Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?

Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?

Bwana Majjid Mjengwa,

Makala zako huwa nazisomasoma kwa mbali na mara zote nimekuwa nikihisi kuwa wewe ni mkereketwa,mfurukutwa,mshabiki na kada wa Chama Cha Majambazi-CCM. Nakumbuka kusoma makala zako kuhusiana na ufisadi nyingi zilikuwa zikielemea upande wa mafisadi.

Ninachotaka kukwambia Bwana Majjid ni kuwa hoja zako ni dhaifu sana kwa kujaribu kuwatetea CCM ambao ni chama chako. Siwezi kushangaa kuwa pengine kwa miaka kadhaa ijayo tukakusikia na wewe umependekezwa kugombea ubunge wa majimbo ya huko kwenu Uheheni(Iringa).

Bwana Mjengwa nataka nikufahamishe tu kuwa enzi za uandishi wakuwalaghai Watanzania kwa propaganda za kipuuzi umekwisha. Time is no more of fooling Tanzanians. This shall stand quoting.

Kwa maneno yako uliyo andika hapo juu huna TOFAUTI NA MHARIRI WA THE DAILY NEWS ALIYEANDIKA UPUUZI WAKE KUWAAMBIA WATANZANIA KUWA DR. SLAA HAWEZI KUWA RAIS WA AWAMU YA 5. Yawezekana wewe ni mmoja wa vibaraka wanaotumia na CCM kupotosha ukweli kwa kutumia kalamu zao!!!

Mimi nakushauri uache hizi propaganda za kizushi za kutaka kuwachagulia Watanzania Rais kabla hata ya kura kupigwa. Najua kabisa CCM sasa hivi hawalali wanakesha wakiweka mikakati ya namna watakavyoiba kura ili Kikwete ashinde.

Kuna maswali ambayo nataka uyajibu kupitia hii forum:
  1. Unafikri ni kwanini ratiba za Kikwete za kampeni zimebadilishwa kutoka kwamba baada ya kuanguka Jangwani alipashwa apumzike lakini mpaka sasa hajapumzika kwa kuhofia kushindwa na Dk. Slaa?
  2. Kwanini Serikali ya CCM wamepeleka waraka wa kuwaambia wakuu wa Idara za serikali wakiwemo Polisi,Wakurugenzi wa Wilaya na Mikoa,Wakuu wa Idara za usalama(mashushu) kwamba wafanye KILA WAWEZALO KUHAKIKISHA CCM INASHINDA???
  3. Wao kama chama unachosema kina advantage ya 3Ks yaani Kikubwa,Kikongwe na Kinachotawala why use all those powers to win the Election. Kwanini???
  4. Wao ni chama tawala kinachopendwa na kila mtu na kimeleta maendeleo ya elimu,afya na BORA MAISHA KWA KILA Mtanzania. Kwanini wahangaike na Dk. Slaa paroko ambaye hata ndoa yake kwao CCM imekuwa ni mtaji???Why all those worries???
  5. Kama CCM wanapambana na ufisadi kweli na kuna kesi ziko mahakamani za kina MRAMBA na CHENGE, kwanini Kikwete anakula matapishi yake kwa kuwapigia debe mafisadi hao hao warudi tena Bungeni au kwenye serikali yake?????
  6. Je, huoni kwamba hizo kesi za EPA ni viini macho,danganya toto na funika kombe mwanaharamu apite???Kwanini CCM wasipishe Ikulu ili chama chenye dhamira na nia ya kupambana na rushwa kikaendesha nji hiii???
Bwana Mjengwa Majjid napenda nikuhakikishie kwamba KAMA CCM HAWATAIBA AU KUCHAKACHUA MATOKEO YA KURA ZA UCHAGUZI WA MWAKA HUU WA 2010 HISTORIA INAENDA KUANDIKWA na wewe utakuwa wa kwanza kutafuta kamba ya kujitudika kwenye mti maana najua hasira zenu za kihehe!!!!!!!.Tehetehe,Hahaahaaaa!!

Wasaalamu.

Makoye.

Tatizo la Mjengwa ni shule.Anajitahidi sana kujitambulisha kama mwandishi wa makala mwenye upeo mkubwa ilhali ametawaliwa na na udini na mapenzi yaliyokubuhu kwa Kikwete.Laiti angekuwa na upeo stahili,asingekurupuka na takwimu outdated.Yeye na JK wake wanatufanya Watanzania wajinga,wanaamini chochote watakachosema kitakuwa hivyo.

Ni mlevi pekee anayeweza kudai eti CUF itashika nafasi ya pili bara....unless huo ndio mkakati wa Usalama wa Taifa,kuiba kura za Chadema ziiwezesha CCM kushinda na zitakazosalia wapewe CUF.

