KiuyaJibu
JF-Expert Member
- Aug 29, 2007
- 852
- 204
Unajua tuwe wa kweli kama tulikuwepo hapa Tanzania kwa kipindi chote Mkapa alichokuwa madarakani.
Unajua Mkapa kwa kiasi kikubwa katurudisha nyuma tofauti na kuanzia pale alipoachia Mwinyi;alikuja kufanya dili na watu wake kwa kivuli cha kuchapa kazi.Ndiyo maana mikataba yote ambayo haina maslahi kwa Taifa iimesainiwa katika kipindi chake cha uongozi na mbaya zaidi wanaonufaika na hiyo mikataba ni makampuni ya kigeni.
Wazawa katika miradi mikubwa hakuwapa nafasi na huku akiwadharau badala ya kuwawezesha ili waweze kumiliki miradi mikubwa ya kiuchumi kwa manufaa ya Taifa na siyo vinginevyo.
Huyu jamaa(Mkapa) alitokea kusifiwa sana na wazungu(Mataifa ya kigeni) lakini hiyo yote ilisababishwa na yeye mwenyewe kuwababaikia mno mpaka kufikia hatua ya kuwapa rasilimali za Taifa hili bila hata kutozwa kodi(Tax holiday);kwa maana hiyo ya kusifiwa na wageni kama mlikuwa hamjui ndiyo kigezo cha wengi kumuona alikuwa rais bora.
Halafu na yeye mwenyewe na watu wake wa karibu ikifuatilia kwa makini utagundua kwamba waligeuza nchi hii kama vilevile kampuni yao.
Hapa kuhusu Kikwete bado ana muda wa kuonyesha nini atatufanyia ukizingatia anatakiwa kurudisha nchi katika hali ya kuwa nchi na siyo kampuni.
Suala la kiongozi bora katika hawa Mkapa hakuna kitu na Kikwete kidogo afadhali kwasababu bado hajafikisha kipindi kama cha Mkapa katika haya madaraka ya urais;ila kama kuna watu wanasema Mkapa ni bora basi ni kwa vigezo vya wazungu ambao kwao ni mtu aliewamegea fedha kibao bureee wakati nchi yenyewe ni masikini kichizi.