Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mkamap,
Mkuu umeshasema wala unga, njoo huku uwaone hao wala unga wanapewa kila kitu toka nyumba posho kubwa kuliko mishahara ya baadhi ya watu lakini hadi leo hii hali zao ndio kama hivyo....
Na kuwapa wala unga mashamba ni moja ya UONGOZI mbaya! kiongozi mzuri hata siku moja humpi shamba mtumia bwibwi... huyu anatakiwa kupelekwa hospital kupata matibabu!..

mbona unaongelea kundi moja wakati nimetaja makundi yote wasio na kazi.
 
Ngoja turudi nyuma:

(a) Mwishoni mwa utawala wa Mwinyi, wahisani waliitishia kusitisha misaada kutokana na misamaha ya kodi. Ndipo wakati huo wakaisimamia serikali kuimarisha ukusanyaji wa kodi. Hiyo iliendana na kumwondoa Professor malima kutoka kwenye Wizara ya fedha, na kuanza tartibu za kuundwa kwa TRA kama tasis inyojitegemea isiyoingiliwa na wanasiasa.

(b) kwenye mkutano wa viongozi wa G7 ( baadaye G8) uliokaa June 1995 huko , Halifax, Canada, pamoja na mambo mengine waliongelea jinsi ya kuzisaidia nchi maskini kiuchumi, na mojawapo ya makubaliano yao ilikuwa ni kusamehe madeni kwa nchi maskini sana ikiwemo Tanzania. Makubaliano hayo ya G7 kuhusu kusamehewa madeni hayakuwa na uhusiano wowote na utawala wa Mkapa; wakati huo Mkapa alikuwa bado ni Waziri wa Elimu ya Juu. Taarifa kamili iliyotolewa baadaye na mawaziri wa fedha wa nchi hizo kuhusiana na utaratibu wa kusamehe madeni kwa nchi fukara nimeimabatanisha hapa chini.

(c) Mkapa alipoingia madarakani, alikuta taratibu zote za uundwaji wa TRA kwa ajili kuthibiti ukusanyaji kodi na zile za G8 kuhusu kusamehe madeni na kutoa misaada zaidi kwa kwa nchi maskini zikiwa zimekamilika. Ni kutokana na mazingira hayo ndipo wahisani walipoanza kutoa fedha tena kwa utawala wa Mkapa hata wakiwa hawajui kama atakuwa ni kiongozi wa namna gani.

(d) Pamoja na kusamehewa madeni, kupewa misaada zaidi, na kuboreka kwa ukusanyaji wa kodi, Mkapa alijikita tena katika uuzaji wa mashirika ya umma hata yale ambayo yalikuwa yanafanya kazi kwa faida na nyumba za serikali kwa kisingizio cha kuwekeza na kuindoa serikali kwenye biashara. Yote haya yalichangia kwa kiasi kikubwa sana kujaza fedha kwenye sefu za serikali kuliko ilivyokuwa kwenye serikali zilizopita. Kabla sijaongelea hilo la fedha, labda nikumbushe kuwa swala la uuzwaji wa mashirika halikuwa jambo baya; ubaya wa Mkapa ni jinsi uuzwaji huu ulivyofanyika, kwani sasa kuna ushahidi kuwa kuwa rushwa ilikuwa inatumika sana kiasi kuwa maslahi ya taifa hayakuangaliwa. Mkapa akiwa na kama rais wa nchi, ilikuwa ni wajibu wake kulinda maslahi ya nchi kwa gharama yoyote ile, lakini hakufanya hivyo.

(f) Baada ya serikali kuwa inapata pesa nyingi sana kuliko serikali zote zilizoitangulia kama nilivyoeleza hapo (d), serikali ya Mkapa ilikuwa na uwezo wa kufanya mambo mengi sana ya kuindeleza nchi lakini hawakufanya hivyo. Fedha zilzotumika kwa maendelo zilikuwa ni kidogo sana kuliko zile zililotumika kwa mambo ya kuwanufaisha viongozi. Kwa mfano, kwenye bajeti ya mwaka 2001, matumizi halisi kwa ajili ya maendeleo ilikuwa ni asilimia 13 tu, nyingine zote zikiishia kwenye recurrent expenditure; data zote ziko hapa. Mpangilio huu ni tofauti sana na bajeti ya mwaka 1970 ambapo sehemu ya maendeleo ilikuwa ni zaidi ya asilimia 30.