Dawa ya wababaishaji kama Mjengwa ni kuwapuuza tu.Huyu hana tofauti na Sheikh Yahya

Ukosefu wa Elimu+Njaa =
 
Lugha anayotumia ni lugha iliyozoeleka ya usalama wa taifa. Hutumia kauli za kujaribuu kukatisha tamaa. hata waziri wa habari wa Iraq alifanya hivyo hivyo wakati akiongea huku nyuma yake vifaru vinaonekana.
Kama hatuoni basi tuambie. Lakini tunaona umetengeneza maoni yafanane na matamanio yako. Naona hujaona wananchi walivyoamka Nyamagana, Kiteto, Moshi, Mbeya Mjini, Iringa, Arusha, Ubungo, Rombo, Hai, Karatu, Mbulu, Babati, Laiti ungejua kuwa mikutano ya CCM watu wanatolewa mbali na kwa gharama. Basi jaribu kutembea kidogo. Hata Lipumba akiwa mkweli hakubaliana na maoni yako. Nani amekuambia matokeo unayoyasema ndivyo yalivyokuwa? Tuulize tutakueleza mambo yalivyokuwa. Muone Mrema atakuambia ukweli. Hata Mwai Kibaki inasemekana alishinda ndio maana ni rais.
 
Na Maggid Mjengwa,

Mwalimu Nyerere alipata kusimulia kisa cha mbwa wa Manzese. Nilikuwa bado kijana mdogo sana niliposikia kisa kile. Ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 80. Ni kwenye kilele cha Sherehe za Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi. Sherehe zile zilifanyika pale Uwanja wa Taifa. Nilibahatika kuwapo uwanjani.

Baadhi ya mabango ya wafanyakazi yaliyopita mbele ya Mwalimu siku ile yaliwakilisha ujumbe juu ya hali ngumu ya kimaisha iliyokuwa ikiwakabili wafanyakazi; mishahara midogo na mengineyo.

Wakati huo, Serikali ya Mwalimu ilikataa masharti ya Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia pia. Hii ni kwa sababu, licha ya athari nyingine mbaya kwa masharti hayo kwa nchi yetu, uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu nao ulikuwa hatarini.

Ilipofika wakati wa kutoa hotuba yake, Mwalimu Nyerere alisema;

“ Ndugu zangu watu wa Dari Salama ebu nisikilizeni; kulikuwa na mbwa wawili, mmoja wa Manzese na mwingine wa Oysterbay. Ikatokea siku moja mbwa wa Manzese akatembea hata akafika Oysterbay.

Kwenye moja ya nyumba za huko Oysterbay akamwona mbwa mwenzake aliye ndani ya geti. Mbwa yule wa Manzese akasogea getini huku akimshangaa mbwa wa Oysterbay. Mbwa yule wa Oysterbay alinenepeana huku manyoya yake yakiwa yameteremka hadi machoni. Mbwa wa Oysterbay naye alimshangaa mwenzake wa Manzese. Mbwa yule wa Manzese alionekana kukondeana huku masikio yake yakiwa yameteremka hadi shingoni. Mbwa wa Oysterbay kwa mshangao akamwuliza mwenzake wa Manzese; “ Hivi nawe ni mbwa kama mimi?!
“Naam, miye ni mbwa kama wewe.” Alijibu mbwa wa Manzese.
“ Sasa mbona umekondeana hivyo, njoo humu ndani kwa bwana wangu nawe uwe kama mimi.”
Mbwa wa Manzese akajibu;
“ Lakini wewe umefungiwa, mwenzio niko huru!”

Sitakisahau kamwe kisa kile alichosimulia Mwalimu Nyerere pale Uwanja wa Taifa. Naamini katika alichokisema Mwalimu. Nitaendelea kuamini hivyo hata katika muda wangu uliobaki humu duniani. Mwalimu alizungumzia dhana ya uhuru. Ingawa ni neno fupi sana, lakini neno uhuru lina maana kubwa. Asiye na uhuru ni mtumwa.
Mimi ni mtu huru. Na siku zote nimepigania nibaki kuwa mtu huru. Kwa uhuru kabisa nakutana na kuongea na watu wengi; vijijini na mijini. Nakutana na kuongea na wasomi na wasio wasomi, matajiri na masikini. Sijapata maishani mwangu kulazimishwa au hata kulipwa ujira ili niongee au niandike mawazo yasiyo yangu au nisiyokubaliana nayo.
Ni bahati mbaya pia, katika jamii yetu, kila anayeandika makala magazetini kama nifanyavyo, basi, atasemwa kuwa ni mwandishi wa habari. Wengi hawatofautishi baina ya mwandishi wa habari na mwandishi wa makala.

Napenda sana kuandika fikra zangu huru kwa azma ya kuchochea mijadala. Jana niliandika fikra zangu kwenye Jamii Forums. Nimefanya hivyo huko nyuma. Lakini jana nimepata watu wengi walioshiriki mjadala. Wametoa fikra zao, kuna walionitukana pia. Nimeshazoea. Nayasoma matusi hayo, nikiamini, hata kwenye matusi hayo kuna cha kujifunza. Kufahamu fikra za watoa matusi hayo.

