Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?

Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?

Maggid nimeipenda sana ile hadithi ya Mbwa wa Manzese na yule wa Oysterbay...
Sasa wewe ni mbwa wa Manzese au Oysterbay maanake mambo yako sii mabaya!.

Naona yeye (Maggid) ni mbwa wa Oysterbay, anakula chakula kizuri na kulala mahali pazuri kuliko hata maofisa wengi wa serikalini. Tehetehetehetehetehe!

majidi kaolewe na kikwete uwe mke wa tatu....mjengwa si yule wa global kila siku?wale wale wanaotafuta kujikomba kwa kikwete kama michuzi....viherehere wakubwa...tired of ccm...eti tathmni yako pwani...what about arusha and other regions?

du! Wadau tupunguze jazba na maneno yasiyo ya kistaarabu . Ni vizuri tujibu kwa hoja na lugha laini kwani naamini hili ni jukwaa la wastaarabu

kwani walio wengi wanataka nini? Mwaka 1991 ilifanyika kura ya maoni tanzania na waliowengi walitaka mfumo wa chama kimoja!!, uchaguzi mkuu wa 1995 waliowengi waliichaguwa ccm, 2000 waliowengi wakaichaguwa ccm, 2005 waliowengi wakaichagua ccm, mwaka huu 2010 waliowengi ni wale wale watakaoirudisha ccm madarakani!!!! Au kwa maoni yako unataka kutuambia waliowengi ni wafuasi wa chadema? Au mtu kama si mpenzi wa chadema basi si mtanzania?

Kwangu mimi naona kama wengi wanataka mabadiliko ya aina fulani ktk mfumo wetu wa utawala. Kama naona vibaya basi ni suala langu binafsi,lisikupe taabu. Mambo ya vyama niko mbali nayo sana mkuu,ila napenda kushiriki kwa vitendo kuleta mabadiliko kwa njia ya kura siku ikifika. Naamini umenielewa.

Hivi hamuwezi kutoa comments zenu bila kucopy na kupaste post nzima ya mtu???

Japo kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo,lakini uhuru huo ukitumika pasipo nidhamu inakuwa kama vurugu.

Utafiti mdogo tu ungeweza kukufahamisha kuhusu mwelekeo wa kampeni za uchaguzi,na pengine hata kubashiri matokeo kwa usahihi zaidi.Ukiangalia kura za maoni zinazoendeshwa na vyombo mbalimbali vya habari,zote zinaonyesha Dokta Slaa akiongoza kwa mbali.Daily News (kabla ya kuamua kuondoa kura hizo),Majira,Radio Free Africa na hapa JF kote huko kunaonyesha Slaa anaongoza.Sasa mwenzetu ubashiri wako unaelemea kwenye vigezo gani?

ANGALIZO: Mods,utaratibu wa kufuta posts zangu pasipo sababu si uungwana.

Kwa nini mbwa wa manzese ndio alienda oystebay na wala sio wa oystebay kuja manzese? Huyu wa oystebay ndie anaetaka kumkaribisha ndani ya geti huyu wa manzese. Sasa vita nyenyewe ndoo ipo hapo, kwamba kuna kundi dogo la mafisadi ndani ya system likisaidiwa na waandishi njaa wachache kuwanyanyapaa wale wote walio wazalendo na kuwatishia kwa kila aina ya kuhofisha ili wajisalimishea kwenye utumwa ulio ndani ya geti. Kama inavyosemwa kila jambo lina wakati wake, kulikuwa na wakati wa kudanganyika nao umepita sasa ni saa ya ukombozi na hivyo mbwa wa manzese tunasema hatudanganyikii, mbwa wa oystebay(kibaraka) ni lazima tumchomoe kwa nguvu kutoka kwa bwana wake(ccm) na tutamwadhibu huyu bwana kwa kura zetu.
SISIEM KWAHERI YA KUTOKUONANA TENA. TO HELL WITH U'R LIES.

