Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Vipimo gani unatumia, Keynessian economists theory?? kuna maendeleo fulani lakini maendeleo ya msing, uchumi unaokua kwenye "quick sand" haudumu ndio maana tikiso kidogo tu hoi inflation inapanda kama kichaa. Ni vizuri tukawa na vipimo vingine, hivyo vya mahesabu yasio na research data hayafai. Ukitumia data za NBS umelewa maana hazina ukweli wowote, na ni kwa sababu hawana hela za ku-update data angalau kila miaka miwili hivyo data zote ni projections tu. Ukitaka kuangalia kama uchumi umekuwa angalia ni bidha ngapi hapa ndani zinazalishwa hapahapa bongo tutengeneze kazi kwa wabongo???? pamba inalimwa shinyanga, inauzwa UK na kwingineko mashati yanarudi hapa kama VanHussein bei mbaya, hata furniture tunaagiza malasia, haya matunda ya kiwi yanatoka Nwezealand.
Sidhani kama uchumi umekuwa tunavyoambiwa, ila tu kwa vile vipimo ni data mbovu tulizonazo.
 
tusiwe na watu ambao watakuwa kama miungu watu. binadamu ni binadamu anaweza kukosea.
na wala tusitegemee viongoz wa dini peke yake - eti kwamba viongoz wetu watamuogopa mungu kutenda mabaya kwa nchi zao.
pia tusijiaminishe kuwa mtu akiukwaa uraisi atatenda mema - eti automatically hatojimilikisha mali za taifa japo mianya itakuwepo.

suluhisho ni kuwafanya wajue kuwa wakifanya ovyo, sheria itachukua mkondo wake.
hatutokaa tupate mtu kama nyerere ambaye hakuwa na nia ya kujitwalia mali.
watakaofuata wote wakiingia tu kule watakuwa bize kujitwalia mali. hii ni dunia ya kutafuta mali
 
Nimejaribu kusoma post ya ndugu Mkandara mara kadhaa ili kuelewa ni kwa vipi Mkapa hakuwa BEST President (so far) ila nimeshindwa kupata maelezo yoyote yanayohusiana na Mkapa kutokuwa Best President.

Mimi naamini kabisa kuwa Mkapa alikuwa Rais bora kabisa tangu tupate Uhuru. Nakubali pia kulikuwa na mapungufu mengi tu katika uongozi wake. Ila ukweli kuwa alikuwa Best so far unabaki pale pale.

Mkapa alifanikiwa sana kuendeleza elimu nchini. Alijenga (kwa mara ya kwanza kabisa tangu Uhuru) shule nyingi sana za msingi na sekondari. Alijitahidi sana kuweka maslahi bora kwa walimu (na baadhi ya uthibitisho ni utulivu wa walimu uliokuwepo wakati wake). Uanzishwaji wa MMEM na MMES ulifanikiwa sana na mwenye upeo wa kuona ataweza kuona hilo.

Mkapa alifanikiwa sana ku-control inflation. Itakumbukwa wakati akiingia madarakani, inflation ilikuwa ya kupaa. Ukapa ukikumbukwa utasaidia kuelezea zaidi.

Mkapa alisaidia kukuza uwekezaji wa ndani na wa nje (uwekezaji wa kweli). Ikumbukwe wakati wa awamu ya kwanza ilikuwa ngumu kuwekeza (Pesa haikuwa msingi wa maisha). Wakati wa awamu ya pili, uwekezaji haukuwa rasmi. Wasomi waliacha kazi na kukaa vijiweni (maana huko pesa ilipatikana kwa urahisi zaidi). Uchumi ukadumaa, na ikafikia mahali nchi ikawa haikopesheki tena.

Nadhani niishie hapa kwa sasa. Mkapa ataendelea kukumbukwa kwa kazi nzuri sana.

Mzee ni vizuri kusema hayo, lakini ujue kuwa watanzania wengi tu ni wepesi sana wa kudakia hoja bila kupata hata dakika moja ya kufukiri na kujiuliza then waamue. Wakisikia jambo tu basi......ndiyo ukweli na comments zinaanza kutoka dakika hiyohiyo, hii ndiyo iliyo tufanya tuuziwe mbuzi kwenye gunia mwaka 2005 eti watu tukaambiwa huyu kama "JK Orijino" sasa hivi kila mwenye upeo anajua huyu ni "JK chipolopolo", Watu waliamini tu bila kufikiri. Na mapesa akatumia mengi tu ya kuwanunua wanahabari na kadhalika... lakini wapi bwana ...si tumeambiwa Nyerere huyu!! hakukuwa na kujiuliza!
Basi bwana, baadhi ya watu wamesema Ben ashtakiwe.... hakuna anejiuliza kitu! ni mashindano tu jinsi yamtukana yule mzee, ashtakiwe,ashtakiwe eh!
Hivi ujiulize tu kabisa kwa ukweli kabisa wa dhati watu wamesahau matakataka ya Mzee Ruksa! au wengi wetu wadogo humu? JK alipoingia madarakani alisema (anashukuru kuipokea nchi kwenye hali nzuri kuliko Mkapa alivyoipokea kwa Ruksa!
 
for that mchungaj no comment everything done katika awamu ya tatu ,ni lazima ashitakiwe huyu presdaa mstaafu
Jinsi kila kitu kinavyosambaratika na kuangamia, uharamia, uzembe, ukosefu uadilifu, kukosa uungwana na utu, hujuma, wizi, ufisadi na dhuluma zikiongezeka, vifole vyote vinabidi vimnyokee mtu mmoja, Benjamin William Mkapa, Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndiyo, Mchungaji kanena msilishangae. Ndiyo, Mchungaji kanena pamoja na kumshikia bango Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuwa mgumu kufanya maamuzi mazito kuisafisha nchi yetu, lakini badala ya kuendelea kumwagia Kikwete lawama, Mchungaji anasema, turudi kwa yule aliyekuwa madarakani kabla ya Kikwete.

Wengine wenu mtadai turudi nyuma kwa Mzeee Mwinyi hata kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, mimi nasema hapana, tunaanzia na Mkapa wala si kulitafakari Azimio la Zanzibar bali ni utendaji kazi wa Serikali ya Mkapa na uongozi wake Serikalini, Chama cha Mapinduzi na Taifa zima.

Nilipoandika mada kuhusu Andrew, Omari, Cornell na Robert, niliwataja wakuu wa mambo ya sheria na dola, usalama wa Taifa na nchi, katiba na haki na kuwatuhumu kuwa wao katika nyadhifa zao na wakati wa uongozi wao, Tanzania iligeuka kuwa dangulo na handaki la kila aina ya uharamia kuliibia Taifa wazi wazi bila woga wala aibu.

Kikwete katuambia, tumuache "Mzee Mkapa" astaafu kwa amani, mimi nasema hapana, hatuwezi kuendelea mbele bila Mkapa kufikishwa kizimbani na kujibu mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka, kushindwa kulilinda Taifa kutoka maadui na uhalifu na mbaya zaidi kuliingizia Taifa hasara.

Simtuhumu Mkapa kwa wizi, bali nalisema wazi kuwa ndani ya utawala wa Mkapa wa miaka 10, makovu na majeraha tunayoyaona leo hii ya uhujumu na ufisadi, yalianzia nyakati hizo, michubuko na mikwaruzo ilifanyika nyakati hizo na tulichobakishiwa ni uozo ambao unatambaa kama algae na fungi.