Na hakika, kuna wanaofikiri wananifahamu. Wamenipa majina, wamenihusisha na huyu na yule. Kimsingi hawanijui. Wamekuwa ni wakandamizaji wa fikra huru na wanaamini kila anayeandika mawazo yasiyofanana na yao, basi, amenunuliwa. Huu ni udhaifu, ni unyonge wetu pia. Hatujiamini.

Nitaendelea kuandika fikra zangu huru, napenda sana kuandika mawazo yangu. Nimefanya hivyo tangu nikiwa Sekondari pale Tambaza, tena kwa kuazisha kijarida cha shule. Niliandika mwenyewe kwa mkono, nilikuwa na wasomaji wangu pia. Tuliokuwa nao Tambaza miaka ile ya 80 ni mashahidi wa hilo.

Najua kuwa wakati mwingine kuna wanaokerwa na niandikayo. Hao wapo siku zote. Hatuwezi kufanana kimitazamo. Na tumekuwa wepesi sana, kila tusomapo mawazo ya mtu, kutafuta droo ya kabati la kumpachika. Siku hizi kuna droo za CCM, CHADEMA, CUF, Uislamu, Ukristo, Uchaga, Usukumuma na kadhalika.
Na ni bahati mbaya sana, kuwa wengi tumeisahau "Droo ya Tanzania". Hii ni droo muhimu sana na ilipaswa iwe ya kwanza. Kwa kila tutendalo liwe kwa MASLAHI YA TANZANIA KWANZA. Maslahi ya Taifa. Na Hilo Ni Neno La Leo.

Maggid,
Iringa,
mjengwa
 
Majid:
yawezekana umepewa pesa na ccm ili kutoa tathmini za namna hiyo, lakini dhamira
inakusuta, maana nakuona kama unawajibika si kwa akili na ufahamu wako zaidi kama
unashurtishwa na watu fulani kwamba ni lzima ukitoa tathimini zako lazima ziiweke ccm juu
hata kwenye mazingira yanayoonekana kuwa ni magumu.
Nimejaribu kuisoma mara dufu hiyo tathimini yako lakini naona ina mapungufu mengi ya
ni ushahidi gani gani unaokusaidia kuwa kama uchaguzi ungefanyika leo basi Kikwete angekuwa
mshindi wa kwanza na Lipumba wa Pili na Slaa wa tatu,
Ama kuwa wazi na uweke wazi nini kiko nyuma za tathimini zako ikiwa ni kweli wewe uko huru na
nini unakiona, jaribu kuturidhisha na mambo muhimu yanayokubarikia kwa mwenye ufahamu ulio simama
juu ya nini kinakusaidia kutoa tathimini kama hizo,
 
Ama hawa wachadema bado wamelala ,hivi wanasahau kuwa CUF ni kinara wa siasa hapa Tanzania ,CUF imeikomalia Zanzibar ,chadema mnapoambiwa kuwa badu nyinyi ni watawaliwa basi mkubali tu hamna na hamuwezi kufanya siasa angalau kuikaribia CUF ,maggid amewagusa na amewapopoa vibaya sana pale alipowambia kuwa hata nafasi ya tatu hamuipati, waulizeni CUF itawambia vipi wanakutoa kapa ?

hiyo ni ilimu na siyo elimu hayo ni mawzo yua kisonge huko znz, na siyo humu jf
 
Na Maggid Mjengwa,

Mwalimu Nyerere alipata kusimulia kisa cha mbwa wa Manzese. Nilikuwa bado kijana mdogo sana niliposikia kisa kile. Ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 80. Ni kwenye kilele cha Sherehe za Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi. Sherehe zile zilifanyika pale Uwanja wa Taifa. Nilibahatika kuwapo uwanjani.

Baadhi ya mabango ya wafanyakazi yaliyopita mbele ya Mwalimu siku ile yaliwakilisha ujumbe juu ya hali ngumu ya kimaisha iliyokuwa ikiwakabili wafanyakazi; mishahara midogo na mengineyo.

Wakati huo, Serikali ya Mwalimu ilikataa masharti ya Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia pia. Hii ni kwa sababu, licha ya athari nyingine mbaya kwa masharti hayo kwa nchi yetu, uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu nao ulikuwa hatarini.

Ilipofika wakati wa kutoa hotuba yake, Mwalimu Nyerere alisema;

" Ndugu zangu watu wa Dari Salama ebu nisikilizeni; kulikuwa na mbwa wawili, mmoja wa Manzese na mwingine wa Oysterbay. Ikatokea siku moja mbwa wa Manzese akatembea hata akafika Oysterbay.