Msanii,
Ahsante sana.
Tunasema; ukichagua mchezo wa masumbwi usiogope ngumi za usoni. Haya ni ya kawaida. Najiona mwenye bahati, kwa kuwa najifunza mengi. Nikiri kuwa mimi si msomi sana. Nina ‘kadigrii kangu kamoja tu’. Bado najifunza.
Na hata bila hiyo digrii yangu moja bado nina uwezo wa kuandika haya ambayo kwa wengine wanasema ni ya ‘ mtoto wa Darasa la Saba’ na mwingine anaona ni ‘ pumba tu’. Hata kama ni pumba , ni zangu, wala sizionei aibu.

Ni bahati mbaya, kuwa kuna wengi wenye kuamini, kuwa kila mwandishi Tanzania anapokea bahasha. Hii ni dhana potofu.
Nakumbuka uchaguzi wa mwaka 2005 niliandika makala mbili kwenye gazeti la RAI zenye kumwelezea Dr Salim Ahmed Salim na hususan kuwalaani wale waliomwandama kutokana na rangi ya ngozi yake.

Basi, kwa makala zile mbili kuna walioniweka kwenye ‘droo la Dr Salim’. Nakumbuka uchaguzi ulipokwisha, nilikutana na Mhariri wa Gazeti la Mwananchi. Nae akaniambia; “ E bwana Bosi wako kaenda Darfur”. Nilijisikia vibaya sana. Maana, sikumfahamu Dr Salim zaidi ya kumwona kwenye vyombo vya habari. Sikuwa na mawasiliano nae mpaka mwaka juzi Februari 5 nilipokutana nae kwa mara ya kwanza ofisini kwake pale Masaki, kwa mazungumzo ya kawaida tu.

Mfano mwingine ni pale nilipoanzisha gazeti la kijamii la ‘ KWANZA JAMII’, kuna wanaolizungumzia gazeti hilo hapa JF. Wanalizungumzia wakionyesha kufahamu wasichokifahamu kuhusiana na 'KWANZA JAMII'. Wanaona tabu hata kuniuliza. Ni udhaifu tu, ni unyonge wetu.

Kwa vile nilimiliki kagazeti kadogo ka ‘ KWANZA JAMII’ , basi, siku moja nikapanga mihadi na bwana mmoja mfanyabiashara na mmiliki wa vyombo vya habari. Nikafika ofisini kwake; nikamwaleza kuwa nilikuwa na mawili tu yaliyonipeleka kwake; Mosi; kufahamiana nae, pili, kumwomba anisaidie ‘ KWANZA JAMII’ lisomwe redioni na kwenye tv zake nyakati za asubuhi kwenye vipindi vya ‘ Leo Magazetini’ .

Bwana yule alikubali ombi langu pale pale, kisha akaniuliza kama nilikuwa na shida nyingine iliyonileta. Aliniuliza zaidi ya mara mbili. Jibu langu likawa hapana. Nilihisi, kuwa kwenye fikra zake aliamini kuwa mie ni wale aliowazoea. Kuwa labda ningemwambia shida ya senti za matumizi au hata fedha za kuchapia gazeti langu. Pamoja na dhiki zangu , miye ni kama yule ‘ Mbwa wa Manzese!’. Ndivyo nilivyo.

Nina mifano mingi mingine ya niliyokutana nayo. Tukipata fursa tutajuzana mbele ya safari kwa minajili ya kuelimishana na kubadilishana uzoefu.

Msanii,

Ahsante sana.

Tunasema; ukichagua mchezo wa masumbwi usiogope ngumi za usoni. Haya ya kawaida. Najiona mwenye bahati, kwa kuwa najifunza mengi. Nikiri kuwa mimi si msomi sana. Nina ‘kadigrii kangu kamoja tu'. Bado najifunza.

Na hata bila hiyo digrii yangu moja bado nina uwezo wa kuandika haya ambayo kwa wengine wanasema ni ya ' mtoto wa darasa la saba' na mwingine anaona ni ' pumba tu'. Hata kama ni pumba ni zangu, wala sizionei aibu.

