Japo ambalo si la siri kwamba kambi zote za wagombea uraisi CCM zinamuogopa sana Lowassa, hivyo kuna kila aina ya jitihada ya kuhakikisha jina la Lowassa halipitishwi kugombea nafasi ya uraisi.
Huku wapinzani wakijipanga kukata jina lake lakini Lowassa yeye anaendelea na mikakati yake ikiwa ni pamoja na kugawa fedha kama njugu kwani anaamini yeye ni raisi wa Tanzania 2015-2025 "PIGA UA"
Lowassa anatishia kukiua chama (CCM) endapo hata pitishwa kugombea uraisi.
Wakati huo huo, endapo jina la Lowassa halitapitishwa CCM wanyetishaji wetu wanasema mkakati wa Lowassa kugombea kupitia UKAWA kwakuwa tayari ana mtaji wa wanaCCM wengi hivyo ni rahisi kwake kushinda nafasi ya uraisi.
Inasemekana kuwa tayari Lowassa ameshaanza mazungumzo ya chini chini na viongozi wa UKAWA lakini bado hawajafikia makubaliano rasmi.
Posted by:
MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)