MOSSAD: "A" "BE" na "CHE" ya mashetani wenye ithibati ya mauaji

SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
5,613
2,000
Kumekuwa na haja na kiu kubwa ya baadhi ya watu humu kutaka kuifahamu MOSSAD na kazi zake. Kwa msukumo wa hilo, nimeona si mbaya tukajuzana angalau machache juu ya hawa watu na baadhi ya mifano hai ya kazi zao.

Jiandae kwenye karatasi zijazo kujifunza namna gani tumishi za Israel, zikiongozwa na Mossad, zinavyopambana, usiku na mchana, kulinda nchi yao, na pia kwa ziada nchi za magharibi vilevile.Kwa muono wa Israel, hawana la kupoteza kwenye vita yoyote ile. Hawana chaguzi nyingi zaidi ya kushinda kila muda. Lolote litafanyika kuhakikisha hilo. Na nadhani mimi na wewe twaweza kuwa mashahidi kwenye hili. (Rejelea vita kubwa ya mataifa kadhaa ilivyomalizwa na taifa la Israel ndani ya siku sita tu, watu wakaomba poh!)Siku za migogoro zaja. Iran anaweza jaribu kufanya kitu fulani kwa mujibu wa nguvu yake kinyuklia; magaidi pia waweza jaribu kufanya jambo hatarishi, au vyote kwa pamoja vikatukia. Raisi wa Marekani, kwa uhakika kabisa, atauliza;
"Kipi Israeli wanasema juu ya hili? Kipi wanajua? Ni nini wanachodhamiria kufanya ambacho sisi hatukifahamu?"
Na mwishowe;
"Nini Mossad watafanya? (Kupanga, kutekeleza, ama vyote)."
Marekani ni taifa kubwa, sina haja ya kuelezea kwenye hili. Kijografia huwezi ukailinganisha na Israeli hata kidogo, nchi ambayo itakulazimu uwe na microscope ili upate kuiona kwenye ramani ya dunia.Kitendo cha nchi kubwa kama Marekani, kijografia na kiuchumi, kuiulizia Israeli, ni jambo la kufikirisha kichwa. Lakini pia la kutufumbua macho kwamba kuna kitu ndani ya Israel; Kuna kitu cha kurejelea Israel; Kuna kitu cha kukitazama ndani ya Israel; kuna kitu cha kuhofia ndani ya Israel.
Na si kingine, hata kama kuna kingine basi kinazungukia hapa, kwenye taasisi nyeti ya kijasusi ya Mossad. Taasisi ambayo kwa mujibu wangu naweza sema ndiyo taasisi bora zaidi ya kijasusi kuwahi tokea duniani, hapa hatuhitaji kubishana.Kama vile sanamu la uhuru (statue of liberty) pale Marekani ama McDonald zilivyokuwa majina ya uwakilishi wa nchi hiyo kubwa, basi Mossad imekuwa ikitambuliwa kama "brand name" ya taifa la Israel. Hakuna Israel bila Mossad.
Shirika hili la kijasusi limekuwa kiungo kikubwa sana, japo kwa maficho, kwenye mambo mengi yanayotukia kwenye muda wetu, haswa mashariki ya kati.Lakini tusisite kujiuliza, Hivi Mossad ni wazuri kiasi hiki, cha kusemwa, kuogopwa, na kuongelewa?
Ndani ya zaidi ya miaka sitini, shirika hili la kijasusi la Israel limefanya pia makosa. Kufanikiwa ama kushindwa kwake kulitokana na ubora na ufanisi wa watu wake kazini. Wanapewa motisha. Lakini haibadilishi dhana kwamba na wao ni binadamu, hivyo hukosea ama kushindwa.Jina kamili la shirika hili la kijasusi ni HaMossad l’Modi’in u’l’Tafkidim Meyuchadim, kiebrania kinachomaanisha shirika la ujasusi na kazi maalum. Shirika hili lina wafanyakazi elfu ndogo, na katika muda mfupi hapo nyuma lilijipambanua kiasi kidogo kwa hadhira kwa kutumia tovuti ya Mossad.gov.il likienenda na motto rasmi usemao;
"Pale ambapo hamna shauri (counsel), watu huanguka; lakini penye wingi wa washauri (counselors) pana usalama."
Motto huu ulitoholewa toka kwenye biblia, Methali 11:14. Mstari huo ukisema;
"Pasipo na ulinzi (guidance), taifa huanguka; ila penye washauri wengi pana usalama."Lakini basi, je pana shaka lolote kuhusu motto huo? Aidha twaweza sema kwamba kwakuwa umetoholewa kwenye Biblia, basi dhamira yaweza kuwa njema, safi na yenye utukufu. Ila Mossad je, walidhamiria vivyo?
Neno "counsel" kwa lugha ya kiebrania hutafsiriwa kwa neno "takhbulot." Neno hili halina maana moja (ambigious word). Humaanisha maana kadhaa kama zifuatazo; ulaghai (deception), ujanja ujanja (trickery), mbinu (stratagem), au mwelekeo wenye hekima (wise direction). Hivyo basi kutokana na maana hizi tunashindwa haswa kujua dhamira halisi ya Mossad ndani ya motto huo. Kwani yaweza pia maanisha:

"Bila ya ujanja ujanja, Israel itaanguka ..."

Ama,

"Bila ya mbinu, Israel itaanguka ... "

Au,

"Bila ya ulaghai, Israel itaanguka ... "

Nani anajua?

Aliyewahi kuwa kiongozi (director) wa Mossad, bwana Efraim Halevy aliwahi kusema kwamba motto mwingine wa Mossad ungeweza kuwa;

"Kila kitu kinawezekana (kufanyika)." "Everything is do-able." Msukumo huu ndio ambao umekuwa ukiwasukuma Mossad, wakiamini kila kitu kinawezekana. Udogo wa nchi yao hauwazuii kwa njia yoyote ile wala kuwafanya wadhaifu.
Mbele ya macho yao (Mossad) kila kitu chao kina faida; kuanzia udogo wa nchi yao, upungufu wa wafanyakazi wao n.kHeshima ya shirika hili la kijasusi kwenye kufanya maamuzi ya tija, na kufanya shughuli zilizozidi hata ufanisi, imepelekea mambo makubwa kujiri; wana nguvu, wanajua karibia kila mambo, katili na wanaweza kupenya kona yoyote ya ulimwengu.
Israel wanaweza wakawa wamelitengeneza hili pasipo kujua, ila mpaka sasa wananufaika nalo. Pale ambapo jambo kubwa limetokea. Vyombo vya habari vikiwa vinabweka huku na huko wakitaja jina la Mossad, wakilituhumu ama kulipongeza. Hawa majasusi (Mossad) hawatii hata haladari ya neno. Hali hii ikajenga hofu ndani ya mioyo ya maadui zao, kwani hata pale Mossad wanapokuwa hawajahusika, bado hawabakizwi kutotajwa.Lakini wahenga na washenga walishawahi sema; "avumaye baharini papa lakini si kwamba wengine hawamo."Unapoongelea ujasusi wa dunia nzima, au haswa wa Israel, jina la kwanza kuja ni Mossad. Ila hawa hawafanyi kazi peke yao, na hata kwenye mafanikio hayo kuna mchango pia wa shirika lingine pacha "Domestic Shin Bet" ama kwa jina lingine hujulikana kama Shabak. Shirika hili uhusika sana na ulinzi wa ndani (internal/domestic affairs) ya taifa la Israel. Lakini pia juu ya hizi shirika, kuna 'mama' aendaye kwa jina la "Military - Aman", ama kwa kifupi; Aman.
Miongoni mwa hizi ogani tatu, zenye kuhusiana, Military Aman ndiyo yenye rasilimali kubwa kifedha na hata kinguvu kazi na ndiyo ambayo imechangia usalama wa Israel kwa kiasi kikubwa sana.Lakini pia mbali na hapo, katika mwendelezo wetu huuhuu tutapata nafasi ya kufunua vijisehemu vidogovidogo vya ulinzi wa siri (clandestine defense) wa nchi ya Israel, mbali na Mossad. Aidha utakuwa hauvifahamu vijishirika hivi, au basi kama wavifahamu basi si kiundani. Moja; ni ile inayoitwa ujasusi wa kiyahudi "Jewish Intelligence", ambayo hii husaidia wayahudi kuendesha ama kusimamia haki ya kisheria ya Israel kurejea kwenye ardhi wanayoamini wao kuwa ni ya mababu zao (ancients), ambapo huko hupewa uraia - lakini pia huendelea kuwalinda dhidi ya matamko, miongozo na nguvu za mataifa ama oganaizesheni kubwa za kimataifa kuligusa ama kutishia uwepo wa taifa hilo.Kijishirika kingine kidogo kilikuwapo kwa minajili rasmi ya ushirikiano wa karibu sana wa kisayansi "science liaison", ambacho husemekana kilifutwa baada ya jasusi; Jonathan Pollard kukamatwa akiwa anaipeleleza Marekani mwaka 1985. Kijishirika hiki kilifanikiwa sana kitunza siri za nguvu ya kisayansi ya Israel ikiwamo nyuklia, na taarifa zingine za kisayansi ambazo mpaka sasa hatuzijui, na ambazo mpaka sasa hazijathibitishwa na serikali ya Israel.
MEZA MATE ... HAYA, TUANZE TARATIBU...
Taifa la Israel limekuwa vitani tokea kipindi David Ben-Gurion alipotangaza utaifa wa jamii hiyo mnamo mwaka 1948. Na viongozi wa Israeli bado wanajichukulia wapo vitani kila siku. Lakini 'vita' hii siyo ile ya utaifa (1948), wala ile ya siku sita za mapambano (1967). La hasha! Jumuia zao za kijasusi zinataka kuhakikisha kwamba haitokuja kujirudia yale ya vita ya Yom Kippur, ama vita ya Ramadan (1973), ambapo shambulizi la ghafla la waarabu (Egypt na Syria), kama lipizo la vita ya siku sita (six days war), lililoigharimu nchi ya Israel, lingeweza kuzuiwa endapo kama majasusi waliopandikizwa nchini Misri wangepata kutiliwa maanani.
Kama ilivyo kazi ya taasisi ama shirika lolote la kiusalama, kazi yao ya kwanza si kupambana vita, bali ni kuzuia vita ama basi kuimaliza vita kabla ya 'kupambana vita'.