Ni bahati mbaya, kuwa kuna wengi wenye kuamini, kuwa kila mwandishi Tanzania anapokea bahasha. Hii ni dhana potofu.

Nakumbuka uchaguzi wa mwaka 2005 niliandika makala mbili kwenye gazeti la RAI zenye kumwelezea Dr Salim Ahmed Salim na hususan kuwalaani wale waliomwandama kutokana na rangi ya ngozi yake.

Basi, kwa makala zile mbili kuna walioniweka kwenye ‘droo la Dr Salim'. Nakumbuka uchaguzi ulipokwisha, nilikutana na Mhariri wa Gazeti la Mwananchi. Nae akaniambia; " E bwana Bosi wako kaenda Darfur". Nilijisikia vibaya. Maana, sikumfahamu Dr Salim zaidi ya kumwona kwenye vyombo vya habari. Sikuwa na mawasiliano nae mpaka mwaka juzi Februari 5 nilipokutana nae kwa mara ya kwanza ofisini kwake pale Masaki, kwa mazungumzo ya kawaida tu.

Mfano mwingine ni pale nilipoanzisha gazeti la kijamii la ‘KWANZA JAMII', kuna wanaolizungumzia gazeti hilo hapa JF wakionyesha kufahamu wasichokifahamu kuhusiana na KWANZA JAMII. Wanaona tabu hata kuniuliza. Ni udhaifu tu, ni unyonge wetu.

Kwa vile nilimiliki kagazeti kadogo ka ‘KWANZA JAMII' , basi, siku moja nikapanga mihadi na bwana mmoja mfanyabiashara na mmiliki wa vyombo vya habari. Nikafika ofisini kwake; nikamwaleza kuwa nilikuwa na mawili tu yaliyonipeleka kwake; Mosi; kufahamiana nae, pili, kumwomba anisaidie ‘KWANZA JAMII' lisomwe redioni a na kwenye tv nyakati za asubuhi kwenye vipindi vya ‘Leo Magazetini' .

Bwana yule alikubali ombi langu pale pale, kisha akaniuliza kama nilikuwa na shida nyingine iliyonileta. Aliniuliza zaidi ya mara mbili. Jibu langu likawa hapana. Nilihisi, kuwa kwenye fikra zake aliamini kuwa mie ni wale aliowazoea. Kuwa labda ningemwambia shida ya senti za matumizi au hata fedha za kuchapia gazeti langu. Pamoja na dhiki zangu, miye ni kama yule ‘Mbwa wa Manzese!'. Ndivyo nilivyo.

Nina mifano mingi mingine ya niliyokutana nayo. Tukipata fursa tutajuzana mbele ya safari kwa minajili ya kuelimishana na kubadilishana uzoefu.

PUMBA HATA SIJASOMa

Tukaanza kwa kujibu hata bila kusoma...! what exceptional skills is it. Hii ni sawa na yule anayesema nimejibu hata kabla sijaulizwa swali. Sasa sijui kajibu nini.

uandishi wa darasa la saba

Bila kusoma tukagundua kuwa, fani, mtiririko, maudhui na sarufi zilizopo ni za kiwango cha chini sana..... darasa la 7 vile.

Naona yeye (Maggid) ni mbwa wa Oysterbay, anakula chakula kizuri na kulala mahali pazuri kuliko hata maofisa wengi wa serikalini. Tehetehetehetehetehe!

Hapa ukatolewa ufafanuzi wa hoja, kisha tukamalizia kwa kucheka. Ishara ya kuridhika kwa kazi tuliyofanya juu ya pumba za wenzetu........!

Hivi hamuwezi kutoa comments zenu bila kucopy na kupaste post nzima ya mtu???

Kisha huyu akakereka zaidi juu ya wanajamvi.........!