  • Benki Kuu na kashfa zote; Meremeta, Epa, CIS, Tangold, Minara na menginewe.
  • Miundombinu na Nishati: ATC, TRL, Rada, IPTL, Richmond, Kiwira, Ndege ya Rais, Helikopta za Jeshi na mengine.
  • Demokrasia butu: uonevu kwa vyama vya siasa na wafuasi wa vyama ambavyo si CCM, kwa kutumia nguvu ya dola kama kule Pemba, mauaji ya Mwembechai, kufilisi au kutoza ushuru na kodi ya kukomoa kwa mwenye kuipinga CCM na Serikali ya Mkapa na mengineyo.
  • Uwekezaji: Mikataba mibovu, sheria mbovu ambazo zinawapendelea wawekezaji na kulipunguzia Taifa mapato.
  • Sheria na Katiba: kuendelea kuwepo kwa sheria na mambo mabovu katika sheria na katiba ambayo yameondoa kabisa mihimili ya Bunge na Mahakama kuwa na nguvu za kikatiba na mamlaka kuihakiki Serikali kuu.
  • Uchumi wa nchi, kudorora kwa uchumi kwa hali halisi ya uzalishaji mali, kudumaa kwa kilimo na kukimbilia utegemezi wa kuagiza chakula, kupungua uzalishaji mali kutokana na kosekana kwa umeme, maji, barabara nzuri.
  • Elimu na Afya: kushuka kwa kiwango cha elimu Tanzania kwa kuruhusu matakwa binafsi ya watu wachache waamue kubadili mfumo wa Elimu bila kupata ushauri wa wataalamu wa Elimu. Afya kuendelea kudorora huku kukiwa na uhaba mkubwawa vifaa, madawa na wataalamu wa afya.
  • Uongozi mbovu; kukosekana kabisa kwa uwajibikaji ndani ya serikali ambako kumezaa tabaka la viongozi wa Serikali na Mashirika ambao wanajiona ni Miungu wasio na makosa (Mattaka, Chenge n.k). Kukosekana na Sauti ya kuheshimiwa kuliongoza Taifa.
Pamoja na yale machache tuliyoyashuhudia ambayo tunayaona kuwa ni chanya, kama kufutiwa madeni yetu na harakati za kuendeleza Mkukuta na Mkurubita, lakini ukweli wa mambo unabakia kuwa kama kweli Mkapa aliacha misingi imara, basi pamoja na Kikwete kujenga baraka la mawaziri kubwa na la kifahari, uchumi na pato la Taifa lisingeporomoka jinsi lilivyoporomoka kwa haraka.

Ni wajibu wetu wote kama taifa kuwajibika na kuchapa kazi ili kulikwamua Taifa kiuchumi ili kuwepo na elimu na afya bora, ajira na tumaini la kuwa Taifa linalojitegema, lakini kinara, kiranja mkuu ambaye alitutukana kuwa tuna wivu wa kike na ni wavivu, matusi na lawama za Taifa kushindwa kusonga mbele zinarudi kwake na si mtu mwingine.

Ni haki yetu kama Wananchi, kutaka Mkapa awajibishwe kwa kuvurunda kazi. Hata pamoja na kuwa hawezi kupigiwa kura tena, lakini anapaswa afikishwe mahakamani kwa uzembe na matumizi mabaya ya madaraka yake.

Suala la Kinga ni la kitoto na linaendelea kulea uozo, ujuvi na ubabe wa kutishana na kulindana.

Atakapofikishwa Mkapa mahakamani, hata kina Rostam, Lowassa, Chenge na wengine watabaini kuwa Watanzania, hatutaki mchezo. Kila mwenye ndoto ya Ufisadi, Uzembe, utumiaji vibaya madaraka, uvivu na kukosa kuwajibika ama itabidi atafute nchi nyingine ahamie au anyooke na kuanza kuishi kama Mtanzania Mzalendo.

Kura zile za Tsunami hazikuwa za kutuletea Ze Comedy! Bwana Kikwete nakuomba fanya kazi yako, ondoa magugu, visiki na viwavi jeshi walio ndani ya Serikali na Chama chako.

Jaruzelski, pamoja na yote aliyofanya kwa madai ya kutumia madaraka au kwa mujibu wa sheria, leo hii yuko mahakamani kujibu mashitaka. Kila kona dunia hii, kiongozi aliyebainika alifanya kosa anavuliwa kinga na kufikishwa mahakamani, kama rafiki yetu Chiluba alivyofanyiwa.

Hivyo basi, tupaze sauti zetu kwa nguvu tukimtaka Kikwete amfunge paka kengele.

Rais Kikwete, nakuomba usicheze nalenale, ushamfikisha Mramba, Yona na Mgonja, tunamtaka Lowassa, Rostam na zaidi ya yote, tunamtaka Mkapa.

La sivyo, unatupa kazi moja, nikinukuu maneno ya mmoja wa viongozi wa chama cha wafanya kazi Ugiriki walipofanya fujo kutokana na Polisi kuua mtoto mdogo "It is very simple, we want the government to fall". Sentenzo hiyo ilitolewa kwa ghadhabu kwa Serikali kushindwa kufanya kazi yake ipaswavyo.

Ukishindwa kufanya kweli, basi nasi kwetu itakua "it is very simple, we want the government to fall" na kweli kwa kiapo cha kilio cha machungu Serikali yako itashindwa na kuanguka yenyewe. Usitufikishe hapo kwenye mchanga tukakuchukia na kugotesha meli yetu na kutoa kauli hiyo ya kutakia maangamizo ya Serikali yako.

Ili tuendelee mbele, fungua kesi, Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Benjamin William Mkapa.
 
Mkapa hachunguzwi-Takukuru
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,December 23, 2008 @21:15

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, hachunguzwi kwa kosa au tuhuma yoyote ya jinai, imeelezwa. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa Dar es Salaam jana, ilisema uvumi kuwa Rais huyo mstaafu anachunguzwa na vyombo vya dola ikiwamo taasisi hiyo, hauna ukweli wowote.

Tamko la taasisi hiyo limekuja huku kukiwa na uvumi katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa kiongozi huyo anachunguzwa na Takukuru, kutokana na vitendo vingi vya ufisadi vinavyodaiwa kufanywa wakati wa uongozi wake.

Tayari mawaziri wawili Basil Mramba na Daniel Yona waliowahi kushika nyadhifa nyeti katika Serikali ya Awamu ya Tatu ukiwamo uwaziri wa Fedha, wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.

Lakini pia baadhi ya watuhumiwa katika kesi za kuchota mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT), ambao wamefikishwa mahakamani, wanadaiwa kufanya wizi huo kati ya mwaka 2004 na 2005 kipindi ambacho Rais Mkapa alikuwa madarakani.

Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kipwani alisema jana kuwa, taasisi yake haina uwezo wa kumchunguza kiongozi huyo kutokana na Katiba ya nchi kutotoa nafasi hiyo katika Ibara ya 46 (3) ya Katiba ya Tanzania. Kapwani alieleza kuwa taasisi yake inaheshimu Katiba na ina wajibu wa kuilinda na kuheshimu matakwa hayo ya Katiba.

"Takukuru inawafahamisha wananchi kwamba uvumi huu hauna ukweli wowote, hatumchunguzi kiongozi huyu kwa kosa au tuhuma yoyote ya kijinai," alisema. "Ni kwa msingi huu, Takukuru imeona ni vyema kuwafahamisha wananchi ukweli dhidi ya uvumi huu.