Kwenye moja ya nyumba za huko Oysterbay akamwona mbwa mwenzake aliye ndani ya geti. Mbwa yule wa Manzese akasogea getini huku akimshangaa mbwa wa Oysterbay. Mbwa yule wa Oysterbay alinenepeana huku manyoya yake yakiwa yameteremka hadi machoni. Mbwa wa Oysterbay naye alimshangaa mwenzake wa Manzese. Mbwa yule wa Manzese alionekana kukondeana huku masikio yake yakiwa yameteremka hadi shingoni. Mbwa wa Oysterbay kwa mshangao akamwuliza mwenzake wa Manzese; " Hivi nawe ni mbwa kama mimi?!
"Naam, miye ni mbwa kama wewe." Alijibu mbwa wa Manzese.
" Sasa mbona umekondeana hivyo, njoo humu ndani kwa bwana wangu nawe uwe kama mimi."
Mbwa wa Manzese akajibu;
" Lakini wewe umefungiwa, mwenzio niko huru!"

Sitakisahau kamwe kisa kile alichosimulia Mwalimu Nyerere pale Uwanja wa Taifa. Naamini katika alichokisema Mwalimu. Nitaendelea kuamini hivyo hata katika muda wangu uliobaki humu duniani. Mwalimu alizungumzia dhana ya uhuru. Ingawa ni neno fupi sana, lakini neno uhuru lina maana kubwa. Asiye na uhuru ni mtumwa.
Mimi ni mtu huru. Na siku zote nimepigania nibaki kuwa mtu huru. Kwa uhuru kabisa nakutana na kuongea na watu wengi; vijijini na mijini. Nakutana na kuongea na wasomi na wasio wasomi, matajiri na masikini. Sijapata maishani mwangu kulazimishwa au hata kulipwa ujira ili niongee au niandike mawazo yasiyo yangu au nisiyokubaliana nayo.
Ni bahati mbaya pia, katika jamii yetu, kila anayeandika makala magazetini kama nifanyavyo, basi, atasemwa kuwa ni mwandishi wa habari. Wengi hawatofautishi baina ya mwandishi wa habari na mwandishi wa makala.

Napenda sana kuandika fikra zangu huru kwa azma ya kuchochea mijadala. Jana niliandika fikra zangu kwenye Jamii Forums. Nimefanya hivyo huko nyuma. Lakini jana nimepata watu wengi walioshiriki mjadala. Wametoa fikra zao, kuna walionitukana pia. Nimeshazoea. Nayasoma matusi hayo, nikiamini, hata kwenye matusi hayo kuna cha kujifunza. Kufahamu fikra za watoa matusi hayo.

Na hakika, kuna wanaofikiri wananifahamu. Wamenipa majina, wamenihusisha na huyu na yule. Kimsingi hawanijui. Wamekuwa ni wakandamizaji wa fikra huru na wanaamini kila anayeandika mawazo yasiyofanana na yao, basi, amenunuliwa. Huu ni udhaifu, ni unyonge wetu pia. Hatujiamini.

Nitaendelea kuandika fikra zangu huru, napenda sana kuandika mawazo yangu. Nimefanya hivyo tangu nikiwa Sekondari pale Tambaza, tena kwa kuazisha kijarida cha shule. Niliandika mwenyewe kwa mkono, nilikuwa na wasomaji wangu pia. Tuliokuwa nao Tambaza miaka ile ya 80 ni mashahidi wa hilo.

Najua kuwa wakati mwingine kuna wanaokerwa na niandikayo. Hao wapo siku zote. Hatuwezi kufanana kimitazamo. Na tumekuwa wepesi sana, kila tusomapo mawazo ya mtu, kutafuta droo ya kabati la kumpachika. Siku hizi kuna droo za CCM, CHADEMA, CUF, Uislamu, Ukristo, Uchaga, Usukumuma na kadhalika.
Na ni bahati mbaya sana, kuwa wengi tumeisahau "Droo ya Tanzania". Hii ni droo muhimu sana na ilipaswa iwe ya kwanza. Kwa kila tutendalo liwe kwa MASLAHI YA TANZANIA KWANZA. Maslahi ya Taifa. Na Hilo Ni Neno La Leo.

Maggid,
Iringa,
mjengwa

PUMBA HATA SIJASOMa
 
uandishi wa darasa la saba
 
Neno La Leo: Wanavyonisema Na Mbwa Yule Wa Manzese!

"Ndugu zangu watu wa Dari Salama ebu nisikilizeni; kulikuwa na mbwa wawili, mmoja wa Manzese na mwingine wa Oysterbay. Ikatokea siku moja mbwa wa Manzese akatembea hata akafika Oysterbay.

Kwenye moja ya nyumba za huko Oysterbay akamwona mbwa mwenzake aliye ndani ya geti. Mbwa yule wa Manzese akasogea getini huku akimshangaa mbwa wa Oysterbay. Mbwa yule wa Oysterbay alinenepeana huku manyoya yake yakiwa yameteremka hadi machoni. Mbwa wa Oysterbay naye alimshangaa mwenzake wa Manzese. Mbwa yule wa Manzese alionekana kukondeana huku masikio yake yakiwa yameteremka hadi shingoni. Mbwa wa Oysterbay kwa mshangao akamwuliza mwenzake wa Manzese; " Hivi nawe ni mbwa kama mimi?!

"Naam, miye ni mbwa kama wewe." Alijibu mbwa wa Manzese.