Haina shida. Tanzania imara itajengwa na sisi watanzania wenyewe kwa kupanga na kuzichambua hoja zetu wenyewe kisha tukasimamisha wazo moja kuu lililosanifiwa kwa kina, ambalo litaleta mabadiliko ya kweli. Huko tutafika watanzania tusife moyo, maana natambua hata babu zetu walicheza bao kwa vipande vya almasi na dhahabu ila leo tunawaona wapuuzi. Amini nawaambieni sisi tutaonekana wapuuzi zaidi ya wao maana hatuitambui hata ipi ni tunu yakuifumbata kwaajili ya kesho yetu. Masikini sisi watanzania.....!

Maggid,
Mkuu wangu acha hadithi nyingi ambazo hazihusiani na mada uloiweka wewe mwenyewe kwa Utabiri wako ambao hukutoa details za kutosheleza. Kama kweli wajifunza basi fahamu kwamba unapofikia kutoa hukumu ya maono yako ni bora sana yafuatane na picha halisi ukisheresha na takwimu za uchunguzi wako ili usipoteze maana ya mwandishi wa habari.

Sisi hapa tunakusoma wewe kama mwandishi wa habari kinyume cha akiandika Msanii au mtu mwingine. Tunakuwa kama vile unatuhabarisha zaidi ya mawazo yako binafsi. Na hata waandishi wa nchi za majuu hukubali kufungamana na chama au mtawala ikiwa wao wanakubaliana na sera za mgombea au chama. Sii aibu kuwapigia debe CCM ikiwa wewe unakubaliana na sera zao au mgombea wake, pia sio aibu kuwapigia debe Chadema au CUF maadam wewe kama mwandishi una sababu za zinazoweza kumhabarisha mwananchi.

Kifupi hata mimi nilikubaliana nawe ktk bandiko lako la kwanza nikitegemea pengine umefanya Utafiti na niliwaambia wanabodi wakusikilize kwanza kabla hawajarukia kukukashifu hali mwenzetu umefanya utafiti wa kutosha. Lakini kusema kweli hadi sasa hivi unachapia tu na fikra zako binafsi kama mimi nilivyokuwa naamini kwamba Dr. Slaa anaweza kabisa kumshinda JK ktk uchaguzi huu. Sikuwa na sababu yoyote zaidi ya kufikiria mapungufu ya Kikwete na Utawala wake, na kusema kweli nisingeweza kusema Dr.Slaa atashinda kwa asilimia kadhaa akifuatiwa na JK au Lipumba hali sina takwimu za utafiti toka kwa wananchi wapiga kura.

Maadam unakubali kujifunza basi karibu kuwa mwandishi wa Habari mwenye kutumia takwimu na ukweli unalojitenga badala ya fikra zako binafsi kama kina sisi ambao hatuna tukijuacho zaidi ya yale tunayoyafahamu. Ni rahisi sana kwa wananchi ku quote maelezo yako na kuyatumia kwa sababu wewe ni mwandishi wa habari tofauti na mimi ambaye watu watafikiria mara mbili kabla hawajakubaliana nami.
Ni ushauri tu tunaokupa....

Hongera Maggid kwa kuamua kutoa mawazo yako kwa uwazi. Naamini kabisa mgongano wa mawazo ni muhimu ili kuweza kutusaidia kubadilika na kuyachukulia mambo yanayotuzunguka kwa uzito unaostahili.
Tukumbuke kwa muda mrefu tumewaachia watu wachache wawe wanafikiri na kuamua yote juu ya hatima yetu kama wananchi wa Taifa la Tanzania. Juhudi zozote za kuondokana na mfumo huo zitapata upinzani, hasa kwa wale wanaonufaika na hali iliyopo sasa.
Ila tutafanya makosa kama leo tutasalimu amri na kukubali kuruhusu zile zile fikra za watu wachache ambao kwa hakika wametusahau tulio wengi waendelee kushika hatamu na kijineemesha wao na familia zao.

