Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?

Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?

watu wote kwenye mitandao yote wameshamchoka JK

Mkuu Pasco. Kama huu sio uongo basi mwenzenu sijui definition ya UONGO.

Very unfortunately hao wanaopiga kura za on line opinion polls sio wapiga kura!, wapiga kura wenyewe hata umeme hawana, kula ya shida, ukiwapatia fulana tuu na kofia, shibe ya siku moja na nusu kilo ya sukari, basi ndio umemaliza kila kitu, na hawa ndio Watanzania anaowazungumzia Mjengwa.

Hapa kula tano mtu wangu.

Mjengwa na Michuzi ni mapandikizi ya Chama Cha Majambazi.

Nakumbuka kuzungumza na kijana mwuza ‘chipsi' pale sokoni Bagamoyo. Huyu aliniambia; " Braza, Jakaya huwa anapita hapa kwa miguu akienda nyumbani kwake. Na kichochoro anachopita hiki hapa. Ukimaliza kichochoro hiki nyuma hapo utaukuta mti wa mkungu, mbele kidogo kuna kiwanja cha watoto, nyumba yake inaonekana kwa mbele".

Watu kadhaa walinipa simulizi zenye kufanana juu ya Jakaya Kikwete aliye karibu na watu. Jakaya waliyezoea kumwona akikatisha mitaa ya Bagamoyo kwa miguu na kuzungumza na wananchi. Kwa namna moja au nyingine, simulizi hizi zilionyesha ni kwa jinsi gani mtu huyu Jakaya Kikwete asivyo na makuu.

Maggid ni mtu wa ovyo sana! Unasifia raisi eti hapendi makuu, anahudhuria misiba, hitima, harusi na vipairama! Pamoja na kufanya kazi kwa muda mrefu na jenerali ulimwengu bado uko mtupu namna hii! Usitake kutuaminisha wewe hajapokea fungu kufanya uanchokifanya, kumbuka watanzania hawadanganyiki. Mifano yako ni ya kijinga hakuna hata logic

Umenisikitisha sana

Mch Mas

bila shaka bahasha imetembea,sikutegemea mtu kama mjegwa ashabikie uchafu.

August, humu kwenye forum, tunafahamiana kwa threads na posts tuu, lakini tungekuwa tunafahamiana kiukweli, usingeweza kunifananisha na Mjengwa au maoni ya Redet. Kitu ninachojaribu kufanya ni kusimama kwenye ukweli na kwenye haki kuitetea haki muhimu sana iitwayo "freedom of expression" ambayo Mjengwa ndio katoa opinion yake, asishambuliwe yeye binafsi kama bali hoja zake ndizo zipanguliwe kwa hoja na sio kwa bezo. Mnyonge, mnyongeni, haki yake mpani.

Mkuu Pasco,

• Unaweza kutupa tathmini yako kuhusu makala kama haya ya Maggid na ile tahariri iliyotolewa kwenye gazeti la Daily News na Mkumbwa Ally ?
• Kama Daily News waliweza kutamka kuwa Dr. Slaa hawezi kuwa Raisi wa nchi hii, kwa nini tushangazwe na maoni au ripoti ya utafiti ya Redet ?
• Maggid haishii tu katika kumpa ushindi Jakaya Kikwete, anamsifia kwa alivyoweza kumudu nafasi yake ya Uraisi kwa miaka mitano na kuwashawishi wananchi wamchague tena.
• Na mwisho si kweli kuwa wananmtandao wote wamempa mgongo Kikwete - humu JF kwa mfano liko kundi kubwa tu likiongozwa na Mkuu Kibunango ambao naamini hata rangi ya damu yao ni kijani na Maggid ni moja wao.

Jameni, tujadili mada zingine, hii ya magig naona tanamwongezea umaarufu kwa pointi zisizo makini, huyu jamaa an mkono wa CCM. Na hili utaijua tu haihitaji kusoma shule.

Mkuu Pasco. Kama huu sio uongo basi mwenzenu sijui definition ya UONGO.
MgonjwaUkimwi, opinion polls ni factual issue sio feeling wala ushabiki, ukifanya opinion poll yoyote kuhusu JK na CCM yake, atabwagwa chini vibaya. Nlishasema kule nyuma, siku zote CCM inacapitalise kwenye ignorance ya Watanzania na ndio mtaji wake mkuu.

