Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

- Hivi karibuni kumekuwa na kauli nyingi za kukingana kati ya Pinda na Muungwana, hapa Muungwana alisema Mkapa aachwe apumzike, lakini Pinda anasema haogopwi.

- Wanaoyajua vizuri ya huko ndani wananiambia niogope Pinda maana huwa hasemi bila matendo na kwamba hii ya Kisutu ni operation yake, sasa anaposema hamuogopi Mkapa, ninapata faraja sana kwamba hii ngoma ya Kisutu inogile eh! he! he! he! inogile mwananagu! Tanzania inogile ooh! ooh! inogile!!!!

Na mimi nilikuwa nalifikiria hili. Kama tujuavyo JK alishatoa kauli kwamba, "Mwacheni Mzee wetu apumzike kwa amani." Je, JK ataweza kutoa kauli kama hii ya Pinda kwamba "Tunatakiwa kuafiki juu ya utawala wa sheria. Sheria kwa urahisi kabisa inasema hakuna mtu aliye juu yake. Hivyo kama utafanya kosa, hasa la jinai, sheria inakutaka ufikishwe kwenye chombo kinachohusika ambacho ni mahakama," alisema Pinda.
Bado JK ana kazi nzito maana swala la Mkapa halikwepeki na atajisafishia njia zaidi na kujiweka kwenye nafasi nzuri katika kinyang'anyiro cha 2010 kama akiamua kulishughulikia mapema na kuacha sheria ifuate mkondo wake na wakati huo huo kurudisha miliki ya Kiwira kwa Watanzania.
 
Takukuru yaamua kuvunja ukimya, yasema Mkapa hawezi kuchunguzwa

Posted by Dullonet Tanzania
Written by: Mwandishi Maalum, Dar Es Salaam.
Dullonet Tanzania | Just Call it Real Solutions for News and Informations


Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, hachunguzwi kwa kosa au tuhuma yoyote ya jinai, imeelezwa.


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa Dar es Salaam jana, ilisema uvumi kuwa Rais huyo mstaafu anachunguzwa na vyombo vya dola ikiwamo taasisi hiyo, hauna ukweli wowote.

Tamko la taasisi hiyo limekuja huku kukiwa na uvumi katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa kiongozi huyo anachunguzwa na Takukuru, kutokana na vitendo vingi vya ufisadi vinavyodaiwa kufanywa wakati wa uongozi wake.


Tayari mawaziri wawili Basil Mramba na Daniel Yona waliowahi kushika nyadhifa nyeti katika Serikali ya Awamu ya Tatu ukiwamo uwaziri wa Fedha, wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.


Lakini pia baadhi ya watuhumiwa katika kesi za kuchota mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT), ambao wamefikishwa mahakamani, wanadaiwa kufanya wizi huo kati ya mwaka 2004 na 2005 kipindi ambacho Rais Mkapa alikuwa madarakani.


Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kipwani alisema jana kuwa, taasisi yake haina uwezo wa kumchunguza kiongozi huyo kutokana na Katiba ya nchi kutotoa nafasi hiyo katika Ibara ya 46 (3) ya Katiba ya Tanzania. Kapwani alieleza kuwa taasisi yake inaheshimu Katiba na ina wajibu wa kuilinda na kuheshimu matakwa hayo ya Katiba.


“Takukuru inawafahamisha wananchi kwamba uvumi huu hauna ukweli wowote, hatumchunguzi kiongozi huyu kwa kosa au tuhuma yoyote ya kijinai,” alisema. “Ni kwa msingi huu, Takukuru imeona ni vyema kuwafahamisha wananchi ukweli dhidi ya uvumi huu.


Tukumbuke wakati wote kwamba taifa letu lina Katiba ya Nchi ambayo imeweka misingi mikuu ya kuendesha nchi yetu, haki na wajibu wa kila Mtanzania. Katiba kama sheria mama imeweka pia mipaka katika kushughulikia mambo mbalimbali ya nchi na kwa mantiki hii, haina budi kuheshimiwa wakati wote.”


Kifungu hicho cha Katiba kinaeleza kuwa “Ni marufuku kumshitaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.”


Kapwani alisisitiza kuwa Takukuru itaendelea kufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba na sheria ya nchi na sio vinginevyo. Katika siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinaripoti kuwa Mkapa anachunguzwa na Takukuru licha ya kuwa ana kinga ya kutoshitakiwa.


Vyombo hivyo vimekuwa vikimwandama kwa madai kuwa ufisadi mkubwa umefanyika katika kipindi ambacho alikuwa madarakani. Watu wenye mtazamo huo wamekuwa wanataka kiongozi huyo aondolewe kinga na afikishwe mahakamani kujibu tuhuma mbalimbali za ufisadi.