Uchambuzi wako nimeukubali umegusa kila angle, response uliyopata usistuke watu wa chadema hulka yao ni jazba badala ya kutafkari hoja na kuifanyia kazi, sansana ulipo sema akiondoka kiongozi mkutatononi huku nyuma hakuna viongozi wa kufuatilia yale mambo..

nasikitika sana kuisoma hii thread very late... Mchungaji masa nisamehe sikukuelwa wakati ule

Maggid ni mtoa habari na si mchambuzi, imejidhihirisha wazi kwani ameandaa forecast yak e kwa kutumia past experience bila hata kurejea variables zake muhimu na namba moja ni ukuaji wa teknohama, utandawazi na upeo na ujaribu wa wananchi!!!!!! hakuangalia basic indicators za maisha na wala hakujali hali ya sasa si ile ya mbwa wa masaki na wa manzese

Hata kama majibu yatakua kama alivyobashiri, hawezi kusema kwamba he did any analysis... atakua ni mbashiri tu

sikitiko kubwa kwangu jinsi maggid alivyogeuka sheikh yahya

inawezekana hujui kwamba uchaguzi wa serikali za mitaa ni wakina hupiga kura na walipiga kura kwa kiasi gani? walikuwa asilimia 30 ya wapiga kura wote je unatushawishi kuwa asilimia 30 ndio watakaopiga kura msimu huu kumbuka wabongo wamezinduka sana:llama:

Msanii,

Ahsante sana.

Tunasema; ukichagua mchezo wa masumbwi usiogope ngumi za usoni.
Haya ni ya kawaida. Najiona mwenye bahati, kwa kuwa najifunza mengi. Nikiri kuwa mimi si msomi sana. Nina ‘kadigrii kangu kamoja tu’. Bado najifunza.

Na hata bila hiyo digrii yangu moja bado nina uwezo wa kuandika haya ambayo kwa wengine wanasema ni ya ‘ mtoto wa Darasa la Saba’ na mwingine anaona ni ‘ pumba tu’. Hata kama ni pumba , ni zangu, wala sizionei aibu.

Ni bahati mbaya, kuwa kuna wengi wenye kuamini, kuwa kila mwandishi Tanzania anapokea bahasha. Hii ni dhana potofu.

Nakumbuka uchaguzi wa mwaka 2005 niliandika makala mbili kwenye gazeti la RAI zenye kumwelezea Dr Salim Ahmed Salim na hususan kuwalaani wale waliomwandama kutokana na rangi ya ngozi yake.

Basi, kwa makala zile mbili kuna walioniweka kwenye ‘droo la Dr Salim’. Nakumbuka uchaguzi ulipokwisha, nilikutana na Mhariri wa Gazeti la Mwananchi. Nae akaniambia; “ E bwana Bosi wako kaenda Darfur”. Nilijisikia vibaya sana. Maana, sikumfahamu Dr Salim zaidi ya kumwona kwenye vyombo vya habari. Sikuwa na mawasiliano nae mpaka mwaka juzi Februari 5 nilipokutana nae kwa mara ya kwanza ofisini kwake pale Masaki, kwa mazungumzo ya kawaida tu.

Mfano mwingine ni pale nilipoanzisha gazeti la kijamii la ‘ KWANZA JAMII’, kuna wanaolizungumzia gazeti hilo hapa JF. Wanalizungumzia wakionyesha kufahamu wasichokifahamu kuhusiana na 'KWANZA JAMII'. Wanaona tabu hata kuniuliza. Ni udhaifu tu, ni unyonge wetu.

Kwa vile nilimiliki kagazeti kadogo ka ‘ KWANZA JAMII’ , basi, siku moja nikapanga mihadi na bwana mmoja mfanyabiashara na mmiliki wa vyombo vya habari. Nikafika ofisini kwake; nikamwaleza kuwa nilikuwa na mawili tu yaliyonipeleka kwake; Mosi; kufahamiana nae, pili, kumwomba anisaidie ‘ KWANZA JAMII’ lisomwe redioni na kwenye tv zake nyakati za asubuhi kwenye vipindi vya ‘ Leo Magazetini’ .