Sasa kwa vile online polls zinapigwa na watu walio na mwanga kidogo, kwa watu wenye akili timamu na wapenda haki genuinely hawawezi kuivote CCM ambayo ndio imetufikisha hapa! Ila pia nakubali wako wasomi wazuri tuu tena wenye akili timamu ambao watai-vote in CCM sio kwasababu wanaipenda kihivyo, bali kwa sababu ni beneficiaries wa CCM.

Nimempongeza Mjengwa kwa opinion yake kwa sababu huo ndio ukweli wake lakini amini nakuambia wapenda haki wote, mimi nikiwa ni mmoja wao, wangependa kuona CCM ikipumzishwa, sio kwa kuichukia, bali we need change!

Mkuu Pasco,

• Unaweza kutupa tathmini yako kuhusu makala kama haya ya Maggid na ile tahariri iliyotolewa kwenye gazeti la Daily News na Mkumbwa Ally ?
• Kama Daily News waliweza kutamka kuwa Dr. Slaa hawezi kuwa Raisi wa nchi hii, kwa nini tushangazwe na maoni au ripoti ya utafiti ya Redet ?
• Maggid haishii tu katika kumpa ushindi Jakaya Kikwete, anamsifia kwa alivyoweza kumudu nafasi yake ya Uraisi kwa miaka mitano na kuwashawishi wananchi wamchague tena.
• Na mwisho si kweli kuwa wananmtandao wote wamempa mgongo Kikwete - humu JF kwa mfano liko kundi kubwa tu likiongozwa na Mkuu Kibunango ambao naamini hata rangi ya damu yao ni kijani na Maggid ni moja wao.

Well said Mjomba.

Mjengwa,

You are entitled to your own opinion but not to your own facts.

tatizo lako wewe vs mjengwa mtoa makala ni lileli , yaani hitimisho hata hapa nilipo ku-quote nikiangalia hitimisho unamuelewa huyu mtu yupo poje objective au sio objective? sasa kama ungependa kujitofautisha na sisi tusio wajuvi wa uwandishi wa habari rekebisha hitimisho zako toa habari tu? mfano slaa alikuwa njombe jana/leo kasema dash dash na watu walizome/walishangilia basi sio kuweka hitimisho.
maanake wewe umekuwa prosecutor jaji na mtuhumiwa vyote at ze same time
Pasco who? who? huna comment kuhusu hitimisho???????
au na wewe ni sehemu ya biashara ya Slaa/kikwete/lipumba

MgonjwaUkimwi, opinion polls ni factual issue sio feeling wala ushabiki, ukifanya opinion poll yoyote kuhusu JK na CCM yake, atabwagwa chini vibaya. Nlishasema kule nyuma, siku zote CCM inacapitalise kwenye ignorance ya Watanzania na ndio mtaji wake mkuu.

Sasa kwa vile online polls zinapigwa na watu walio na mwanga kidogo, kwa watu wenye akili timamu na wapenda haki genuinely hawawezi kuivote CCM ambayo ndio imetufikisha hapa! Ila pia nakubali wako wasomi wazuri tuu tena wenye akili timamu ambao watai-vote in CCM sio kwasababu wanaipenda kihivyo, bali kwa sababu ni beneficiaries wa CCM.

Nimempongeza Mjengwa kwa opinion yake kwa sababu huo ndio ukweli wake lakini amini nakuambia wapenda haki wote, mimi nikiwa ni mmoja wao, wangependa kuona CCM ikipumzishwa, sio kwa kuichukia, bali we need change!

Pasco,

Moja...nadhani unaposema online polls huna maana na hapa JF ambako watu wanamajina kedekede na majina mengine yakitumiwa na watu kedekede...

Pili kuhusu wasomi nadhani utakuwa unatoa layman analysis. Ukweli ni kuwa wasomi wengi wapo CCM kwa sababu mbili kuu

MOJA. HAWAAMINI KUWA BILA YA USHIRIKIANO VYAMA VYA UPINZANI VINAWEZA KUCHUKUA NCHI LAKINI ZAIDI HATA KUWEZA KUENDESHA NCHI
PILI, HAWAONI CHAMA KAMA WANASIASA WA UPINZANI AMBAO WANA TOFAUTI NA WA CCM HIVYO HAWAJAPATA MBADALA BORA WA KURISK KUTUMIA NGUVU ZINAZOHITAJIKA KUIONDOA CCM

YOTE HAYA YANATOKANA NA KUWA WENGI WA WASOMI WANAWAJUA VIONGOZI HAO WA UPINZANI ZAIDI YA KWENYE LUNINGA NA MAGAZETI HIVYO WANAJUA UWEZO, NIA NA HATA UAMINIFU/UADILIFU WAO.

