya nchi, inaeleza vizuri tu ni majukumu gani rais wa nchi anatakiwa afanye, biashara binafsi halimo, hivyo kila biashara ya kujinufaisha kama Benjamin Mkapa ilikuwa ni batili....Just a common sense tu hapo.

Kweli bwana... kifungu gani cha sheria kilimzuia kufanya hivyo?

Mh. Ali Hassan Mwinyi alivyokuwa ikulu aliendelea na kuwa na mashamba yake...

Mh. Julius K. Nyerere Marehemu, alikuwa na mashamba yake hata alipokuwa ikulu... swali hizo hazikuwa kazi binafsi kwa kizungu business...

Mpaka sasa muda mwingi tunaongelea ana kinga, hana kinga... lakini anatakiwa ashitakiwe kwa lipi?

Pili; Kwani kesi lazima aipeleke Felesi, Huyo Dr. Slaa si anaweza peleka kesi mahakamani?

Kwa nini tunapenda kuongea sana?
 
Kasheshe,
Kila mtanzania anaruhusiwa au anaweza kuwa na shamba hata yule mfanyakazi wa Posta, machinga au dereva wa daladala.. Lakini sio kila mtu anaweza kufungua ofisi ya biashara Ikulu hata Nyerere hakuweza isipokuwa Mkapa tu.
 
Mkuu Field Marshall ES;

Heshima mbele; Kwa hili la Mh. Mkapa naomba nitofautiane na wewe na Niwe kwenye kambi yakina Gembe etc!!! Kama nilivyosema Katiba haijazuia afunguliwe kesi akiwa amefanya kosa kama yeye binafsi.

Hoja yangu imejikita kwenye Utengamano wa Taifa!

Nchi hii ambayo inasifika kwa utulivu... (yes, nimesema utulivu sijasema amani) ni miongoni mwa nchi ambazo ziko vulnerable sana na mambo fulani fulani... hivyo amani kupotea haraka sana sio jambo la ajabu hapa Tanzania. mifano ya vulnerabilities nyingi za nchi yetu ni issue ya Dini, Siasa etc. Wakati mambo kama Ukabila na Usehemu mtu anapotoka hayana nguvu ya kuporomosha taifa... isipokuwa tu... sehemu kama unaongelea Unguja na Pemba

Mifano ya Mataifa yaliyopata misukosuko kwa kumshitaki Rais mstaafu ni Zambia... etc.

Best Practices:
Majirani zetu walikuwa na uhalali mkubwa sana wa Kumshitaki Mh. Daniel Arap Moi, ambaye alikuwa na kashfa nzito sana tena sana... lakini hawakufanya hivyo kwa ajili ya mstakabali wa Taifa lao.

Kumshitaki Mh. Rais Mstaafu Mkapa... sio jambo rahisi, kumbuka wanadamu wana mioyo... na kumbuka Jamii yetu... inaweza kugeuzwa kimawazo kirahisi sana huenda kuliko jamii nyingi sana... rejea uchaguzi wa 2005(Imani waliyokuwa nayo Wananchi juu ya Mh. Kikwete); 1995(Imani waliyokuwa nayo wananchi juu ya Mzee wa Kiraracha);

Ikumbukwe kwamba Mh. Mkapa alikuwa na Record nzuri ya utendaji... ikumbukwe pia Marais hawa wawili wanatoka Dini tofauti, ikumbukwe akitokea Mchungaji au Sheikh... akapandikiza kwamba hili linafanyika kwa chuki... ya dini, waaumini wataitikia AMEN/AMIN. hapatakalika hapa nchini kwetu.

Mwisho tujadili namna ya kumfanya mtanzania afanye kazi angalau 4hours a day, ili ajitosheleze kwa chakula na aweze kuwa taxable... ana eventually awezekuwa pensionable.

Mwisho:
Ni jambo lililo wazi kwamba at least mlioko hapa kwenye jamvi hili mna uelewa mzuri zaidi kuliko waheshimiwa wengine ambao hata kompyuta hawajawahiiona... of course wapo wachache wazuri zaidi, sasa kama sisi tunataka kutoana macho,,, pamoja na kwamba hatuonani je... kwa watu mitaani itakuwa je? Matusi yaliyoandikwa already hapa kuhusu hili suala... maneno kama mpuuzi,etc... ni miongoni mwa viashiria kwamba hili si jambo rahisi.