Kumuacha adui aanze kurusha kombora ni hatari sana kwani huwezi jua hilo kombora lina uwezo gani, laweza kukusambaratisha ama kukupoteza kabisa kwenye uso wa dunia. Na hapa Mossad ndio wanahangaika usiku na mchana kuhakikisha adui haanzi, bali anaanzwa na kumalizwa ikilazimika. Lengo ni ushindi tu, kuharibu ama kuchelewesha mipango ya adui bila ya kuhatarisha usalama wa wanajeshi lukuki na rasilimali ama wananchi wa Israel.HARAKATI KAZI ZA MOSSAD; MISHENI YA KWANZA. MPELELEZI NYUMA YA KINYAGO CHA CHUMA.Makazi ya watu wenye uwezo nje ya kitongoji cha Afeka kaskazini mwa Tel Aviv, yalikuwa yanatumika kumtazamia mwanaume ajulikanaye kwa jina la Rafael “Rafi” Eitan. Mwanaume mzee, mwenye uono hafifu na pia kiziwi wa sikio lake moja la kulia tangu apambane katika vita ya uhuru wa Israel.
Muonekano wake wa kimavazi ambao haupendezi machoni, huwafanya majirani zake kuamini kwamba ni mojawapo ya njia ya mwanaume huyo kuyakwepa, kiakili, yale mambo ya kikatili aliyowahi kuyafanya. Majirani hawa wanajua wazi bwana Rafi aliua watu kadhaa kwa ajili ya nchi yake (Israel), lakini si kwenye uwanja wa wazi wa vita (open battle) bali kwenye uwanja wa siri (secret battle) ambao ndio uwanja pendwa kwa Israel, uwanja wenye vita isiyokoma dhidi ya maadui zake.
Hakuna jirani anayejua haswa idadi ya watu waliouawa na Rafi, aidha kwa silaha ama kwa mkono wake wenye nguvu. Yale yote aliyokuwa anasema bwana huyo (Rafi) kwa majirani zake ni kwamba;
"Punde nilipotaka kuua, nilitaka kuyaona macho yao, uweupe wa macho yao. Basi nilikuwa mtulivu sana na mwenye mwongozo, nikifikiria kile tu ninachotakiwa kufanya. Alafu nikafanya. Hivyo ndivyo ilivyokuwa."Maneno hayo alikuwa akiyaambatanisha na tabasamu, tabasamu ambalo unaweza ukalifananisha na la mtu mwenye nguvu aliyedhamiria kumtisha mdhaifu.Kwa karibu robo karne, Rafi amekuwa naibu kiongozi wa harakati za Mossad. Sio kwa kukaa nyuma ya meza akisoma ripoti na kutuma wemgine kufanya kazi. Kwa kila fursa iliyotokea, alienda kwenye uwanja wa mapambano, alikuwa mbele akiwa anaongozwa na falsafa aliyofanikiwa kuifupisha ndani ya sentensi moja isemayo; "Kama wewe si sehemu ya jibu, basi ni sehemu ya tatizo."
“If you are not part of the answer, then you are part of the problem.”
Hakukuwahi kuwapo kama yeye (Rafi) kwa ukatili usio na huruma hata punje (cold-blooded ruthlessness), mipango ya ulaghai na ushawishi, na uwezo wa haraka mno wa kuandaa jambo ghafla. Ujuzi wa kupanga, na kutochoka kwenye ufwatiliaji wa mlengwa wake. Sifa zote hizo zilikuja kwake kwenye oparasheni moja tu iliyompa umaarufu mkubwa usiokoma kwenye nyanja ya ujasusi. Oparasheni hiyo si nyingine bali ni ile ya kumteka kiongozi mkubwa wa utawala wa ki- Nazi, Adolf Eichmann, ambaye ni mojawapo wa wahusika wa maamuzi ya mwisho yaliyotolewa na Adolf Hitler ya kuwaua Jews (6 million).Kwa majirani zake (Rafi) kwenye mtaa wa Shay, Rafi ni mfano mtakatifu, mwanaume aliyelipiza kisasi cha ndugu zao waliokufa, mwanaume mpiganaji aliyepewa fursa ya kuukumbusha ulimwengu kwamba hakuna kiongozi yeyote wa Nazi aliye salama baada ya kuwaangamiza watu milioni sita.
Hawachoki (majirani) kutembelea nyumba ya Rafi na kumsikiliza tena na tena akielezea oparasheni ambayo bado inatikisa kwa uthubutu wake.Akiwa amezungukwa na vitu vya thamani, Rafi angefungua mikono yake yenye misuli na kukaa kimya kwa muda, akiwaruhusu wasikilizaji wake wazame fikirani kipindi kile taifa la Israel linazaliwa. Alafu kwa sauti yenye nguvu, pasipo kuacha kitu, alianza kuwaambia majirani zake hao namna gani alipanga kumkamata Adolf Eichmann.
Kwanza, alitengeneza mazingira mazuri mno ya kuelezea simulizi yoyote ya utekaji nyara kwa muda wowote.Baada ya vita vya pili vya dunia, zoezi la kuwafuatilia wahusika wa mauaji ya Jews lilianza kufanywa na wale walionusurika na mauaji hayo. Walijiita "Nokmin" wakimaanisha walipiza kisasi. Hawakujisumbua kufuata mfumo wowote wa kisheria, wao walikuwa wanamnyonga mhusika yeyote wa Nazi waliyemtia mikononi.Rafi Eitan hajui wala hakumbuki kama kuna mahali popote walipowahi kumuua mtu asiyestahili kufa.
Lakini liwekwe rasmi kwamba, ndani ya Israel kulikuwa kuna haja hafifu sana ya kuwatafuta wahusika wa mauaji ya watu wao. Lilikuwa ni jambo la kipaumbele. Kama taifa, Israel walikuwa bado wachanga, tena wakizungukwa na mataifa adui ya kiarabu. Walikuwa na mambo mengi kwanza ya kuyazingatia kabla ya hilo, ila si kwamba walikuwa wamelipuuza. La hasha! Taifa la Israel lilikuwa mlemavu, lisilo na nguvu, na kama vile linapotea baada ya siku moja mbele.Ndani ya mwaka 1957, Mossad walipokea taarifa za kusisimua kwamba Adolf Eichmann, ameonekana nchini Argentina. Rafi, ambaye alikuwa ni nyota inayong'aa kutokana na ufanisi wa kazi zake dhidi ya waarabu, aliteuliwa kwenda kumkamata Eichmann na kumleta Israel kwa ajili ya kupewa anachostahili.Rafi aliambiwa oparasheni hiyo itakuwa na faida lukuki endapo ikitimia. Itakuwa ni hatua moja takatifu kwa watu wake kueleka kutendewa haki dhidi ya kile walichofanyiwa na wa -Nazi. Itaikumbusha ulimwengu wa kambi za vifo (death camps) na uhitaji wa kuhakikisha jambo kama lile haliji kutokea tena duniani. Lakini mwisho ni kwamba itaifanya Mossad kuwa mbele ya shirika zote za kijasusi ulimwenguni.Hakuna tumishi yoyote ya kijasusi ambayo ingethubutu kufanya oparasheni kama hiyo. Hatari yake ilikuwa ni kubwa mno. Rafi atafanya kazi maelfu ya maili toka nyumbani, atatumia dokumenti za kufoji, na kutegemea kwa kiasi kikubwa rasilimali zake mwenyewe kwenye mazingira adui. Argentina ilikuwa ni mahala salama kabisa kwa wa - Nazi, hivyo wana - Mossad wangeweza kukamatwa, kufungwa na mwishowe hata kuuawa punde tu wakigundulikana.Kwa miaka mirefu miwili, Rafi Eitani kwa uvumilivu alingojea wakati kuonekana kwa mara ya kwanza kwa Adolf Eichmann kunathibitishwa kwamba mwanaume huyo alikuwa yupo katikati ya kitongoji cha watu wa daraja la kati Buenos Aires akitumia jina la Ricardo Klement.
Pale amri ya mwisho ya kufanya tukio ilipotoka (go order), Rafi alikuwa 'barafu.' Alishafanya mafikirio yake yote juu ya nini kinaweza kikaenda kombo. Kisiasa, kidiplomasia, na kwake pia bila kusahau madhara yatakayofuata baadae.Alijiuliza nini kitatukia akimkamata Eichmann na polisi wa Argentina wakaingilia ama kumzuia?
"Niliamua nitamnyonga kwa mikono yangu mpaka afe. Kama nikikamatwa, nitasema mahakamani kwamba nimefuata maneno ya biblia; jino kwa jino." Alisema Rafi.El Al, shirika la ndege la taifa, ambalo ndege yake (hii iliyotumika) ilitoka kwenye shirika la kutengenezea ndege la Uingereza huku pesa ikitoka mfukoni mwa Mossad, ndilo lilimsafirisha Rafi kwenda Argentina. Rafi alisema;
"Tulimtuma mtu Uingereza akanunue moja. Alitoa pesa tukapewa ndege."
Lakini rasmi ndege hiyo iliyoelekea Argentina ilikuwa ni kwa ajili ya kubebelea maafisa wa ki Israel waliolenga kuwasili kwenye sherehe ya maadhimisho ya uhuru wa Argentina (115th). Hakuna afisa hata mmoja aliyekuwa anajua kwanini walikuwa wanaongoza na wao (Rafi na wenzake), na wala hawakuwa wanajua kama ndani ya ndege hiyo kulikuwa kuna chumba mahususi cha kumuhifadhia Adolf Eichmann.Rafi na timu yake walifika Buenos Aires May mosi, 1960. Walichukua nyumba moja iliyokodiwa na mkubwa wao, ambaye alipewa kificho (code) cha kiebrania "Maoz". Na mahali hapo ndipo palikuwa mahususi kama eneo la kuendeshea oparesheni yao. Walitengeneza pia mahali pengine maalum kwa ajili ya kumtunzia Adolf Eichmann baada ya kumkamata. Nyumba zingine pia zilikuwepo lakini mahususi kwa ajili ya kukabiliana na presha ya msako inayoweza kutokea toka kwa polisi wa ki Argentina. Pia magari kadhaa yakaandaliwa kwa ajili ya kazi.
Kila kitu kikiwa sawa, Rafi alitulia na kuzingatia. Shaka lolote lingeweza kupelekea wao kushindwa, lilikuwa limekabiliwa na sasa msukumo mkubwa ukawa kwenye kungojea.
Kwa siku tatu, Rafi na timu yake walifanya upelelezi kumfatilia Adolf Eichmann, ambaye awali alikuwa akiendeshwa ndani ya gari refu Mercedes limousine. Sasa siku hiyo Adolf Eichmann alikuwa anasafiri kwa basi na alishuka kwenye kona ya mtaa wa Garibaldi.Usiku wa siku hiyo, May 10, 1960. Rafi alikuwa ndani ya gari akiwa na dereva mwenye mafunzo ya kutosha, pamoja pia na mmojawapo wa wanaume wenye uwezo wa kumtageti mtu wanayemtaka mtaani. Yeye (Rafi) alikuwa pembeni ya dereva tayari kusaidia lolote litakalotokea. Walipopata walichokuwa wanakihitaji waliondoka wakilenga kufanya oparesheni jioni ya kesho yake.
Kwenye majira ya saa mbili usiku May 11, gari lililobebelea timu ya Rafi liliwasili kwenye mtaa wa Garibaldi. Hakuna yeyote aliyekuwa na presha. Hakuna yeyote aliyeongea. Hakukuwa na kitu cha kuongea bali kutenda. Rafi alitazama saa yake ya mkononi, saa mbili na dakika tatu. Walisogeza gari mpaka eneo fulani pweke.Mabasi kadhaa yalikuja na kuondoka. Kwenye majira ya saa mbili na dakika tano, basi lingine likaja. Wakamuona Eichmann akishuka.
"Mtaa bado ulikuwa mtupu. Nyuma yangu nilimsikia mtaalamu wetu wa ukamataji (snatchman) akifungua mlango wa gari. Tuliendesha gari taratibu kumfuata Adolf Eichmann. Alikuwa anatembea haraka kama mtu anayewahi chakula cha usiku nyumbani. Nilimsikia mkamataji mtaalamu wetu akihema taratibu, namna alivyofundishwa mafunzoni." Alisema Rafi."Alikuwa ana sekunde kumi na mbili tu za kufanya tukio. Kutoka ndani ya gari, kukamata shingo ya Eichmann na kumvutia ndani ya gari kisha tuondoke upesi!"Gari lilisonga karibu na Eichmann, aligeuka nusu kumtazama mtaalamu wetu aliyekuwa anashuka toka kwenye gari, ambaye hakufika mbali kabla ya kudakwa na kamba ya kiatu iliyokuwa haijafungwa vizuri. Nusura imwangushe.Kwa huo muda Rafi alitamani ashuke akamalize kazi. Alitoka karibia nusu ya dunia mpaka kufika pale kwa ajili ya kumkamata mtu anayehusika na kifo cha watu milioni sita wa nchi yake, na sasa walikuwa wanaelekea kumpoteza kwa sababu ya kamba za viatu! Eichmann aliongeza mwendo, ni kama alishajua yupo kwenye mazingira hatarishi. Akianza kutupa miguu yake, Rafi aliruka toka kwenye gari."Nilimdaka shingo kwa nguvu ambayo kama ningeiongeza kidogo tu basi ningemuua. Macho yake yalitoka nje. Mtaalamu wetu alifungua mlango upesi, nikamrushia Eichmann viti vya nyuma, haraka mtaalamu naye akajitupia humo ndani na kuketi juu ya nusu ya mwili wa Eichmann. Tukio hilo lilidumu kwa sekunde tano tu!"
Toka kwenye siti ya mbele, Rafi alikuwa anasikia Eichmann akihangaika kuhema. Mtaalamu wao alikuwa amemdhibiti mwanaume huyo vema kiasi kwamba kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele, alizidi kuwa mpole zaidi. Ilifikia mahali akauliza nini ilikuwa maana ya kile anachofanyiwa.Hakuna aliyemjibu. Kwa ukimya walifika kwenye nyumba salama iliyoko umbali wa maili tatu toka eneo la tukio. Rafi alimtaka Eichmann avue nguo kisha akamkagua akitazama vipimo vya kifizikia vya mwanaume huyo kama kweli ndiye. Rafi hakushangazwa na hali ya kutokuta tattoo ya SS (Schutzstaffel) mwilini mwa mwanaume huyo kama ilivyokuwa kwa wa - Nazi wengine, ilikuwa imeondolewa. Lakini vipimo vingine vyote vilikuwa sawa kabisa. Walimfungia Eichmann kitandani kwa pingu. Kwa masaa kumi wakamwamcha mwanaume huyo gizani pasipo na sauti yoyote."Lengo lilikuwa ni kuchochea hisia za kukosa matumaini ndaniye. Mpaka asubuhi tayari Eichmann alikuwa yu mnyong'ofu kiakili. Nilimuuliza jina lake akanitajia la kihispania ... Nilisema hapana, hapana, hapana, jina lako la kijerumani, akataja jina alilotumia kukimbilia nalo huko Ujerumani, nikasema tena hapana! Nataka jina lako la ukweli, jina lako la SS. Alijinyoosha kitandani kisha akasema kwa nguvu akisikika 'Adolf Eichmann'. Sikumuuliza tena, sikuwa na hitaji hilo."Kwa siku saba zilizofuata, Eichmann alikuwa bado gizani. Alikula na kulala gizani. Hakuna yeyote aliyemuongelesha."Kumuweka kimya na gizani kilikuwa ni zaidi ya matakwa ya oparesheni. Hatukutaka kumwonyesha Eichmann namna tulivyokuwa na hofu kwani hilo lingempa matumaini. Na matumaini humfanya asiye na matumaini kuwa hatari. Nilihitaji ajisikie hana msaada wowote kama vile watu wangu walivyokuwa kabla ya kupelekwa kuteketezwa kwenye kempu za vifo." Anaeleza Rafi.
**Siku ya kumsafirisha Adolf Eichmann.**Kwanza Eichmann alivalishwa nguo za wafanyakazi wa ndege ya El Al, ambazo nguo hizo zililetwa na Rafi toka Israel. Alafu alinyeshwa chupa nzima ya Whiskey na kumwacha katika hali ya kulewa chakari.
Rafi na timu yake walivalia suti zao na kidogo wakanywa Whiskey. Walimvalisha Eichmann kofia ya shirika la ndege na kumweka kwenye viti vya nyuma.Rafi aliendesha gari mpaka kwenye kambi ya jeshi huko ambapo ndege ilikuwa inawangojea, injini tayari zikichemka. Katika geti la kambi hiyo ya jeshi, gari likasimamishwa na wanajeshi wa Argentina. Kwenye viti vya nyuma Eichmann alikuwa anakoroma.