(g) Sasa ngoja tuliangalie hili la uchumi kukua chini ya serikali ya Mkapa. Kipimo kikubwa kinachotumika kupima ukuaji wa uchumi ni GDP. Formula itumikayo katika kukokota GDP ni hii:

GDP = Matumizi ya ndani + Uwekezaji ndani ya nchi + matumizi ya Serikali + (mauzo ya Nje − manunuzi kutoka nje)

Baada ya serikali kuwa ina pesa nyingi, matumizi ya serikali yalipanda,, na hivyo kuchangia kukua kwa GDP. Vile vile kwa vile serikali ya Mkapa iliuza ardhi yote ya madini na viwanda vyote, waliouziwa walileta vifaa vya kuwawezesha kufanya bishara zao. Hiyo iliongeza kiwango cha uwekezaji wa ndani ya nchi na hivyo kukua kwa GDP zaidi. Inawezekana pia matumizi ya ndani yaliongezeka kwa kiasi fulani lakini siyo significant sana kiasi cha kuweka dent kweny GDP kwa vile idadi kubwa ya wanachi wamebaki katika maisha ya kimaskini huku wengine wakiwa hawamudu kula milo miwili. Mauzo yetu ya nje yaliendelea kubaki ya chini ingawa manunuzi ya nje yalikuwa makubwa lakini yakwa offset na mehsabu ya uwekezaji ndani ya nchi.

Ni kutokana na facts za namna hii ndiyo maana sikubaliani na watetezi wote wa Mkapa. Kama angekuwa kiongozi bora na amejenga misingi imara ya uchumi na uongozi kama watetezi wake wanavyodai, bajeti ya nchi hii isingeendela kuwa tegemezi, na idadi ya watu wetu wengi wangekuwa wanaishi maisha bora kidogo kuliko walivyo sasa.
 
Attachments

Tujadilini na mambo ya kusaidi ndugu zetu
yani jinsi ya kujenga vyuo pia ku create ajira ,Swala la maisha bora ni jukumu la kila mtanzania haswa aliyesomeshwa na serikali ya TZ tokea chekechea.

Swala la Ufisadi linatosha kuubuliwa na kuachiwa vyombo vya sheria kufanya kazi na sio Jf kujifanya ndio chombo cha sheria.

JF wasomi wengi waliosomeshwa na serikali masikini kazi yetu kubwa iwe jinsi ya ku create idea za kutengeneza ajira na namna ya kuongeza vyuo kwa namna bora yakuviendesha ili visaidie wananchi wengi.

Kutoka kifua mbele eti kwa kuwatumia vijidola ndg zako kule TZ hakuwasaidii bali kunawadumaza zaidi.
 
Ngoja turudi nyuma:

(a) Mwishoni mwa utawala wa Mwinyi, wahisani waliitishia kusitisha misaada kutokana na misamaha ya kodi. Ndipo wakati huo wakaisimamia serikali kuimarisha ukusanyaji wa kodi. Hiyo iliendana na kumwondoa Professor malima kutoka kwenye Wizara ya fedha, na kuanza tartibu za kuundwa kwa TRA kama tasis inyojitegemea isiyoingiliwa na wanasiasa.

(b) kwenye mkutano wa viongozi wa G7 ( baadaye G8) uliokaa June 1995 huko , Halifax, Canada, pamoja na mambo mengine waliongelea jinsi ya kuzisaidia nchi maskini kiuchumi, na mojawapo ya makubaliano yao ilikuwa ni kusamehe madeni kwa nchi maskini sana ikiwemo Tanzania. Makubaliano hayo ya G7 kuhusu kusamehewa madeni hayakuwa na uhusiano wowote na utawala wa Mkapa; wakati huo Mkapa alikuwa bado ni Waziri wa Elimu ya Juu. Taarifa kamili iliyotolewa baadaye na mawaziri wa fedha wa nchi hizo kuhusiana na utaratibu wa kusamehe madeni kwa nchi fukara nimeimabatanisha hapa chini.

