Mmmhhh!
Kazi kweli kweli!
Bwana Maggid kuna tofauti kubwa kati ya fikra huru na biased expression of thought.
Makala yako ni dhahiri ina ujumbe wenye nia ya kushawishi kiupotoshaji kwa manufaa ya kisiasa.
Sababu ni nyingi na nitaziainisha:
1.Unasema "WENYE kupanga mikakati ya kivita wanajua, kuwa matokeo ya ushindi wa kivita hufahamika kabla risasi ya kwanza kupigwa. Inahusu matayarisho, malengo, mbinu na mikakati."
Historia na hata matokeo ya vita vya hivi karibuni yanathibitisha kwamba premise yako ni false!Wamarekani walipoingia vietnam waliamini watashinda kwa vile walikuwa na "matayarisho, malengo, mbinu na mikakati."Lakini leo tunajua kilicho wakuta mpaka wakakimbia bila ushindi.Wavietnam walizidiwa kila kitu,Pesa,Vifaa,Nyenzo za kivita,ujuzi na uzoefu wa kivita....Lakini walikuwa na kitu ambacho haya yote yasingeweza kukishinda "the human will" na determination yao.Vivyo hivyo Somalia.
2.Unasema "Leo, zikiwa zimebaki wiki nne kabla ya siku ya uchaguzi naiona hali iliyobadilika katika uwanja huu wa mapambano ya kisiasa. Naiona hali ifuatayo kama uchaguzi ungefanyika kesho".Hivi nini hasa kilichobadilisha hali hiyo ya mapambano ya kisisasa?Ahadi hewa na zisizotekelezeka za Kikwete?Taarifa za upotoshaji katika vyombo vya habari vya serikali?Ni nini hasa?Au container ya vifaa vya CCM vilivyoingizwa juzi?Makala yoyote yenye kutoa conclusions lazima ieleze conclusions hizo zimefikiwaje,kwa kutumia utaratibu upi na sample iliyotumika ilikuwa na muundo upi na ya ukubwa gani ili tuweze kuverify conclusions zako sio kutumia tu abstract conceptualizations!
3.Unasema bila haya "Huko nyuma nilibainisha, kuwa viashria vya jamii inayotaka mabadiliko vimeshaonekana. CCM itakuwa na mawili ya kuchagua; kuchukua jukumu la kuyaongoza mabadiliko hayo au kusubiri kuzamishwa na mkondo wa maji ya mabadiliko hayo"
False again!CCM si sehemu ya mabadiliko unayoyataja,Kwa kweli CCM ndio chanzo cha kiu ya mabadiliko hayo!Sasa unaposema CCM ichukue jukumu la kuyaongoza mabadiliko hayo unataka kutuambia kuwa SASA mbu anaweza kuongoza kampeni ya kutokomeza malaria kwa mafanikio!
Wewe Majjid vipi?Chadema wanasema tunataka gharama za kuwekeza katika elimu na afya zibebwe na serikali,CCM wanasema hayo hayawezekani!Halafu hao hao CCM ndio wasimamie kiu ya watanzania kupata elimu bora na si bora elimu kama kipaumbelele cha uwekezaji
wa Taifa?
Pili,Kwa taarifa yako mkondo wa maji hautakuja 2015! Uko sasa!Mkondo ni 2010 si 2015!
4.Angalia taarifa hii; Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Oktoba mwaka jana ulimalizika kwa kukipa ushindi mnono Chama Cha Mapinduzi. Chama hicho kilipata ushindi wa asilimia 91.71 za kura, kikifuatiwa kwa mbali na CUF iliyopata asilimia 3.94 na Chadema asilimia 2.76.
uchaguzi wa serikali za mitaa haukuwa na hamasa wala haukuamsha hisia zenye wimbi la mabadiliko kama ilivyo sasa!Watanzania wengi bado tulikuwa na chembe chembe za matumaini kwamba hali itaboreka,Kwamba CCM itajisafisha,lakini sasa ni dhahiri kuwa CCM haiwezi kujisafisha!Uchafu wao uko ndani ya mwili wenyewe,si kwenye nguo au ngozi tu bali ndani kabisa.Its in its very DNA if you will.Tumeona kwenye uteuzi wao,tumeona kwenye kulana wenyewe kwa wenyewe bila aibu-rejea masakata la Bashe,Mwakalebele,DED arusha,DED hai,DC kasulu,Na kadhalika mara kumi!