Hii ni kama una maana wasomi ni wale walioelimika zaidi ya lecture za madarasani na kuweza kutumia upeo wa elimu ya kuchambua masuala kwa mapana yake na sio katika muono wa hisia kama ambavyo wengi wa wanaoitwa wasomi huishia kufanya

What if they just dont see any alternative out there???

Two wrongs do not make a right.Not seeing an alternative does not in any way whatsoever justify trumping up some inconceivable predictions.

bila shaka bahasha imetembea,sikutegemea mtu kama mjegwa ashabikie uchafu.

Mjengwa nimjuaye mimi, sio bahasha type. Huyo ni mt wa msimamo usioyumba ndio maana amespeak his mind freely bila kuogopa na akaitundika humu akijua wazi mwelekeo wa kundi kubwa la members humu. Mwisho wa siku mtakuja mkubali Mjengwa ni shujaa aliyewaandaa kupokea habari mbaya kabla hazijatokeo hivyo kupunguza impact ya sad news kwa vile mlishaambiwa.

Pasco,

Moja...nadhani unaposema online polls huna maana na
hapa JF ambako watu wanamajina kedekede na majina mengine yakitumiwa na watu kedekede...

Pili kuhusu wasomi nadhani utakuwa unatoa layman analysis. Ukweli ni kuwa wasomi wengi wapo CCM kwa sababu mbili kuu

MOJA. HAWAAMINI KUWA BILA YA USHIRIKIANO VYAMA VYA UPINZANI VINAWEZA KUCHUKUA NCHI LAKINI ZAIDI HATA KUWEZA KUENDESHA NCHI

PILI, HAWAONI CHAMA KAMA WANASIASA WA UPINZANI AMBAO WANA TOFAUTI NA WA CCM HIVYO HAWAJAPATA MBADALA BORA WA KURISK KUTUMIA NGUVU ZINAZOHITAJIKA KUIONDOA CCM

YOTE HAYA YANATOKANA NA KUWA WENGI WA WASOMI WANAWAJUA VIONGOZI HAO WA UPINZANI ZAIDI YA KWENYE LUNINGA NA MAGAZETI HIVYO WANAJUA UWEZO, NIA NA HATA UAMINIFU/UADILIFU WAO.

Hii ni kama una maana wasomi ni wale walioelimika zaidi ya lecture za madarasani na kuweza kutumia upeo wa elimu ya kuchambua masuala kwa mapana yake na sio katika muono wa hisia kama ambavyo wengi wa wanaoitwa wasomi huishia kufanya

Omar, msomi ninaemzungumzia mimi ni msomi layman kabisa mwenye uwezo tuu wa kwenda net cafe na kupost poll sio wasomi in sense ya level ya academia.

Ila pia naamini, wana CCM wengi makini na genuine kama bosi wako, hawaridhishwi na maroroso anayofanywa na chama chao ila pia hawana guts za kutoka kwa vile ni benefisharies wa CCM. Mpendazoe alijiona shujaa, sasa anajuta!.
Pia nakubaliana na wewe kuhusu hii fragmented opposition kamwe haiwezi kushinda uchaguzi japo naamini there is still hope, kabla ya uchaguzi Lipumba na wagombea wengine wote wa urais wakubali kumback Dr. Slaa, ili ngoma ibaki timu mbili kama Simba na Yanga.

Mkandara, kwa uelewa wangu, Maggid Mjengwa sio mwandishi wa habari, he is not a kournalist but only a writer, yaani ni mwandishi wa makala, wengi hushindwa kuwatofautisha waandishi makala na waandishi habari kwa vile vyote huchapishwa gazetini.

Kwa mwandishi wa habari, opinion is not part of the news story, lakini kwenye makala, opinion inaruhusiwa. Kwa wanaomuona Mjengwa ni mwandishi, basi watawaona waandishi makala wote ni waandishi.

Mkuu Pasco,

Kama Mjengwa si Mwandishi wa Habari, ni kigezo gani ambacho huwa kinatumika kumwita atumike kuendesha mafunzo (resource person) kwa waandishi wa habari na hasa kwenye somo la UANDISHI WA KIRAIA. Some thing is wrong some where na utanifanya niongeze doubt zaidi kwa huyu mtu.