Wiki hii, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alieleza kusudio la kuwasilisha hoja binafsi katika kikao kijacho cha Bunge kuomba kifungu kinacholinda marais wastaafu kutoshitakiwa kirekebishwe. Mkapa anatajwa katika tuhuma kuhusu ununuzi wa ndege ya Rais, ununuzi wa rada, wizi wa mabilioni ya EPA, uuzaji wa nyumba za serikali, mikataba yenye utata kama ya NetGroup, Alex Stewart na ubinafsishaji wa mgodi wa Kiwira. .
 
Ukweli ni kwamba issue ya Rais Mstaafu haihusiani na ile ile kinga ya kutofikishwa mbele ya sheria. Hapa wanachanganya mambo mawili ya president kama institution na president kama person.

Bwana Pasco,
hakuna President kama institution duniani hapa.Tuna President kama person tuu full stop.NA KAMWE HUWEZI KUTOFAUTISHA MKAPA KAMA RAIA MWINGINE NA MKAPA KAMA RAIS KUANZIA November 1995 hadi November 2005.Kitu unachotakiwa kujua tu ni kuwa Rais Mkapa ni mtanzania na siyo watanzania wote ni Rais.

Nawapa Tahadhali nyie wenye hulka na silka kama ya huyo Pinda.Msifikiri Mkapa ni mjinga.Kukaa kwake kimya msifikiri anawaogopa sana ninyi wavivu wa kufikiri.Mkitaka mjue Tanzania mawe na marungu yananunuliwa wapi mkamateni Mkapa muone.Na msifikiri mimi napenda mnavyomdharirisha rais wetu mstaafu.Mngejua ni haki rais kushitakiwa mngebadili ako ka katiba kenu siku nyingi.Wewe Pinda na jamii ya watu mnaofanana nakushauri HUSIKURUPUKE eti kisa unataka kumridhisha balozi wa kijiji.Hata mbinguni kuna malaika wateule ije kuwa Tanzania?????

-Mangapi Nyerere kafanya ya ajabu na hakushtakiwa???
-Mangapi Mwinyi kafanya ya AJABU zaidi ya Mkapa na hakushtakiwa???
-Kwa nini awe Mkapa???

Wewe pinda si ni Usalama wa taifa wewe??unafikiri hakuna wanaomtii Mkapa 100%,unafikiri jeshini na Polisi mkapa yupo yupo tu??Acheni hizo nyie.Kama mmemaliza kahawa na kashata semeni.Unajua sometimes amani nayo ikizidi inakuwa karaha.Haya ngoja tujaribu na machafuko kidogo ili tuheshimiane.
Majita
 
Majita;348007 [COLOR="Navy" said:
-Mangapi Nyerere kafanya ya ajabu na hakushtakiwa???
-Mangapi Mwinyi kafanya ya AJABU zaidi ya Mkapa na hakushtakiwa???
-Kwa nini awe Mkapa???
[/COLOR]

Mkuu Majita
Hata kama tulikosea tusijirekebishe? I beg to differ. Ina maana basi waliopanda Kisutu wameonewa, waachiwe wote. Hatuendi hivyo.
Tusiogope UWT kama vile ni viranja wa pepo. Ni watoto wetu, wakwe zetu na zaidi wake zetu. Kuanza kutishia kuwa Mkapa anawafuasi UWT wanaomtii, kumbuka kama Obama anavyosisitiza, "kuna raisi mmoja tu kwa wakati mmoja" Hatuwezi kukubali kuwa na Mkapa wa Kiputin, tukabaki tukisema ni sawa wakati si sawa. Watanzania si watu wa kutishiwa nyau tena!
 
Mkuu Majita
Hata kama tulikosea tusijirekebishe? I beg to differ. Ina maana basi waliopanda Kisutu wameonewa, waachiwe wote. Hatuendi hivyo.
Tusiogope UWT kama vile ni viranja wa pepo. Ni watoto wetu, wakwe zetu na zaidi wake zetu. Kuanza kutishia kuwa Mkapa anawafuasi UWT wanaomtii, kumbuka kama Obama anavyosisitiza, "kuna raisi mmoja tu kwa wakati mmoja" Hatuwezi kukubali kuwa na Mkapa wa Kiputin, tukabaki tukisema ni sawa wakati si sawa. Watanzania si watu wa kutishiwa nyau tena!


mkuu Mwl Zawadi,
Napenda sana ulivyosema kuwa kama tulifanya kosa tusirekebishe??jibu ni kuwa tunatakiwa kurekebisha.Na ndo maana nasema kama kuna haja ya kufanya hivyo basi tuanze na kurekebisha katiba.Lakini ikumbukwe kuwa kinga hiyo ya kirais bado ina work kwa mheshimiwa Mkapa.