Mungu Mbariki Mkapa apumzike vyema Rais Wetu Mstaafu!
Mungu Ibariki Tanzania.

Mkuu Kasheshe,

- Heshima mbele mkuu, eti huu utengamano unaousema Mkapa hakuuona alipoamuru wananchi wa Pemba wauliwe kwa risasi kwa sababu ya maandamano tu? Na vipi alipoamuru wananchi pale Mwembechai wapigwe na FFU bila sababu ilikuwa ni kuboresha huu utengamano wa taifa kama unavyousema au?

- Record yake ya kazi kama ni hoja mbele ya sheria, basi itamsafisha mbele ya sheria, otherwise kama hoja yako inasimama basi taifa zima lipitie record za wafungwa wote walioko jela zetu kuona kama waliwahi kulifanyia taifa mema na waachiwe maramoja, maana Mkapa amelifanyia mema mengi sana taifa hili kwa hiyo kuendeleza utengamano asiguswe na sheria, what a joke idea! Mkuu Kashehse lazima kuna mtu ameiba code yako!
 
hahahahahahah! Kazi kweli kweli kama unategemea ear says za wanasiasa na wanasheria ndugu yangu. Inatakiwa personal analysis na indepth follow-up kwa hivi vitu. Makini ya hali ya juu sana.
Ok. Ngoja nikuache hapo.

'Ear says' ndo nini...LOL! Mimi nina uwezo pia wa kuchanganua mambo kwa kina. Si unakumbuka tuliambiwa Mafisadi wa EPA wakishtakiwa nchi itawaka moto na kushindwa kuiongoza. Nadhani umejionea mwenyewe mafisadi wa EPA na pia vingunge waliowahi kushika nyadhifa za juu ndani ya awamu mbali mbali za serikali za Tanzania kufikishwa mahakamani na nchi haijawaka moto wala haitawaka moto, bado wengine wanakuja na Mkapa atakuwa miongoni mwao. Kapiga chini kama alidhani ataogopwa na kuchwa akitafuna mali alizotuibia Watanzania.
 
1.
Hapo bado utata. Uporaji ni kufanyeje? Kujiuzia Kiwira kwa bei ya chini? nini comments zako kuhusu TBL, NBC etc? Angekuwa yeye kanunua angekuwa amepora, au siyo! Yeye kama raia wa nchi, kama ulivyo wewe na mwingine, anao uhuru wa kufanya atakacho ikiwemo biashara. Sheria haimzuii kufanya biashara. Na wale wanaosema alifanya akiwa Ikulu, alitakiwa aende wapi ndiyo akafanye?

- Uporaji wa mali za wananchi ni pamoja na kujiuzia Kiwira kwa bei poa, kama rais wa jamhuri huwezi kujiuzia mradi wa taifa kwa shillingi millioni 700 tu, mradi ambao unaingiza mamilioni ya dola za kimarekani kama faida, huu ni uporaji tena wizi wa mchana.

- TBL, NBC zimeuzwa kwa bei poa, chini ya uwaziri wa Yona, Mramba, na Idd Simba, hapa lazima uongeze Sumaye na Mkapa mwenyewe na yule mkulu wa ubinafsishaji wote wamehusika na kula mgawo. Sheria haimzuii kufanya biashara kama mwananchi wa kawaida, lakini inamzuia kupora mali za wananchi akiwa rais, hivi wananchi wengine mnakuwa mmerogwa nini? Katika urais wa Mkapa wa ten years tu ameweza kukusanya mali za kuwekea rehani mkopo wa ANBEN enough mpaka kuweza ku-secure mkopo wa dola laki tano mkuu uko serious au huelewi vizuri aliyoyafanya Mkapa Ikulu?

- Alitakiwa akafanyie nje ya Ikulu, taifa tumeamua kwamba rais wa jamhuri tutamtunza mpaka mwisho wa maisha yake ili kumuepusha na tamaa kama hizi za fisi, I mean tamaa gani hii mpaka unajinyakulia miradi ya taifa wewe mwenyewe rais wa Jamhuri? Sasa Yona na Mramba wanafanya nini Kisutu kama Mkapa aliyekuwa akiwatuma tunamuacha? Hivi unahitaji kuwa Doctor kama Kikwete kuelewa hili?