(c) Mkapa alipoingia madarakani, alikuta taratibu zote za uundwaji wa TRA kwa ajili kuthibiti ukusanyaji kodi na zile za G8 kuhusu kusamehe madeni na kutoa misaada zaidi kwa kwa nchi maskini zikiwa zimekamilika. Ni kutokana na mazingira hayo ndipo wahisani walipoanza kutoa fedha tena kwa utawala wa Mkapa hata wakiwa hawajui kama atakuwa ni kiongozi wa namna gani.

(d) Pamoja na kusamehewa madeni, kupewa misaada zaidi, na kuboreka kwa ukusanyaji wa kodi, Mkapa alijikita tena katika uuzaji wa mashirika ya umma hata yale ambayo yalikuwa yanafanya kazi kwa faida na nyumba za serikali kwa kisingizio cha kuwekeza na kuindoa serikali kwenye biashara. Yote haya yalichangia kwa kiasi kikubwa sana kujaza fedha kwenye sefu za serikali kuliko ilivyokuwa kwenye serikali zilizopita. Kabla sijaongelea hilo la fedha, labda nikumbushe kuwa swala la uuzwaji wa mashirika halikuwa jambo baya; ubaya wa Mkapa ni jinsi uuzwaji huu ulivyofanyika, kwani sasa kuna ushahidi kuwa kuwa rushwa ilikuwa inatumika sana kiasi kuwa maslahi ya taifa hayakuangaliwa. Mkapa akiwa na kama rais wa nchi, ilikuwa ni wajibu wake kulinda maslahi ya nchi kwa gharama yoyote ile, lakini hakufanya hivyo.

(f) Baada ya serikali kuwa inapata pesa nyingi sana kuliko serikali zote zilizoitangulia kama nilivyoeleza hapo (d), serikali ya Mkapa ilikuwa na uwezo wa kufanya mambo mengi sana ya kuindeleza nchi lakini hawakufanya hivyo. Fedha zilzotumika kwa maendelo zilikuwa ni kidogo sana kuliko zile zililotumika kwa mambo ya kuwanufaisha viongozi. Kwa mfano, kwenye bajeti ya mwaka 2001, matumizi halisi kwa ajili ya maendeleo ilikuwa ni asilimia 13 tu, nyingine zote zikiishia kwenye recurrent expenditure; data zote ziko hapa. Mpangilio huu ni tofauti sana na bajeti ya mwaka 1970 ambapo sehemu ya maendeleo ilikuwa ni zaidi ya asilimia 30.

(g) Sasa ngoja tuliangalie hili la uchumi kukua chini ya serikali ya Mkapa. Kipimo kikubwa kinachotumika kupima ukuaji wa uchumi ni GDP. Formula itumikayo katika kukokota GDP ni hii:

GDP = Matumizi ya ndani + Uwekezaji ndani ya nchi + matumizi ya Serikali + (mauzo ya Nje − manunuzi kutoka nje)

Baada ya serikali kuwa ina pesa nyingi, matumizi ya serikali yalipanda,, na hivyo kuchangia kukua kwa GDP. Vile vile kwa vile serikali ya Mkapa iliuza ardhi yote ya madini na viwanda vyote, waliouziwa walileta vifaa vya kuwawezesha kufanya bishara zao. Hiyo iliongeza kiwango cha uwekezaji wa ndani ya nchi na hivyo kukua kwa GDP zaidi. Inawezekana pia matumizi ya ndani yaliongezeka kwa kiasi fulani lakini siyo significant sana kiasi cha kuweka dent kweny GDP kwa vile idadi kubwa ya wanachi wamebaki katika maisha ya kimaskini huku wengine wakiwa hawamudu kula milo miwili.
Mauzo yetu ya nje yaliendelea kubaki ya chini ingawa manunuzi ya nje yalikuwa makubwa lakini yakwa offset na mehsabu ya uwekezaji ndani ya nchi.