Kuhusu hapo nilipo Bold hapo as swali lako kama waliopanda kisutu waachiwe,mimi napenda kukuuliza kuwa,Je hao waliopanda kisutu nao walikuwa na kinga ya ki-rais au ya kiu-waziri???
Zaidi tuko pamoja ila again mnamuonea na kumdharirisha Mkapa,period
 
mkuu Mwl Zawadi,
Napenda sana ulivyosema kuwa kama tulifanya kosa tusirekebishe??jibu ni kuwa tunatakiwa kurekebisha.Na ndo maana nasema kama kuna haja ya kufanya hivyo basi tuanze na kurekebisha katiba.Lakini ikumbukwe kuwa kinga hiyo ya kirais bado ina work kwa mheshimiwa Mkapa.

Kuhusu hapo nilipo Bold hapo as swali lako kama waliopanda kisutu waachiwe,mimi napenda kukuuliza kuwa,Je hao waliopanda kisutu nao walikuwa na kinga ya ki-rais au ya kiu-waziri???
Zaidi tuko pamoja ila again mnamuonea na kumdharirisha Mkapa,period

Majita
Kinga ilikuwa CV ya pesa zao. Mmoja ni 'mbunge' na mwenzie 'katibu mkuu mstaafu mtarajiwa likizoni' labda hizo ndio zinaweza kuwa na 'kinga' za hadhi kuliko nyingine. Majita usiamini Mkapa anaonewa. Kumbuka Tanzania sio nchi kama enzi za Mwalimu ..ujamaa na kujitegema...na Mzee Ruksa ...kipofu kaona mwezi... Mkapa ametokea kipindi chenye mabadiliko makubwa, si kwa Tanzania tu bali kiulimwengu. Hivyo kama ni kizazi cha sasa kitamhukumu atahukumiwa kwa kwa sheria za kizazi cha sasa. Na kama hoja ya kumyang'anya kinga itaanzia kwake, basi historia itamkumbuka kwa hilo. Tusiogope kuerekebisha hata kama 'vitone vya damu' vitamwagika kama wanavyotutishia. Kwani wameshakufa wangapi kwa ajili ya nchi hii? Hatuna hesabu
 
Ukweli ni kwamba issue ya Rais Mstaafu haihusiani na ile ile kinga ya kutofikishwa mbele ya sheria. Hapa wanachanganya mambo mawili ya president kama institution na president kama person.

Bwana Pasco,
hakuna President kama institution duniani hapa.Tuna President kama person tuu full stop.NA KAMWE HUWEZI KUTOFAUTISHA MKAPA KAMA RAIA MWINGINE NA MKAPA KAMA RAIS KUANZIA November 1995 hadi November 2005.Kitu unachotakiwa kujua tu ni kuwa Rais Mkapa ni mtanzania na siyo watanzania wote ni Rais.

Nawapa Tahadhali nyie wenye hulka na silka kama ya huyo Pinda.Msifikiri Mkapa ni mjinga.Kukaa kwake kimya msifikiri anawaogopa sana ninyi wavivu wa kufikiri.Mkitaka mjue Tanzania mawe na marungu yananunuliwa wapi mkamateni Mkapa muone.Na msifikiri mimi napenda mnavyomdharirisha rais wetu mstaafu.Mngejua ni haki rais kushitakiwa mngebadili ako ka katiba kenu siku nyingi.Wewe Pinda na jamii ya watu mnaofanana nakushauri HUSIKURUPUKE eti kisa unataka kumridhisha balozi wa kijiji.Hata mbinguni kuna malaika wateule ije kuwa Tanzania?????

-Mangapi Nyerere kafanya ya ajabu na hakushtakiwa???
-Mangapi Mwinyi kafanya ya AJABU zaidi ya Mkapa na hakushtakiwa???
-Kwa nini awe Mkapa???

Wewe pinda si ni Usalama wa taifa wewe??unafikiri hakuna wanaomtii Mkapa 100%,unafikiri jeshini na Polisi mkapa yupo yupo tu??Acheni hizo nyie.Kama mmemaliza kahawa na kashata semeni.Unajua sometimes amani nayo ikizidi inakuwa karaha.Haya ngoja tujaribu na machafuko kidogo ili tuheshimiane.
Majita

nguvu ya mkapa polisi, usalama wa taifa, jeshini ni ndogo saana, usidanganyike kwamba alikula n a Mboma ukafikiri hiyo mihimili yao ipo, sasa hivi sasa wana mingo na yeye mwenyewe anajua hivyo, na ni tabia ya mwizi kuleta hali ya vitisho ili asishikwe, na nafiki na wewe mwenyewe waelewe, lakini kwa sababu za hofu yatakayo mkuta mwizi wetu ungependa kuleta hiyo hali ya hofu ili tusimshike mwizi kama vile mahabusu wanavyo jipaka kinyesi au kuwatupia kinyesi Polisi, ndivyo hali ilivyo mfikia mwizi wetu. na hao unao waita wafuasi wake wana hofu ya maisha yao, iliyo baki ni kwamba kila mtu aubebe mzigo wake mwenyewe
 
Kwa rapsharapsha tu,
Hatuna wanasheria waliobobea kwenye Katiba humu JF Ville?