Waandishi wa makala huwa hawajui ethics za uandishi wa habari na ndio maana kuna makala inaweza kuandikwa na isichapishwe gazetini. Sasa huyu Mjengwa anapokwenda kufundisha/kuendesha kozi ya uandishi wa kiraia na ilihali hajui hata ethics za uandishi si ndio anakwenda kutuzalishia "manjanja" zaidi?

Nimempongeza Mjengwa kwa opinion yake kwa sababu huo ndio ukweli wake lakini amini nakuambia wapenda haki wote, mimi nikiwa ni mmoja wao, wangependa kuona CCM ikipumzishwa, sio kwa kuichukia, bali we need change!

Mkuu Pasco Pole sana maana naona na wewe umeingia kichwa kichwa katika kumtetea na Kumpongeza Mjengwa kwa hiyo makala yake, Lakini kwa wana JF wanaofatilia mijadala na kuweka kumbukumbu vizuri hawatashangazwa na namna Ndugu Mjengwa alivyo mrate Dr. Slaa

Labda nikukumbushe tu kidogo ni Kwamba Mjengwa amekuwa ni Mtu Asiyempenda Dr. Slaa na hata kumzushuia baadhi ya mambo katika Gazeti lake lililokufa kwa kukosa Wasomaji

Unaikumbuka hii toka Kwanza Jamii

Kamati ya Dk. Wilbroad Slaa yalamba posho mara mbili

12 May 2009

Na Mwandishi Wetu

MAELEZO yalivowahi kutolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, kwamba wapo baadhi ya wabunge wanaopokea posho mara mbili, yamethibitishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.

Ripoti hiyo ya CAG inathibitisha hali hiyo kutokana na ukaguzi wa hesabu za Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, ikidhihirika kuwa malipo yaliyofanywa kupitia vocha ya malipo yenye namba 1/8/066145, yaliyosainiwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo yalitumika kulipa wabunge posho.

Katika hali ya kawaida, wabunge hulipwa posho na ofisi ya Bunge hususan wanapokuwa katika shughuli za kawaida zinazohusiana na kamati za Bunge.

“Katika ukaguzi tulioufanya tuliweza kubaini matumizi yasiyostahili yenye thamani ya Sh 8,472,200 ambayo yasingeweza stahili kulipwa kwa kutumia fedha za miradi ya TASAF,” anasema CAG kupitia ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka ulioshia Juni 30, mwaka 2008, ripoti ambayo hata hivyo imekwishawasilishwa bungeni.

Maelezo yaliyotolewa kwa CAG kuhusu malipo hayo yanasema; “Posho kwa ajili ya vikao vya kamati ya Bunge ya hesabu za serikali za mitaa Agosti 7 hadi 16 mwaka 2007 yalikuwa Sh 1,050,000.

Kutokana na kubainika kwa hali hiyo huenda hadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Dk. Wilbroad Slaa, Mbunge wa Karatu, ikaingia doa mbele ya umma wa Watanzania.

Aprili 2, mwaka huu, Dk. Hosea aliwaeleza wabunge waliojaribu kuhoji uhalali wake wa kuiongoza TAKUKURU wakati akiwa anakabiliwa na tuhuma za kusafisha kashfa ya zabuni ya mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, kuwa kama watafanya hivyo basi nao pia wawe tayari kusikia kashfa zao mbele ya umma. Mara baada ya kutoa kitisho hicho kwa wabunge wakati wa semina ya miundombinu ya uadilifu iliyoandaliwa na Takukuru na Chama cha Wabunge wa Afrika (APNAC) na kufanyika kwenye Hoteli ya Whitesands, jijini Dar es salaam, Dk. Hosea alijikuta katika wakati mgumu.

“Inakuwaje wakati wa mjadala wa Richmond, wewe mkururugenzi wa Takukuru ulikanusha kuwapo rushwa na uchunguzi wa kamati ya Bunge ulibaini kuwepo rushwa ndani ya kampuni hiyo?

Je ni nani mwenye dhamana ya kukuadhibu wewe na taasisi yako kuhusu rushwa’’ alihoji Mbunge wa Busega, Dk.Raphael Chegeni katika semina hiyo.
Swali hilo halikutegemewa na Dk Hosea na lilionekana kumuudhi na kulazimika kuchukua kipaza sauti na kusitisha maswali na kuanza kujibu kwa ghadhabu.