This is a proffesorial analyis! Asante kwa darasa

Asha
 
Baada ya serikali kuwa ina pesa nyingi, matumizi ya serikali yalipanda,, na hivyo kuchangia kukua kwa GDP.

Mkuu kichuguu nafurahi kwa analysis yako...Ila nina kaswali...GDP=GROSS DOMESTIC PRODUCT.
Swali langu ni hili...Je ulimaanisha kuwa matumizi ya serikali kupanda ndiyo yaliifanya GDP kukuwa?
 
wanakijiji wamewatuma watanzania wasomi kwenda sokoni kuhemea na watakachopata huko wawapelekee wana kijiji na hatimaye wapate maisha bora.

wanakiji wanachotegemea kwetu ni kuona tuna create ajira kwao,tuna create namna ya wao kuifikia elimu bora itakayotokomeza umasikini,

Tukianza kufanya kazi ambazo wanakijiji wanaweza kufanya inakua tumewasaliti kwa kiwango kisichopimika.

Kulalamika lalamika na kupiga mayowe hata mwanakijiji kazi hiyo anaiweza.
 
Fungua thread yako ya kuendelea kuandika huo upupu usiohusiana na suala la "Mkapa ni mtu safi". Vipi mwenzangu, mbona Mkapa kuanikwa imekugusa hivyo? Jibu hoja basi, kama huna majibu-nyamaza!

Nani anamiliki mali za wananchi kama vile migodi na mashirika muhimu ya kiuchumi?

Mkulima mnampigia domo la kisiasa na mihotuba yenu halafu mnampelekea chuki za kidini na za kisiasa badala ya elimu na kuwawezesha kutumia kilimo bora.

Hayo mashangingi ya mawaziri na wabunge ukibadilisha na kununuwa trekta unajuwa zitakuwa ni trekta ngapi?

Tena ukizingatia hazina ushuru?

Nyie watu acheni jamani!

Watu hata kuroga waroge halafu hata hamuwaonei wananchi huruma?

Wananchi hawahitaji kumiliki kila kitu...Wananchi wanataka kunufaika na UTAJIRI WAO ILI WASIFE NJAA..WAPATE ELIMU WATOTO WAO WAPELEKWE SHULE NA BARABARA ZITENGENEZWE WAJENGEWE MAZINGIRA MAZURI YA KUFUNGUWA VIWANDA!

SASA NYIE MNAOIMBA KILA SIKU KUWA WANANCHI NI MASIKINI NA PIA NI WABOVU HATUWAHITAJI TENA!

WE NEED INSPIRING PEOPLE...PEOPLE WHO TELLS US THAT WE ARE A BETTER AND UNIQUE PEOPLE!

THAT WE CAN!

NA SI KUTUITA WABOVU KWA KUTUMIA VIGEZO VIBOVU KAMA VILE MBONGO ZENU ZINAVYOONYESHA UBOVU WA HALI YA JUU!

HIVI NYIE WATU MNA AKILI TIMAMU KWELI?
 
Mkuu kichuguu nafurahi kwa analysis yako...Ila nina kaswali...GDP=GROSS DOMESTIC PRODUCT.
Swali langu ni hili...Je ulimaanisha kuwa matumizi ya serikali kupanda ndiyo yaliifanya GDP kukuwa?

Yes Mushi, kunachangia
 
Mashairi hayo hapo chini ni ya SONGI NINALOLIZIMIA KWA SANA TU LA LUKY DUBE..."HOUSE OF EXILE"

Freedom fighter standing on a mountain
In a foreign country
Trying to send a message
To his people, back in the ghetto
He had a home one time
Love of a girl
But he left all that behind
Oh yes I can hear him clearly as he whispers in the air
His voice came out loud and clear
All he asked for was a prayer and as he turns to walk away he said

Chorus:
I'm still here in the house of exile
For the love of the nation

Sun went down on the mountain
Birds flew back to their hiding places
Leaving him standing there like a telephone pole
In the still of the night
You and I dream
Dreaming of Romeo & Juliet
All he dreams about is the freedom of the nation
When every man will be equal In the eyes of the law
As he closes his eyes
For the last time he said again

Chorus till fade
 
Fungua thread yako ya kuendelea kuandika huo upupu usiohusiana na suala la "Mkapa ni mtu safi". Vipi mwenzangu, mbona Mkapa kuanikwa imekugusa hivyo? Jibu hoja basi, kama huna majibu-nyamaza!