Tukumbuke wakati wote kwamba taifa letu lina Katiba ya Nchi ambayo imeweka misingi mikuu ya kuendesha nchi yetu, haki na wajibu wa kila Mtanzania. Katiba kama sheria mama imeweka pia mipaka katika kushughulikia mambo mbalimbali ya nchi na kwa mantiki hii, haina budi kuheshimiwa wakati wote."

Kifungu hicho cha Katiba kinaeleza kuwa "Ni marufuku kumshitaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii."

Kapwani alisisitiza kuwa Takukuru itaendelea kufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba na sheria ya nchi na sio vinginevyo. Katika siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinaripoti kuwa Mkapa anachunguzwa na Takukuru licha ya kuwa ana kinga ya kutoshitakiwa.

Vyombo hivyo vimekuwa vikimwandama kwa madai kuwa ufisadi mkubwa umefanyika katika kipindi ambacho alikuwa madarakani. Watu wenye mtazamo huo wamekuwa wanataka kiongozi huyo aondolewe kinga na afikishwe mahakamani kujibu tuhuma mbalimbali za ufisadi.

Wiki hii, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alieleza kusudio la kuwasilisha hoja binafsi katika kikao kijacho cha Bunge kuomba kifungu kinacholinda marais wastaafu kutoshitakiwa kirekebishwe. Mkapa anatajwa katika tuhuma kuhusu ununuzi wa ndege ya Rais, ununuzi wa rada, wizi wa mabilioni ya EPA, uuzaji wa nyumba za serikali, mikataba yenye utata kama ya NetGroup, Alex Stewart na ubinafsishaji wa mgodi wa Kiwira.
 
Babu alinena...na namnukuu kiunagaubaga...
"Tunahitaji mgombea ambaye tunaweza kumuuliza, naye aweze kutujibu, kwa moyo wa dhati...

'Wewe unapinga rushwa?'
'Utaweza kukidhi matarajio ya mwananchi-Mtanzania?'

'Wewe unajua nchi hii ni ya masikini?

'...naye aweze kutujibu kwa moyo wa dhati!!!'

Kama hayo hapo juu yalijibiwa kwa dhati basi...

Hayo hapo juu kunanipeleka kuuliza...
Raisi Mstaafu, unaweza kutujibu sisi wananchi,wapigakura, Watanzania- Ulihusika vipi na hayo maovu yanayokulenga?

Toka uache ofisi hiyo ya uraisi, dhamana yake ambayo ni sisi tuliyokupa, Ulipigana vita ya rushwa?

Je Unaweza kutujibu kwa dhati kuwa rushwa haikutendeka wakati unayo dhamana yetu?

Je unafikiri tunayo haki yakukuburaza mahakamani ilituweze kupata majibu haya?😡
 
Last edited:
kama wabunge wetu kweli wana akili na nia ya kuiendeleza tanzania ya leo, basi bunge likikaaa hiyo January na Moja wao akawasilisha hoja ya Kumshtaki Mkapa au kubadili katiba Basi kwa kutumia Hoja hiyo wasikubali kujadili kitu kingine , mpaka hoja kuu ya Mstaafu imejadiliwa vya kutosha, kama nchi za wenzetu wanaweza kwa nini sisi tushindwe, na kuna haja gani ya kujadili sheria au miswada mingine ambayo mwisho wake ina vurugwa na Raisi. Ama sivyo ndio hivyo tena hao wabunge wataendelea kula Pipi, wakati Ma-raisi na marafiki zao wanakula Kuku kwa Mrija.
 
Recta,
Mkuu shukrani sana kwa hoja yako na nadhani nimejaribu kuelezea mambo ambayo Mkapa kasifiwa wakati hakuna hata mmoja wenu anaweza kuweka record hapa Ubaoni tukaona wote zaidi ya nukuu za % ambazo serikali imekuwa ikizitumia.
Ni kweli Mkapa kafanya mazuri (kazi yake ama agizo lake) ambayo ni pamoja na kuandaa policy zinazoweka UCHUMI kama kipaumbele nambari moja kikifuatiwa na UWAZI na katika kufanya hivyo aliweka sawa taasisi zinazoweza kushughulika kuhakikisha kwamba tunaondokana na Umaskini..Lakini pamoja na yote hayo tumebakia ktk Umaskini na utekelezaji wa strategies zote zilizowekwa ulifanyika kwa njia za Ufisadi hivyo kuondoka credits zote ambazo mnataka kumpa..Uongosi sio kupanga Policies na strategies isipokuwa ni pamoja na Usimamiaji ktk Utekelezaji wake!..Uki-fail utekelezaji sioni sababu ya kupewa sifa ya aina yoyote!
Nitatumia mfano mdogo sana hapa..

Binafsi nitasema hivi, sioni sababu ya kumpa sifa daktari ambaye kamkuta mgonjwa (Uchumi wetu) mahututi hawezi hata kutembea, akamtazama na kugundua maradhi yake kuwa ni cancer changa inayoweza kutibika. Sasa katika dose alizopewa mwanzo mgonjwa wetu alionekana kupata nafuu kwani alikuwa hawezi kutembea mara akaweza kuinuka Kitandani...very encouraging...au sio!
Lakini baada ya muda mgonjwa wetu akarudia hali ile ile mbaya wakati alipobadilisha Daktari (Kikwete).. Na Uchunguzi ulipofanywa ilionekana kuwa Mgonjwa wetu (Uchumi)alikuwa hapewi dawa ya cancer isipokuwa steroid ambazo zilimwezesha kupata nguvu ya misuri, Mishipa na kimwili kwa muda wote wakati hilo gonjwa Cancer ndio kwanza lilizidi kusambaa mwilini...
Sasa ndio nasema inakuwaje tumsifie Mkapa? Je ni kwa sababu aligundua kuwa mgoinjwa wetu ana cancer?.. au hiyo dawa iliyotakiwa kutumika ambayo dakari yeyote wa maradhi hayo angeipendekeza (meaning ni somo la uchumi)..
Je, hizo sifa bado zitaendelea kama tukigundua kuwa hata hayo maradhi na dawa yake hakuyagundua yeye isipokuwa ushauri wa dakari mwingine (IMF) hivyo alikuwa tu akifuata ushauri aliopewa!..
Na mwisho kabisa, wakati tukimpa sifa za udaktari tunakuja gundua tena kuwa Mkapa kwanza hakuwa na muda kabisa wa kumtibu mgonjwa wetu zaidi ya kutumia muda mwingi ktk ulevi, na kibaya zaidi kafungua kiji zahanati chake cha kuuza madawa ya cancer chini ya meza ili kujitajirisha yeye mwenyewe..
Now, mimi sitazami kujitajirisha kwake kama hoja kubwa hapa, isipokuwa Mkapa kashindwa kumtibu mgonjwa wetu Tanzania kwa dawa zinazotakiwa badala yake kampa steroids..na leo hii ni mahututi kiasi kwamba tunaanza kujiuliza huyu kweli Mkapa alikuwa daktari mzuri!.. Zile monitor ukutani zinazoonyesha mapigo ya moyo (inflation rates) haziwezi kutumika kama kigezo cha tiba ikiwa dawa alizopewa mgonjwa wetu ni steroid. Kama unapinga hili nipe data za uhakika..