"Gari lilikuwa linanuka kama kiwanda cha pombe. Tulijifanya kama Jews walioparamia na kushindwa kuendana na vinywaji vikali vya ki-Argentina. Wanajeshi wale walifurahishwa na hilo jambo, hawakumtazama Eichmann mara mbili." Anaeleza Rafi.Ikiwa ni saa sita kasoro tano siku ya tarehe 21, May 1960, ndege iliacha ardhi ya Argentina huku Adolf Eichmann akiendelea kukoroma, sasa akiwa katika chumba chake mahususi ndani ya ndege.Baada ya kusikikizwa kwa urefu kwa kesi yake (Adolf Eichmann), alikutwa ana makosa dhidi ya ubinadamu. Kwenye siku yake ya kunyongwa, May 31, 1962, Rafi alikuwa kwenye chumba cha unyongaji."Eichmann alinitazama na kusema 'muda wako unakuja, myahudi', nikamjibu, 'lakini sio leo, Adolf, sio leo.Shingo yake ilimezwa na kitanzi, Eichmann akatoa sauti ndogo sana ya kukabwa. Kisha kukawa kunasikika sauti ya mwili wake tu ukibembea. Sauti ya kuridhisha sana." Anasema Rafi.Jiko maalum liliandaliwa kwa ajili ya kuuchoma mwili wa Adolf Eichmann. Ndani ya masaa majivu yake yalimwagiwa baharini ndani ya eneo kubwa. Hakikutakiwa kibakie kiashiria chochote cha Adolf Eichmann juu ya uso wa dunia.
Baada ya hapo, jiko lililomchoma liliharibiwa na kutotumika tena. Jioni hiyo Rafi alisimama ufukweni na kutazama bahari, akijisikia amani kabisa."Kumaliza kazi yangu, hilo siku zote ni hisia nzuri."