Asha

Swala la maendeleo kwa tz ni upupu .Ila swala la Chadema ndilo mhimu.

kinachonigusa hapa kwa kujadili mambo ya chama badala ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Mkapa ni FISADI ndio achieni vyombo vya sheria vifanye kazi.Na sio wewe kutumia Mabega yake kama ngazi ya kupandia .

Naamini Na bado Naamini hao mnaowaita mashujaa wengi wao ni mbwa mwitu tu wanao Jaribu kutumia Mabega kama ngazi yao ili wafike mahala walipolenga.

Haiwezekani uwe maarufu eti kwa kufumania mke wa jirani yako akifanya vya tumbaku .
Hata mwehu /kichaa ana uwezo wa kufaminia .

Kama sikosei Kigunge ama mzee Ndakaya kati yao naye alijijengea umarufuu wa kufumania na aka achisha kazi baadhi ya mawaziri leo yuko wapi??

Umaarufu upatikane kwa kuletea wananchi maendeleo na si kufumaniana ,japo kufumania pia ni jambo zuri lakini lisiwe ndio kigezo cha kujipatia umaarufu na hatimaye kutumia mabega ya waarifa kama mtaji .
 
Watanzania wazembe ,wavivu ,wanafiki.

Kwa macho yangu nimeona mateja,waulaji,wamachinga wakikamatwa pale Dar na kupelekwa pwani wakigawiwa mashamba ya bure walime badala yake walikimbia na kumwita Dikiteta aliyepwapeleka.

Najua walichotaka ni kupewa pesa na sio shamba na hata hivyo pesa wangezipiga mvinyo na matanuz.

Najua walitaka ma trekta wapewe bure lakini hata wangeyafilisi na kuuza vifaa kama yalivyofilisiwa RTC,viwanda kuwa nyumba za Nguchiro.
Kwa uzembe wetu wa kufikiri tuko lazi kusema maisha bora yanaletwa na serikali ama kiongozi wakati sisi tunachapa siasa vijiweni

Mkamap,

Mada hii inayoongelewa ilianzishwa na BongoTZ na kichwa cha mada yenyewe ni Mkapa ni mtu safi. Period. Tunayemjadili humu ni Mkapa kuwa msafi. Period.

Wewe umesema Mkapa alikuwa the Best President. Hukuishia hapo tu ukaongezea kuwa Watanzania ndio wabovu. Maovu na ufisadi wa Mkapa umetajwa na wengi tu. Kama unakubaliana hata na moja kati ya yote hayo inatosha kuonyesha kuwa Mkapa hakuwa safi.

Hebu nieleze mkazi wa Bunda, Mara aliona unafuu gani wa maisha kati ya mwaka 1995 na 2005 pamoja na ukusanyaji wa kodi unaousifia. Mkazi wa Makambaku, Mbeya uchumi wake ulikuwa kwa kiwango gani katika kipindi hicho pamoja na msamaha wa madeni ambao yeye Mkapa hajui hata ulipatikana vipi. Na mwisho mkazi wa Maneromango aliona ahueni ipi katika mihangaiko yake ya kila siku pamoja na pesa yote ilyopatikana baada ya uuzaji holela wa mashirika yetu.

Waliofaidika zaidi kwenye awamu ya tatu nikianzia na Mkapa mwenyewe na familia yake wanajulikana. Sitawataja wengine kwa sababu wametajwa sana humu. Gold medal inaenda kwa Mkapa as the worst and dangerous President so far. While Kikwete anatumia proxies kwa hands off policy, Mkapa did it with impunity and in broad daylight - some of us know WHY.
 
wa tanzania sio wavivu kama watu wanavyo taka kuwapakazia, bali wananyimwa an equal playing field, hiyo ni moja ya pili ni kunyimwa mitaji, wakati wengine wanapewa kwa mlango wa nyuma, na infact viongozi kama mkapa ndio wavivu kufikiria kwa sababu wana take risk kwa hela ya wizi hivyo , hivyo hawana uchungu wakati wengine wanabidi watake risk kwenye hela walioipata kwa jasho, then wakiinvest wanakuta wenzao wanapendelewa na wao wanapoteza mitaji yao
 
Nani anamiliki mali za wananchi kama vile migodi na mashirika muhimu ya kiuchumi?

