Kimsingi sioni shida kwa mzee Mkapa ku-own shamba, na kama katiba au maadili ya uongozi yanamzuia kufanya hivyo nadhani hizo instruments ndio zenye matatizo na zinapaswa kurekebisha.
Kinachoudhi ni kwamba umiliki unafanywa siri na kumekuwa na upendeleo kwa sababu ya influence ya madaraka aliyokuwa nayo. Kwa mfano ni kwa nini yeye halipi michango kwa Association ya wakulima kama wakulima wengine?
Mkuu mimi nafikiri tumezidi ,kila kitu kulaumu laumu tu hakusaidii
Mkapa kumiliki Mtibwa ama shamba si tatizo na ni haki ya kila mtanzania labda kama kuna sheria inayosema ukishakua Rais basi hutakiwa kumiliki biashara yoyote hapo itakua sawa lakini kama haipo tatizo la mkapa lipo wapi??
Mimi nafikiri sisi watanzania tuna wivu,roho ya korosho na wavivu wa kufikiri,kwanini yani mfano ukianzisha leo kibanda cha kuuza nywere pale mwenge na watanzania wakakuona unapata fedha utaona mwingine naye analeta kibanda chake palepale ulipo na yeye anaanza kuuza nywere cha ajaabu zaidi badala ya kukubali ushindani yeye ataanza kukulaumu tena wewe kuwa unamnyang'anya wateja.
Kama ni mashamba yapo mengi tu na lunch zipo nyingi tu na zimekufa zimegeuka pori na wala hatuzipigi kelele ,wewe unayepiga kelele kuhusu shamba la mkapa nawewe katafute shamba ulime harafu uoombe uhisani na mtibwa .
Leo hii mashamba yaliyogeuka mapori yapo mengi tu wakiambiwa wanaachi wayachukue walime hakuna hata mmoja atayejitokeza lakini Kikwete ama Lowasa ama Azizi ama Amani akijitokeza na akaamua kuyaendeleza na akafanikiwa kwa wivu na kinyongo tulicho nacho tutajitokeza na kuanza kuhoji jinsi alilivyolipata shamba hilo.
Acheni kuogopesha watu na neno UFISADI wewe chukua basi nenda Tanga ,chukua basi uelekee mwanza ,chukua basi uelekee tunduma utaona mashamba mengi yaliyo kufa na kugeuka pori ,luch nyingi zilizokufa nazo utaziona.
Ukiona cha elea usifikiri ni chepesi kimeundwa
Ubinafishaji ulikua na lengo nzuri sema kila jambo lazima liwe na hasara zake na wajanja kujipenyeza kufanya mambo yao hilo haliepukiki.
Kabla ya ubinafishaji kagera sugar,mwatax,mutex viwanda vyote vya nguo ukitoa urafiki vilikua vimekufa.
Yale mashirika ya mikoa sijui RTC yako wapi? leo hii mtu akiyarudisha na yakabinafisishwa watu wataibuka na kuhoji.
Viwanda vingi,mashirika mengi kabla ya mkapa yalikua yamekufa,kabla ya mkapa Shule nyingi ziliteteleka waalimu waliaacha kazi na kufanya biashara wafanyakazi serikalini walikimbia kazi zao wakawa wafanya biashara.
Tatizo la la Tanzania ni tatizo kua mWatanzania .