Bwana yule alikubali ombi langu pale pale, kisha akaniuliza kama nilikuwa na shida nyingine iliyonileta. Aliniuliza zaidi ya mara mbili. Jibu langu likawa hapana. Nilihisi, kuwa kwenye fikra zake aliamini kuwa mie ni wale aliowazoea. Kuwa labda ningemwambia shida ya senti za matumizi au hata fedha za kuchapia gazeti langu. Pamoja na dhiki zangu , miye ni kama yule ‘ Mbwa wa Manzese!’. Ndivyo nilivyo.

Nina mifano mingi mingine ya niliyokutana nayo. Tukipata fursa tutajuzana mbele ya safari kwa minajili ya kuelimishana na kubadilishana uzoefu.

Mkuu Magid Mjengwa, kwa nakupa pole kwa yaliyokusibu kutokana na ile thread yako ya jana. Mimi niliisoma asubuhi nikielekea kwenye mahangaiko yako, mara baada tuu ya kukusoma, nikawa provoked nikujibu hapo hapo, ila kwa vile nilikuwa natumia mobile version, nikasema nitakujibu vizuri nikitulia kwenye pc.

Bahati nzuri nakufahamu toka Tambaza enzi hizo, mpaka Sweden pale Upsula. Kitendo cha kuandika makala iliyoprovoke debate ni uthibitisho wa the power you have within you.

You have the guts za dare devil to speak your mind. You will be called all sort of names ila utabaki umesimama. Nilipojiunga tuu humu JF, nilikuwa impresed na provocations za kuibua mijadala kwenye threads za Mzee Mwanakijiji, hivyo ni kawaida kupokea hayo matukano na ndio heathy debate inayoifanya jf iendelee to stand firm kupokea maoni yoyote.

Kwa kumaintain msimamo wa uhuru wako na kotoendekeza njaa na kushikilia msimamo wa kutojikomba komba kwa wenye nazo, there is a price to pay ikiwa ni pamoja na kuendelea kuishi kama unavyoishi sasa, hivyo kuendelea kukondeana. Mimi mwenzako price kama hizo nimeshazilipia sana na naendelea kuzilipia. Ni heri kuendelea kuwa mbwa wa Manzese, ambae kula yake ni majalalani lakini yuko huru kuliko mbwa wa uzunguni anayenenepeana ndani ya geti.

Just keep it up, hata kama kati ya watu 100, ni mmoja tuu ndiye anayekuelewa, bora achana na hao 99 wa kwenye ubatili na kushikamana na huyo mmoja wa kwenye ukweli.

Mjengwa naye ni binadamu, njaa inamsumbua.

Na Maggid Mjengwa,

Mwalimu Nyerere alipata kusimulia kisa cha mbwa wa Manzese. Nilikuwa bado kijana mdogo sana niliposikia kisa kile. Ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 80. Ni kwenye kilele cha Sherehe za Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi. Sherehe zile zilifanyika pale Uwanja wa Taifa. Nilibahatika kuwapo uwanjani.

Baadhi ya mabango ya wafanyakazi yaliyopita mbele ya Mwalimu siku ile yaliwakilisha ujumbe juu ya hali ngumu ya kimaisha iliyokuwa ikiwakabili wafanyakazi; mishahara midogo na mengineyo.

Wakati huo, Serikali ya Mwalimu ilikataa masharti ya Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia pia. Hii ni kwa sababu, licha ya athari nyingine mbaya kwa masharti hayo kwa nchi yetu, uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu nao ulikuwa hatarini.

Ilipofika wakati wa kutoa hotuba yake, Mwalimu Nyerere alisema;

Ndugu zangu watu wa Dari Salama ebu nisikilizeni; kulikuwa na mbwa wawili, mmoja wa Manzese na mwingine wa Oysterbay. Ikatokea siku moja mbwa wa Manzese akatembea hata akafika Oysterbay.

