Hapo kwenye daraja linalounganisha Crimea na eneo lingine la Urusi majeshi ya Urusi yanafanya smoke screen ila haisaidii sana kwa kuwa daraja ni stationary target, smoke screen huwa na msaada zaidi kama target ni movable kwahiyo inabidi uipate yenyewe hivyo moshi unakupumbaza ujue sio hicho unachotafuta. Mbinu mwenzake na smoke screen ni camouflage.
HIMARS pamoja na kwamba zinafanya kazi ila ni za gharama kubwa sana. Maroketi hayo yana range kubwa na accuracy kuliko maroketi ya Warusi kina Grad, Smerch na Tornado (ambazo hizi kwa sasa sijaona zimetumika wapi).
HIMARS zina uharaka wa kupakia maroketi na kuwasha mfumo mzima tangu target acquisition, tracking, firing hadi kufunga mfumo na kutoweka eneo la tukio. Hii inasaidia kwamba HIMARS inaweza toka uko ikasogea karibu na adui ikamkaribia kama 20km hivi, ikafyatua maroketi yakaenda ndani kwa adui kama 120km (range yake kubwa ni 300km ila hizi roketi hazijapelekwa). Uko yakaharibu enemy fortification, command center, ammunition dump, etc. Hivi vitu ni lazima viwe vya thamani kubwa maana HIMARS ni ghali. Ndani ya dakika baada ya kufyatua mfumo unafungwa na gari lake linakimbia mbio kurudi mafichoni, si lazima lirudi kituoni. Hapo kule kwa Urusi kuna counter battery radar ambayo husoma ni wapi makombora ya adui yanatokea, hii hutoa pinpoit location kabisa. Warusi wakishasoma hii inabidi waagize howitzers zilizopo mbele kushambulia ambapo HIMARS zimesomeka. Huo muda HIMARS zishakimbia zamani sana.
Lengo ni kwamba HIMARS zikishashambulia deep behind enemy lines ndipo uku mbele majeshi ya Urusi yanakosa ammunition kama zimelipuka kule nyuma, au command center imeshambuliwa haitoi maagizo. Hii inapunguza nguvu na kasi ya kushambulia ya Urusi.
Kidogo nisahau. HIMARS zinaweza fanya coordinated attack, moja iko Mbezi nyingine Kigamboni na nyingine Mlimani City zikashambulia parking ya magari iliyopo Mlandizi kwa pamoja. Hii ina msaada mkubwa kwenye mazingira fulani