Watuchambulie kwa kina! (may be President-Elect atusaidie)

Vinginevyo...

Watafanya hii 'Uraisi' ugombaniwe kwa njia yeyote...halafu?

Hiyo ibara, inamtaja Benjamin Mkapa?

Mnisaidie, labda nipo kwenye dumbwi!

Thanks Wakuu.
 
Siujua tumwamini Pinda au TAKUKURU.Nadhani communication breakdown ni miongoni mwa dalili za uongozi dhaifu.
 
Hivi miongoni mwa wanasheria wetu hakuna hata mmoja anayeweza kuwa na uzalendo wa "kununua" kesi hii?Hivi wana JF hatuwezi kufanya jitihada za fundraising na kumpata mwanasheria wa kumburuza Mkapa mahakamani?
 
- Mimi wakuu nimeamua kumuaminia Pinda, maana hivi karibuni niliwahi kumuuliza kiongozi mmoja wa juu kwamba nini kinaendelea huko serikalini na mafisadi, akaniambia siku zote angalia sana maneno ya Pinda, maana huwa hachanganyi na ndiye bosi wa hii operation nzima na inakwenda mpaka 2010, wote watakuwa wameshatinga Kisutu,

- Mkapa it is only a matter of time kabla, hayajamfikia mlangoni, halafu kumbuka style ya Muungwana, ni kuruhusu pressure toka kwa wananchi kwanza ipande kila kona na mwishowe kukutosa the last minute akidai kuwa hawezi kukuokoa maana maji yameshamwagika ili akuokoe itabidi na yeye aondoke kumbe yale maji ameyaleta mwenyewe kwa ujanja, haya maneno ya Takukuru na Sendeka tumeyazoea sana sasa, ingawa bado ninampa Sendekea a benefit of the doubt kwanza mpaka nitakapojua kilichomjiri maana hayo sio maneno yake.

Otherwise, hapa tulipofikia na hivi vita, either wote watinge Kisutu au serikali ya sasa iondoke, lakini haiwezekani ninasema tena kwamba haiwezekani tukaishia na Mramba, Yona na Mgonja tu, it is just impossible na it does not make a sense na siamini kwamba Muunwgana ni mjinga kiasi hicho kuruhusu sheria ifanyike nusu nusu, no way!
 
Date::12/24/2008
Wasomi wataka bunge limwondolee kinga Mkapa
Waandishi Wetu
Mwananchi

WANASHERIA, wasomi na wanasiasa wamezungumzia hoja ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kufikishwa mahakamani na kulitaka Bunge kumwondolea kinga ili aanze kuchunguzwa kwa tuhuma zinazomkabili.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, walisema katiba inayompa rais kinga ya kutoshtakiwa ina kasoro, kwani inamlinda bila kueleza kikomo cha mamlaka yake wala kiasi cha mali anachostahili kumiliki.

Walisema hayo walipokuwa wakizungumzia kauli kinzani za Takukuru kwamba, haimchunguzi Mkapa kwa tuhuma za Kiwira na ile ya Waziri Mkuu kuwa serikali haimwogopi kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Onesmo Kyauke alisema, kuna haja ya Bunge kuangalia uwezekano wa kumwondolea rais kinga kwa kuwa yeye ni binadamu na anaweza kutumia vibaya madaraka yake.

"Bunge litumie busara katika kuangalia hili, likiona kuna sababu za msingi za kufanya hivyo lifanye kwa masilahi ya taifa," alisema Kyauke na kuongeza: Kyauke ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema makosa yaliyopo ni sheria ya nchi kutozuia rais kumiliki mali au kumwekea mipaka ya umiliki awapo madarakani.

Alisema katiba imemwekea kinga rais, lakini haimzuii kumiliki mali, hali inayosababisha kutegemea uadilifu binafsi wa rais aliye madarakani.


Akizungumzia Takukuru Kyauke alisema, taasisi hiyo inapaswa kuwa huru na mkurugenzi wake asiwe wa kuteuliwa na rais, chama cha siasa wala kutoka serikalini, vinginevyo anaweza kufanya kazi kwa kulipa fadhila waliomweka madarakani, hivyo kuharibu wajibu wa kazi yake.