Mkuu Inflation iliyokuwepo wakati wa Mwinyi ni ipi haswa ikiwa Nyerere mwenyewe alikataa kabisa kukubali thamani halisi ya shilingi yetu..Na alipoingia Mwinyi nakumbuka tulitoka Tsh. 17 hadi 21 kwa muda mfupi wakati change mitaani ilikuwa Tsh. 175 kwa dollar..By July, 1985 tukaruka hadi Tsh 110 kwa Usd 1 miezi sita tu Mwinyi alipoingia Ikulu na bado thamani ya shilingi yetu ilitakiwa kuwa adjusted hadi ikafikia hata shilingi ya Kenya iwe mara 10 ya shilingi yetu.
Mnashindwa kukumbuka kwamba Mwinyi alikuwa rais wakati wa mabadiliko ya Kiuchumi na mambo mengi muhimu Kiuchumi yalitakiwa kurekebishwa kwani kama unakumbuka hata Daladala tulikuwa tukipanda kwa Tsh 5 back then mara Mwinyi alipoingia tukarusha nauli hadi Tsh. 100...
Sasa chukulia Mwinyi ambaye alilazimika toka Tsh. 21 to Tsh 500 by the time anaondoka, tazama uzalishaji nchini na bei za vitu wakati ule kisha linganisha na Mkapa ambaye alichukua toka Tsh. 500 akatuacha Tsh 1100 alipoondoka, Uzalishaji ndani ulikuwa vipi kama sio Imports tupu ku supply demand iliyokuwepo! na watu hawakuweza ku afford hata kidogo isipokuwa kwa kutumia wizi wa fedha za Umma na kuzisambaza mitaani..

Kibaya zaidi ni kwamba kati yao wote hakuna aliyejenga miundo mbinu ya uzalishaji zaidi ya kutumia urithi alioacha Nyerere au kuruhusu Imports na uwekezaji toka nje wakati wananchi wenyewe wamesahauliwa kabisa.
Makusanyo ya kodi, tumeona waliokuwa wakiumia ni wananchi tena ktk Imports kwani hatukuwa na kitu cha ku export zaidi na hao wawekeshaji wakifaidika na nafuu za kodi..

Chini ya Mkapa ATC ilikufa na kuingia Ubia wa kuibiwa na SAA. TRC chombo cha kusafirishia mazao na mali ghafi kuja bandarini ilikufa taratibu hadi kufungwa kabisa chini ya Mkapa..Mashirika karibu yote tunayojutia leo yamekufa wakati wa Mkapa aidha kwa kufungiwa kanyaboya ama kuchukuliwa na viongozi wenyewe..Na umezungumzia shule mkuu umesahau kuwa ni wakati wa Mkapa hata Primary school zilikuwa zote za kulipia.. Na record inaonyesha drop kubwa ya wanafunzi kujiandikishwa shule miaka ya Mkapa kuliko wakati wowote ule! - How can you guys forget that..
Hizi sifa mnazompoa Mkapa ni zipi jamani!..
Mkuu kama kweli tumefikia sisi Watanzania kumwita Mkapa Mr. Clean na ati kafanya mazuri na mtawala bora kuliko viongozi wote.. then sisi Wadanganyika TUNA TATIZO kubwa sana! Na inatisha sana kuona hivyo labda tu iwe kwamba kundi lenu ni asilimia ndogo sana ukilinganisha na wale wanaopinga. Hata Bush Kichaka ana % ya watu wanaosema He is the best Presidaa baada ya Reagan kwa sababu ati kaifanya Marekani imekuwa SAFE.
Mimi nashindwa kabisa kuwaelewa Wamarekani hao, kwani kabla ya Bush kushika madaraka Marekani haijawahi kushambuliwa ama kuvamiwa toka mashambulizi ya Wajapan -Pearl Harbor mwaka 1941, iweje leo waseme nchi imekuwa safe kwa miaka 7 tena ya Bush hali ni wakati yeye akiwa kiongozi Marekani ndio ilishambuliwa baada ya miaka 60 ya Usalama...
 
Mkuu Mkandara, natanguliza heshima kubwa.

Mfano wako wa Mgonjwa hapo juu nimeupenda. Ila hiyo ndio sababu ya MUSEVENI Kung'ang'ania madaraka. Maana kila siku anaona hakuna anaeweza kuendeleza gurudumu akiliachia. Ila nakusihi ukumbuke kuwa hata Madaktari bingwa huanza kutibu mgonjwa mahututi kwa kumpa nguvu kabla ya kumpa dozi kubwa. na kutegemea hali ya mgonjwa, dozi kubwa inaweza kuchukua muda mrefu kabla haijawa administered.

Anyway, nimekuelewa. Ila miaka kumi (10) ya uongozi wa nchi si mingi sana. Na katiba hairuhusu ziada. Inachotegemewa ni kiongozi anaefuata kuendeleza yaliyoanzishwa na kuyaboresha ili yafae zaidi. Hilo lisipofanyika, kumsengenya na kumlaumu aliepita ni uonevu mkubwa. Mkapa aliweka misingi ya maendeleo endelevu. Sina haja ya kurudia ubinifu katika makusanyo ya kodi hadi mipango ya kukuza uchumi.

Umenichanganya kidogo kwenye tathimini zako za inflation. Maana naona unaonyesha kuwa kulikuwa na inflation zaidi wakati wa awamu ya 2 kuliko ilivyokuwa awamu ya 3 (kinyume na hoja yako). Nakuomba utumie % za inflation kati ya awamu hizo mbili bila kutumia data tofauti. utagundua kuwa tuko pamoja. 21 to 500 ni ongezeko la asilimia zaidi ya 1000. 500 to 1100 ni ongezeko la asilimia 100. Sijui kama nimekuelewa vizuri. Maana kama ni hivyo umenitisha kuliko nilivyodhani Mkuu.

Kukusanya kodi ni lazima kwa taifa lolote. Na hakuna anaependa kutoa pesa. Sasa ulitaka nani atoe kodi zaidi ya mwananchi? Maana nchi hii ni yao. Miundo mbinu iliyoachwa na Nyerere ni ipi? Labda useme iliyoachwa na mkoloni. Ila kwa kweli Mkapa alijenga sana barabara, madaraja, shule, na kadhalika. Nadhani ukisema alirithi miundombinu utakuwa sahihi kiasi kidogo sana.

Ni kipindi cha Mkapa ndipo elimu ya msingi ilipoondolewa ADA. Nadhani unakumbuka Mkuu. hiyo iliongeza sana usajili wa wanafunzi na ndio challenge ya awamu ya 4 katika mpango wa MMES (uliobuniwa awamu ya 3), ili kuongeza shule za sekondari kutosha mahitaji yanayozalishwa na shule za msingi. Please Mkuu Mkandara, give credits where it is deserved.
 
Sasa chukulia Mwinyi ambaye alilazimika toka Tsh. 21 to Tsh 500 by the time anaondoka, tazama uzalishaji nchini na bei za vitu wakati ule kisha linganisha na Mkapa ambaye alichukua toka Tsh. 500 akatuacha Tsh 1100 alipoondoka, Uzalishaji ndani ulikuwa vipi kama sio Imports tupu ku supply demand iliyokuwepo! na watu hawakuweza ku afford hata kidogo isipokuwa kwa kutumia wizi wa fedha za Umma na kuzisambaza mitaani..

Kibaya zaidi ni kwamba kati yao wote hakuna aliyejenga miundo mbinu ya uzalishaji zaidi ya kutumia urithi alioacha Nyerere au kuruhusu Imports na uwekezaji toka nje wakati wananchi wenyewe wamesahauliwa kabisa.
Makusanyo ya kodi, tumeona waliokuwa wakiumia ni wananchi tena ktk Imports kwani hatukuwa na kitu cha ku export zaidi na hao wawekeshaji wakifaidika na nafuu za kodi..