Mkulima mnampigia domo la kisiasa na mihotuba yenu halafu mnampelekea chuki za kidini na za kisiasa badala ya elimu na kuwawezesha kutumia kilimo bora.

Hayo mashangingi ya mawaziri na wabunge ukibadilisha na kununuwa trekta unajuwa zitakuwa ni trekta ngapi?

Tena ukizingatia hazina ushuru?

Nyie watu acheni jamani!

Watu hata kuroga waroge halafu hata hamuwaonei wananchi huruma?

Wananchi hawahitaji kumiliki kila kitu...Wananchi wanataka kunufaika na UTAJIRI WAO ILI WASIFE NJAA..WAPATE ELIMU WATOTO WAO WAPELEKWE SHULE NA BARABARA ZITENGENEZWE WAJENGEWE MAZINGIRA MAZURI YA KUFUNGUWA VIWANDA!

SASA NYIE MNAOIMBA KILA SIKU KUWA WANANCHI NI MASIKINI NA PIA NI WABOVU HATUWAHITAJI TENA!

WE NEED INSPIRING PEOPLE...PEOPLE WHO TELSS US THAT WE ARE A BETTER PEOPLE!

THAT WE CAN!

NA SI KUTUITA WABOVU KWA KUTUMIA VIGEZO VIBOVU KAMA VILE MBONGO ZENU ZINAVYOONYESHA UBOVU WA HALI YA JUU!

HIVI NYIE WATU MNA AKILI TIMAMU KWELI?

Tatizo Jmushi ndilo liko hapo wewe unadhani nani ?ana jukumu la kuwaletea watanzania maisha bora??
 
Mkamap,

Mada hii inayoongelewa ilianzishwa na BongoTZ na kichwa cha mada yenyewe ni Mkapa ni mtu safi. Period. Tunayemjadili humu ni Mkapa kuwa msafi. Period.

Wewe umesema Mkapa alikuwa the Best President. Hukuishia hapo tu ukaongezea kuwa Watanzania ndio wabovu. Maovu na ufisadi wa Mkapa umetajwa na wengi tu. Kama unakubaliana hata na moja kati ya yote hayo inatosha kuonyesha kuwa Mkapa hakuwa safi.

Hebu nieleze mkazi wa Bunda, Mara aliona unafuu gani wa maisha kati ya mwaka 1995 na 2005 pamoja na ukusanyaji wa kodi unaousifia. Mkazi wa Makambaku, Mbeya uchumi wake ulikuwa kwa kiwango gani katika kipindi hicho pamoja na msamaha wa madeni ambao yeye Mkapa hajui hata ulipatikana vipi. Na mwisho mkazi wa Maneromango aliona ahueni ipi katika mihangaiko yake ya kila siku pamoja na pesa yote ilyopatikana baada ya uuzaji holela wa mashirika yetu.

Waliofaidika zaidi kwenye awamu ya tatu nikianzia na Mkapa mwenyewe na familia yake wanajulikana. Sitawataja wengine kwa sababu wametajwa sana humu. Gold medal inaenda kwa Mkapa as the worst and dangerous President so far. While Kikwete anatumia proxies kwa hands off policy, Mkapa did it with impunity and in broad daylight - some of us know WHY.

Unajua kawaida ya mwananchi ama tabia ya binadamu
Ni gumu mno kuona barabara aliyojengewa highway ya lami ilikua na makorongo ya kufa mtu kutoka mwanza-kisesa hadi bunda kama imemtia ahueni.
Ila ni rahisi sana kuona maendeleo kama amejenga nyumba na kupata milo 2 kwa siku .kwa biashara yake kutoka Bunda kwenda mwanza kuuza mitumba.
 
