Mjomba tutaua wangapi ndio turidhike?

Mjomba tutaua wangapi ndio turidhike?

Mjomba anadhani atatawala milele amesahau umri unaenda atawaachaje vijukuu vyake watoto wake wataishije!? Juzi nasikia amezidi kujiimarisha kijeshi kwa kuunda kikosi maalumu cha special ops yote hiyo kuwatisha wakosoaji wake..mjomba nna mengi ya kukuandikia kwa Leo naishia hapa..
Duuu
 
Mazingira Sasa hivi yamebadilika Sana Sasa hivi. Watu wanajenga nchi, mambo ya msituni hawayataki kwa Sasa. Lakini hao madogo wanayo nafasi ya kujaribu bahati yao. Ila kwa ushauri tu, sumu haionjwi kwa kulambwa, ni ushauri tu. Waje tuijenge Rwanda yetu nzuri.
Tuijenge rwanda vizuri ila wahutu wasiwe watawala milele.
NB:TUTSI MINDSET
 
Sidhani Kama unaongea ukweli. Jeshi la RPF lilikuwa na wahutu wengi ingawa kwa idadi watutsi walikiwa wengi. Usisahau Rais wa Kwanza wa Rwanda mpya alikuwa mhutu wa RPF. Ndio maana nashauri tusirudie huko nyuma, ambako akina Habrarimana na wenzake walitufikisha kwa kuona wahutu ndio wenye haki miliki na Rwanda.
Sasa mjomba nae anatufikisha kwa kuona watusi ndio wenye haki ya kutawala pekee
 
Mjomba wale askari 600 waliokufa Kisangani kwa mahesabu yako mabovu ya kupigana na waganda....wazazi wao wanatulaumu...
Wale watu tuliowaua kwa kulipiza kisasi...na watoto wao sasa wanataka kulipiza kisasi.
Mjomba kila mtu anakuchukia ila tunakuchekea kinafiki sababu wewe ndio mkuu wa ukoo kwa sasa.
Tumeua wangapi mpaka sasa,,,,,????
Kuanzia ndani ya ukoo mpaka nje ya ukoo.???
Mjomba najua unajiita baba wa ukoo ila unadhani wewe ni bora kuliko alivyokua mjomba Fred???
Unadhani wewe ni bora kuliko Babu Dia Wamba???
Lengo lilikua kuwaondoa watu wafupi nyumbani.....maana waliua wana ukoo na walifanya mabaya mengi kwa miaka 45.
Lakini mbona baada ya kukupa uongozi wa ukoo na wewe umekua muuaji..???
Mjomba hupendi kuambiwa ukweli.
Mjomba umejigeuza mfalme wa ukoo..
Mjomba si wewe ndio ulipanga mpango wa kumuua mjomba Abby???
Afu ulitutenga wanao ambao wazazi wetu walikua mchanganyiko wa wana ukoo warefu na wafupi..
Unasema umoja wa kitaifa...lakini mbona unawatenga watu wafupi???
Mjomba sasa unavuka mipaka na kutaka kuwapangia majirani zetu waswahili na cha kufanya....
Mjomba wewe si ndio ulimsaliti babu Kaguta afu unatuambia uongo.
Mjomba ukichokoza vita sisi tutakususa kama tulivyomsusa anko Ntaganda....
Hao waswahili ukiwachokoza watakuja hadi kwenye boma na sisi tutakutekeleza.
Mjomba mpaka sasa kwenye rekodi kwa mkono wako au kwa maagizo umeua watu milioni 9 na bado huchoki...
Kwa kifupi mjomba wewe hauna tofauti na anko Abby na nyote ni wauaji tu.
Tumechoka kuua mjomba...sababu hata tukiua hatutowamaliza watu wafupi...
Afu kwani watu wafupi na warefu hatuwezi kuishi pamoja kwa amani???
Wewe kila siku unatuambia kila mtu mbaya...
Waswahili wabaya.
Warundi wabaya.
Wakongo wabaya.
Watu wafupi wabaya.
Sasa familia imechafuka na watu kwenye ukoo wanataka kukuua mjomba...ndio maana umetununia wana ukoo.
Mjomba watoto wako wanakula bata wakati sisi wapwa zako hatupati fursa.
Unadhani tutakenua meno???
Na sisi tunataka keki ya taifa.
Kwa taarifa yako mjomba tutakususia ukoo tuone kama utaenda frontline mwenyewe.
Wewe mtu gani unapenda kuua wanaukoo kila siku.
Sasa tukubaliane hv...na siku wewe wakikuuua usilalamike...sawa.
Mjomba gani ushauriki.....na ndio maana shangazi anakunyimaga unyumba afu unampiga makofi.....
Mjomba..
Sisi sio vitendea kazi vyako tuelewane.
Sisi sio ngombe wa nyama...unajichinjia mda wowote unaojisikia.
Sisi sio wajinga tumeshakushitukia.
Kama hautaki kikao cha ukoo tuchague mkuu wa ukoo mwingine,,bas njia ileile uliyoingia ndio utakayotokea...
Afu kua na aibu mjomba.....wamekufanyia oparesheni ya tezi dume....kapumzike tuachie uongozi wa ukoo..
Mjomba tumeshaua wanaukoo wengi sana na tumechoka hatutaki kuendelea kumwaga damu kwa niaba yako.
Watu wafupi na wenyewe wana haki ya kuishi....
Sasa tutakususia ukoo ubaki wewe na watoto wako tuone.
Mjomba mpaka mgambo wa ukoo unawaua kisa wamesahau kukupigia saluti...
Rekodi zetu watu milioni tisa na laki nane wameshakufa tokea 1992 na je tuendelee kuua???
Hapana mjomba huko tunakoelekea tutakususa ubaki peke yako....kama tulivyomsusa mjomba Abby...
Babu Kaguta yeye mwenyewe majirani washaanza kumsusa na sisi tunatazama tu......
Tutaua watu wangapi mjomba???
Tutafunga watu wangapi???
Vizazi vya wapwa zako vitaishije wewe ukiondoka??
Mjomba na wewe unamuiga Edorgan mpiga konyagi????
Sisi tumechoka mjomba....
Safari hii dirty work utafanya mwenyewe...
Mpwa wako nipo nimetulia na najua siwezi kuja kwenye ukoo sababu umeninunia kisa nakuambia ukweli..
Ila kumbuka damu nzito kuliko maji ndio maana nakuambia ukweli.
Pamoja na yote mjomba tusichukiane......sisi watoto tuna tabia ya kuropoka na mjomba mama.
Mjomba Slim anahitaji sala ya toba kwa kweli
 