"Sasa mbona umekondeana hivyo, njoo humu ndani kwa bwana wangu nawe uwe kama mimi."
Mbwa wa Manzese akajibu;

"Lakini wewe umefungiwa, mwenzio niko huru!"

Sitakisahau kamwe kisa kile alichosimulia Mwalimu Nyerere pale Uwanja wa Taifa. Naamini katika alichokisema Mwalimu. Nitaendelea kuamini hivyo hata katika muda wangu uliobaki humu duniani. Mwalimu alizungumzia dhana ya uhuru. Ingawa ni neno fupi sana, lakini neno uhuru lina maana kubwa. Asiye na uhuru ni mtumwa.

Mimi ni mtu huru. Na siku zote nimepigania nibaki kuwa mtu huru. Kwa uhuru kabisa nakutana na kuongea na watu wengi; vijijini na mijini. Nakutana na kuongea na wasomi na wasio wasomi, matajiri na masikini.

Sijapata maishani mwangu kulazimishwa au hata kulipwa ujira ili niongee au niandike mawazo yasiyo yangu au nisiyokubaliana nayo.

Ni bahati mbaya pia, katika jamii yetu, kila anayeandika makala magazetini kama nifanyavyo, basi, atasemwa kuwa ni mwandishi wa habari. Wengi hawatofautishi baina ya mwandishi wa habari na mwandishi wa makala.

Napenda sana kuandika fikra zangu huru kwa azma ya kuchochea mijadala. Jana niliandika fikra zangu kwenye Jamii Forums. Nimefanya hivyo huko nyuma. Lakini jana nimepata watu wengi walioshiriki mjadala. Wametoa fikra zao, kuna walionitukana pia. Nimeshazoea. Nayasoma matusi hayo, nikiamini, hata kwenye matusi hayo kuna cha kujifunza. Kufahamu fikra za watoa matusi hayo.

Na hakika, kuna wanaofikiri wananifahamu. Wamenipa majina, wamenihusisha na huyu na yule. Kimsingi hawanijui. Wamekuwa ni wakandamizaji wa fikra huru na wanaamini kila anayeandika mawazo yasiyofanana na yao, basi, amenunuliwa. Huu ni udhaifu, ni unyonge wetu pia. Hatujiamini.

Nitaendelea kuandika fikra zangu huru, napenda sana kuandika mawazo yangu. Nimefanya hivyo tangu nikiwa Sekondari pale Tambaza, tena kwa kuazisha kijarida cha shule. Niliandika mwenyewe kwa mkono, nilikuwa na wasomaji wangu pia. Tuliokuwa nao Tambaza miaka ile ya 80 ni mashahidi wa hilo.

Najua kuwa wakati mwingine kuna wanaokerwa na niandikayo. Hao wapo siku zote. Hatuwezi kufanana kimitazamo. Na tumekuwa wepesi sana, kila tusomapo mawazo ya mtu, kutafuta droo ya kabati la kumpachika. Siku hizi kuna droo za CCM, CHADEMA, CUF, Uislamu, Ukristo, Uchaga, Usukumuma na kadhalika.

Na ni bahati mbaya sana, kuwa wengi tumeisahau "Droo ya Tanzania". Hii ni droo muhimu sana na ilipaswa iwe ya kwanza. Kwa kila tutendalo liwe kwa MASLAHI YA TANZANIA KWANZA. Maslahi ya Taifa. Na Hilo Ni Neno La Leo.
Maggid,
Iringa,http://mjengwa.blogspot.com
 
Tatizo TZ ni kwamba hakuna pollster ya kuaminika. Hiyo vaccum inajazwa na wapotoshaji kama hawa ambao wanaotoa maoni tu yasiyokuwa na mbele wala nyuma bila kuwa na support ya uptodate data.
 
Maggid nimeipenda sana ile hadithi ya Mbwa wa Manzese na yule wa Oysterbay...
Sasa wewe ni mbwa wa Manzese au Oysterbay maanake mambo yako sii mabaya!.
 
Nikimsoma Maggid naona Gado hakukosea kabisa!

90cart01102006oo6.jpg
 
Na Maggid Mjengwa,

Mwalimu Nyerere alipata kusimulia kisa cha mbwa wa Manzese. Nilikuwa bado kijana mdogo sana niliposikia kisa kile. Ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 80. Ni kwenye kilele cha Sherehe za Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi. Sherehe zile zilifanyika pale Uwanja wa Taifa. Nilibahatika kuwapo uwanjani.

Baadhi ya mabango ya wafanyakazi yaliyopita mbele ya Mwalimu siku ile yaliwakilisha ujumbe juu ya hali ngumu ya kimaisha iliyokuwa ikiwakabili wafanyakazi; mishahara midogo na mengineyo.

Wakati huo, Serikali ya Mwalimu ilikataa masharti ya Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia pia. Hii ni kwa sababu, licha ya athari nyingine mbaya kwa masharti hayo kwa nchi yetu, uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu nao ulikuwa hatarini.