2.
Hayo mengine ya kujichanganya kwangu siyo issue ya kubishana. Suala ambalo tunakubaliana mimi na wewe ni kwamba sheria lazima ichukue mkondo wake. Lakini kwa nini sheria iende kwa Mkapa peke yake na isiende kwa Kikwete wakati na yeye alitajwa kwenye list of shame?

- Hatusemi sheria iishie kwa Mkapa, tunasema hivi hata kama rais wa sasa au zamani atakutwa amevunja sheria zetu wote waende Kisutu, tutachyambua huko huko mbele kwa mbele, tunasema sheria ichukue mkondo hata kama Kikwete anahusika, yasemwe wazi na kila mmoja abebe mzigo wake au mshaurini Mkapa akifika Kisutu, aseme kama alishirikiana na Kikwete.

3.
Hapo ndipo nilipokuja na maoni kwamba kwa sababu katiba yetu ni mbovu na viongozi wana madaraka makubwa tunajenga kautamaduni kakujipendekeza. Fikiria watu wanataka kwenda bungeni kumtungia sheria mtu mmoja yaani Mkapa huoni kama wanasiasa wanatufanya kama sisi hamnazo. Waende bungeni watunge katiba ambayo itaondoa kinga kwa marais wanapovurunda. Mbona Clinton alichunguzwa wakati ni rais. Kwa nini tusubiri mpaka rais asitaafu ndiyo tuanze kujifanya tunataka utawala bora. Utawala bora uwe wakati tunapoongozwa maana hicho ndicho kipindi wanachotuibia. Hawatuibii wanapokuwa wamestaafu. Kwa hiyo badala ya kufikiria kukamata wezi lazima tutunge katiba ambayo itafanya wezi wasiibe.

- Hapa mkuu umechanganya ishus nyingi sana, kwanza unasema mapungufu ya katiba yetu, ukweli ni kwamba kwenye suala la kumfikisha Mkapa kwenye sheria zetu za jamhuri, at this point tatizo sio upungufu wa katiba isipokuwa ni interpretation tu ya sheria tuliyonayo tayari, ambayo pia wala sio ishu ila inasubiriwa amri ya rais tu.

- Hakuna mtu anayetaka kwenda bungeni kumtungia sheria Mkapa, sheria ipo tayari ila watu wanataka kwenda bungeni kufanya wajibu wao wa kazi ya ubunge, ambayo ni pamoja na ku-interprate sheria inapobidi as of this case. Kwenye Richimonduli tuliambiwa maneno kama yako na Takukuru, lakini tukafuata katiba na kuwakabidhi wabunge you know the rest of the story.

- Ya Mkapa kupora mali za wananchi hatukuyajua mpaka alipotoka Ikulu, kama vile ya EPA yote tumeyajua baada ya yeye kutoka Ikulu, lakini tungeyajua mapema basi angekiona cha moto kama tunachompa sasa, huyu Mkapa tunaye mpaka kieleweke, halafu it does not matter kuhusu time cha muhimu ni tumemshitukia kabla hajaenda mbali.

Ndugu zangu wananchi wengine naomba kuwaambia hivi wakati ni huu, rais wa sasa huwa ana-respond kunapokuwa na strong political pressure kutoka kwetu wananchi, ndio maana majuzi amemwambia Makamba kwamba hataki kumsikia Mbeya kwenye uchaguzi, tena point blank bila kumung'unya maneno wala diplomasia ni kutokana na pressure ya wabunge wa CCM na wananchi wa Mbeya kwamba hawataki not only Makamba bali viongozi wote mafisadi wasiguse huko, sasa amemuomba jm na kundi la viongozi wasio mafisadi kwenda huko na ni kweli wanaenda akiwemo kijana shujaa Nape na Kinana, my point ni kwamba hawa mafisadi wameshikwa pabaya sana na walahi tukifanya mchezo tukawakosa sasa basi hatutawapata tena, Kikwete ana respond only kukiwa na pressure ya nguvu kwa hiyo tuendelee ku-press tu mpaka kieleweke!