Chini ya Mkapa ATC ilikufa na kuingia Ubia wa kuibiwa na SAA. TRC chombo cha kusafirishia mazao na mali ghafi kuja bandarini ilikufa taratibu hadi kufungwa kabisa chini ya Mkapa..Mashirika karibu yote tunayojutia leo yamekufa wakati wa Mkapa aidha kwa kufungiwa kanyaboya ama kuchukuliwa na viongozi wenyewe..Na umezungumzia shule mkuu umesahau kuwa ni wakati wa Mkapa hata Primary school zilikuwa zote za kulipia.. Na record inaonyesha drop kubwa ya wanafunzi kujiandikishwa shule miaka ya Mkapa kuliko wakati wowote ule! - How can you guys forget that..
Hizi sifa mnazompoa Mkapa ni zipi jamani!..
Mkuu kama kweli tumefikia sisi Watanzania kumwita Mkapa Mr. Clean na ati kafanya mazuri na mtawala bora kuliko viongozi wote.. then sisi Wadanganyika TUNA TATIZO kubwa sana! Na inatisha sana kuona hivyo labda tu iwe kwamba kundi lenu ni asilimia ndogo sana ukilinganisha na wale wanaopinga. Hata Bush Kichaka ana % ya watu wanaosema He is the best Presidaa baada ya Reagan kwa sababu ati kaifanya Marekani imekuwa SAFE.
Mimi nashindwa kabisa kuwaelewa Wamarekani hao, kwani kabla ya Bush kushika madaraka Marekani haijawahi kushambuliwa ama kuvamiwa toka mashambulizi ya Wajapan -Pearl Harbor mwaka 1941, iweje leo waseme nchi imekuwa safe kwa miaka 7 tena ya Bush hali ni wakati yeye akiwa kiongozi Marekani ndio ilishambuliwa baada ya miaka 60 ya Usalama... MKANDARA UMESEMA MENGI SANA, KTK YOTE UNAYOYASEMA SIONI CONVICTION AGAINST MKAPA BALI NI LAWAMA ZA MAKUSUDI UNAZOTAKA JAMII IAMINI KUWA MKAPA ALIKUWA HEAD PREFECT, MSIMAMIZI WA USAFI, ASKARI WA ULINZI NA USALAMA, MGAWA CHAKI,MGAWA UJI YEYE N.K
MKUU, NI VEMA UKAANZA KUELEWA NA WEWE KUWA TUPO WENGI SANA TUNAOFAHAMU GAME YENU, NARUDIA KUSEMA HISTORIA HUJENGWA NA MUHUSIKA NA SI VINGINEVYO, TSHS 21-500 NI MARA NGAPI KULINGANISHA 500-1100!!!! INGAWAJE KWA VILE UMEAMUA KUPOTOSHA, DOLA NA MKAPA ILIANZA KWA TSHS 600 NA SIYO 500 KAMA UNAVYOJARIBU KUTUAMINISHA HAPA,MWINYI ALIANZA NA TSHS 20 KWA PAUNDI SIYO DOLA JIBU UNALO WEWE. ATC NI KAMPUNI ILIYOKWISHA POTEZA MUELEKEO KABLA HATA BEN HAJAINGIA IKULU ILA KAMA SEHEMU YA SERIKALI ALIRITHI MPANGO WA AWAMU YA II BY THEN MUNGAI NDIYE M/KITI WA BODI, USITUDANNYE MKUU TUNAFAHAMU YALIYOJIRI TANGU MWANZO HUKO ATC, SHIRIKA LA RELI LILIKUWA HOI TANGU ENZI YA KAMBARAGE, MUULIZENI JANGUO NA BAKILANA. MCHAKATO WA MAGEUZI ULIANZIA AWAMU YA III NA JK AKARITHI MCHAKATO HUO KAMA MKAPA ALIVYORITHI ATC. NAJIULIZA HIZI FACT KWENU HAZIPO AU KWA MAKUSUDI MMENUWIA KUWA WAPOTOSHAJI TU?!!!! SERIKALI NI TAASISI INAYOKUWA KIUTENDAJI KADRI SIKU ZINAVYOENDA, CHANGAMOTO NI NYINGI NA NAMNA YA KUZI TACKLE UTATOFAUTIANA NA KADRI MKUU WA NCHI ALIYEPO, NAKUBLIANA NA YULE ALIYESEMA KUWA ASIGNMENT NAMBARI WANI KWA JMK NI KUFUTA MAAMUZI AMBAYO YALICHUKULIWA NA WATANGULIZI WAKE PALE SERIKALI INAPOJIRIDHISHA KUWA UMUHIMU WAKE KWA MAZINGIRA YA SASA NI MDOGO SANA/HAUPO. NA HILI LINAFANYIKA SANA TANGU ENZI YA MWINYI-MKAPA NA SASA JMK, SASA HIZI BEZO NA DHARAU ZA NINI KWA MKAPA?!!!
NILISHAWAHI KUMWAMBIA FMES KUWA 2008 ITAPITA NA NDOTO YA KUMPELEKA MKAPA KWA PILATO HAITATIMIA KAMWE, AKASEMA NINAMTISHA NA YEYE HATISHIWI, NIKAMUELEZA KWA UPOLE KUWA KUWA MIMI SI KITISHO KWAKWE KWA LOLOTE BALI IMENIPASA KUSEMA YALE KWA IMANI NA HESHIMA YANGU KWAKE KUWA TUNAHESHIMU SANA CONTRIBUTION ZAKE HUMU JAMVINI ILA HAPA ANAPOTOKA NA SIKU YA SIKU ATASHINDWA KUSIMAMA NA KUUKANA UBASHIRI WAKE. MKANDARA JITAHIDI KUWA MUUNGWANA KWA NAFSI YAKO KWANZA KABLA YA KUTUFANYIA MAJUMUISHO YA KILE UNACHOAMINI NA KUPENDA WEWE KIWE NDIO MSIMAMO, DHAMIRA NA MUELEKEO WETU SOTE, TUNAHESHIMU MAONI YAKO ILA NI VEMA UKARUHUSU UKWELI NAO UPATIKANE TOKA KWAKO PIA, SIPENDELEI WATU WANASHIKILIA MSTARI MMOJA WA BIBLIA KAMA NDIO MSINGI WA MAAGANO YOTE YA MUNGU NA WANA ISRAEL. NAWASILISHA
 
Naona tunapoteza mwelekeo hapa... ishu ni huyu mtu Mkapa kwanini asifikishwe kwa pilato kwa makosa yalioainishwa na Rev,,,, hayo ya kafanya kazi ya kujenga shule, sijui kukusanya kodi ni kutimiza wajibu,...kwanza kazi aliiomba mwenyewe. Na nasisi watanzania tulimuhakikishia maisha mazuri for life kwa kutumia kodi yetu, kama malipo ya kutimiza wajibu wake kwa taifa... tuache blah blah hapa, madudu ya Mkapa ni mengi, yame overwhelm mazuri machache(yapo)...kwa walio yasahau, pengine kutokana na kufaidi asali ya hayo madudu yake..... nawawekea tena hapa kwa mujibu wa Rev. kwa uchache ni....

