Ni wakati muafaka bunge likamuondolea kinga ben ili awajibishwe.
Mwalimu alisema ikulu ni patakatifu na sio sehemu ya kufanya biashara
Kwa nini usianzishe thread yako ukawajadili Mwinyi na Mama Sitti? au ukaanzisha thread kusifu aliyofanya Mkapa? kwa nini utulazimishe kuongea unalotaka na usilianzishie hoja?
rev. Kishoka,
Swala la kumuondolea kinga Mkapa na kumpeleka mahakamani ni hoja finyu na hatari. Kama Mkapa alifanya makosa akiwa rais, basi rais aliyeko madarakani atengue maamuzi hayo na kuyarekebisha. Tuchukue mfano rahisi, wamarekani wamemchagua Obama kuwa rais wao katika kipindi kigumu kabisa. Rais Bush amefanya maamuzi mengi mabaya ambayo yameitumbukiza Marekani na dunia katika msukosuko mkubwa sana, lakini kamwe hautasikia wamarekani wakisema Bush aburuzwe mahakamani kama ambavyo wengi wetu hapa tunavyomshupalia Mkapa aburuzwe kisutu! na hautasikia kamwe Obama akisema 'amerithi' matatizo ya nchi kutoka kwa Bush, wamerekani watampima kwa uwezo wake wa kutatua matatizo yao na sio kwa kisingizio cho chote kile. Vile vile JK hatakiwi kutoa lawama zozote kwamba amerithi matatizo kwa Mkapa. kama kuna maamuzi yeyote mabaya aliyofanya Mkapa, basi atengue (reverse) na abadilishe.
Kumpeleka Mkapa mahakamani kuta -set precedence, ambapo baada ya Mkapa atafuata mzee ruksa, na wakati huo huo JK akijitayarisha kutia nywele zake maji maana baada tu ya kumaliza kipindi chake naye ataburuzwa mahakamani!
kinachotakiwa kufanyika kama nilivyosema ni kutengua maamuzi yote mabaya aliyofanya Mkapa akiwa madarakani tu!
nawasilisha.
Mmmh mtazamo na utetezi wa aina hii ni hatari sana kwa maendeleo yetu na utatutukanisha waafrika kama si watanzania,Makosa ya Bush ni makosa ya 'policy' na si makosa ya kushiriki au kufumbia macho uhalifu dhidi ya mali ya umma kwa faida ya viongozi na wafanyabiashara wachache.
Makosa ya Bush ni makosa ya policy? are you sure? unakumbuka kampuni ya Enron? fuatilia kidogo. haya na vita ya Iraq? is that policy au wendawazimu? kwa namna ye yote ile, Wamarekani wana sababu nyingi nzito za kumburuza bwana kichaka mahakamani, lakini hawafanyi hivyo! sasa jiulize ni kwa nini hawafanyi hivyo?
Sasa unataka awamu ya nne atengue ????!!!! una maanisha auze rada, abomoe majengo pacha ya BOT awarudishe netgroup solution walete fedha walizochukua na kuifilisi TANESCO au awape ATCL ndege ya Rais hayo ni machache kwa mfano tu. naomba ufafanue namna ya ulunganifu uliopo kwa Bush Marekani na Mkapa Tanzania hasa juu ya makosa waliyoyatenda dhindi ya nchi zao.