Mkapa hawezi kulisambaratisha taifa letu kwa kutakiwa kujibu mbele ya sheria jinsi alivyopora mali za wananchi na kujilimbikizia utajiri usio mfano kwa kipindi kifupi cha miaka kumi tu ninasema no way! Na likisambatratika then let it be on ourbloods, lakini huwezi wafikisha Mramba, Yona na Mgonja Kisutu bila baba yao Mkapa ni kuwaonea bure!

Mungu Aibariki Tanzania!
 
Hapo bado utata. Uporaji ni kufanyeje? Kujiuzia Kiwira kwa bei ya chini? nini comments zako kuhusu TBL, NBC etc? Angekuwa yeye kanunua angekuwa amepora, au siyo! Yeye kama raia wa nchi, kama ulivyo wewe na mwingine, anao uhuru wa kufanya atakacho ikiwemo biashara. Sheria haimzuii kufanya biashara. Na wale wanaosema alifanya akiwa Ikulu, alitakiwa aende wapi ndiyo akafanye?

Mkuu kuna kitu kinaitwa Conflict of Interest. Pili sio kweli kwamba Rais ni kama raia mwingine yeyote na ana uhuru wa kufanya chochote atakacho ikiwemo biashara. Ukiwa ndani ya Ofisi ya Raisi kama kiongozi wa nchi anayezijua siri nzito za nchi...hauruhusiwi kujishughulisha na shughuli zingine zozote zile ambazo zitakuwa za kukupa wewe (Rais) manufaa kiuchumi. Unaweza kuwa mfanya biashara kabla ya kuwa Rais ama baada ya kipindi chako lakini sio wakati wa utawala wako. Thats a big no, na sidhani kama imeandikwa kwenye katiba yetu.
 
Mkuu FM ahsante sana. Nimekuvulia kofia. Huyu Mkapa asipopelekwa mbele ya sheria hapo ndio tutakuwa tumeliweka taifa rehani. Hakuna uhakika wa nini kitatokea mbeleni. Mnakumbuka hata mwanasheria wa Chenge (yule Mmarekani) aliwahi kutishia kwamba Chenge akipelekwa mahakamani watamwaga siri zote za serikali? Ilikuwa ni kutisha toto kwamba watamtaja Mkapa wakijua kwamba kwa sababu ya nguvu alizonazo basi mafisadi wote wa wakati wake watapona.

Mkapa akipelekwa kisutu hakutakuwa tena na mtu wa kututishia TZ. Tutakuwa na uhakika hata baada ya Kikwete kumaliza ngwe yake nchi haiwezi kuchukuliwa na mafisadi. Mkapa akiwa huru ninawahakikishieni kiongozi atakayefuata atakuwa kibaraka wake kutoka kundi la mafisadi na hata uongozi wa Kikwete utayumba sana. Kumbukeni jinsi alivyokwamishwa kwenye lile suala la muafaka wa Zanzibar? Kwa sasa hivi nguvu na matumaini ya mafisadi yako kwa Mkapa. Akishughulikiwa kila kitu kitakuwa swafi. Hata muafaka Zanzibar utapatikana kirahisi sana! Trust me!
 
I would like to get an explanation from the Third Republic on why after privatizing the once 'mali ya umma' none of us get paid back since we were all shareholders in the public corporation. Where is the money? What did it do for Tanzanians.

This could probably be one good charge against BM -that is, swindling us from the proceeds of privatisation in Tanzania.
 
1. Mkapa akipelekwa kisutu hakutakuwa tena na mtu wa kututishia TZ. Tutakuwa na uhakika hata baada ya Kikwete kumaliza ngwe yake nchi haiwezi kuchukuliwa na mafisadi.

2. Mkapa akiwa huru ninawahakikishieni kiongozi atakayefuata atakuwa kibaraka wake kutoka kundi la mafisadi na hata uongozi wa Kikwete utayumba sana.

3. Kumbukeni jinsi alivyokwamishwa kwenye lile suala la muafaka wa Zanzibar? Kwa sasa hivi nguvu na matumaini ya mafisadi yako kwa Mkapa. Akishughulikiwa kila kitu kitakuwa swafi.