5. Mwanakijiji atatembea kwa miguu kilomita kumi kwenda kuhudhuria mkutano wa CCM. Atakwambia amepewa taarifa ya mkutano na Balozi wake wa Nyumba Kumi. Hivyo basi, CCM wanajivunia mtandao wao wa kichama kuanzia ngazi ya Balozi wa Nyumba Kumi, shina, tawi na kuendelea. Na hata mtandao wa Kiserikali.
Hilo tunalijua,N hasa hili la pili la mtandao wa Kiserikali.Ingawa wengi wa wanavijiji hao hawakuwa na mahali pa kukimbilia kwa maana ya "Credible and strong opposition" sasa wanapo!Tofauti na mawazo yako mimi natembea sana vijijini na huko nimekuta mwamko wa ajabu.Alama zinazoonekana bado ni za CCM kama vile mabango,picha,bendera nk lakini mioyo ya watu wengi ambao walikuwa wanachama na wapenzi wa CCM haiko tena huko!Wanaona afadhali upinzani kwa vile hali ya maisha imezidi kuwa duni kupindukia!Mfumuko wa bei haushikiki,bei za mazao hazijaboreka,Gharama za matibabu zinapanda kila siku,maji hakuna,umeme ndio ndoto ya alinacha....KIMSINGI WANAJIULIZA AHADI YA "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" IKO WAPI?NA KWA NINI KIKWETE HUYU HUYU ANATULETEA AHADI NYINGINE WAKATI ILE TULIYOIPENDA KUKAMCHAGUA YA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA HAJATUTIMIZIA?No,Majjid!Kikwazo nambari wani kwa watanzania kuingoa CCM sio wanachama,wapenzi wala wananchi wa vijijini na watanzania kwa ujumla wao!Ni mfumo ulioko madarakani!Ni serikali inayojitahidi kila kukicha kukikicha chama tawala unfair advantage!
6.Unasema "Inaonekana sasa, kuwa zama za ' First Lady' kuwa ' Mama wa nyumbani' Ikulu zimepita. Ni dhahiri, kuwa kwa mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, amenufaika sana na ushiriki wa karibu wa mkewe na mwanawe Ridhiwani. Na si kwa Jakaya Kikwete tu, CCM kama chama, wagombea ubunge wake wananufaika kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Mama Salma Kikwete na Ridhiwani kwenye kampeni.
Wote wawili, Salma Kikwete na Ridhiwani Kikwete wana mvuto wa kisiasa unaoongezewa nguvu na wao kuwa wanafamilia ya Rais aliye madarakani na ambaye bado, kiukweli, ana mvuto kwa Watanzania walio wengi."
Ukweli ni kwamba mvuto wa kikwete umepungua sana sana!Hivi sasa hana analoweza kujivunia katika utawala wake wa miaka mitano.Na ndio maana hata kauli mbiu yao ya "Maisha bora kwa kila mtanzania" si tu kuwa wameizika rasmi lakini hata kutamkika haitamkiki.Hata yeye binafsi anaona kuwa kutamka kauli mbiu hiyo kwa sasa ni kejeli kwa watanzania.Na kwa raisi mwenye sifa ya kuropoka na kutotumia busara katika kauli zake kama kiongozi wa nchi-kuliona hili basi ujue ameboronga kweli kweli!(Rejea kauli zake kuhusu wanafunzi na waathirika na ukimwi,Ukitaka kula lazima na wewe uliwe n.k)
Salma na Ridhiwani!
Salma asingekuwa anatumia rasilimali zetu sote kwa kampeni ya mumewe nadhani baadhi yetu tusingejali sana kwa vile ukweli ni kwamba hana ujumbe mpya wenye mvuto kwa watanzania.Binafsi nadhani ana "add insult to injury" kwa wengi wanaochambua masuala ya nchi yetu.Hanishawishi kwamba kikwete ni bora....On the contrary mm namwona kama kielelezo cha udhaifu wa kikwete mwenyewe na serikali yake.