Kwenye moja ya nyumba za huko Oysterbay akamwona mbwa mwenzake aliye ndani ya geti. Mbwa yule wa Manzese akasogea getini huku akimshangaa mbwa wa Oysterbay. Mbwa yule wa Oysterbay alinenepeana huku manyoya yake yakiwa yameteremka hadi machoni. Mbwa wa Oysterbay naye alimshangaa mwenzake wa Manzese. Mbwa yule wa Manzese alionekana kukondeana huku masikio yake yakiwa yameteremka hadi shingoni. Mbwa wa Oysterbay kwa mshangao akamwuliza mwenzake wa Manzese;  Hivi nawe ni mbwa kama mimi?!
Naam, miye ni mbwa kama wewe. Alijibu mbwa wa Manzese.
Sasa mbona umekondeana hivyo, njoo humu ndani kwa bwana wangu nawe uwe kama mimi.
Mbwa wa Manzese akajibu;
Lakini wewe umefungiwa, mwenzio niko huru!

Sitakisahau kamwe kisa kile alichosimulia Mwalimu Nyerere pale Uwanja wa Taifa. Naamini katika alichokisema Mwalimu. Nitaendelea kuamini hivyo hata katika muda wangu uliobaki humu duniani. Mwalimu alizungumzia dhana ya uhuru. Ingawa ni neno fupi sana, lakini neno uhuru lina maana kubwa. Asiye na uhuru ni mtumwa.
Mimi ni mtu huru. Na siku zote nimepigania nibaki kuwa mtu huru. Kwa uhuru kabisa nakutana na kuongea na watu wengi; vijijini na mijini. Nakutana na kuongea na wasomi na wasio wasomi, matajiri na masikini. Sijapata maishani mwangu kulazimishwa au hata kulipwa ujira ili niongee au niandike mawazo yasiyo yangu au nisiyokubaliana nayo.
Ni bahati mbaya pia, katika jamii yetu, kila anayeandika makala magazetini kama nifanyavyo, basi, atasemwa kuwa ni mwandishi wa habari. Wengi hawatofautishi baina ya mwandishi wa habari na mwandishi wa makala.

Napenda sana kuandika fikra zangu huru kwa azma ya kuchochea mijadala. Jana niliandika fikra zangu kwenye Jamii Forums. Nimefanya hivyo huko nyuma. Lakini jana nimepata watu wengi walioshiriki mjadala. Wametoa fikra zao, kuna walionitukana pia. Nimeshazoea. Nayasoma matusi hayo, nikiamini, hata kwenye matusi hayo kuna cha kujifunza. Kufahamu fikra za watoa matusi hayo.

Na hakika, kuna wanaofikiri wananifahamu. Wamenipa majina, wamenihusisha na huyu na yule. Kimsingi hawanijui. Wamekuwa ni wakandamizaji wa fikra huru na wanaamini kila anayeandika mawazo yasiyofanana na yao, basi, amenunuliwa. Huu ni udhaifu, ni unyonge wetu pia. Hatujiamini.

Nitaendelea kuandika fikra zangu huru, napenda sana kuandika mawazo yangu. Nimefanya hivyo tangu nikiwa Sekondari pale Tambaza, tena kwa kuazisha kijarida cha shule. Niliandika mwenyewe kwa mkono, nilikuwa na wasomaji wangu pia. Tuliokuwa nao Tambaza miaka ile ya 80 ni mashahidi wa hilo.

Najua kuwa wakati mwingine kuna wanaokerwa na niandikayo. Hao wapo siku zote. Hatuwezi kufanana kimitazamo. Na tumekuwa wepesi sana, kila tusomapo mawazo ya mtu, kutafuta droo ya kabati la kumpachika. Siku hizi kuna droo za CCM, CHADEMA, CUF, Uislamu, Ukristo, Uchaga, Usukumuma na kadhalika.
Na ni bahati mbaya sana, kuwa wengi tumeisahau "Droo ya Tanzania". Hii ni droo muhimu sana na ilipaswa iwe ya kwanza. Kwa kila tutendalo liwe kwa MASLAHI YA TANZANIA KWANZA. Maslahi ya Taifa. Na Hilo Ni Neno La Leo.