  • Benki Kuu na kashfa zote; Meremeta, Epa, CIS, Tangold, Minara na menginewe.
  • Miundombinu na Nishati: ATC, TRL, Rada, IPTL, Richmond, Kiwira, Ndege ya Rais, Helikopta za Jeshi na mengine.
  • Demokrasia butu: uonevu kwa vyama vya siasa na wafuasi wa vyama ambavyo si CCM, kwa kutumia nguvu ya dola kama kule Pemba, mauaji ya Mwembechai, kufilisi au kutoza ushuru na kodi ya kukomoa kwa mwenye kuipinga CCM na Serikali ya Mkapa na mengineyo.
  • Uwekezaji: Mikataba mibovu, sheria mbovu ambazo zinawapendelea wawekezaji na kulipunguzia Taifa mapato
.
 
Date::12/24/2008
Pinda: Serikali haimwogopi Mkapa

Exuper Kachenje na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amevunja ukimya na kuzungumzia mjadala wa kutaka Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumiliki mgodi wa Kiwira akisema hilo linawezekana kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Katika mahojiano maalum na gazeti dada la Mwananchi la The Citizen, Pinda alisema kuwa serikali haina sababu ya kuhofia suala hilo kwa kuwa kila anayetuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani.

"Tunatakiwa kuafiki juu ya utawala wa sheria. Sheria kwa urahisi kabisa inasema hakuna mtu aliye juu yake. Hivyo kama utafanya kosa, hasa la jinai, sheria inakutaka ufikishwe kwenye chombo kinachohusika ambacho ni mahakama," alisema Pinda.

Waziri Mkuu alisema hayo alipotakiwa kueleza endapo serikali yake haitishwi na madai ya jamii kutaka rais huyo mstaafu akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zinazomkabili za kumiliki Mgodi wa Kiwira kinyume cha sheria.

Hata hivyo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyosambazwa jana jioni, imesema haifanyi uchunguzi wowote wa kijinai dhidi ya kiongozi huyo.

"Sina hofu kuhusu suala la Kagoda wala Kiwira, wanachosema watu ni suala la wakati kwa sababu sheria inasema hakuna mtu aliye juu ya sheria," alisema Pinda.
Kwa muda mrefu sasa wanasiasa wa upinzani na baadhi ya wananchi wamekuwa wakishinikiza kuchukuliwa kwa hatua kadhaa dhidi ya rais mstaafu wa awamu ya tatu Mkapa akamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za makosa aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake.

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Mkapa analindwa na sheria ya kinga dhidi ya rais, inayozuia kumfikisha mahakamani na kumshtaki kwa makosa aliyoyafanya alipokuwa madarakani.

Suala hilo limeonekana kuviweka njia panda vyombo mbalimbali vya maamuzi ikiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambalo baadhi ya wabunge wake wameripotiwa kutaka kuwasilisha hoja ya kumwondolea kinga Mkapa ili aweze kufikishwa mahakamani.

Takukuru ambayo taarifa yake kwa vyombo vya habari ilimwita Mkapa kama Rais mstaafu wa awamu ya pili (usahihi ni Rais mstaafu awamu ya tatu), ilisema imeamua kutoa ufafanuzi huo kutokana na taarifa mbalimbali ambazo zimejitokeza katika vyombo vya habari.

"Katika siku za karibuni kumekuwapo na uvumi ambao umekuwa ukitolewa katika baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari ukibeba ujumbe kwamba Rais mstaafu wa Awamu ya Pili (awamu ya tatu), Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, anachunguzwa na vyombo vya dola, ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa," inasema sehemu ya taarifa ya Takukuru.

Taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na rushwa imesema uvumi kwamba taasisi hiyo inamchunguza Rais mstaafu Mkapa hauna ukweli wowote na kwamba Takukuru haimchunguzi kiongozi huyu kwa kosa lolote au tuhuma yoyote ya kijinai kama inavyodaiwa.

Taarifa hiyo ya Takukuru iliukumbusha umma wa Watanzania juu ya matakwa ya katiba ya nchi ambayo Takukuru inawajibika kuilinda na kuiheshimu hasa Ibara ya 46(3) ambayo inazuia kumshtaki Rais mstaafu.

Ibara hiyo ya katiba inatamka kwamba, "Isipokuwa kama ataacha, kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara 46 a (10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa katiba hii."

Takukuru ikisisitiza ilisema, kama sheria mama (katiba) imeweka pia mipaka katika kushughulikia mambo mbalimbali ya nchi, ni mantiki hiyo hiyo ambayo inaonyesha haja ya kuheshimiwa wakati wote.

Kuhusu hoja ya kutaka kuandikwa kwa Katiba mpya ya Tanzania, Pinda alisema serikali yake haiogopi suala hilo na kwamba cha msingi ni kuyafanyia mabadiliko mapungufu yanayobainika na kukubalika.

Akitoa mfano wa nchi ya Marekani, Waziri Mkuu Pinda alisema nchi hiyo imefanya mabadiliko mengi ya katika katiba yake, lakini hawajawahi kuzungumzia kuandikwa kwa Katiba mpya kama ilivyo kwa baadhi ya Watanzania.

Alisema kimsingi kuandika katiba mpya ni sahihi kwa taifa lililotoka katika makucha ya utawala wa kikoloni na kwa taifa kama Tanzania kuandika Katiba mpya inamaanisha kusimamisha matumizi ya katiba iliyopo.

"Suala si kuandika katiba mpya, bali ni kuweza kuiboresha katiba iliyopo," alisema Pinda.

Mkapa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, kinyume na taratibu za madaraka ya umma wanatuhumiwa kuanzisha Kampuni ya Tanpower Resources na kununua Mgodi wa Kiwira kwa fedha ambazo haziendani na thamani ya mgodi huo.

Tanpower Resources inatuhumiwa kununua Mgodi wa Kiwira wenye thamani ya Sh 4 bilioni, lakini yenyewe ikatoa Sh 700 milioni.

Pia Mkapa anatuhumiwa kuanzisha Kampuni ya Anben wakati akiwa Rais.

Tayari Daniel Yona na Basil Mramba ambao walikuwa mawaziri katika serikali ya Mkapa wanashtakiwa kwa tuhuma za kutumia madaraka vibaya na kulisababishia taifa hasara ya Sh 11.9 bilioni, ikiwemo misamaha ya kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart Asseyers.
 
Recta, FDR.Jr,
Wakuu zangu kwanza nami natanguliza heshima kubwa ktk kuendeleza huu mjadala... Na nasikitika tu ndugu zangu mnaposema tuna NJAMA ktk ukweli ambao nimejaribu kuuzungumzia kwa uwazi zaidi bila kumpendelea mtu ama kundi fulani.
Swala la ongezeko ama kushuka kwa thamani ya shilingi yetu wakati wa Mwinyi nadhani mmeshindwa kuelewa kwamba nimesema wakati wa Mwinyi ulikuwa wakati wa mageuzi ya Uchumi na nimeonyesha sababu ambazo zilitulazimu kufanya. Hata nikamweka Nyerere kuwa ndiye sababu ya ya kuithamanisha shilingi yetu juu pamoja na kwamba mitaani dollar ilikuwa ikinunuliwa kwa Tsh. 175.
Hakuna hata mmoja wetu angefanya tofauti iwe Nyerere mwenyewe, Mkapa au Kikwete inapofikia thamani halisi ya shilingi hivyo sio swala la Mwinyi kuishusha shilingi isipokuwa shilingi yetu ilithaminiwa kuliko ukweli uliopo.
Chukulia, Wall street ambako kampuni moja imethaminisha pato lake na kupandisha hisa zake kinyume cha ukweli, kisha shirika linapoanza kuanguka itokee kubainika kwamba hesabu hizo hazikuwa sawa.. mfano chukua shirika la Enron.. Hatuwezi kumlaumu kiongozi aliyefuata kwa kutoa figures za kweli kushusha thamani ya shirika hilo isipokuwa anapongezwa kwa kuonyesha ukweli..
Kwa hiyo nilipotaja ya Mwinyi nimeonyesha sababu ambayo ni nje ya uwezo wake sio kwamba nimetetea kwamba hapakuwepo inflation... na ndio maana nimezungumza huko nyuma kuwa mambo mengi Tanzania hupikwa kimahesabu bila kufuata sababu haswa za maradhi yetu..