4. Hata muafaka Zanzibar utapatikana kirahisi sana! Trust me!

- Mkuu Nurujamii, heshima yako sana haya maneno yako yakiweza kuongewa na wananchi millioni moja tu wa taifa letu, ujue basi tutalikomboa hili taifa kwa muda mfupi sana ni lazima tuendelee ku-press mbele zaidi na tukatae kudanganywa,

- wewe look here wananchi wa Mbeya tu wamekataa viongozi mafisadi huko kwenye uchaguzi na rais amekubali na kuwasikiliza, sasa kwa nini tusikaze kamba kwenye taifa pia wote watinge Kisutu?

Halafu pia tuondokane na hizi dhana pootofu kwamba kwenda Kisutu ni kufungwa au kuwa na hatia, hapana innocent ni until proven guilty lakini symbolically na results, ni heshima kwa utawala wa sheria, that is all!
 
taifa haliwezi kusambaratika kwa kufuatilia wezi na kurudisha mali walizoiba,wizi kama huu wa mkapa ndio unaosababisha wakati mwingine jeshi kuchukua nchi kama serikali iliopo haifuatilii wezi na wahujumu wa mali za taifa.mkapa alidhani baada ya kumzika mwalimu nyerere kusingekuwa na kikwazo kwa lolote atakalofanya.angalia alianza kwa kuweka lowassa(kiongozi wa mafisadi) kwenye baraza la mawaziri wakati nyerere alikwisha mwambia hafai.ule uadilifu aliokuwa nao kabla ya mwalimu akautumia kama kivuli cha kujifichia wakati anaiba,wajanja wote wa ufisadi kama mramba,yona,chenge,lowassa,rostam,megji,balali,hosea,mahita na wengine aliwaweka kwenye nafasi nzuri za kuweza kuiba kivyao ili wasiweze kumfuatilia,lakini mungu amewafichua wote sasa wasishughulikiwe warudishe mali walizoiba?lazima warudishe mali walizoiba hatakama siyo sasa lakini siku ipo watakapopatikana viongozi wenye uchungu hasa na nchi hii inayofilisiwa mchana kweupe.wezi hawa mishahara na marupurupu yao wakiwa kazini yanajulikana,sasa je mali walizonazo zinalingana na hivyo vipato vyao?
edward amerejea ktk baraza la mawaziri mwaka 1997 akiwa ktk ofisi ya makamu wa rais -mazingira, mwalimu alikuwepo hai. Punguza jazba mkuu maana unaanza kutuongopea hata sisi wenzako sasa
 
Mheshimiwa Dr. Slaa, endelea hivyo hivyo nasi tuko nyuma yako. Dr.Slaa anasema kuna wasomi wanaozungumza..., hapa Dr.Slaa anatupatia changamoto kuwa wasomi wengi sana wa nchi wameridhika na "eti digrii first class, up second na ...mengineyo", ambao wanashindwa kujiendeleza na hasa kuchambua mambo kiyakinifu. Mhe.Dr.Slaa endelea dozi.
 
1.

- Uporaji wa mali za wananchi ni pamoja na kujiuzia Kiwira kwa bei poa, kama rais wa jamhuri huwezi kujiuzia mradi wa taifa kwa shillingi millioni 700 tu, mradi ambao unaingiza mamilioni ya dola za kimarekani kama faida, huu ni uporaji tena wizi wa mchana.

- TBL, NBC zimeuzwa kwa bei poa, chini ya uwaziri wa Yona, Mramba, na Idd Simba, hapa lazima uongeze Sumaye na Mkapa mwenyewe na yule mkulu wa ubinafsishaji wote wamehusika na kula mgawo. Sheria haimzuii kufanya biashara kama mwananchi wa kawaida, lakini inamzuia kupora mali za wananchi akiwa rais, hivi wananchi wengine mnakuwa mmerogwa nini? Katika urais wa Mkapa wa ten years tu ameweza kukusanya mali za kuwekea rehani mkopo wa ANBEN enough mpaka kuweza ku-secure mkopo wa dola laki tano mkuu uko serious au huelewi vizuri aliyoyafanya Mkapa Ikulu?

- Alitakiwa akafanyie nje ya Ikulu, taifa tumeamua kwamba rais wa jamhuri tutamtunza mpaka mwisho wa maisha yake ili kumuepusha na tamaa kama hizi za fisi, I mean tamaa gani hii mpaka unajinyakulia miradi ya taifa wewe mwenyewe rais wa Jamhuri? Sasa Yona na Mramba wanafanya nini Kisutu kama Mkapa aliyekuwa akiwatuma tunamuacha? Hivi unahitaji kuwa Doctor kama Kikwete kuelewa hili?