*** HAYA, TUENDELEE. NA LEO TUTAZAMIE VISA VYA 'WAUAJI' ***
ASSASSINS - "WAUAJI"Kidon ni moja ya "unit" ya siri sana ya Mossad. Aidha ni Mossad ndogo (Mini - Mossad) au ni sayari ya pekee yenye mzunguko tofauti na nyinginezo. Ukweli ni kwamba, oparesheni za KIDON hukingwa na na siri mno (strict secrecy) na zaidi hulindwa na usiri wa jumla wa jeshi la Israel mbele ya vyombo vya habari.
Lakini yote hayo hayatoshi kutufanya tusipate taarifa juu ya hii taasisi siri; Namna inavyoopareti, saikolojia za watendaji wake na hata pia hisia tendaji (mood) za wauaji hawa. Tuwe pamoja kwenye hili ...Hii taasisi kisu ni ndogo lakini lakini fanisi, na huajirisha wanaume na wanawake ambao tayari wameshajithibitisha kwenye huduma zao za kijeshi au kwenye shirika ama kazi zingine za kijasusi. Watu hawa huchambuliwa kwa hatua mbalimbali ikiwemo kupembuliwa na kutunzwa katika saikolojia dakizi. Na hata zaidi kwenye ujuzi wa kuwafanya wakamilishe oparesheni zilizo kwenye 'kingo'.Wengi wao hutokea kwenye vikosi maalum vya upambanaji ndani ya Israel kama vile; Sayeret Matkal na Flotilla 13. Sayeret Matkal ni kikosi maalum cha ujasusi kinachojihusisha zaidi na ukusanyaji data (data/ information gathering) ambayo ndiyo huwa chachu ya mipango kutandazwa. Ndani ya kikosi hiki ndipo alipotokea aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Israel, bwana Netanyahu.Flotilla 13 ama Shayetet 13, hiki ni kikosi cha makomando ndani ya jeshi la ulinzi la Israel. Hawa ndiyo 'wanaume' waliohusika na mgogoro wa Gaza na vita ya Israel dhidi ya Lebanon.Watu hawa (KIDON) hufundwa na walimu wenye motisha ya hali ya juu na hufanya kazi kwenye timu ndogo ya watu wawili au wanne kwa kila timu — timu hizi huenda kwa jina la kiebrania "khuliya" (a “team” or “connected link”). Japokuwa hakuna mahali idadi ya KIDON imewekwa wazi, lakini kuna "Khuliyot" kadhaa ndani ya KIDON, na kwa ujumla hukusanywa kwa kuitwa "The team."
KIDON wamejigawa katika vipengele mbalimbali (compartmentalised) kiasi kwamba hata ofisi zao hazipo ndani ya jengo la Mossad pale makutano ya Glilot. Kwa ugumu sana huwa wanaenda kwenye ofisi za Mossad, na hata kwa baadhi ya wafanyakazi wachache wa Mossad wanaofanya nao kazi, (KIDON) hutumia majina ya kufikirika ili wasijulikane.