Kauli ya Kyauke iliungwa mkono na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad aliyesema kuwa, pamoja na sheria kumpa kinga Mkapa, Bunge lina uwezo wa kusimamia jambo hili kwa mujibu wa katiba na akafikishwa mahakamani.

"Kisheria bunge lina uwezo wa kumwondolea kinga iwapo Takukuru watakuwa na ushahidi wa kuthibitisha kuwa Mkapa anahusika na tuhuma hizo."

Alisisitiza kuwa japo kuwa hilo linaweza kuwa gumu kwani idadi ya wabunge wengi ni wa CCM, Maalim Seif alisema wabunge wote wamechaguliwa na wananchi na hivyo wapo kwa masilahi yao na si ya chama.

"Bunge lipo kwa ajili ya wananchi, kwani ndio waliowapigia kura na wanawatumikia wao, hivyo kwa mambo ya masilahi ya taifa kama hilo, ni vema wabunge wakafanya maamuzi kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla," alisema.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro ambaye ni mtaalam wa biashara za nje, Dk Elisante Gabriel alisema, serikali inatakiwa kuongeza uwazi katika suala la Kiwira ili iendelee kujenga imani ya wananchi inayoanza kupotea kutokana na kauli zinazopingana zinazotolewa na viongozi kuhusu suala la Mkapa.

Dk Elisante alisema endapo serikali itaendelea kufanya mambo yake kwa kificho, hali hiyo itawafanya wananchi wawe na mashaka juu uwajibikaji wake.


Alisema kama mtu ana uhakika kuwa hana makosa, hakuna haja ya yeye wala serikali kuwa na hofu na kufichaficha mambo ambayo kwa upande mwingine yanaleta maswali yasiyo na majibu.

Kumekuwapo na shinikizo kutoka kwa watu mbalimbali wakiwapo wanasiasa wakitaka Mkapa afikishwe katika vyombo vya sheria kwa tuhuma za kutumia madaraka aliyokuwa nayo kufanya biashara ambapo anadaiwa kumiliki Mgodi wa Kiwira.

Hivi karibuni, Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika mahojiano yake na The Citizen alisema kuwa, serikali ya awamu ya nne haitasita kumfikisha mahakamani Rais mstaafu Mkapa kama itabainika kuwa amefanya kosa la jinai kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Waziri Pinda alisisitiza kuwa, serikali haina sababu ya kuhofia suala hilo kwani kila anayetuhumiwa ni lazima afikishwe mahakamani.

Hata hivyo,Takukuru baadaye ilitoa taarifa yake ikikanusha kuwepo na taarifa za kumchunguza Mkapa kama ilivyokuwa ikiripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini.
 
Hivi miongoni mwa wanasheria wetu hakuna hata mmoja anayeweza kuwa na uzalendo wa "kununua" kesi hii?Hivi wana JF hatuwezi kufanya jitihada za fundraising na kumpata mwanasheria wa kumburuza Mkapa mahakamani?


Mimi kinachonimaliza ni siasa za kitanzania. Kuna jambo fulani linalonikera sana. Huyu Waziri kijana ambaye anaonekana yumo kwenye serikali ya JK kwa kishindo, ana uhusiano gani na mafisadi?

Hii inatokana na sababu kwamba, ana ukaribu mkubwa sana na Lowassa, na wengine ambao wamo kwenye UFISADi. Pia habari za ndani zinasema kwamba ana vikao kadhaa nyeti kila mwezi in secret venues na baadhi ya hawa viongozi wa zamani ambao ni wana CCM wanaoshutumiwa na mambo ya wizi wa umma, je anajitayarishia mazingira mengine hapo 2010 au vipi?

Wenye data zaidi mtupe mapya........... nina uhakika kwamba mnamfahamu waziri kijana wa mambo ya ndani. There is something very fishy with this guy, he may end up being a big liability to the JK leadership. Ila ninachoona ni kwamba anakuja kuchuana na JK 2010, kuna wengi sana CCM na bungeni ambao wameanza tetesi za chini kwa chini



_________________________
"Power to the people"
 
Recta,
Mkuu wala sina ubishi ktk swala zima la Utawala zaidi ya kusema kwamba nimechukua sifa za Mkapa (low inflation rate) ambazo zimewekwa kumfanya Mkapa kuwa kiongozi bora zaidi ya wote waliotangulia..
Hapa ndipo nilipopatwa na matatizo na wala sina maana kabisa kuwa Mkapa hakufanya jambo jema kwani hata Hitler na ubaya wote aliyafanya mazuri kwa Ujarumani.. Na kuna uwezekano Wajarumani wenyewe wanampenda ama kumtazama kama kiongozi bora Ujarumani.... sasa Usemi kama huo ndio mimi naupinga kutokana na sababu zilizowekwa ndio maana nikatumia muda kuchambua Inflation na yanayoajiri.