Ridhwani!Hivi maggid unapozungumzia mvuto wa kisiasa unamaana nisha nini hasa?Haiba?Smiling faces?Ninavyo jua mimi mvuto wa kisiasa unatokana pamoja na mambo mengine ni falsafa inayotegemeza convictions zake, uwezo wa kupanga na kuelezea hoja zenye mafiko,Uzito na umuhimu wa ujumbe anaouwasilisha muhusika na jinsi muhusika anavyo fanikiwa kujitanabasisha na wanaomtazama au kumsikiliza.Katika haya yote sioni jinsi huyu bwana mdogo anavyofiti.Picha tunayoipata wengi linapotajwa jina lake ni mtoto wa baba (au mama),aliyeoteshwa kama uyoga kwenye medani za siasa za kitaifa bila kuwa na merits,anayetafuta cheap popularity lakini mwenye visasi na visa.Hatuona chochote kinacho mdifine yeye kama yeye anachoweza kukitumia kuwa impress watanzania.He is just another liability!
7. Udhaifu wa CHADEMA
Unajidhihirisha kwenye eneo la oganaizesheni na kifedha. Hilo nililibainisha katika makala yangu yaliyopita. Bado CHADEMA haina uwakilishi mpana katika ngazi za mashina na matawi. Niliandika, kuwa Dr Slaa anaweza kutua na helikopta Pawaga Iringa, lakini mara ile akiruka, huku nyuma hakuna watendaji wa CHADEMA wa kufanya kazi ya CHADEMA. Kuna taarifa pia za wagombea wake ubunge na udiwani kukosa nguvu za kifedha kuendesha kampeni .Hapa walau umesema ambacho wengi wetu tumekiona na ni changamoto ya kweli(Rejea post yangu juu ya kujitoa kwetu katika struggle ya kuleta mabadiliko jana hapa JF).Ingawa si kweli kwamba chadema haina uwakilishi katika ngazi za mashina na matawi.cha msingi hapa ni kukubali kuwa bado tuna kazi kubwa ya kufanya ingawaje haimananishi kwamba tuwaache CCM watupeleke ICU mwaka huu wakati tukiimarisha ngazi hizi tajwa,la hasha,ni afadhali turekebishe mapungufu haya wakati jahazi liko katika mikono salama ya Dr.Slaa.Hili la kukosa fedha limo ndani ya uwezo wetu,Kama kweli tunayahitaji mabadiliko yatakayotuletea Tanzania yenye neema ni lazima yatugharimu.Ni lazima tujitoe kwa hali na mali ili kuliangamiza zimwi liitwalo CCM.
Sijui kama utanikumbuka rafiki yangu maggid,Enzi zile za JKT Itende pale mbeya,enzi ambazo tulisafirishwa bure kwa warranti kwenda kujenga nchi yetu baada ya kusomeshwa kwa gharama za serikali zilizochangiwa na wananchi wote!
Enzi zile ambapo watumishi walikuwa wakiwajibika na kutimiza wajibu wao,Enzi ambazo kauli za kiongozi wa nchi ilikuwa ikimaananisha utashi wetu kama taifa,Enzi ambapo watoto hawakuwa wapiga debe wa baba zao,Enzi ambayo kichefuchefu cha kiongozi mkuu anayewasafisha na kuwakumbatia mafisadi papa bila aibu na kisha kutugeukia na kutuomba kura hakikutusumbua kama sasa!Enzi ambayo tuliamini katika kuweza na si katika mawazo mgando ya HAIWEZEKANI!!Enzi ambayo ilikuwa AIBU kuwa omba omba wakati sasa ni fahari ya TAIFA!
Nitaendelea kukufunulia udhaifu wa hoja na mkakati wenu kesho panapo majaaliwa.
:llama:
"True freedom must be expressed through the human ability to think critically, to analyze and to make informed decisions about oneself, his society and the world "- Sidanganyiki2010