2.

- Hatusemi sheria iishie kwa Mkapa, tunasema hivi hata kama rais wa sasa au zamani atakutwa amevunja sheria zetu wote waende Kisutu, tutachyambua huko huko mbele kwa mbele, tunasema sheria ichukue mkondo hata kama Kikwete anahusika, yasemwe wazi na kila mmoja abebe mzigo wake au mshaurini Mkapa akifika Kisutu, aseme kama alishirikiana na Kikwete.

3.

- Hapa mkuu umechanganya ishus nyingi sana, kwanza unasema mapungufu ya katiba yetu, ukweli ni kwamba kwenye suala la kumfikisha Mkapa kwenye sheria zetu za jamhuri, at this point tatizo sio upungufu wa katiba isipokuwa ni interpretation tu ya sheria tuliyonayo tayari, ambayo pia wala sio ishu ila inasubiriwa amri ya rais tu.

- Hakuna mtu anayetaka kwenda bungeni kumtungia sheria Mkapa, sheria ipo tayari ila watu wanataka kwenda bungeni kufanya wajibu wao wa kazi ya ubunge, ambayo ni pamoja na ku-interprate sheria inapobidi as of this case. Kwenye Richimonduli tuliambiwa maneno kama yako na Takukuru, lakini tukafuata katiba na kuwakabidhi wabunge you know the rest of the story.

- Ya Mkapa kupora mali za wananchi hatukuyajua mpaka alipotoka Ikulu, kama vile ya EPA yote tumeyajua baada ya yeye kutoka Ikulu, lakini tungeyajua mapema basi angekiona cha moto kama tunachompa sasa, huyu Mkapa tunaye mpaka kieleweke, halafu it does not matter kuhusu time cha muhimu ni tumemshitukia kabla hajaenda mbali.

Ndugu zangu wananchi wengine naomba kuwaambia hivi wakati ni huu, rais wa sasa huwa ana-respond kunapokuwa na strong political pressure kutoka kwetu wananchi, ndio maana majuzi amemwambia Makamba kwamba hataki kumsikia Mbeya kwenye uchaguzi, tena point blank bila kumung'unya maneno wala diplomasia ni kutokana na pressure ya wabunge wa CCM na wananchi wa Mbeya kwamba hawataki not only Makamba bali viongozi wote mafisadi wasiguse huko, sasa amemuomba jm na kundi la viongozi wasio mafisadi kwenda huko na ni kweli wanaenda akiwemo kijana shujaa Nape na Kinana, my point ni kwamba hawa mafisadi wameshikwa pabaya sana na walahi tukifanya mchezo tukawakosa sasa basi hatutawapata tena, Kikwete ana respond only kukiwa na pressure ya nguvu kwa hiyo tuendelee ku-press tu mpaka kieleweke!

Mkapa hawezi kulisambaratisha taifa letu kwa kutakiwa kujibu mbele ya sheria jinsi alivyopora mali za wananchi na kujilimbikizia utajiri usio mfano kwa kipindi kifupi cha miaka kumi tu ninasema no way! Na likisambatratika then let it be on ourbloods, lakini huwezi wafikisha Mramba, Yona na Mgonja Kisutu bila baba yao Mkapa ni kuwaonea bure!

Mungu Aibariki Tanzania!