Kusema kweli binafsi simpongezi Mwinyi hata kidogo kama kiongozi bora lakini kulingana na mada hii sioni sababu ya kumfikisha yeye mahakamani...Anaweza kuwa alikuwa mtovu wa Uongozi bora kama rais, lakini madhambi yake hayawezi kunifanya mimi nifikirie kumfikisha mahakamani ama kinyume chake kumpa sifa ya kiongozi bora tuliyewahi kuwa naye...Hapa nitakuwa napotosha maana kamili ya neno Kiongozi bora..Inflation iliyotakana na Mwinyi ilieleweka na kama ulivyosema Nyerere aliboronga kiuchumi, ni kweli kabisa wakati wa Nyerere kila kitu kilikuwa karibu na bure toka Umeme, maji, efya, elimu, chakula, nauli za usafiri yaani karibu huduma zote na maisha kwa ujumla yalikuwa ya dunia nyingine kabisa acha mbali matatizo ya price control...
N:B - Uchumi hauendeshwi hivyo, pamoja na kwamba hujengwa kama alivyofanya Nyerere!

Huwa nasema Uchumi wa Tanzania ni sawa kabisa na Mradi wa maji wa Mtera. A huge and very important infrastructure for the nation economy Nyerere aliifanya (bravo) lakini hakuwa na mbinu ya jinsi ya mradi huo uwezo kujiendesha..why?.. hata sielewi!.. akili yake ilikuwa kutazama Ujamaa na huduma kwa wananchi as if bwawa hilo linajiendesha lenyewe kama vile ziwa ama bahari sujui!..
Hivyo Mwinyi alipoingia alikuta Mtera imejaa mchanga haiwezi kuzalisha tena umeme kwa kiasi kinachotakiwa akafunga na kuanza kusafisha(bravo)..Tatizo la Mwinyi linakuja pale aliporuhusu Mtera kufunguliwa tena yaani RUKSA, na kwamba ile pressure ya maji yaliyokuwa yamefungwa ndio sababu kubwa ya inflation na uchafu ndani ya mabomba ya maji (monetary items) yetu na ndio sababu ya kutetea kwangu.

Sasa ukija kwa Mkapa mkuu wangu ni swala la growth in money supply..Yes, ni kweli Mkapa alitaka kuhakikisha kuwa maji ya Mtera hayapatikani bure (taxes) which is a good Idea na ina make sense kiuchumi. Mkuu wetu aka set strategies zake kulingana na matakwa ya IMF ambao walikuwa tayari kujenga mradi mwingine wa Umeme (very good)..Lakini ukweli ni Upi?...Fedha ya mikopo ilipokuja tu wajomba wakaanza kugawana wakati Mtera ndio kwanza inaelemewa kutokana na Population kubwa kisha inajaza tope hakuna mpango wa ukarabati wala utaratibu wa ugawaji.. Huyo Mkapa ndio kwanza yeye alifikiria kukusanya kodi za wananchi toka matumizi ya maji tena machafu. Hali ilipozidi kuwa mbaya zaidi (maradhi na maji ya mgao) huyu mkuu akatafuta an easy way out -SALE IT!!
Na kwa jeuri akisema, hao watakao sema au kulalamika ni wajinga tu hawana akili wanafikiria maji yatatolewa bure kama wakati wa Nyerere na Ujamaa alaaa!...hapa mkuu kweli nambie, swala la Nyerere na Ujamaa linaingia vipi ktk uharibifu wa Mkapa! Huyu ndiye leo kuna watu wanamwita Kiongozi bora kuliko wote..