Kwenye uwanja wa mapambano, KIDON hutumia jina la tatu (third name), na muda mwingine hata jina la nne ama utambulisho wa tano kabisa.Mafunzo yao uhusisha karibia kila kitu ambacho mtu anaweza kughani kichwani wakiamini kwamba vitu hivyo vinahitajika katika ndaki ya ujasusi. Lakini pia utazamaji yakinifu (close observation), kuukwepa utazamaji yakinifu (shaking off surveillance) na namna ya kuvisoma na kuvichambua vitu, watu, majengo na mwishowe kuzimeza hizo taarifa na kuzitunza kichwani (memorizing info).Ni wazuri mno kwenye ukumbuzi wa vificho (codes) na namna zao za siri za kuwasiliana bila ya kuamsha tahamaki yoyote, mifano ya mawasiliano yao ni kama vile: jasusi kukuna pua yake ama kuvuta sikio, au njia yoyote ya kutumia viungo vyake kumpa taarifa mwenzake. Moja ya ujuzi wao ni kuwa "mpole" (as cool as a cucumber) katika hali yoyote na pasipo kushtushwa ama kukereshwa na uingiliwaji wowote usiotegemewa, maswali ama kukaribiwa.Kwenye riwaya ya mtu mkubwa sana kwenye swala la uhuru wa Israel, bwana Ben-David Gurion, mwanamke mmoja mhusika wa KIDON pamoja na mwanaume aliyemfunza, walitumwa kwenda kupenya kwenye kiwanda cha nchi ngeni ambacho kilikuwa kinatengeneza vijisehemu (parts) vya silaha za Iran. Wakiwa katika eneo la kazi, waliingiliwa na mwenzao, mwana KIDON, aliyekuwa anayehusika na nyanja ya ulinzi akiwataarifu kwamba kuna ugeni wa ghafla eneo hilo, ambao unaweza ukafanya kazi yao isitendeke, kisha baada ya hiyo taarifa, mlinzi huyo akatokomea.
Wahusika wale wawili wa KIDON waliokuwapo ndani (yule mwanamke na mwanaume) walikuwa wanafahamu fika wapi pa kuelekea kukutana na gari la kuwaondoa eneo hilo, na walifanya hivyo pasipo papara. Kila mtu alikuwa mtulivu kama barafu. Kwenye "unit" hii (KIDON), neno "kuogofya" halipo kabisa kwenye kamusi yao.
Wahusika wote wa KIDON ni maradufu kwenye ujuzi shirikishi na nguvu (manual skills) ambazo uhitajika wawapo kwenye uwanja wa mapambano, mathalan: kuchagua na kuvunja kufuli, kuchukua picha kwa siri, kupandikiza vifaa vya umeme mahali mbalimbali. Pia hujifunza kuongoza vyombo mbalimbali vya moto, sio tu magari bali pia pikipiki, ambayo ndiyo njia ya usafiri inayopendwa sana na KIDON, kwani huacha viashiria vichache nyuma, na pia unyumbulikaji (flexibility) wa chombo hicho ni faida kubwa kwao.
Wahusika wa KIDON mara kwa mara hufanya mazoezi ya kutumia silaha mbalimbali zilizopo ulimwenguni, kuanzia silaha baridi kama vile kisu mpaka kwenye silaha moto kama vile bunduki.(KIDON) Ni wazuri sana kwenye kufyatua risasi, haswa zikiwa zimeminywa na kiwamba cha kumezea sauti, aidha wawe wamesimama, wakikimbia, wakiendesha gari ama wakiendesha pikipiki. Wanajua namna ya kutengeneza, kupandikiza na hata kutegua mabomu yakiwemo hata yale yaliyosadifiwa kisasa.Wanajua namna ya kucheza na kisu mkononi kama silaha pekee, pia kumkita adui na sindano za sumu ama kuweka sumu katika njia yoyote ile inayofaa kuwasilishwa kwa adui.
Kwa nyongeza, wahusika wa KIDON wamekubuhu kwenye mafunzo ya sanaa ya mapigano (martial arts). Mhusika yeyote wa KIDON uhesabu mikono na miguu yake kama silaha ya kwanza. Wanajua namna ya kuvitumikisha watakavyo ili kuleta majibu watakayo.Kwasababu hawa watu wamekamilika kwenye kila idara, na wao ndio uhesabiwa kama majasusi wa juu kabisa (supreme intelligence), ndio ambao kiongozi wa Mossad huwateua kwa ajili ya kazi za hatari sana — ikiwemo ukusanyaji wa taarifa nyeti sana — ambazo kufanikisha unahitaji wataalamu wa juu (top professionals).Kwa miaka, simulizi za KIDON zimekuwa zikienezwa na hata kuhusishwa na oparesheni kadhaa, lakini ukweli ni kwamba tangu uundwaji wa Mossad kwenye miaka ya mwanzo ya 1950, KIDON wamehusika na oparesheni chache sana za mauaji, zisizozidi hamsini. Lakini kwasababu tayari umma umekuwa ukiwahusisha na mauaji kadha wa kadha na shirika za kijasusi za Israel hazijitokezi kukanusha, basi habari hizi huonekana za kweli. Na kwa namna moja ama nyingine, Israel hupenda watu wawe wanafikiria hivyo.Kweli, Israel imeua mamia ya watu wanaoonekana ni hatari kwao, katika historia yao kwa ujumla, lakini wengi wao hao wameuawa na vikosi vya jeshi, haswa wakiwa ndani ya sare, wakivuka mipaka ya nchi za maadui. Aidha huko Gaza, au kwenye uvamizi wa PLO huko Beirut.Mossad hawajawahi kukiri kuhusika na jaribio wala mauaji yoyote yale, tofauti na pale jeshi linapofanya. Utofauti mwingine wa jeshi na Mossad ni pale wawapo vitani (the deniability factor); wanajeshi wawapo kwenye misheni wanajua kuna watu wa kuwasaidia (back up) ambao wapo tayari pale wanapozidiwa.Lakini kwa upande wa Mossad hilo ni tofauti. Timu ndogo ya Mossad inapokuwa kwenye oparesheni hawana watu wa kuwasaidia. Wanajitegemea wao wenyewe tu, hamna watu wa kusema watakuja kuwakomboa pindi wanapokuwa wamezidiwa.
Kwa jasusi za ki- Israel, kumuua mlengwa wao (target) ni jambo la mwisho kabisa. Kabla ya kumuua, wanajaribu kumgeuza mtu huyo kuwa wakala ama mtumishi wao, kumuonya ama kumtisha kwa kiasi kikubwa (terrorize). Yote hayo yakishindikana basi mtu huyo humalizwa, huondolewa kwenye uwanja wa mapambano.Ukichambua mauaji lukuki ya Mossad katika vipindi tofauti tofauti utajikuta walengwa wao (targets) wamegawanyika katika makundi matatu: Mosi; waliowahi kuwa washiriki na viongozi wa utawala wa ki-Nazi, Pili; wanasayansi wanaofanya kazi kwenye nchi maadui, na tatu; viongozi wakubwa (senior operatives) na viongozi wa kawaida wa vikundi vya ugaidi.
Msako wa viongozi wa ki - Nazi haikuwahi kuwa kipaumbele cha mipango ya Mossad, na mauaji ya wahalifu hao wa ki-Nazi yalikoma mnamo mwaka 1965, February 23, kwa mauaji ya Herbert Cukurs, komando ambaye pia alihusika na mauaji ya wa Jews milioni sita.
Hizi ndizo zilikuwa kesi chache sana ambapo Mossad waliua kwasababu ya kulipiza kisasi (revenge as the motive).Kwa upande wa wanasayansi, wa kwanza kabisa, waliokuwa lengo (target) ya Mossad - na hili lilikuwa kabla ya kuzaliwa kwa KIDON - walikuwa ni wanasayansi wa kijerumani. Hawa hawakuwa viongozi wa ki- Nazi, lah!, lakini waliajiriwa na viongozi hao kutimiza malengo yao. Mbali na hawa pia wanasayansi wengine waliokumbana na balaa la Mossad walikuwa ni wale waliokuwa wanaingiza pesa kwa kuuza ujuzi na maarifa yao kwenye kusaidia ujenzi wa bomu la masafa marefu la Misri (Egyptian Missile) ambalo malengo yake ilikuwa ni kufika Tel Aviv, Israel.Hii projekti ilikuwa ni moto kwenye nusu ya kwanza ya miaka ya 1960.
Kuua hao wanasayansi wa Misri ilikuwa ni hatua moja tu ya kuangamiza mpango huo wa Misri, lakini si kwamba Israel waliishia hapo. Barua za vitisho zilitumwa kwa watu na hata mataifa mbalimbali kuonya usaidizi wowote kwa Misri. Na mwishowe kwasababu mbalimbali, mpango wa Misri ulikufa na kupotea.
Wanasayansi hao (walikuwa ni wajerumani), sio tu kwamba waliuawa. Zilitumika pia njia zingine kama vile kwa familia zao kufuatiliwa na hata pia kupewa presha ya kuwakanya waachane na wanachokifanya.Lakini mbali na yote hayo, sikio la kufa la Misri halikusikia dawa. Kwenye miaka ya 1980, walifufua tena mpango wao wa bomu la masafa ya mbali. Na kwa kutambua kwamba hawawezi kufanikiwa na mpango huo "nyumbani" basi wakaamua kushirikiana na Argentina ambao walikuwa wanaendelea vizuri sana na mipango yao ya mabomu ya masafa ya mbali (condor missile).
Israel alipata taarifa hiyo na kuvutika kuusoma mpango wote huo wa mabomu ya masafa marefu. Wataalamu toka kwenye jeshi la Israel, Aman, walifanikiwa kupata mwaliko kwenda Argentina na hata wakapata fursa ya kuuchambua mpango huo wa mabomu.Bahati kwa ujasusi wa Israel ni kwamba, walikuwa wana mahusiano ya kijeshi ya muda mrefu na mji wa Buenos Aires — mahusiano na viongozi wa kidikteta ambao walichochea ukosoaji mkubwa wa Israel, lakini pia mfano mzuri wa namna ya kuwa na mahusiano na aina hizo za uongozi zinavyoweza kupelekea matunda mazuri muda mwingine.Pasipo kukoma Mossad wakaanzisha mpango wao wa vitisho (terrorizing campaign) sasa KIDON wakifanya kazi yao huku na kule wakiwalenga wataalamu wa Ulaya ambao walikuwa wanasaidia mpango huo wa Condor.
Injinia mmojawapo wa kijerumani aliyekuwa anaishi jijini Monaco akiwa na ofisi zake karibu na Salzburg, Austria, alifuatwa taratibu na jasusi wa Mossad, akaombwa aachane kabisa na mpango wa Condor. Jasusi huyo wa Mossad hakuongea maneno mengi zaidi tu ya huo ujumbe. Injinia huyo wa kijerumani akachukulia hilo tisho kama futuhi, akaendelea na kazi yake.Haikupita siku nyingi, gari lake likalipuliwa kama onyo. Lilifanyika hilo kumuonyesha kwamba uhai wake waweza kuondolewa muda wowote. Lakini pasipo kukoma, injinia huyo akaendelea na kazi yake. Wiki chache mbele, ofisi yake karibu na Salzburg ikachomwa moto. Na huo ndio ukawa mwisho wa injinia huyo kujihusisha na mpango wa Condor.Mwishowe Argentina alichoka kupambana na presha ya Israel juu ya mpango wake wa Condor, na hata pia USA walitia msukumo sana juu ya mpango huo kukoma, na kweli ukaja kukoma na kuisha. Misri aliachwa mikono mitupu, na akavimba kudai arejeshewe "kitu" toka kwenye uwekezaji wake hapo Argentina. Akaamua kuuza mabaki ya vifaa vyake kwa Iraq chini ya dikteta Saddam Hussein.Dikteta huyu (Saddam) alikuwa amejishibisha madaraka, na akiwa mkorofi katika mambo yote anayoona yeye anaweza kutia ubabe. Alikuwa anaendesha utengenezwaji wa silaha za kikemikali, kibaiolojia na nyuklia vilevile. Kwenye mwanzo wa mwaka 1990, alitishia 'kuifyeka nusu ya Israel', maneno ambayo taasisi ya ulinzi wa Israel, Aman, uliyachambua kama kiashiria kikubwa cha lengo la Saddam kuitupia Israel mabomu na silaha za kikemikali vile vile.Tangu hapo mipango yote ya Iraq ikawa inachukuliwa kama tishio kubwa kwa Israel, na pengine uwepo wa taifa hilo la kiyahudi. Kwenye vipaumbele vya jasusi za Israel, Iraq ikawa namba moja sasa.Mossad waligundua mwanasayansi wa mambo ya nyuklia ambaye alikuwa Mmisri kitaifa, bwana Yehia Meshad, alikuwa ndiye mtu anayetoa mchango mkubwa kwenye ujenzi na ukakamavu wa mambo ya kisayansi ya adui yao, Iraq. Kwa mujibu wa taratibu zao, Mossad walianza kumshawishi mwanasayansi huyo kushirikiana na Israel.Alipokataa, KIDON wakatumwa kutafuta makazi yake. Msako ukajibu kuwa yupo kwenye hoteli moja huko Paris, Ufaransa. Mahali ambapo ni rahisi sana kupashambulia kuliko Baghdad. Meshad aliuawa chumbani mwake June, 1980. Polisi wa Ufaransa hawakukuta alama yoyote ile ya muuaji, mwishowe walihitimisha kwa kusema kazi ile ilifanywa na wataalamu wa hali ya juu.Pasipo kukoma, Iraq waliendelea na mpango wao wa nyuklia, na utawala wa Saddam ukawekeza sana katika namna ya kuuzindua na kurusha bomu mahali alipokuwa anapataka. Saddam alivutiwa sana na wazo la kiubunifu la "Super Gun" silaha maridhawa, ambalo lilikuwa limetoka kwa mwanasayansi mkanada bwana Gerald Bull, ambaye alikuwa anamtengenezea silaha mtu yeyote ambaye angempatia fedha za kutosha.Bwana huyu alimfanyia kazi Mwamerika, Mwafrika Kusini na wateja wengineo, na kisha akahamisha kazi yake bara la Ulaya.
Akiwa anafanya kazi yake, Israel walishawahi kumshawishi awafanyie kazi, akakubali. Lakini hakuwa na kipya, vyote alivyokuwa anatoa tayari Israel walikuwa navyo ikiwemo ndege za vita na mabomu ya masafa ya mbali. Kwahiyo mtu pekee ambaye alivutiwa na kandarasi za bwana Bull akawa ni Saddam Hussein pekee. Tena kwa malengo ya kuwatishia maadui zake. Hivyo Bull akaajiriwa na kuanza kufanya kazi ya Iraq huko jangwani. Na kazi yake yote majaribio ilikuwa ni kutazama kama bomu linaweza fika Israel.Bull alikuwa anafanya kazi akitokea nyumbani kwake katika mji wa Brussels, Ubelgiji. Makazi yake hayo alikodiwa na mchumba wake. Yeye (Bull) alikuwa anaishi ghorofa ya sita katika jengo hilo lililo ndani ya wilaya ya Uccle.Mossad, wakiwa na Yitzhak Shamir waliamua kummaliza bwana Bull wakihofia shughuli yake italeta madhara kwa Israel, hivyo alikuwa ni mtu hatari. Timu ya KIDON ilimfuatilia na kumsoma bwana Bull kwa muda kabla ya kummaliza. Walipata kujua hulka ya Bull, safari zake, na nyumbani kwake.Kabla ya muda mrefu, "wamorocco" watatu walikodisha chumba katika jengo hilo hilo analoishi Bull, ila upande wa kushoto. Funguo yao haikuweza kufungua upande wa kulia wa jengo hilo walilokuwa wanaishi, ambapo huko ndipo alipo bwana Bull. Lakini pande hizi mbili (kushoto na kulia) zilikuwa zinaunganishwa na karakana ya chini (underground garage). Hili lilikuwa jambo jema lakini bado haikuwa karibu sana na chumba cha Bull, ambacho ndiyo kilikuwa lengo.Siku moja mwezi wa tatu mnamo mwaka 1990, Bull alikuwa anatembea kuelekea kwenye makazi yake - na baada ya kutazama kuhakikisha mchumba wa Bull hakuwepo ndani, timu ya KIDON walifunika vinywa vya bunduki zao na viwamba vya sauti, kisha wakamngojea Bull nje ya mlango wake.(Bull) Akiwa anatembea kupanda juu, alimiminiwa risasi za kichwa, na kisha KIDON wakatokomea isijulikane wameenda wapi.Baadae mtoto wa kiume wa Bull alikuja kukiri kwa wapelelezi kwamba kulikuwa kuna watu wageni waliokuwa wanampigia simu babaye mara kadhaa na kumuonya dhidi ya kuwafanyia kazi utawala wa Iraq.