Hata hivyo, mmeshindwa kuelewa swali langu ktk kutoa hoja ya Tsh 21 hadi Tsh. 500 ukilinganisha na Tsh.500 kwenda 1100.. hoja yangu haikusimama ktk kulinganishadepreciation ya shilingi ktk nyakati mbili tofauti isipokuwa kutazama mfumko wa bei (inflation) kulingana na wakati..

Kama unakumbuka vizuri nimewahi kusema mwaka 1995, nyumba za Kariakoo zilikuwa zikiuzwa kwa dollar 20,000, wanunuzi wa kutafuta na kukamatia..hata wahindi wenyewe walishindwa kuzichukua wakisema ni ghali. Ilipofika mwaka 2000 tayari nyumba hizi ziligonga 400,000 na kwaka 2005 zilifIkia 800,000. Hizi bei zote zimepikwa na hali halisi mitaani na raia wenyewe wanaathirika na Inflation wakati serikali inazi value nyumba hizi chini ya 100,000. tazama nyumba walizouziana ndio hesabu serikali inataka watu tuamini wakati wao leo hii wako mahakamani nyumba hzile zile zimepanda bei kwa aslimia 100..

Recta, Mkuu wangu Mwinyi ndiye aliyekuwa akitumia dawa ya kuongeza nguvu UV (drip water) kwa mgonjwa wetu Tanzania na wakati huo huo akitazamwa na madaktari kibao kutafuta kilichosababisha gonjwa la uchumi wetu...Ujamaa peke yake haiwezi kutosha ni sawa na kusema tulikuwa tukivuta sigara sana hiyo ndio sababu,, Ni muhimu kufanhamu ni kitu gani ndani ya sigara kinachosababuisha cancer ili tuepuke kuvuta vitu vyote vinavyotengenezwa na hizo chemical sijui nicotine, benzine na cyanide, lakini tumbaku yenyewe (Ujamaa) haina madhara..
Na ndilo tatizo kubwa la nchi yetu kwamba pamoja na kuingia Ubepari tumetupa hata zao la tumbaku na Ujamaa umepewa tafsiri nyingine mbaya ambayo inazidi kututenganisha..

FDR. Jr,
Mkuu wangu kama hukuona ktk maisha yako sababu ambazo zinamfanya Mkapa kutokuwa kiongozi mzuri na nimejaribu kuyaeleza hapa bado hujaona basi mkuu wangu Tanzania tunakoelekea ni kubaya na inanifanya niamini kwamba Ndivyo Tulivyo..
 
Nashukuru sana Mkuu Mkandara. Tunaendelea vizuri. Ila kukusahihisha tu katika mambo machache, ongezeko la bei hutokana na demand kuongezeka kulingana na supply iliyopo. Najua unaelewa hili vizuri tu.

Ukisema awamu ya 2 ilifanya udaktari, nitakubaliana nawe kwa sehemu ndogo. Maana nakubali kuwa Nyerere aliiacha nchi ikiwa hoi. Naamini aliondoka baada ya kuona hakuna la kuongoza tena. Mwinyi alirekebisha sana hasa katika kipindi chake cha 1. Maana alitutoa matongotongo yaliyokuwepo kuwa "Pesa sio Msingi wa Maisha". Sasa hivi ukisema maneno hayo, unaweza kupigwa mawe. Ila kipindi cha 2 cha awamu yake, mambo hayakuwa shwari. Maana uchumi uliporomoka, rushwa ikakua sana kiasi kwamba hata wahisani wakagoma kuendelea kushirikiana nasi kiuchumi (TULIKUWA HATUKOPESHEKI. Licha ya kusaidiwa kwa misaada mingine). Mkuu takwimu zinaonyesha ukuaji wa uchumi, kushuka kwa inflation katika awamu ya pili. Kama hilo unalibishia, naomba utupe takwimu zako, tuziangalie. Ili mradi zitoshe kuangalika tu.
 
Ukweli ni kwamba issue ya Rais Mstaafu haihusiani na ile ile kinga ya kutofikishwa mbele ya sheria. Hapa wanachanganya mambo mawili ya president kama institution na president kama person. Kinga ya rais inahusiana na kutofikishwa mahakamani kwa maamuzi ama matendo yoyote aliyoyatenda wakati akiwa madarakani as a person lakini maamuzi aliyoyafanya as a presideatial institution.
Maamuzi kama kusaini hati ya kunyongwa. Baada ya hukumu kutekelezwa wana ndugu wenye uwezo wakaamua kuseek 'court review' na hatimaye mahakama ikajiridhisha kweli mtuhumiwa alihukumiwa kimakosa na adhabu imeshatekelezwa. Haya ndiyo baadhi ya makosa ambayo rais anaweza kuyatenda akiwa madarakani mengine ni kama kurevoke title deeds. Kustaafisha maofisa kwa manufa ya umma nk.
Suala la ununuzi wa Kiwira, Rais Mstaafu amelifanya kama Ben Mkapa at personal capacity na sio kwa presidential institution. Hapa ametumia haki yake ya kikatiba kupitia private office yake na kusajili kampuni ya AnnBen na mamaa kama ambavyo wewe na mkeo mnao uhuru huo.
Swali ni kama jee ni kosa kwa mujibu wa sheria zetu rais akiwa - madarakani kusajili kampuni?. Haijakatazwa popote. Haya baada ya kusajili hiyo kampuni jee utaratibu uliofuatwa mpaka AnnBen
Wakauziwa Kiwiri ni wa kawaida kama kampuni ingekuwa ya mimi na wewe?.
Hapo ndipo kinga ya Mhe. Ilipoishia, kama kuna upendeleo wa aina yoyote Mhe. Ben anafikishwa mahakamani kama mhalifu mwingine yoyote.
Japo sheria ya Tanzania mashitaka yote ya jinai ni lazima yapelekwe na Jamuhuri baada ya OK ya DPP, sheria pia inatoa option ya Private Prosequition ambapo mtu ama taasisi binafsi inaomba kibali mahakama kuu cha kuendesha mashitaka ambayo serikali kupitia ofisi ya DPP inaonekana wazi haiwezi kuyaendesha kwa haki. Mahakama Kuu ikiridhika na hizo sababu inatoa kibali na Mhe anaburuzwa mahakamani. Hapa hakuna issue ya kinga.
Ni kama vile rais alipokuwa madarakani, akamtwaa mke wako akazini nae na unao ushahidi. Kutembea nje ya ndoa sio kosa la jinai bali ni kosa la madai. Wewe una uhuru wa kumfungulia kesi ya madai na anafikishwa mahakamani bila kinga yoyote maana kutembea na mke wa mtu sio miongoni mwa majukumu ya rais ndani ya taasisi ya urais
(president under presidential institution).
 
mamlaka zinazungukazunguka bila kufanya chochote wka sababu aidha hawajaliona kosa lilofanya Mkapa au na wao wanaogopa wakimtndea Mkapa hivi, basi na wao watatendewa kama hivyo hivyo siku za usoni
 
- Hivi karibuni kumekuwa na kauli nyingi za kukingana kati ya Pinda na Muungwana, hapa Muungwana alisema Mkapa aachwe apumzike, lakini Pinda anasema haogopwi.