Bila shaka Nyerere alikuwa na mapungufu mengi tu ya Uongozi na hakuna anayebisha isipokuwa siye anayetakiwa kupelekwa mahakamani zaidi ya hapo tutakuwa tunakosea sana tukishindwa kutenganisha yote yale yanayotokana na Uongozi bora kwa sababu Ukimtazama Nyerere alishindwa swala moja la UCHUMI ktk Ubepari yaani biashara..Ujenzi wa Miundombinu na innovation za viwanda alizofanya ni Uchumi pia isipokuwa kosa kubwa la mwalimu ni kuwa investments hizo hazikuweza kujiendesha/ kujihudumia zenyewe kama mfano wa Mtera hapo juu..
Pili, kama kiongozi wa nchi, SIASA zake mkuu wangu sidhani kama kuna mtu anampata ama kuwa naye ligi moja - Afrika nzima. Nyerere aliongoza nchi pamoja na kwamba wapo wanaoamini kuwa Nyerere aliburuza nchi wakiwa na maana Kiuchumi. Lakini hata hivyo ukichunguza sana utagundua kwamba Uchumi sio sawa na sayansi ni moja linayotakiwa akili ya biashara zaidi ya darasa pamoja na kwamba usimamizi wake ktk uzalishaji na utendaji unahitaji elimu ya darasa kuweza kupanuka ama kuwa sustainable.
Hata ktk maisha ya wananchi utaona kwamba kina Bill Gates wanaojivunia Utajiri sio wasomi hivyo lakini nyuma ya Microsoft kuna vipara waliobobea ktk IT kama vichaa vile..lakini swali linabaki pale pale kiongozi wa Microsoft ni nani apete sifa!.
Mkuu hii ndiyo mifano yangu ambayo hupenda kuitumia ili kujaribu kuwaweka wananchi wenzangu karibu na matatizo yanayotukuta lakini kwa bahati mbaya mara nyingi huwa nawapoteza wengine mitaani...
Nitamalizia kwa kukumbusha kidogo nyuma mwaka jana tu..
Nakumbuka sana, nikiwa Tanzania niliongea na Mwanakijiji na kumwabia jinsi watu wanavyojirusha na kuzungumzia Mamillioni ya dollar.. nyumba zimepanda bei kichizi na watu wanajenga kama vile fedha ziunaokotwa - sijawahi kuona. Akaniuliza hiyo loss ya purchansing power imetokana na kitu gani haswa! hakika nilishindwa kumjibu kwa sababu sikufahamu kabisa hadi pale nilipoanza kuelewa michongo inayochezwa toka Utawala wa juu..Hiyo bank kuu yetu ambayo ilitakiwa ku control money supply ndiko mchezo unakofanyika wakimwaga mahela mitaani na kuzua inflation ya kujitakia kabisa! Mkapa ndiye kinara aliyemwajiri Balali, Yona na Mramba ambao ni magwiji wa kwanz ktk Ufisadi..

Kwa hiyo mkuu wangu mimi nakubaliana sana na maneno ya Jujuman hapo juu na ndio haswa kichwa cha mada hii lakini kumtetea Jambazi kuwa alikuwa kiongozi bora na sifa kem kem ambazo hazina sura kabisa wakati swala hapa ni - People of Tanzania versus Benjamin William Mkapa! - hainigii akilini hata kidogo.

MERRY CHRISTMAS!.. Ho! ho! Ho! ho!
 
- Mimi wakuu nimeamua kumuaminia Pinda, maana hivi karibuni niliwahi kumuuliza kiongozi mmoja wa juu kwamba nini kinaendelea huko serikalini na mafisadi, akaniambia siku zote angalia sana maneno ya Pinda, maana huwa hachanganyi na ndiye bosi wa hii operation nzima na inakwenda mpaka 2010, wote watakuwa wameshatinga Kisutu,

- Mkapa it is only a matter of time kabla, hayajamfikia mlangoni, halafu kumbuka style ya Muungwana, ni kuruhusu pressure toka kwa wananchi kwanza ipande kila kona na mwishowe kukutosa the last minute akidai kuwa hawezi kukuokoa maana maji yameshamwagika ili akuokoe itabidi na yeye aondoke kumbe yale maji ameyaleta mwenyewe kwa ujanja, haya maneno ya Takukuru na Sendeka tumeyazoea sana sasa, ingawa bado ninampa Sendekea a benefit of the doubt kwanza mpaka nitakapojua kilichomjiri maana hayo sio maneno yake.

Otherwise, hapa tulipofikia na hivi vita, either wote watinge Kisutu au serikali ya sasa iondoke, lakini haiwezekani ninasema tena kwamba haiwezekani tukaishia na Mramba, Yona na Mgonja tu, it is just impossible na it does not make a sense na siamini kwamba Muunwgana ni mjinga kiasi hicho kuruhusu sheria ifanyike nusu nusu, no way!

Mkuu hii naona ni sign of hope. Lakini bado naona kizunguzungu kidogo kuhusu hii issue nzima, mashitaka ya kina Mgonja, Yona na Mramba so far yanaonesha kuwa watakwepa lupango(kulitia hasara taifa na sio kuliibia taifa), sana sana adhabu yao ni kuwa kisiasa tayari wamekufa, at least tusiwategemee 2010. Sielewi kwanini hawajawekwa kwenye EPA wakati baadhi yao wanahusika. Naangalia issue kwa kuiforward beyond 2010 naona kizunguzungu kidogo, ni kama wanataka kuitumia issue hii kisiasa, kama kuunda kundi jipya between au linalohusisha mtandao na CCM asili, na sio kuishughulikia vilivyo.
Lakini ukumbuke kuwa Ben is also very smart, nasubiri tu kuanza kuona anavyocheza karata zake, dalili zikianza kuonesha kuwa mkono una mkaribia anaweza kucheza tic-tak ya ajabu sana, pamoja na kuwa inawezekana hawaivi vizuri na mafisadi wakubwa wa EPA kutoka Mbeya, lakini kapu moja linaweza kuwaunganisha na wakacheza mchezo mmoja wa ajabu sana. So far amekuwa anaonesha ku-keep low profile na kidogo anaonesha kufura akigusiwa issues za ufusadi wa serikali yake. Tusubiri karata zake.
 