Mkuu hivi umeandika habari hii kwa kusimuliwa ama!.. inashangaza sana kuona Mtanzania akisifia vitu ambavyo viko wazi na kila Mtanzania anafahamu kwamba Utawala wa Mkapa umetufikisha hapa tulipo leo..Mkapa mtu asiye mvuto, aliyepewa nchi na jkn, aliapa kuli shape taifa, nathubutu kusema kuwa aliianza kazi hiyo kwa ujasiri mkubwa lakini shughuli ni pale alipowagusa wazee, kuna ushahidi kuwa mwalimu ndiye aliyemtaka kuacha kuwafuata wazee na kusaka wachawi na ajikite kujenga nchi aliyopewa, alifanya kazi yake kimyakimya akiwagusa mmoja baada ya mwingine huku akirejea maagizo ya mzee jkn, baadaye akaamua sasa afanye kazi ya ku-shape utawala wa nchi, serikali na idara zake, ajira serikalini,elimu kwa vyuo vya elimu ya juu na baadae msingi na mwisho sekondari,ujenzi wa barabara na madaraja,usambazaji wa umeme,ufutaji wa kodi za maendeleo, kupunguza ada za elimu ya sekondari,kuruhusu mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu visivyo vya serikali, akaamua kama noma na iwe noma pale alipoyaswaga makampuni ya umma psrc kwa kasi ya sunami, akaingia ktk maliasili ya madini hapa kwa kutumia tic ya samwel sitta shughuli ikaanza kwa kasi, taratibu serikali ikajirejeshea ile sifa ya kuwa mteja mkubwa ktk biashara na sekta binafsi kwa kununua na kulipa kwa wakati, taratibu heshima ya mfanyakazi ikarejea serikalini kwa japo hata mabenki kuanza kuwakopesha ingawaje kwa riba kubwa, akaajiri watendaji ndani na nje ya nchi.
rev. Kishoka,
Swala la kumuondolea kinga Mkapa na kumpeleka mahakamani ni hoja finyu na hatari. Kama Mkapa alifanya makosa akiwa rais, basi rais aliyeko madarakani atengue maamuzi hayo na kuyarekebisha. Tuchukue mfano rahisi, wamarekani wamemchagua Obama kuwa rais wao katika kipindi kigumu kabisa. Rais Bush amefanya maamuzi mengi mabaya ambayo yameitumbukiza Marekani na dunia katika msukosuko mkubwa sana, lakini kamwe hautasikia wamarekani wakisema Bush aburuzwe mahakamani kama ambavyo wengi wetu hapa tunavyomshupalia Mkapa aburuzwe kisutu! na hautasikia kamwe Obama akisema 'amerithi' matatizo ya nchi kutoka kwa Bush, wamerekani watampima kwa uwezo wake wa kutatua matatizo yao na sio kwa kisingizio cho chote kile. Vile vile JK hatakiwi kutoa lawama zozote kwamba amerithi matatizo kwa Mkapa. kama kuna maamuzi yeyote mabaya aliyofanya Mkapa, basi atengue (reverse) na abadilishe.
Kumpeleka Mkapa mahakamani kuta -set precedence, ambapo baada ya Mkapa atafuata mzee ruksa, na wakati huo huo JK akijitayarisha kutia nywele zake maji maana baada tu ya kumaliza kipindi chake naye ataburuzwa mahakamani!
kinachotakiwa kufanyika kama nilivyosema ni kutengua maamuzi yote mabaya aliyofanya Mkapa akiwa madarakani tu!
nawasilisha.
mchungaji tafadhari linda heshima yako kwa kuwa mwepesi wa kupokea hoja zinazopingana nawe.
FDR,
Mtarajiwa hakuleta hoja kujibu hoja, kaleta madai bila kujibu hoja na kushurtisha madai yake kama hoja mpya, ndiyo maana hata nimejinukuu tena kumuonyesha ni nini nilikidhamiria katika hoja hii.
Naomba nikuulize mchungaji, hivi JK hakuwahi kuwa waziri katika serikali ya Mkapa? Kama Mkapa aliendesha serikali corrupt JK ni msafi kiasi gani kuweza kumfikisha Mkapa mahakamani?
Nakubalina na wewe kwa kitu kimoja tu kuwa Mkapa alifanya makosa. Na hapa nakupa angalizo siyo Mkapa peke yake viongozi wetu wengi (wakiwemo marais wamekuwa wakifanya makosa na wanaendelea kufanya makosa). Kwa hiyo kumpa JK kisingizio kuwa mambo mengi yameharibika kwa sababu ya Mkapa ni ukosefu wa kufikiri. Ni jukumu lake kurekebisha hayo makosa na kufanya kazi yake sawa sawa. Lakini biashara ya kumwondoa JK katika serikali ya Mkapa ni unafiki usiovumilika kati ya watu wenye kufikiri.
Tumpe hadidu za rejea JK za kufanya kazi, na siyo kazi ya kukamata kamata (bila kujenga mfumo wa utawala bora) wakati Dar inakosa maji, wanafunzi wanafukuzwa na kuteua mawaziri ambao hata hawajui majukumu yao ni nini.