Yes Mushi, kunachangia

Kichuguu..Let me start by this...Najuwa huu mjadala unaweza kuwa mrefu.

Lakini the reason for us to trade globaly during the globalization process in the third world...The global VISION WHEN IT COMES TO COMPETING IN THE GLOBAL MARKET...

THIS IS THE GLOBAL VISION..."The ability to recognize and react to international business opportunities,be aware of the threats from foreign competition, and effectivelly use the international distribution networks to obtain raw materials and move finished products to customers"

Sasa ebu niambie kilichofanyika. Raw materials ndiyo tuna export kila siku..Kilimo ni ZII,Viwanda ndiyo usiseme...Ni wawili watatu tu kina Bhakressa na wenzake.
Hakuna mtu anayemjali mwananchi...Kisa ni MBOVU!

Mimi ninafikiri kuwa hata GDP yetu kukuwa ni kutokana mali inayowapa kibri cha kufanya matumizi...Na hivyo nakubaliana na wewe kwenye pointi ya matumizi!

Ila sisi wazalendo formula yetu ni maslahi ya wananchi na wala si REPORT ZA IMF...Hao wanaona fungu linalowekezwa na pia kina sinclair si ndio ma lobbyists tu wa kumanipulate news ili mataifa wafadhili waone hamna noma?

Sasa na mipesa ya ukimwi na kila kitu bado wanakula tu!

Yani ubinadamu hakuna kabisa!

Sasa hiyo global vision haikufuatwa na wananchi hawakuandaliwa na sasa wanaitwa WABOVU!
 
Haya..Mkuu Kichuguu..Umezungumzia kuhusu GDP...Vipi kuhusu BALANCE OF TRADE?
We dont have trade surplus...We just have trade deficts...Sasa ni kivipi uchumi ulihesabika kuwa umekuwa?
Ni vigezo gani?
Hicho cha matumizi ya serikali?
 
Bado si rahisi kuona barabara ya lami zinazounganisha Nzega -dodoma japo watanzania ndio wanaitia zengwe isiishe.

Lakini ni Rahisi kuona maendeleo yake anayofanya kwa biashara ya mabasi yke Nzega-Dodoma.

Si Rahisi kuona maendeleo ya barabara ya lami kutoka Geita kupitia Chato ,Mganza pori la Kasidanga hadi mleba kua si maendeleo ,wakati ni rahisi kuona maendeleo yake kwa kupitia barabara hizo badala ya kutumia siku tatu anatumia masaa kadhaa.

Si rahisi kuona Wilaya ya Biharamulo ambayo ilikua haina umeme tangu kuanzishwa kwa dunia .Na sasa wamepelekewa umeme.

Comeon. Kazi y serikali ni kukuwekea nyezo mhimu kama umeme,barabara,maji yani huduma nzuri mengine ni wananchi mkichwa.
 
PRSC Ilikuwa ni VIONGOZI AKILI KUMKICHWA AMA NI WANANCHI AKILI KUMKICHWA?
 
Unajua kawaida ya mwananchi ama tabia ya binadamu
Ni gumu mno kuona barabara aliyojengewa highway ya lami ilikua na makorongo ya kufa mtu kutoka mwanza-kisesa hadi bunda kama imemtia ahueni.
Ila ni rahisi sana kuona maendeleo kama amejenga nyumba na kupata milo 2 kwa siku .kwa biashara yake kutoka Bunda kwenda mwanza kuuza mitumba.

Mkamap,

Umenithibitishia kitu kimoja. Ama huijui Tanzania au kwa makusudi unakataa kukubali hali halisi. On average mwananchi kijijini Bunda uwezo wake kupata mahitaji yake ulipungua kwa kiasi cha kutisha katika kipindi hicho - labda iwe kwa vigezo vyako vya kutumia indicators za kupikwa, system ambayo imetokea kuwa fashion kwa watawala wetu. Huwezi kupima uchumi kwa mwananch moja kula na kusaza huku wananchi kumi wanalala njaa. Ninahisi uko miongoni mwa hao walafi mkiongozwa na Mkapa huku mkiwaita wengine wavivu, wabovu nk..
 
Back
Top Bottom