Ilipofika wakati wa kutoa hotuba yake, Mwalimu Nyerere alisema;

" Ndugu zangu watu wa Dari Salama ebu nisikilizeni; kulikuwa na mbwa wawili, mmoja wa Manzese na mwingine wa Oysterbay. Ikatokea siku moja mbwa wa Manzese akatembea hata akafika Oysterbay.

Kwenye moja ya nyumba za huko Oysterbay akamwona mbwa mwenzake aliye ndani ya geti. Mbwa yule wa Manzese akasogea getini huku akimshangaa mbwa wa Oysterbay. Mbwa yule wa Oysterbay alinenepeana huku manyoya yake yakiwa yameteremka hadi machoni. Mbwa wa Oysterbay naye alimshangaa mwenzake wa Manzese. Mbwa yule wa Manzese alionekana kukondeana huku masikio yake yakiwa yameteremka hadi shingoni. Mbwa wa Oysterbay kwa mshangao akamwuliza mwenzake wa Manzese; " Hivi nawe ni mbwa kama mimi?!
"Naam, miye ni mbwa kama wewe." Alijibu mbwa wa Manzese.
" Sasa mbona umekondeana hivyo, njoo humu ndani kwa bwana wangu nawe uwe kama mimi."
Mbwa wa Manzese akajibu;
" Lakini wewe umefungiwa, mwenzio niko huru!"

Sitakisahau kamwe kisa kile alichosimulia Mwalimu Nyerere pale Uwanja wa Taifa. Naamini katika alichokisema Mwalimu. Nitaendelea kuamini hivyo hata katika muda wangu uliobaki humu duniani. Mwalimu alizungumzia dhana ya uhuru. Ingawa ni neno fupi sana, lakini neno uhuru lina maana kubwa. Asiye na uhuru ni mtumwa.
Mimi ni mtu huru. Na siku zote nimepigania nibaki kuwa mtu huru. Kwa uhuru kabisa nakutana na kuongea na watu wengi; vijijini na mijini. Nakutana na kuongea na wasomi na wasio wasomi, matajiri na masikini. Sijapata maishani mwangu kulazimishwa au hata kulipwa ujira ili niongee au niandike mawazo yasiyo yangu au nisiyokubaliana nayo.
Ni bahati mbaya pia, katika jamii yetu, kila anayeandika makala magazetini kama nifanyavyo, basi, atasemwa kuwa ni mwandishi wa habari. Wengi hawatofautishi baina ya mwandishi wa habari na mwandishi wa makala.

Napenda sana kuandika fikra zangu huru kwa azma ya kuchochea mijadala. Jana niliandika fikra zangu kwenye Jamii Forums. Nimefanya hivyo huko nyuma. Lakini jana nimepata watu wengi walioshiriki mjadala. Wametoa fikra zao, kuna walionitukana pia. Nimeshazoea. Nayasoma matusi hayo, nikiamini, hata kwenye matusi hayo kuna cha kujifunza. Kufahamu fikra za watoa matusi hayo.

Na hakika, kuna wanaofikiri wananifahamu. Wamenipa majina, wamenihusisha na huyu na yule. Kimsingi hawanijui. Wamekuwa ni wakandamizaji wa fikra huru na wanaamini kila anayeandika mawazo yasiyofanana na yao, basi, amenunuliwa. Huu ni udhaifu, ni unyonge wetu pia. Hatujiamini.

Nitaendelea kuandika fikra zangu huru, napenda sana kuandika mawazo yangu. Nimefanya hivyo tangu nikiwa Sekondari pale Tambaza, tena kwa kuazisha kijarida cha shule. Niliandika mwenyewe kwa mkono, nilikuwa na wasomaji wangu pia. Tuliokuwa nao Tambaza miaka ile ya 80 ni mashahidi wa hilo.

Najua kuwa wakati mwingine kuna wanaokerwa na niandikayo. Hao wapo siku zote. Hatuwezi kufanana kimitazamo. Na tumekuwa wepesi sana, kila tusomapo mawazo ya mtu, kutafuta droo ya kabati la kumpachika. Siku hizi kuna droo za CCM, CHADEMA, CUF, Uislamu, Ukristo, Uchaga, Usukumuma na kadhalika.
Na ni bahati mbaya sana, kuwa wengi tumeisahau "Droo ya Tanzania". Hii ni droo muhimu sana na ilipaswa iwe ya kwanza. Kwa kila tutendalo liwe kwa MASLAHI YA TANZANIA KWANZA. Maslahi ya Taifa. Na Hilo Ni Neno La Leo.