Maggid,
Iringa,
mjengwa

Bw. Maggid,
zamani ndivyo nilivyokuelewa hivyo lakini nimefuatilia sana makala zako kwenye magazeti na hitimisho nililofikia ni kuwa sioni tofauti yako na akina Salva na Muhingo Rweyemamu. Kisa cha mbwa wa Manzese na Osterbay kina mantiki kubwa lakini wewe unayekikumbuka na kukiamini huishi hivyo. Wewe unadhani watu makini hawajakutambua kwamba ni kada wa chama cha mafisadi! Basi unajidanganya.

Umefungwa na fedha za mafisadi kusifia mambo yasiyo na vichwa wala miguu. Ni jambo gani jema alilofanya kikwete zaidi ya kuvuruga uchumi wa nchi na kutufukarisha. Mimi siamini kama dunia hii imewahi kuwa na kiongozi msanii wa kiwango cha kikwete. Anaendesha nchi kienyeji mno na wewe unajifanya kumpigia debe.

Ole wako mabadiliko yatakapotokea, utauficha wapi uso wako??

Nimemwandikia mhariri wa mtandao huu ( JF) kumwomba abadilishe title ya thread hii; " Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?".

Hata kama title ya thread imewekwa katika mtindo wa swali bado jibu la swali hilo ninalo, kuwa HAPANA.

Niko Iringa na naendelea na kazi zangu za kila siku katika ajira yangu. Baada ya kazi niko na familia yangu, kazi za kublog na shughuli nyingine za kijamii. Sijajihusisha kwa namna ye yote na kampeni za siasa, iwe Udiwani, Ubunge na Urais, kwa mgombea ye yote na Chama cho chote kile, iwe katika chaguzi zilizopita na hata uchaguzi wa mwaka huu. Anayeweza kuthibitisha kinyume chake aje.

Watu wana uhuru kuchangia maoni yao hata kama wanafikiria hivyo. Lakini kuweka title katika mtindo huo kunaweza kuwafanya wengine waamini ndio ukweli wenyewe.

Ni matumaini yangu mhariri wa JF atatanguliza uungwana na kubadilisha title hiyo ya thread hii. Inanipa usumbufu, mimi na hata familia yangu, kwa vile haina chembe ya ukweli.

Natanguliza shukrani.

Nimemwandikia mhariri wa mtandao huu ( JF) kumwomba abadilishe title ya thread hii; " Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?".

Hata kama title ya thread imewekwa katika mtindo wa swali bado jibu la swali hilo ninalo, kuwa HAPANA.

Niko Iringa na naendelea na kazi zangu za kila siku katika ajira yangu. Baada ya kazi niko na familia yangu, kazi za kublog na shughuli nyingine za kijamii. Sijajihusisha kwa namna ye yote na kampeni za siasa, iwe Udiwani, Ubunge na Urais, kwa mgombea ye yote na Chama cho chote kile, iwe katika chaguzi zilizopita na hata uchaguzi wa mwaka huu. Anayeweza kuthibitisha kinyume chake aje.

Ni matumaini yangu mhariri wa JF atatanguliza uungwana na kubadilisha title hiyo ya thread hii. Inanipa usumbufu, mimi na hata familia yangu, kwa vile haina chembe ya ukweli.

Natanguliza shukrani.

Kuna post moja hapo juu umesema,kama umeamua kuwa boxer basi huna sababu ya kuogopa ngumi za uso. Kaka hizi ndio gharama za uandishi wa habari na bado maoni yako yakija kuwa kweli umma huu unao/tunao kuparura hatutakuja kukuomba msamaha hata kidogo.

Vumulia kaka,utatukuzwa na historia.

Back
Top Bottom