MKUU WA MEDANI TUSAIDIE KTK HAYA UNAYOYAHUBIRI HAPA KTK UWANJA WA SHERIA ZAIDI, MAANA NINAONA MSUKUMO WA MHEMUKO WA ROHO TUPU HAPA, TUAMBIENI HAPA JAMVINI, KUWA SHERIA NA... NA ADHABU NI FULANI DHIDI YA MUHUSIKA......, KASHESHE NA GEMBE WAMETHUBUTU KUWA WAKWELI NA KUMWAGA FACT HADHARANI, NIMEJITAHIDI SANA KUWATAKA NINYI NDUGU ZANGU HUMU KUIANGALIA SHERIA ZAIDI NA TUONE ANABANWA NA SHERIA IPI? HAKUNA MAJIBU WALA VIAMBATANISHO HUMU, IKULU NI OFISI NA MAKAZI YA RAIS, KAMA MTUMISHI ANARUHUSIWA KUKOPA BENKI KWA SABABU ZA BIASHARA WHY NOT RAIS AMBAYE NAYE NI MTUMISHI?!!! KWA HIYO MLITAKA YEYE AWATAJIRISHE NINYI TU NA YEYE ATEGEMEE PENSHENI YA URAIS, JE YEYE HANA FAMILIA NA NDUGU? NAO WAKO ENTITTLED KTK PENSHENI YA RAIS MPAKA KUFA KWAKE? HAYA NI YA KUJIULIZA KIUBINADAMU TU NAYO HAYAHITAJI pHD YA FALSAFA. MLICHOTAKA JAMII IJUE NA KUFANYA VIA IPP MEDIA SASA KINAENDA MWISHO WAKUU, SILAA ANAJUA MCHEZO ANAOUCHEZA DHIDI YA CCM NA SI UCHUNGU WAKE KWA TZ, NDANI YETU WANA CCM TUNAJUA UDHAIFU WETU, VIONGOZI WETU NAO PIA WANAJUA MAPUNGUFU YAO ILA JF NI MAHALA PA KUPUMZISHA HISIA NA KUONGEA KWELI, NASHAURI SANA WAKUU TUNAOWAHESHIMU MSIJIINGIZE KTK HEKAYA ZA ABUNUWASI NA HADITHI ZA ALFU ULELAULELA.

SUBIRINI HUKO BUNGENI JANUARI-FEBRUARI 2009, WENYE MASIKIO NA WASIKIE NA WENYE KUONA WAONE. FEBRUARI 2008 ILIVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI NA KUMPOTEZA THE PREMIER EDWARD LOWASA, JE FEBRUARI 2009 INA NINI KWA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA? TUPO TUNASUBIRI KUONA JEURI YA SAMWEL SITTA, KIMARO, ZAMBI, SLAA NA WENGINEO....

MKUU WA MEDANI NAKUSAHIHISHA KUWA TBL ILIUZWA AWAMU YA PILI NA SI YA TATU
 
Hongera sana DK. Slaa kwa jinsi unavyopambana sana na ufisadi nchini, hakika wewe ni mzalendo na shujaa wa taifa hili, hongera sana.

Lakini sasa kwa hili la kumshtaki Mkapa bila bunge kumondolea kinga ya mashtaka HALIWEZEKANI.

Ukisoma vizuri Ibara ya 46 ya katiba yetu ya Tanzania utaona kwamba rais amepewa kinga kubwa saaana ambapo anaweza kufanya jambo lolote.

"46.-(1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika
madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku
kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake
mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.

(2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka
yake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua
mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa
kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au
baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku
thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais
atapewa au ametumiwa kwamba taarifa ya madai kwa maandishi
kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria
iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo
kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina
lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa
analodai.
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais
kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku
kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya
kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye
kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais
kwa mujibu wa Katiba hii.

_________________________________________________________________
46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani
endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa
mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
inadaiwa kwamba Rais-
Sheria ya …. (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja
Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili
yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa
yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais
wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya
namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja
kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu
kama-
(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa
mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku
thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo
inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa
aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati
Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze
mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa
iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa
masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja
yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja
kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka
Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya
hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na
kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua
theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya
wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.
(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara
hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani-
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye
atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
38
(c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa
Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa
uwakilishi baina ya vyama vya siasa
vinavyowakilishwa Bungeni.
(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum
ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi
na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais
juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewa
dhidi yake.
(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi
kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya
Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda
usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa
yake kwa Spika.
(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya
Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi
kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili
taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura
za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote,
Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais
yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha
Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.
(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya
Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti
cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika
kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge
lilipopitisha azimio hilo.
(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na
mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata
malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo
alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na
Bunge.

Kwa mantiki hiyo sioni kama kuna ywezekano wa kumshitaki rais mstaafu Ben.

Hata hivyo napendekeza katiba ibadilishwe ili kuondolewe kinga ya aina hii ambayo kwayo rais anaweza kujifanyia lolote atakalo
 
Back
Top Bottom