PapoKwaPapo
JF-Expert Member
- Jun 5, 2008
- 380
- 45
Bila shaka baadhi ya waandishi nao mafisadi!!!!
Sumaye kaanza kumtetea Mkapa,mtasikia muda si mrefu Kikwete amtetea Lowasa.
Bila shaka baadhi ya waandishi nao mafisadi!!!!
Mengi yanaibuka baada ya Benjamin Mkapa (Mr Clean) kuanza kujibu tuhuma dhidi yake. Katika listi yupo, sasa ni kuendeleza mapambano!!
Mambo yenyewe haya hapa kama yalivyoandikwa na Gazeti la Nipashe la leo. Nawasilisha:
Mkapa `mbia` Mtibwa
2008-06-07 11:37:37
Na Mwandishi wa PST, Morogoro
Rais mstaafu, Bw. Benjamin Mkapa, ana ubia wa kibiashara na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kilichoko katika Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, imefahamika.
Bw. Mkapa ni mkulima wa nje wa kiwanda hicho anayemiliki shamba la miwa lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 600, katika eneo la Dizungu wilayani humo.
Shamba hilo linahudumiwa na kiwanda hicho tofauti na mengine, na utafiti unaonyesha kwamba alikuwa analimiki toka akiwa Ikulu.
Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Bw. Ahmed Yahaya kwenye kikao cha usuluhishi baina ya wafanyakazi wa Mtibwa, wastaafu na wakulima wadogo wa nje wa miwa wa kiwanda hicho.
Hata hivyo, Bw. Yahya alikanusha madai kwamba Bw. Mkapa ndiye mmiliki wa kiwanda hicho kama ambavyo imekuwa ikidaiwa.
Kikao hicho kiliitishwa na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Morogoro.
Bw. Yahya alizidi kudai kuwa Bw. Mkapa, kama walivyo wakulima wengine wa nje wa Mtibwa, ni mkulima halali anayelipa makato yake kama wakulima wengine isipokuwa ameingia mkataba wa kibiashara kwa kuhudumiwa shamba lake na kiwanda.
Alidai kuwa makubaliano kama hayo yanakubaliwa kwa mkulima yeyote na kwamba kiwanda hakioni tatizo katika suala hilo.
Mkurugenzi huyo alisema kiwanda hicho kinamilikiwa kihalali na Kampuni ya Tanzania Sugar Industry Ltd., yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam na viongozi wake wakuu wakiwa ni Bw. Nassoro Seif na Bw. Seif A. Seif, huku kukiwa na wajumbe watano wa Bodi, akiwemo yeye Yahaya mwenyewe.
Alisema kampuni hiyo ni ya kizalendo kwa asilimia mia moja, hivyo kuwaondoa wasiwasi wananchi, hususani wa wilaya ya Mvomero wanaodhani kuwa kiwanda hicho ni cha Rais mstaafu Bw. Mkapa.
Mapema wananchi wa wilaya ya Mvomero, hususan wakulima wa nje ya kiwanda, walilalamikia kutomfahamu mmiliki halali wa kiwanda hicho kutokana na kushindwa kutekelezwa kwa madai yao mbalimbali na serikali dhidi ya tuhuma wanazowasilisha kwao dhidi ya mwekezaji wa shamba hilo na menejimenti yake.
Malalamiko makubwa dhidi ya shamba hilo ambalo sasa limebainika dhahiri kwamba ni la Mkapa yalijikita juu ya `upendeleo` kutokana na kuhudumiwa vyema, huku mwaka huu kukiwa hakuna makato yoyote kwenda kwenye chama cha wakulima kutoka katika shamba hilo.
Katika kikao hicho, Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Bi. Mary Chatanda, alisema hata yeye alishindwa kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na wananchi hao juu ya umuliki wa kiwanda hicho, hususani walipodai kuwa kinamilikiwa na kiongozi wa Serikali au Chama cha Mapinduzi.
Alisema kufuatia hali hiyo, alipokea maagizo toka kwa Rais Jakaya Kikwete, juu ya kushughulikia matatizo ya Kiwanda cha Mtibwa dhidi ya wastaafu, wakulima wa nje na wafanyakazi ili kupata ufumbuzi na kuinusuru CCM kutokana kwenye lawama.
Akiongea na Nipashe kwa njia ya simu, Meneja Msaidizi wa Mtibwa, Bw. Kiula, alikiri kwamba Bw. Mkapa amekuwa na shamba hilo zaidi ya miaka 10, hali inayoonyesha kwamba alikuwa nalo toka akiwa Ikulu.