Pasco,
Mkuu samahani kidogo kwani ile sahihi ya rais ktk hukumu ya Kifo huja kabla la mahakama ya rufaa!.. Mimi nilidhani rais huwa ndio mtu wa mwisho kabisa kusamehe ama kusaini... akianguka wino ni masaa au dakika tu kwa mtu kunyongwa..naomba ufafanuzi na shria hiyo kusema kweli sifahamu.

Pili, wanabodi wenzangu - Pamoja na maelezo ya kutia nguvu ya Pinda, ningependa kujua hiyo katiba Ibara ya 46(3) ambayo inazuia kumshtaki Rais mstaafu, kulingana na Takukuru inasema exactly kama walivyosema wao:- Kuwa, Isipokuwa kama ataacha, kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara 46 a (10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais.

Kama ndivyo, basi tumeliwa wajomba katiba inatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa na wale wote wanaotetea kutorekebisha kifungu cha katiba kinachomlinda rais na msaafu, wasitokee kabisa kuweka lawama zao kuhusiana na Mkapa au rais yeyote kwa sababu huwezi kupika keki ukataka kula mwenyewe!..
 
Mkandara, maamuzi yeyote rais anayoyafanya ambayo yatam-exempt kutoka kwenye mashtaka ya jinai kutokana na vifungu ulivyovitaja, ni yale yenye maslahi kwa Taifa au ni maamuzi yeyote yale ?

Je, maamuzi ya ujasiriamali aliyoyafanya Mkapa akiwa ikulu aliyafanya akiwa kama rais ? i.e yana manufaa yeyote kwa Taifa ?
 
Hivi miongoni mwa wanasheria wetu hakuna hata mmoja anayeweza kuwa na uzalendo wa "kununua" kesi hii?Hivi wana JF hatuwezi kufanya jitihada za fundraising na kumpata mwanasheria wa kumburuza Mkapa mahakamani?

Hili ni jambo gumu sana kulitekeleza kwa utaratibu huu unaoupendekeza mkuu. Hii ni kwa sababu itabidi utumike utaratibu wa waendesha mashitaka binafsi. Ni vigumu sana kufungua kesi chini ya utaratibu huu hata kama unayemshitaki ni kiongozi wa ngazi za chini. nadhani linapokuja suala la rais mstaafu, vizingiti ndio vitakuwa vikubwa zaidi.
Fikiria, kuna watuw anaghangaika hadi leo kutafuta sanction ya Mahakama kumshitaki Chitatlilo chini ya utaratibu huu baada ya polisi kukiri kuwa aklighushi vyeti lakini wakakataa kumfungulia mashitaka
 
Mama,
Binafsi nimeshindwa kutenganisha vitu ambavyo unaweza kusema ni vya maslahi ya Taifa au maamuzi yake mwenyewe ikiwa matendo yake yanaendana na Maazimio ya taifa ambayo hayamteganishi yeye kama rais na raia wa kawaida..
Hapo ndipo mimi nafikiri tumepigwa bao hasa nikizingatia kwamba Azimio la Zanzibar lilimpa ruksa yeye na viongozi wote nchini kuwa Wajasiamali..Hivyo by law ilikuwa approved na hakuna sehemu ama kifungu cha sheria kinachomzuia rais kufungua ofisi yake Ikulu..Kwanza Ikulu hujulikana kama ndio makazi ya rais wakati akiwa madarakani..

Hili ndio tatizo kubwa, na wengi wetu tunaposoma na kuitafsiri sheria toka ndani ya katiba tu utafikiri ni msahafu ambao haukuacha kitu... na kama unakumbuka kuna sehemu niliwahi kuandika kwamba hiyo misahafu yenyewe (biblia na Kuran) havizungumzii kuharamisha Ubakaji wa watoto wadogo na rape, lakini haina maana inakubalika na ruksa kubaka watoto wadogo..

Kwa hiyo itakuwa tunafanya ujinga tukisimama kumtetea Mkapa kwa sababu ya katiba..tumfikishe mahakamani kama mkosefu maanake sidhani kama kuna kanisa ama Msikiti unaweza kushindwa kumweka kiti moto kiongozi wa dini kwa sababu ati sheria ya dini inampa kinga au swala la kubaka watoto halina Uharamu kulingana na vitabu..
 
Back
Top Bottom