Maggid,
Iringa,
mjengwa

Karibu tena:llama:
 
Ama hawa wachadema bado wamelala ,hivi wanasahau kuwa CUF ni kinara wa siasa hapa Tanzania ,CUF imeikomalia Zanzibar ,chadema mnapoambiwa kuwa badu nyinyi ni watawaliwa basi mkubali tu hamna na hamuwezi kufanya siasa angalau kuikaribia CUF ,maggid amewagusa na amewapopoa vibaya sana pale alipowambia kuwa hata nafasi ya tatu hamuipati, waulizeni CUF itawambia vipi wanakutoa kapa ?
crap
 
Na Maggid Mjengwa,

............Napenda sana kuandika fikra zangu huru kwa azma ya kuchochea mijadala. Jana niliandika fikra zangu kwenye Jamii Forums. Nimefanya hivyo huko nyuma. Lakini jana nimepata watu wengi walioshiriki mjadala. Wametoa fikra zao, kuna walionitukana pia. Nimeshazoea. Nayasoma matusi hayo, nikiamini, hata kwenye matusi hayo kuna cha kujifunza. Kufahamu fikra za watoa matusi hayo.

Na hakika, kuna wanaofikiri wananifahamu. Wamenipa majina, wamenihusisha na huyu na yule. Kimsingi hawanijui. Wamekuwa ni wakandamizaji wa fikra huru na wanaamini kila anayeandika mawazo yasiyofanana na yao, basi, amenunuliwa. Huu ni udhaifu, ni unyonge wetu pia. Hatujiamini.

.........MASLAHI YA TANZANIA KWANZA. Maslahi ya Taifa. Na Hilo Ni Neno La Leo.

Maggid,
Iringa,
mjengwa
Kamanda Mjengwa.
kwanza pole sana kwa ujasiri wa kusoma hoja na matusi tele baada ya kuweka post yako humu. Ama kwa hakika umekutana na gari moshi ambalo halikukusubiri upite bali likakuburuza mpaka umeumia sasa.

Nafahamu kwamba unajua kuwa hivi sasa kuna vuguvugu la mabadiliko na hii yote inatokana na ujinga wa watanzania wachache ambao wanadhani kwa kuwa wao wanaifaudu keki ya taifa basi wanafanya hivyo kwa niaba ya taifa zima. na bila shaka unafahamu kuwa waandishi wa tanzania wananunulika bei chee hasa ktk kipindi hiki cha uchaguzi. Naamini unafahamu pia kwamba asilimia kubwa ya watanzania include waandishi hawana huruma na mafukara wa tanzania. Uongo unaozalishwa kila siku na waandishi walionunuliwa ndio ambao umesaidia kuweka watawala WABAYA madarakani. na watawala hawa wabaya wanawanufaisha waandishi commodities kwa kuwapa hela na nini cha kuandika.

Makala yako ile kwa ukweli imekera wengi na ni haki yao kukerwa kwa kuwa wewe mwandishi huru umeandika hoja huru ambazo kina anayezisoma ana uhuru wa kuziafiki au kutoziafiki. Amini nakwambia kaka yangu, hata nyerere alisema kwamba hakufanya mema peke yake seuse wewe na mimi? Kuna watu humu siyo waandishi kama ulivyo lakini ni wasomaji wazuri wa maandishi ya wenzao na kuyachambua kwa manufaa ya wengine, kuna ambao ukishaandika ndipo wao hupata cha kuandika pia, kuna wale kama mimi ambao tunasubiri uandike kisha tuyasome hayo maandiko yako. Mimi nilishaacha kukusoma loong ago ila huwa nasoma posts zako humu JF pekee.
Bandiko lako (huru) lilinipa uhuru wa kukunanga na kukusuta kama walivyofanya wengine.
 
Maggid,
Mkuu nimekuuliza kule kwingine.. wewe ni mbwa wa Manzese au Oysterbay maanake hali yako nzuri umenenepeana..
 
Nauona mjadala umepamba moto. Nasoma kila kinachoandikwa. Na matusi ninayotukanwa nayasoma pia. Kuna siku pale Kariakoo nilimkanyaga jamaa kwa bahati mbaya. Basi, acha anitolee matusi, mengine ya nguoni. Alipomaliza kunitukana nikwambia; " Ahsante sana!". Nikajiendea zangu.

Ni wale ambao, wameambiwa ukifika mjini lazima uwe ngangari. Mwenzio akikusukuma au kukukanyaga usimnyamazie. Mpe vipande vyake na zaidi mtukane.
Wengine tumefundishwa, kuwa ' Mwungwana' ni kauli na matendo, na si kauli za matusi, tena hadharani. Ahsanteni sana mliochangia na mnaoendelea kuchangia mada hii. Ahsanteni sana, hata mnaonitukana.
Maggid;

Nakala yako sio ya kisayansi na ni ya kisiasa inayoegemea zaidi nadharia za matokeo ya nyuma tena ya zaidi ya miaka zaidi ya 5 iliyopita bila kuingiza ukweli kuwa CCM ya sasa imepasuka!

Maggid;

ulishindwa hata kufanya "sampling" ktk jimbo unaloishi la Iringa mjini ambalo mwaka 2000-2005 lilikuwa salama kwa CCM lkn mwaka huu CHADEMA wana nafasi kubwa ya kulitwaa kutokana na mpasuko mkubwa wa chama hicho mjini Iringa!

