Swali hili pia litajirudia hapa.
Wiki iliyopita Ukraine ilishambulia miundombinu ya Mafuta ndani ya Russia Kwa kutumia vile vidrone (quadcopter) vile vinauzwwa AliExpress na Alibaba Kwa Bei rahisi,je ilikuaje Russia yenye mifumo yenye nguvu ambayo mnaisifu kila siku humu kina S400,S300,Pantsir ishindwe kutungua vile vi-obsolete drone?!
Na mpaka sasa Ukraine hawajarusha hata jiwe kwenye hilo Daraja la Crimea waliishia kutoa vitisho tu sijui hizo habari umezitoa wapi
Lakini pia NI ukweli usiopingika na video zipo YouTube ammunition depot, command post zimepigwa Sana na hizo HIMARS Hadi kuna jamaa mtangazi wa Urusi (jina limenitoka) akawa anasema kwann Putin asiishambulie Marekani moja Kwa moja sababu silaha walizopeleka (HIMARS) zinaua watu wao.
NB:Hizo HIMARS si kwamba haziwezi kuharibiwa,La hasha! Ila NI kwamba ni ngumu kuzitarget sababu baada ya mashambulizi zinahama zinaenda mahali pengine. Warusi wakija kufanya counter attack wanapiga empy target sababu mtambo ushahamishwa. Pia mpaka sasa Ukraine iko outgunned na Russia kwenye kila mizinga 40 wao wanaweza kujibu mmoja (outgunned 40:1)