“Hapa siyo jukwaani hivyo tusilete siasa. Nipo hapa kwa ajili ya kufundisha na kama ni suala la Richmond waziri mkuu alishaliongelea na ndiyo mwenye dhamana ya kujibu hilo. Mimi sina jibu kwa hilo na kama mtu hapendi kuvuliwa nguo kwanini umvue mwenzako,” alisema Dk Hosea.

“Mjadala huu aachiwe Waziri Mkuu Mizengo Pinda na aliyeuliza swali hilo hanitendei haki kwani hakuna hoja nyingine ya maendeleo kwa jamii ambalo inaweza kujadiliwa… mbona mnang’ang’ania kujibu hilo pekee.

“Najua kuna watu wanatumiwa ili niongee halafu nibabaike katika kujibu na nishindwe kufanya kazi yangu. Mbona mnang’ang’ania jambo hilo tu wakati kuna hoja nyingine za maendeleo kwa jamii. Kuhusu suala la Richmond sijibu ng’o.”

Chanzo:
Gazeti la Kwanza Jamii
Huyo ni Mjengwa na Kwanza Jamii yake alivyotaka kuuaminisha Umma wa Watanzania Juu ya Dr. Slaa. Bahati Nzuri Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe akalitolea Ufafanuzi hilo Jambo

Habari ya gazeti la kwanza jamii yaweza kwa njia moja ama nyingine kupotosha kwa kuonesha kuwa Dkt. Slaa aliruhusu Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kutoa posho kwa wajumbe wa kamati yake na hivyo kupata posho mara mbili.

Napenda kueleza kuwa mwaka 2007, Kamati ya LAAC ilikuwa chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Mgana Msindai. Kamati hizi za 'oversight' - ile ya LAAC na ile ya POAC zimeanza kuongozwa na wabunge wa upinzani kuanzia mwezi machi mwaka 2008. Kama kamati hii ililamba posho kutoka Halmashauri masikini kama ya Sumbawanga, jamii ijue kuwa haikuwa kamati ya Dkt. Slaa, ilikuwa kamati ya Msindai na dkt. Slaa hakuwa sio tu mwenyekiti, wala hakuwa mjumbe.

Hivyo, habari hii ya kwanza Jamii inaposomwa izingatie ufafanuzi huu.
Sasa Mwandishi wa Calibre hii anaweza kusimama Jukwaani na kutoa Tathmini Ambayo itakuwa fair? Waandishi kama Mjengwa wanafaa kukemewa na si kupongezwa hata kidogo

Mjengwa na Michuzi ni mapandikizi ya Chama Cha Majambazi.

Ningekuwa Mwalimu na huu ni mtihani, ningekupa 99% kwa kuandika short and perfect answer! Mie ndio maana hata blog ya huyo Mjengwa sina habari nayo!

Mkuu Pasco Pole sana maana naona na wewe umeingia kichwa kichwa katika kumtetea na Kumpongeza Mjengwa kwa hiyo makala yake, Lakini kwa wana JF wanaofatilia mijadala na kuweka kumbukumbu vizuri hawatashangazwa na namna Ndugu Mjengwa alivyo mrate Dr. Slaa

Labda nikukumbushe tu kidogo ni Kwamba Mjengwa amekuwa ni Mtu Asiyempenda Dr. Slaa na hata kumzushuia baadhi ya mambo katika Gazeti lake lililokufa kwa kukosa Wasomaji

Unaikumbuka hii toka Kwanza Jamii

Huyo ni Mjengwa na Kwanza Jamii yake alivyotaka kuuaminisha Umma wa Watanzania Juu ya Dr. Slaa. Bahati Nzuri Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe akalitolea Ufafanuzi hilo Jambo

Sasa Mwandishi wa Calibre hii anaweza kusimama Jukwaani na kutoa Tathmini Ambayo itakuwa fair? Waandishi kama Mjengwa wanafaa kukemewa na si kupongezwa hata kidogo

Ndege ya Uchumi:

Kwani nani amekwambia kuwa kumiliki gazeti ina maana kila habari iliyoandikwa kwenye gazeti husika imeandikwa na mmiliki wa gazeti? Uhuru linamilikiwa na CCM, ina maana kila habari katika uhuru imeandikwa na Mwenyekiti wa Chama hicho? Na Freeman Mbowe anamiliki gazeti la Tanzania Daima. Ina maana Freeman Mbowe ndiye anayeandika habari kwenye gazeti hilo? Gazeti lilikuwa na mhariri na habari hiyo haikuandikwa na mimi. Kama mtu ni mjinga, lakini hajui kama ni mjinga, unafanyaje?

Back
Top Bottom