Kama wewe ni mwadishi wa Nyanda za juu kusini,Kuna majimbo mengi sana ya mfano ktk ukanda wako ambayo kwa urahisi kabisa ungeweza kupata hali ikoje;Kwa mfano Jimbo la Mbeya Mjini mchuano ni mkali sana na yeyote kati ya CHADEMA na CCM anaweza shinda ,au jimbo la Mbeya Vijijini ambapo CCM wameonekana kama wamekwisha kata tamaa tayari!Au ulishindwa kwenda tu hapo karibu na wewe Njombe kuhoji watu kuhusu nafasi ya Thomas Nyimbo kulitwaa jimbo hilo?

Lkn Maggid akang'ang'ania tu kusema kuwa CHADEMA itashindwa na CUF kwa wabunge,akiipamba CUF kama itachukua majimbo zaidi ya 8 kusini lkn hajasema hata kidogo kuhusu majimbo dozens yanayoelekea upande wa chadema ukianzia mikoa ya Dar es salaam,Manyara,Arusha,Kilimanjaro,Geita,Mwanza,Shinyanga,Mara,Mbeya,Iringa anakoishi Maggid na kwingineko!

Kuhusu dhana kuwa CCM eti watapata wabunge wengi kwa sababu tu ya kuongoza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nayo naikataa;Mrema alishinda Temeke bila kuongoza serikali za vijiji kama alivyoshinda hayati Kabuye kule Kyerwa au Slaa kule Karatu;wakati ungine wa TZ wanachagua mtu na wala sio chama!

Waandishi tuandike ukweli sio upendeleo!
 
Kamanda Mjengwa.
kwanza pole sana kwa ujasiri wa kusoma hoja na matusi tele baada ya kuweka post yako humu. Ama kwa hakika umekutana na gari moshi ambalo halikukusubiri upite bali likakuburuza mpaka umeumia sasa.

Nafahamu kwamba unajua kuwa hivi sasa kuna vuguvugu la mabadiliko na hii yote inatokana na ujinga wa watanzania wachache ambao wanadhani kwa kuwa wao wanaifaudu keki ya taifa basi wanafanya hivyo kwa niaba ya taifa zima. na bila shaka unafahamu kuwa waandishi wa tanzania wananunulika bei chee hasa ktk kipindi hiki cha uchaguzi. Naamini unafahamu pia kwamba asilimia kubwa ya watanzania include waandishi hawana huruma na mafukara wa tanzania. Uongo unaozalishwa kila siku na waandishi walionunuliwa ndio ambao umesaidia kuweka watawala WABAYA madarakani. na watawala hawa wabaya wanawanufaisha waandishi commodities kwa kuwapa hela na nini cha kuandika.

Makala yako ile kwa ukweli imekera wengi na ni haki yao kukerwa kwa kuwa wewe mwandishi huru umeandika hoja huru ambazo kina anayezisoma ana uhuru wa kuziafiki au kutoziafiki. Amini nakwambia kaka yangu, hata nyerere alisema kwamba hakufanya mema peke yake seuse wewe na mimi? Kuna watu humu siyo waandishi kama ulivyo lakini ni wasomaji wazuri wa maandishi ya wenzao na kuyachambua kwa manufaa ya wengine, kuna ambao ukishaandika ndipo wao hupata cha kuandika pia, kuna wale kama mimi ambao tunasubiri uandike kisha tuyasome hayo maandiko yako. Mimi nilishaacha kukusoma loong ago ila huwa nasoma posts zako humu JF pekee.
Bandiko lako (huru) lilinipa uhuru wa kukunanga na kukusuta kama walivyofanya wengine.

Ni kweli ana uhuru wa kutoa mawazo,lakini kipindi hiki walio wengi wanataka nini? Watu wana hali mbaya kaka,ila wanashindwa wafanye nini ili kuuondoa utawala mbovu. Kama hajui wengi wanataka nini basi si kosa la waliom-crush. Pole ndio demokrasia hiyo (lazima gharama ziwepo).
 
ni kweli ana uhuru wa kutoa mawazo,lakini kipindi hiki walio wengi wanataka nini? Watu wana hali mbaya kaka,ila wanashindwa wafanye nini ili kuuondoa utawala mbovu. Kama hajui wengi wanataka nini basi si kosa la waliom-crush. Pole ndio demokrasia hiyo (lazima gharama ziwepo).

kwani walio wengi wanataka nini? Mwaka 1991 ilifanyika kura ya maoni tanzania na waliowengi walitaka mfumo wa chama kimoja!!, uchaguzi mkuu wa 1995 waliowengi waliichaguwa ccm, 2000 waliowengi wakaichaguwa ccm, 2005 waliowengi wakaichagua ccm, mwaka huu 2010 waliowengi ni wale wale watakaoirudisha ccm madarakani!!!! Au kwa maoni yako unataka kutuambia waliowengi ni wafuasi wa chadema? Au mtu kama si mpenzi wa chadema basi si mtanzania?
 
Back
Top Bottom