- Wanaoyajua vizuri ya huko ndani wananiambia niogope Pinda maana huwa hasemi bila matendo na kwamba hii ya Kisutu ni operation yake, sasa anaposema hamuogopi Mkapa, ninapata faraja sana kwamba hii ngoma ya Kisutu inogile eh! he! he! he! inogile mwananagu! Tanzania inogile ooh! ooh! inogile!!!!
 
Ukweli ni kwamba issue ya Rais Mstaafu haihusiani na ile ile kinga ya kutofikishwa mbele ya sheria. Hapa wanachanganya mambo mawili ya president kama institution na president kama person. Kinga ya rais inahusiana na kutofikishwa mahakamani kwa maamuzi ama matendo yoyote aliyoyatenda wakati akiwa madarakani as a person lakini maamuzi aliyoyafanya as a presideatial institution.
Maamuzi kama kusaini hati ya kunyongwa. Baada ya hukumu kutekelezwa wana ndugu wenye uwezo wakaamua kuseek 'court review' na hatimaye mahakama ikajiridhisha kweli mtuhumiwa alihukumiwa kimakosa na adhabu imeshatekelezwa. Haya ndiyo baadhi ya makosa ambayo rais anaweza kuyatenda akiwa madarakani mengine ni kama kurevoke title deeds. Kustaafisha maofisa kwa manufa ya umma nk.
Suala la ununuzi wa Kiwira, Rais Mstaafu amelifanya kama Ben Mkapa at personal capacity na sio kwa presidential institution. Hapa ametumia haki yake ya kikatiba kupitia private office yake na kusajili kampuni ya AnnBen na mamaa kama ambavyo wewe na mkeo mnao uhuru huo.
Swali ni kama jee ni kosa kwa mujibu wa sheria zetu rais akiwa - madarakani kusajili kampuni?. Haijakatazwa popote. Haya baada ya kusajili hiyo kampuni jee utaratibu uliofuatwa mpaka AnnBen
Wakauziwa Kiwiri ni wa kawaida kama kampuni ingekuwa ya mimi na wewe?.
Hapo ndipo kinga ya Mhe. Ilipoishia, kama kuna upendeleo wa aina yoyote Mhe. Ben anafikishwa mahakamani kama mhalifu mwingine yoyote.
Japo sheria ya Tanzania mashitaka yote ya jinai ni lazima yapelekwe na Jamuhuri baada ya OK ya DPP, sheria pia inatoa option ya Private Prosequition ambapo mtu ama taasisi binafsi inaomba kibali mahakama kuu cha kuendesha mashitaka ambayo serikali kupitia ofisi ya DPP inaonekana wazi haiwezi kuyaendesha kwa haki. Mahakama Kuu ikiridhika na hizo sababu inatoa kibali na Mhe anaburuzwa mahakamani. Hapa hakuna issue ya kinga.
Ni kama vile rais alipokuwa madarakani, akamtwaa mke wako akazini nae na unao ushahidi. Kutembea nje ya ndoa sio kosa la jinai bali ni kosa la madai. Wewe una uhuru wa kumfungulia kesi ya madai na anafikishwa mahakamani bila kinga yoyote maana kutembea na mke wa mtu sio miongoni mwa majukumu ya rais ndani ya taasisi ya urais
(president under presidential institution).

Well said Pasco. Kinachotokea bongo juu ya Mkapa ni kulindana tu. Sheria zipo wazi kabisa na Mkapa anayo mashtaka ya kujibu kwa madudu aliyoyafanya akiwa ikulu kama "mtu binafsi - mkapa". Kilio hiki ni cha kitaifa. Mkapa haonewi kabisa. Ni muda tu haujafika. Lakini na muda huo ndio unakaribia kwa kasi. Subiri hizi kesi za kina Mgonja, Mramba na Yona. Zinaelekea kumuita Mkapa mahakamani. La sivyo, Mgonja et al. nao hawana kesi ya kujibu, na CCM itakuwa imefikia mwanzo wa mwisho wa kushika hatamu nchi nchi hii.
 
Nimesoma na kusikia tuhuma nyingi dhid ya Mh: Benjamin Wiliam Mkapa,kuna waliojaribu kuziorodhesha kama Rev Kishoka ndani ya makala hii (Trial: People of Tanzania versus Benjamin Wiliam Mkapa) pia Joseph Mihangwa jamiiforums 05 11 2008 (kwa nini Mkapaamekosa tena tunzo ya Mo Ibrahim).
kwa hakika ukisoma mlolongo wa tuhuma hizo cha kwanza kukujia ni Huzuni,unyonge na udhalili kisha Hasira na Ghadhabu kali zinazotaka umuone mh: huyo na umuadhibu ipasavyo.
Wapo wanaodai mbona hamsemi mazuri yake? Hakika Binadamu si kamili tuna mazuri na mabaya,pia tuna mapungufu mengi. Na tuna utamaduni wa kutunzana kwa Mazuri na kuadhibiana kwa mabaya. Na kwa mapungufu yasio ya makusudi husameheana. Hivyo ndivyo ilivyo hata kwa wale tuanaomini sheria za Mungu, Mkapa akidai kuwa moja wao.
Tukumbuke Mkapa Aliaminiwa akaapa kulinda na kutetea katiba. Badala yake akavunja kanuni za katiba alioapa kuilinda na kuitetea, leo tunaambiwa katiba hiyo inamtetea yeye nakumlinda! Basi hayo ni makosa na ibara hiyo haina msingi wa kuzuia maji, hoja ifikishwe Bungeni ijadiliwe namarekibisho yafanwe kama wanavyopendekeza baadha ya Wabunge na wananchi.
Baada ya miaka 47 ya uhuru si Taifa changa tena la kuita jiwe - dongo au mkate - keki, hivyo ikiwa mtu ni fisadi aitwe kwa jina la matendo yake, kama ni mwizi au mbadhirifu aitwe, kwani ndio cheo alichochagua na havunjiwi heshima ila amejivunja.
Urais ni tunu ya hali ya juu( highest privalage) wananchi wanayomtunukia mwananchi mwezao, ati wavivu wa kufikiri? hebu Mkapa akae nawashabiki wake afikirie mamillioni ya wa Tanzania yeye pekee Rais; Nyumba (Ikulu) bure usafiri dezo, ulinzi dezo, marupurupu na kadhalika, na mshahara akalipwa. Na nguvu za dola akapewa, malipo yake? Fadhili ya punda_________________ . Hakuwa na imani chembe ya dini wala ya kibinadamu kwamazuri yake tulimuahidi na kumpatia yaliotajwa hapo juu.
Kwa mabaya yake je? aah katiba inamlinda eeh inamtetea. Waheshimiwa watukururu mlichopaswa kusema swala hili ni letu wananchi tukiamua kurekebisha ibara zinazohusika za katiba nasi tutawajibika. Kauli yenu imekaa kiutetezi mnatutia wasiwasi.
Kumbukeni mshahara wa dhambi ni mauti (warumi 1:10)
 
Back
Top Bottom