*** KARIBUNI TENA, TUENDELEE ***Miezi kumi baadae, Saddam Hussein alionyesha kwamba ahitaji mpango wa bunduki maridhawa (Super Gun) kwa ajili ya kuitwanga Israel. Wakati vita ya Gulf, vita iliyoanzishwa na mataifa shirikishi 34 yakiongozwa na USA dhidi ya Iraq baada ya kuivamia Kuwait, ikiwa inaruruma mwanzoni mwa mwaka 1991, Iraq aliinyeshea Israel mabomu 39 ya mbio kubwa (scud missile). Viongozi wa Israel walitaka kulipiza mapigo hayo kwanguvu, ila raisi wa Marekani, George H.W Bush, aliwawekea vikwazo kufanya hivyo.

Israel walijihisi kuvuliwa nguo. Waliamini kwa namna yoyote walitakiwa kulipiza - sio tu kwa ajili ya kuficha nyuso zao - bali kubakiza ile picha yao waliyokuwa tayari wameshaitengeneza kwamba: mtu yeyote anayediriki kutia kidole chake juu ya Israel basi ataadhibiwa.Mkuu wa majeshi ya usalama wa Israel, bwana Ehud Barak, aliunda mpango dhanifu na hatarishi wa kumuua kiongozi wa nchi ngeni. Lengo lilikuwa ni Saddam, na mpango ungehusisha wanajeshi wa Israel kuingia ndani ya Iraq. Barak alileta wazo lake hilo kwa waziri wa ulinzi bwana Moshe Arens. Wanaume wote hawa walikuwa wamekanganywa na katazo la USA. Arens aliupitisha mpango huo akimruhusu bwana Barak autekeleze.