Mazingira Sasa hivi yamebadilika Sana Sasa hivi. Watu wanajenga nchi, mambo ya msituni hawayataki kwa Sasa. Lakini hao madogo wanayo nafasi ya kujaribu bahati yao. Ila kwa ushauri tu, sumu haionjwi kwa kulambwa, ni ushauri tu. Waje tuijenge Rwanda yetu nzuri.
Rwanda ni kama mole kwenye great lake region.. Ni kama gateway ya baadhi ya mataifa makubwa katika kuvuna kila wanachokitaka

Kwa hiyo hii inaifanya Rwanda kuwa na maadui wa ndani na nje ya nchi walio very strong. Pk ni kiongozi naemkubali sana hasa katika kufanya lobbying na kutengeneza future ya vijana wa Rwanda.

Ila kwenye kutengeneza umoja na stability ya Wanyarwanda ili kuzuia zile series za genocides, naona hapo kafeli kiasi ndio maana Rwanda bado ina ulemavu ule ule alioukuta wakati anachukua nchi na bila huu ulemavu kuisha, sioni Rwanda ikitulia
 
Binafsi napenda aina ya uongozi wa anko wako...

Afrika ukiwa kiongozi ili ufanikiwe kumuokoa mwananchi wa chini kabisa, kuna kima hupaswi kuwasikiliza...

Afrika ina wajinga wengi sana, hawa huelewa dhima nzuri ya kiongozi baada ya miaka kadhaa...

Hata Tanzania tunahitaji mtu aina ya Kagame.
 
Kumbuka kuwa Prof. Mwaikusa ndio alikuwa wakili wa wale washitakiwa wa kesi za mauaji ya Rwanda!
Mtikila alikuwa anamshutumu sana Kagame kuhusu mpango wao wa “ Bahima Empire “ na jinsi anavyowaangamiza wapinzani wake!
PK masterminded these assasinations!
Do you know the Devil's Advocacy Theory?
Hiyo ya sijui alikuwa Wakili wa Washtakiwa wa Mauaji ya Kimbari ya Rwanda just it was a Spinning Propaganda that spreaded by the Pepertrators themselves in order to cover the real cause of the incident.
 
Kwa hiyo lile la mchungaji ni lilikuwa la watu wa humu humu kwetu na si wa jirani kama ilivyokuwa ikisemwa na ata baadhi ya nyuzi humu?
Humu ndani ya Jf wapo watu wa aina na makundi mbalimbali humu, baadhi ya makundi ya watu wamefungua ID fake humu kimkakati ili kutekeleza kazi zao maalumu. "Watu wa Dawati la Propaganda" wapo wengi sana humu Jf na kwenye mitandao mingine ya kijamii huku wakieneza Propaganda zao pamoja na kuendesha Operesheni zao huku mitandani.
 
Back
Top Bottom