Mjomba tutaua wangapi ndio turidhike?

Mjomba tutaua wangapi ndio turidhike?

Binafsi napenda aina ya uongozi wa anko wako...

Afrika ukiwa kiongozi ili ufanikiwe kumuokoa mwananchi wa chini kabisa, kuna kima hupaswi kuwasikiliza...

Afrika ina wajinga wengi sana, hawa huelewa dhima nzuri ya kiongozi baada ya miaka kadhaa...

Hata Tanzania tunahitaji mtu aina ya Kagame.
Tanzania imeizidi karibia kila kitu Rwanda.
 
Ni kweli kama huyo wa ijumaa aliedakwa na familia yake hapapa,nimesikitika sana!katuchafua wakati sisi waswahili ndio tulimlea na kumuingiza hapo alipo!

Kwanini anatudhalilisha aiseh!!?
Mjomba wale askari 600 waliokufa Kisangani kwa mahesabu yako mabovu ya kupigana na waganda....wazazi wao wanatulaumu...
Wale watu tuliowaua kwa kulipiza kisasi...na watoto wao sasa wanataka kulipiza kisasi.
Mjomba kila mtu anakuchukia ila tunakuchekea kinafiki sababu wewe ndio mkuu wa ukoo kwa sasa.
Tumeua wangapi mpaka sasa,,,,,????
Kuanzia ndani ya ukoo mpaka nje ya ukoo.???
Mjomba najua unajiita baba wa ukoo ila unadhani wewe ni bora kuliko alivyokua mjomba Fred???
Unadhani wewe ni bora kuliko Babu Dia Wamba???
Lengo lilikua kuwaondoa watu wafupi nyumbani.....maana waliua wana ukoo na walifanya mabaya mengi kwa miaka 45.
Lakini mbona baada ya kukupa uongozi wa ukoo na wewe umekua muuaji..???
Mjomba hupendi kuambiwa ukweli.
Mjomba umejigeuza mfalme wa ukoo..
Mjomba si wewe ndio ulipanga mpango wa kumuua mjomba Abby???
Afu ulitutenga wanao ambao wazazi wetu walikua mchanganyiko wa wana ukoo warefu na wafupi..
Unasema umoja wa kitaifa...lakini mbona unawatenga watu wafupi???
Mjomba sasa unavuka mipaka na kutaka kuwapangia majirani zetu waswahili na cha kufanya....
Mjomba wewe si ndio ulimsaliti babu Kaguta afu unatuambia uongo.
Mjomba ukichokoza vita sisi tutakususa kama tulivyomsusa anko Ntaganda....
Hao waswahili ukiwachokoza watakuja hadi kwenye boma na sisi tutakutekeleza.
Mjomba mpaka sasa kwenye rekodi kwa mkono wako au kwa maagizo umeua watu milioni 9 na bado huchoki...
Kwa kifupi mjomba wewe hauna tofauti na anko Abby na nyote ni wauaji tu.
Tumechoka kuua mjomba...sababu hata tukiua hatutowamaliza watu wafupi...
Afu kwani watu wafupi na warefu hatuwezi kuishi pamoja kwa amani???
Wewe kila siku unatuambia kila mtu mbaya...
Waswahili wabaya.
Warundi wabaya.
Wakongo wabaya.
Watu wafupi wabaya.
Sasa familia imechafuka na watu kwenye ukoo wanataka kukuua mjomba...ndio maana umetununia wana ukoo.
Mjomba watoto wako wanakula bata wakati sisi wapwa zako hatupati fursa.
Unadhani tutakenua meno???
Na sisi tunataka keki ya taifa.
Kwa taarifa yako mjomba tutakususia ukoo tuone kama utaenda frontline mwenyewe.
Wewe mtu gani unapenda kuua wanaukoo kila siku.
Sasa tukubaliane hv...na siku wewe wakikuuua usilalamike...sawa.
Mjomba gani ushauriki.....na ndio maana shangazi anakunyimaga unyumba afu unampiga makofi.....
Mjomba..
Sisi sio vitendea kazi vyako tuelewane.
Sisi sio ngombe wa nyama...unajichinjia mda wowote unaojisikia.
Sisi sio wajinga tumeshakushitukia.
Kama hautaki kikao cha ukoo tuchague mkuu wa ukoo mwingine,,bas njia ileile uliyoingia ndio utakayotokea...
Afu kua na aibu mjomba.....wamekufanyia oparesheni ya tezi dume....kapumzike tuachie uongozi wa ukoo..
Mjomba tumeshaua wanaukoo wengi sana na tumechoka hatutaki kuendelea kumwaga damu kwa niaba yako.
Watu wafupi na wenyewe wana haki ya kuishi....
Sasa tutakususia ukoo ubaki wewe na watoto wako tuone.
Mjomba mpaka mgambo wa ukoo unawaua kisa wamesahau kukupigia saluti...
Rekodi zetu watu milioni tisa na laki nane wameshakufa tokea 1992 na je tuendelee kuua???
Hapana mjomba huko tunakoelekea tutakususa ubaki peke yako....kama tulivyomsusa mjomba Abby...
Babu Kaguta yeye mwenyewe majirani washaanza kumsusa na sisi tunatazama tu......
Tutaua watu wangapi mjomba???
Tutafunga watu wangapi???
Vizazi vya wapwa zako vitaishije wewe ukiondoka??
Mjomba na wewe unamuiga Edorgan mpiga konyagi????
Sisi tumechoka mjomba....
Safari hii dirty work utafanya mwenyewe...
Mpwa wako nipo nimetulia na najua siwezi kuja kwenye ukoo sababu umeninunia kisa nakuambia ukweli..
Ila kumbuka damu nzito kuliko maji ndio maana nakuambia ukweli.
Pamoja na yote mjomba tusichukiane......sisi watoto tuna tabia ya kuropoka na mjomba mama.
LIe
 
Mkuu uhuru upi.......wa mjomba kujitawaza mfalme na kuwawinda watu wafupi wasichukue madaraka...
Anyway sishangai......hata Babu yetu.....aliwaambia wabelgiji kua hii nchi ni ya watu warefu.
Mbona unaongea kiuoga jirani?????
Unamuogopa BANGUBANGU???
Hajui alisemalo huyo,muambie siku akivuka rusumo akifika kicukiro tu pale aanze kutaja maovu ya pk kama hajaenda kufia gitarama
 
Mazingira Sasa hivi yamebadilika Sana Sasa hivi. Watu wanajenga nchi, mambo ya msituni hawayataki kwa Sasa. Lakini hao madogo wanayo nafasi ya kujaribu bahati yao. Ila kwa ushauri tu, sumu haionjwi kwa kulambwa, ni ushauri tu. Waje tuijenge Rwanda yetu nzuri.
Na teknolojia imebadilika Mr. Pres
 
Back
Top Bottom