Kwa nini usianzishe thread yako ukawajadili Mwinyi na Mama Sitti? au ukaanzisha thread kusifu aliyofanya Mkapa? kwa nini utulazimishe kuongea unalotaka na usilianzishie hoja?
Kwanini unamtaka Mtarajiwa aanzishe thread wakati wewe umeshaianzisha. Anachofanya hapo ni kukujibu shutuma zako, kwa maoni yake. Kama wewe hukubaliani nayo, si umjibu tu?
Kushtakiwa Mkapa ni ndoto za alinacha. Ni afadhali kutumia muda wenu kufikiria mambo mengine, maana hilo halitatokea. Mnajaribu kumfanya Rais wetu kuwa hajui analofanya. Mnakosea sana. Na wengine mnajua kabisa kuwa akifuata ushauri wenu, nini kitakachotokea. Mnataka kujenga wanasiasa wasiojengeka na kutoa fursa za vyama vya upinzani kujikweza. Taifa gani manalolitaka kwa kuliteketeza?
Mazee Ni kweli kabisa Mukapa aliteleza kama mwanadamu wa kawaida.
Lakini nguvu na ushabiki wa kishindo namuma hii kutaka mukapa awajibishwe unatoka wapi?kuna walaikini,yeah,kuna uwalakini....kwani inaboa kupita kiasi kumwandama Mkapa kwa degree hii,hasa ukizingatia amejitahidi kutuletea maendeleo ya uhakiaka ukilinganisha na marais waliopita na hata aliyeko sasa madarakani ni kilza tuuuuuuuu.
1.Mwinyi alitupeleka kubaya kuliko,nchi ilijaa matatizo ya kila aina.Mfano ulio hai,ni kitendo cha mkewe kuwa kinara wa kuuza madawa ya kulevya hapa nchini,haingii akilini kuona kila kiumbe kinafoka juu ya MKAPA wakati kuna uozo wa karne umefanya na viongozi wengi tuuu hapa nchini.
2.Kero na migogoro ya kidini,iliota mizizi ndani ya kipindi cha Mwinyi na sasa tunashuhudia JK akiiendeleza kwa style yake.why Mukapa mazeee?...udini au?
3.Mwinyi huyu huyu ndie alietaka kuibadilisha TZ kuwa the united islamic republic of TZ,leo hatuhoji,...tunamfokea Mukapa mukapa...why?
Mizizi hii ya mwinyi imedumu hadi sasa na JK anataka kutusilimisha nchi nzima bila aibu tujiunge na OIC,bt we don't see..tumebaki mukapa mubaya mubaya....
4.JK mwenyewe ana mabaya yake kupitiliza,laikini hatuyapi msukumo tunaouumia zidi ya nkapa...
$$$$mukapa ana mabaya yake,hao wachache nao wana maovu yao,hivyo iko haja ya kuhoji kila pande,si jambo jema kumwandama MUKapa.
fair game mazeee
* SOURCE: AlasiriBaada ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kutuhumiwa sana kuwa yeye na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati na Madini Bw. Daniel Yona walijiuzia kwa bei poa Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira, hatimaye suala hilo limefikia arobaini yake kwani sasa litaanikwa hadharani na kujadiliwa kipengele kimoja baada ya kingine.
Aidha, wabunge kibao wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanadaiwa kuwa wameshajipanga katika kulijadili kwa undani suala hilo, ambalo linadaiwa kuwa limejaa utata na kuna wakati lilizusha mjadala wa aina yake bungeni.
Kufikia kwa arobaini ya sakata hilo linalodaiwa kumhusisha zaidi Mkapa na Yona, kunatokana na taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja, aliyesema kuwa ripoti kamili juu ya suala la Kiwira iko tayari na kilichobaki ni kuiwasilisha bungeni.
Lakini, baada ya Waziri Ngeleja kusema hayo na kisha Spika wa Bunge kukaririwa vilevile akisema kuwa Bunge linaisubiri kwa hamu ripoti hiyo na nyingine kadhaa, baadhi ya wabunge wamedaiwa kuwa tayari wamejipanga vilivyo katika kumlipua Mkapa na wengine wanaodaiwa kushiriki katika kuuza kwa bei poa mgodi huo wa Kiwira.
