Naona tunapoteza mwelekeo hapa... ishu ni huyu mtu Mkapa kwanini asifikishwe kwa pilato kwa makosa yalioainishwa na Rev,,,, hayo ya kafanya kazi ya kujenga shule, sijui kukusanya kodi ni kutimiza wajibu,...kwanza kazi aliiomba mwenyewe. Na nasisi watanzania tulimuhakikishia maisha mazuri for life kwa kutumia kodi yetu, kama malipo ya kutimiza wajibu wake kwa taifa... tuache blah blah hapa, madudu ya Mkapa ni mengi, yame overwhelm mazuri machache(yapo)...kwa walio yasahau, pengine kutokana na kufaidi asali ya hayo madudu yake..... nawawekea tena hapa kwa mujibu wa Rev. kwa uchache ni....
- Benki Kuu na kashfa zote; Meremeta, Epa, CIS, Tangold, Minara na menginewe.
- Miundombinu na Nishati: ATC, TRL, Rada, IPTL, Richmond, Kiwira, Ndege ya Rais, Helikopta za Jeshi na mengine.
- Demokrasia butu: uonevu kwa vyama vya siasa na wafuasi wa vyama ambavyo si CCM, kwa kutumia nguvu ya dola kama kule Pemba, mauaji ya Mwembechai, kufilisi au kutoza ushuru na kodi ya kukomoa kwa mwenye kuipinga CCM na Serikali ya Mkapa na mengineyo.
- Uwekezaji: Mikataba mibovu, sheria mbovu ambazo zinawapendelea wawekezaji na kulipunguzia Taifa mapato
.