Israel, isipokuwa kwa kesi moja tu, haijawahi kuzingatia kumuua kiongozi wa nchi. Hapa ni mbali na aliyekuwa raisi wa Misri, bwana Nasser. Kama sheria yao kubwa, viongozi wa Israel walishawahi kuhitimisha huko nyuma kwamba njia ya kuua viongozi wa nchi si pendekezi, inaweza ikabadili 'mchezo'. Mgogoro wa mashariki ya kati unaweza ukawa mkubwa zaidi (intesified) na njia hiyo yaweza kurejesha 'moto'.

Kwahiyo, viongozi wa nchi walikuwa nje kabisa ya mipango ya Israel hata kipindi kile uhasama na uadui ulipokuwa mkubwa na ugaidi vilevile.

Kukengeuka huku, kujaribu kumuua kiongozi mkubwa wa nchi (Saddam wa Iraq), kulipewa nguvu kwa kuvunjwa kwa miiko miwili: Mosi, mabomu yake yalijaribu kupiga mji wa Dimona, na pili; alikuwa amelenga kiasi kikubwa raia wa kawaida, huko Tel Aviv, ambapo ndio kibebezi (icon) kikuu cha Israel.

Lakini bado kulikuwa kuna msito ndani ya upande wa Israel. Waziri mkuu Yitzhak Rabin, ambaye alikaimu nafasi ya Shamir na sasa alikuwa anashikilia roho ya wizara ya usalama, alikuwa "shingo upande" na hii misheni ya kummaliza Saddam.

Waziri huyo mkuu alikuja kuungwa mkono na mkuu mpya wa Mossad, Shabtai Shavit, ambaye alimkaimu bwana Nahum Admoni mnamo mwaka 1989. Rabin na Shavit, kwa pamoja, walikubaliana kwamba ni ngumu sana kummaliza Saddam kwa kumtwanga karibu (short range hit). Pia walijua kuwa dikteta huyo wa Iraq huonekana kwenye hadhara kwa nadra sana na mara kadhaa humtuma mtu anayefanana naye (body double).

Rabin alimruhusu Barak kufanyia mazoezi mpango wake alioupanga lakini bila ya kumuahidi kwamba atamruhusu autekeleze huko Iraq.

Mpango huo ulipewa jina la "Bramble Bush" yani ukimaanisha kifasihi "kichaka cha miba." Ukiwa sasa umelowea kwenye kutafuta siku ambapo Saddam atakuwa kwenye hadhira nje ya milango (outdoors). Vikosi vya Mossad na Aman - ambao walitumia satelaiti ya Israel - walifanya kazi kwa bidii kudaka ratiba na harakati zote za Saddam.

Wakala (agents) wa Iraq waliokuwa vibaraka wa Israel walitoa taarifa kwamba Saddam atahudhuria kwenye sherehe ya ufunguzi wa daraja la mto Tigris. Basi "agents" wa kiisrael wakatafuta hotel ambayo, japokuwa ilikuwa mbali, ingewawezesha kutuma chuma cha bunduki kummaliza Saddam mara moja.

Makomando wachache wa Sayeret Matkal (rejea nyuma kuijua taasisi hii) walichaguliwa kuingia ndani ya Iraq kwa siri kwa kutumia helkopta, na wale agents walioko ndani ya Iraq wangewaendesha kuwapeleka kwenye ile hotel ya kufanyia kazi.

Siku ya tarehe 5/11/1992, mwaka mmoja na nusu tangu vita ya Gulf ikome, makomando waliochaguliwa walijikusanya kwenye uwanja wa mafunzo huko jangwa la Negev kwa ajili ya mazoezi. Kwenye jukwaa waliketi watu wazito kwenye ulinzi wa Israel ikiwemo; Barak, mkuu wa Aman: bwana Uri Saguy na maafisa wengiwengi wa kijasusi.

Katika njia ya kushangaza, ukizingatia mafanikio yao kwenye nyanja ya vita, mchanganyiko hatari kabisa ulitokea hapo kwenye makufunzi. Bomu lililotakiwa kutumika kwenye mafunzo, yaani lisilo madhara, kwa jina "mchanganyiko mkavu", kimakosa halikuwepo na lililotumika likawa ni kinyume, yaani "mchanganyiko mbichi". Kumbuka jambo hili halikuwa linajulikana. Hivyo basi mlipuko mkubwa ukatokea katikati ya kundi la wanajeshi wa Sayeret Matkal, likawaua watano!

Kisa hiki hatarishi kikakomesha mpango wa siri wa Israel uliopewa jina la "kichaka cha miba". Taarifa zilianza kuvuja huko nje kuhusu ajali hii japokuwa hili jambo lilifanya siri mno. Magazeti yasiyo ya Israel yaliandika kwamba makomando wa ki Israel wamekufa wakiwa wanapanga kumuua Hassan Nasrallah, mwanasiasa aliyewahi kushika nyadhfa za juu kabisa nchini Lebanon chini ya chama cha Hezbollah.

Miezi michache baadae ndipo ikaja kugundulika kwamba kumbe lengo lilikuwa ni kuuawa kwa Saddam na si mwinginewe. Kumbuka waziri mkuu, bwana Rabin, hakuwahi kuupitisha mpango huu. Na hata wazo lenyewe la kummaliza Saddam likawa limekoma rasmi. Israel, tangu hapo, haijawahi kupanga kumuua kiongozi yeyote wa kitaifa - hata raisi wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, ambaye mbele ya hadhira alishawahi kukiri kwamba ataifutilia mbali Israel.

Sasa jasusi za ki Israel zikahamishia macho na nguvu zake kwenye mpango wao mrefu (long term plan) wa kuwatafuta na kuwamaliza wapalestina waliokuwa wanawaletea vurugu. Huo ulikuwa ni mpango baada ya mauaji ya wa Israel huko kwenye michezo ya Olimpiki jijini Munich, Ujerumani, mnamo mwaka 1972.

Wakati kikosi cha Sayeret Matkal kinafanikiwa kukomesha utekaji nyara wa ndege ya kifaransa iliyokuwa inaelekea Entebbe, Uganda, Mossad wao hawakupumzika mpaka pale walipohakikisha wanajua nani aliyeunda kikundi hicho cha watekaji nyara, ambao kitaifa walikuwa ni waarabu na wajerumani.

Jibu lilikuja kupatikana ni WadiaHaddad, kiongozi wa kikundi kidogo maarufu cha ukombozi huko Palestina. Haddad alikuwa amepanga mashambulizi mengi juu ya Israel na Israel walikuwa wamepanga kumfutia mbali kama lengo lao la kwanza.

Caesarea, kitengo kazi cha Mossad, kilihangaika kutafuta namna ya kumtia Haddad kimyani. Mwanaume huyo alikuwa amejiwezeka huko Baghdad na ilionekana husafiri kati ya Yemen na Iraq tu. Mwisho mwa mwaka1977, Mossad walimwajirisha mtumishi wa kuaminika wa Haddad apate kuwafanyia kazi.

Huyu "mtumishi" ndiye alikuwa mwanaume aliyebebelea chokoleti za sumu na kumpatia Haddad. Kiongozi huyu wa kikundi cha ugaidi akaenda na maji!

Kwa muda Mossad wakawa wanafuatilia kikundi hiki, ambacho kilijiengua toka kwa PLO ya "mnyama" mwingine Yasser Arafat, kama kitaendela kuwapo baada ya Haddad kufariki.

Kwa maono ya Mossad, kikundi kilikuwa tayari kimeshakufa. Utekaji nyara wa ndege ukawa ni "ujinga" wa kale.Katika macho ya ujasusi wa ki Israel, ni faida kubwa kuua "kichwa cha nyoka" pale kikundi kinapokuwa kinaendesha haswa na mtu mmoja kwani kummaliza yeye kunakuwa ni kumaliza kikundi kizima.Hili somo Israel aliliweka tena kwenye matendo, muda huu huko French Riviera ama Côte d'Azur. Mwezi wa saba mnamo mwaka 1979, wauaji wa KIDON walingoja nje ya nyumba ya Zuheir Mohsen, inayopakanana na Casino, wakiwa wamebebelea bunduki zenye viwamba vya kumezea sauti.Lengo lao lilikuwa ni kiongozi wa ki Syria aliyekuwa anadhamini kundi la kipalestima ambalo mnamo mwaka 1975 lilituma magaidi kwenye fukwe za Tel Aviv. Magaidi hao walipambana kwa kurushiana risasi na wanajeshi wa Sayaret Matkal, walishikilia watu kumi na moja mateka, na wapalestina saba waliuawa.