Chanzo chetu kimoja kimedai kuwa bila woga wala kumuonea haya mtu yeyote, baadhi ya wabunge wamepania kulijadili kwa kina suala hilo na hatimaye kutetea raslimali za taifa.
``Kuna mambo mengi yanayotia shaka juu ya uuzwaji wa raslimali za taifa... sasa kuna wabunge kibao waliojipanga katika kuhakikisha kuwa suala hili linajadiliwa bila kufunikwafunikwa,`` kikadai chanzo hicho.
Hatahivyo, akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Mbunge aliyeliibua sakata hilo bungeni na kuwatuhumu wazi Mkapa na Yona, Mhe. Aloyce Kimaro wa Jimbo la Vunjo (CCM), amedai kuwa taarifa hiyo ya Mgodi wa Kiwira anaisubiri kwa hamu bungeni na kwa sababu kila kitu kiko wazi, anaamini kuwa Serikali haitaficha kitu.
Mheshimiwa Kimaro amesema kuwa suala hilo litakapotua bungeni, yeye binafsi atahakikisha kuwa, kama walivyo wabunge wengine, atapigania kwa kila namna kuona kuwa sasa mgodi huo unamilikiwa kihalali.
Akasema hivi sasa, suala sio mmiliki wa mgodi ni nani, bali ni kuona mgodi huo unamilikiwa kihalali na unafanya kazi iliyokusudiwa ili kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.
Akaongeza kuwa kipindi hiki ni cha kusafisha uchafu wote wa ufisadi ili baada ya hapo, nchi ianze kuzungumzia namna ya kujiletea maendeleo.
``Hiki ni kipindi cha kusafisha uchafu. Tuweke mambo yote kwenye mstari, uchafu ufike mwisho na kisha tuanze kupigania zaidi maendeleo yetu,`` akasema Bw. Kimaro.
Akasema lengo ni mgodi huo ufanye kazi ya uzalishaji kama ilivyokusudiwa na kuwa wale wote waliokuwa wakiuchezea kwa madai ya kujiuzia kwa bei poa, sasa wavune walichopanda.
Naye Mbunge wa Viti maalum kupitia CHADEMA, Mheshimiwa Halima Mdee, amedai kuwa ikiwa taarifa hiyo ya Mgodi wa Kiwira itakuwa na maudhui kama watu wengi wanavyolifahamu sakata la mgodi wa Kiwira, inabidi wahusika wake wachukuliwe hatua kama walivyoanza kuchukuliwa watuhumiwa wa wizi wa fedha za Akauti ya Malipo ya Madeni ya Nje, EPA.
``Tunaisubiri kwa hamu taarifa hiyo. Na kama kweli itafanana na taarifa tuliyonayo kuhusu mgodi huo, sioni kama `treatment` yao itatofautiana na ile ya watuhumiwa wa EPA,`` akasema Mheshimiwa Halima.
Akadai kuwa ikiwa sheria za nchi zitafuatwa, ni dhahiri kuwa wahusika kwa kujimilikisha mgodi kinyume cha taratibu ni kosa la jinai na kuwa hawafai kuendelea kuumiliki.
``Kama walinunua kinyume cha utaratibu, hawana uhalali wa kumiliki mgodi huo,`` akasema.
Akaongeza Mheshimiwa Halima kuwa yeye anatarajia kuona wabunge wote wakipitisha maazimio ya kuwanyang`anya wahusika mgodi huo na kuurejesha Serikalini, ili taratibu na sheria zifuatwe.
Kwa taarifa zilizowahi kutolewa na Mheshimiwa Kimaro Bungeni, ni kwamba Mgodi huo uliuzwa kwa bei poa ya shilingi milioni 700 kwa kampuni ambayo wamiliki wake ni pamoja na Mkapa na Yona.
Cha kusikitisha zaidi, ilidaiwa kuwa licha ya kampuni husika kuuziwa kwa bei hiyo poa, bado ililipa Sh. Bilioni 70 pekee.
Hata hivyo, madai hayo yatakuja kubainika kuwa ni ya kweli au la baada ya ripoti kamili kuhusu Mgodi wa Kiwira kutolewa bungeni kama alivyoahidi Waziri Ngeleja.