Bw. Mkapa amekuwa akituhumiwa kujihusisha na biashara wakati akiwa Ikulu, suala ambalo ni kinyume cha maadili ya uongozi wa juu kama aliokuwa nao yeye, kutokana na mgongano wa kimaslahi.
Bw. Mkapa aliyeingia Ikulu mwaka 1995 na kutoka mwaka 2005, baadhi ya mambo anayotuhumiwa nayo ni kuanzisha kampuni binafsi inayojishughulisha na biashara iliyojulikana kama ANBEN Limited mwaka 1999.
Nyaraka za usajili wake zilionyesha kuwa ofisi za kampuni hiyo zipo katika majengo ya Ikulu jijini Dar es Salaam na kulingana na nyaraka za Msajili wa Makampuni (BRELA), Bw. Mkapa na Bi. Anna Mkapa ndio wakurugenzi pekee wa kampuni hiyo binafsi.
Inadaiwa pia kwamba mwaka 2002, Bw. Mkapa bado akiwa Ikulu, kampuni yake ya ANBEN Limited ilipewa mkopo mnono wa Dola za Marekani 500,000 (sawa na Shilingi milioni 620) na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) pamoja na Benki ya CRDB na kwamba mwaka 2004, Bw. Mkapa kwa kushirikiana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Daniel Yona walianzisha kampuni binafsi iitwayo TANPOWER Resources wakiwashirikisha baadhi ya ndugu zao na watoto wao na kuwafanya kama wanahisa.
Katikati ya mwaka 2005, Bw. Mkapa akiwa katika miezi ya mwisho ya kustaafu, inadaiwa kuiwa aliitumia kampuni hiyo ya TANPOWER Resources, kununua hisa kubwa za mgodi wa serikali wa Kiwira ambao kiusajili ulijulikana kama Kiwira Coal and Power Limited.
Kampuni hiyo ndiyo baadaye iliingia katika mkataba mkubwa wa takribani Sh. bilioni 340 na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa ajili ya kuzalisha megawati 200 za umeme kwa kutumia makaa ya mawe katika gridi ya taifa.
Bw. Mkapa hajawahi pia kukanusha madai kwamba ni mshiriki katika Benk M na kwamba alikuwa na mkono katika menejimenti ya kigeni iliyokuwa inaendesha TANESCO ya Net Group Solutions.
SOURCE: Nipashe
Tamaa nyingine bwana mtu kesha zeeka lakini bado tu anachuma hivi hiyo 80% aliona kama haita mtosha mpaka akaingia majaribuni kama hivi?
Dah hii kali sana.Anajidhalilisha mwenyewe kwa tamaa za mzee fisi.
Hawa wanatuvunjia heshima kabisa, cha kushangaza na mamilioni yote aliyonayo leo ukimuonga dolar 500 haziwachi, uchu gani huu?? au ndio laana??
Jamani hivi wenye makali hawaoni madhambi yote haya au hata hizi.........nazo wanamuonea??
Wataunda kamati ingine kujaribu kuficha uchafu wao, lakini wapi! Mume atamkana mke, lakini wapi!, mpaka tuone mwisho wake...Jamani hivi wenye makali hawaoni madhambi yote haya au hata hizi.........nazo wanamuonea??
Tukiangalia vizuri tunaweza kuona mzizi mzima wa UFISADI ktk tanzania kwa kipindi chote cha Mkapa ulianzia IKULU. Ili kuuondoa inatakiwa ashughulikiwe kwanza.
Mzee wa MKUKUTA NA MKURABITA,amejirasimisha rasilimali ili aonde umaskini karibu yake.Huu mradi ulikuwa wa kuwasaidia wananchi/wakulima wa hali ya chini kujipatia ajira, badala yake aliyetakiwa kutengeneza ajira sasa ndio fisadi mkuu
Tatizo la viongozi wetu ni ujasiliamali! hivyo wanatumia nafasi wanayoipata kujijenga kibiashara. Mhe. Mkapa (kwa mujibu wa Nipashe) hajalipa mchango wa chama cha wakulima wa nje. Hii pia ni kuwaumiza na kuwadhulumu wakulima wadogo.
Sijui kama ni hapo Mtibwa tu, ninawasiwasi sana na kiwanda kimoja kule Kilombero Sugar Company. Ukifika pale Kilombero kuna viwanda viwili, kiwanda cha kwanza kinanembo za Illovo (kampuni ya S.A) kiwanda cha pili hakina nembo kabisa. wananchi, wanazungumza kuwa ni cha Mkapa. tutajuaje?...