Kwahiyo Mohsen ilibidi auawe, kwasababu uhai wake unamaanisha kuendesha vikundi zaidi vya kigaidi dhidi ya Israel.Kama ilivyokuwa kwa Haddad, Mohsen aliuawa ila yeye kwa kupigwa risasi ya kichwa. Akazikwa pamoja na kikundi chake. Hakikusikika tena!Shukrani ziende kwa wauaji.
Tutaendelea ...
 
Kafka Bruno

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
302
500
Mkuu naomba nijuze kwann Israel imewaachia Iran wajenge kituo cha nyuklia wakati mataifa mengine kma Syria na Iraqi walivilipua vituo vyao au walijaribu na kushindwa?
 
kawombe

JF-Expert Member
Mar 26, 2015
4,092
2,000
Kumekuwa na haja na kiu kubwa ya baadhi ya watu humu kutaka kuifahamu MOSSAD na kazi zake. Kwa msukumo wa hilo, nimeona si mbaya tukajuzana angalau machache juu ya hawa watu na baadhi ya mifano hai ya kazi zao.

Jiandae kwenye karatasi zijazo kujifunza namna gani tumishi za Israel, zikiongozwa na Mossad, zinavyopambana, usiku na mchana, kulinda nchi yao, na pia kwa ziada nchi za magharibi vilevile.Kwa muono wa Israel, hawana la kupoteza kwenye vita yoyote ile. Hawana chaguzi nyingi zaidi ya kushinda kila muda. Lolote litafanyika kuhakikisha hilo. Na nadhani mimi na wewe twaweza kuwa mashahidi kwenye hili. (Rejelea vita kubwa ya mataifa kadhaa ilivyomalizwa na taifa la Israel ndani ya siku sita tu, watu wakaomba poh!)Siku za migogoro zaja. Iran anaweza jaribu kufanya kitu fulani kwa mujibu wa nguvu yake kinyuklia; magaidi pia waweza jaribu kufanya jambo hatarishi, au vyote kwa pamoja vikatukia. Raisi wa Marekani, kwa uhakika kabisa, atauliza;
"Kipi Israeli wanasema juu ya hili? Kipi wanajua? Ni nini wanachodhamiria kufanya ambacho sisi hatukifahamu?"
Na mwishowe;
"Nini Mossad watafanya? (Kupanga, kutekeleza, ama vyote)."
Marekani ni taifa kubwa, sina haja ya kuelezea kwenye hili. Kijografia huwezi ukailinganisha na Israeli hata kidogo, nchi ambayo itakulazimu uwe na microscope ili upate kuiona kwenye ramani ya dunia.Kitendo cha nchi kubwa kama Marekani, kijografia na kiuchumi, kuiulizia Israeli, ni jambo la kufikirisha kichwa. Lakini pia la kutufumbua macho kwamba kuna kitu ndani ya Israel; Kuna kitu cha kurejelea Israel; Kuna kitu cha kukitazama ndani ya Israel; kuna kitu cha kuhofia ndani ya Israel.
Na si kingine, hata kama kuna kingine basi kinazungukia hapa, kwenye taasisi nyeti ya kijasusi ya Mossad. Taasisi ambayo kwa mujibu wangu naweza sema ndiyo taasisi bora zaidi ya kijasusi kuwahi tokea duniani, hapa hatuhitaji kubishana.Kama vile sanamu la uhuru (statue of liberty) pale Marekani ama McDonald zilivyokuwa majina ya uwakilishi wa nchi hiyo kubwa, basi Mossad imekuwa ikitambuliwa kama "brand name" ya taifa la Israel. Hakuna Israel bila Mossad.
Shirika hili la kijasusi limekuwa kiungo kikubwa sana, japo kwa maficho, kwenye mambo mengi yanayotukia kwenye muda wetu, haswa mashariki ya kati.Lakini tusisite kujiuliza, Hivi Mossad ni wazuri kiasi hiki, cha kusemwa, kuogopwa, na kuongelewa?
Ndani ya zaidi ya miaka sitini, shirika hili la kijasusi la Israel limefanya pia makosa. Kufanikiwa ama kushindwa kwake kulitokana na ubora na ufanisi wa watu wake kazini. Wanapewa motisha. Lakini haibadilishi dhana kwamba na wao ni binadamu, hivyo hukosea ama kushindwa.Jina kamili la shirika hili la kijasusi ni HaMossad l’Modi’in u’l’Tafkidim Meyuchadim, kiebrania kinachomaanisha shirika la ujasusi na kazi maalum. Shirika hili lina wafanyakazi elfu ndogo, na katika muda mfupi hapo nyuma lilijipambanua kiasi kidogo kwa hadhira kwa kutumia tovuti ya Mossad.gov.il likienenda na motto rasmi usemao;
"Pale ambapo hamna shauri (counsel), watu huanguka; lakini penye wingi wa washauri (counselors) pana usalama."
Motto huu ulitoholewa toka kwenye biblia, Methali 11:14. Mstari huo ukisema;
"Pasipo na ulinzi (guidance), taifa huanguka; ila penye washauri wengi pana usalama."Lakini basi, je pana shaka lolote kuhusu motto huo? Aidha twaweza sema kwamba kwakuwa umetoholewa kwenye Biblia, basi dhamira yaweza kuwa njema, safi na yenye utukufu. Ila Mossad je, walidhamiria vivyo?
Neno "counsel" kwa lugha ya kiebrania hutafsiriwa kwa neno "takhbulot." Neno hili halina maana moja (ambigious word). Humaanisha maana kadhaa kama zifuatazo; ulaghai (deception), ujanja ujanja (trickery), mbinu (stratagem), au mwelekeo wenye hekima (wise direction). Hivyo basi kutokana na maana hizi tunashindwa haswa kujua dhamira halisi ya Mossad ndani ya motto huo. Kwani yaweza pia maanisha:

"Bila ya ujanja ujanja, Israel itaanguka ..."

Ama,

"Bila ya mbinu, Israel itaanguka ... "

Au,

"Bila ya ulaghai, Israel itaanguka ... "

Nani anajua?

Aliyewahi kuwa kiongozi (director) wa Mossad, bwana Efraim Halevy aliwahi kusema kwamba motto mwingine wa Mossad ungeweza kuwa;

"Kila kitu kinawezekana (kufanyika)." "Everything is do-able." Msukumo huu ndio ambao umekuwa ukiwasukuma Mossad, wakiamini kila kitu kinawezekana. Udogo wa nchi yao hauwazuii kwa njia yoyote ile wala kuwafanya wadhaifu.
Mbele ya macho yao (Mossad) kila kitu chao kina faida; kuanzia udogo wa nchi yao, upungufu wa wafanyakazi wao n.kHeshima ya shirika hili la kijasusi kwenye kufanya maamuzi ya tija, na kufanya shughuli zilizozidi hata ufanisi, imepelekea mambo makubwa kujiri; wana nguvu, wanajua karibia kila mambo, katili na wanaweza kupenya kona yoyote ya ulimwengu.
Israel wanaweza wakawa wamelitengeneza hili pasipo kujua, ila mpaka sasa wananufaika nalo. Pale ambapo jambo kubwa limetokea. Vyombo vya habari vikiwa vinabweka huku na huko wakitaja jina la Mossad, wakilituhumu ama kulipongeza. Hawa majasusi (Mossad) hawatii hata haladari ya neno. Hali hii ikajenga hofu ndani ya mioyo ya maadui zao, kwani hata pale Mossad wanapokuwa hawajahusika, bado hawabakizwi kutotajwa.Lakini wahenga na washenga walishawahi sema; "avumaye baharini papa lakini si kwamba wengine hawamo."Unapoongelea ujasusi wa dunia nzima, au haswa wa Israel, jina la kwanza kuja ni Mossad. Ila hawa hawafanyi kazi peke yao, na hata kwenye mafanikio hayo kuna mchango pia wa shirika lingine pacha "Domestic Shin Bet" ama kwa jina lingine hujulikana kama Shabak. Shirika hili uhusika sana na ulinzi wa ndani (internal/domestic affairs) ya taifa la Israel. Lakini pia juu ya hizi shirika, kuna 'mama' aendaye kwa jina la "Military - Aman", ama kwa kifupi; Aman.
Miongoni mwa hizi ogani tatu, zenye kuhusiana, Military Aman ndiyo yenye rasilimali kubwa kifedha na hata kinguvu kazi na ndiyo ambayo imechangia usalama wa Israel kwa kiasi kikubwa sana.Lakini pia mbali na hapo, katika mwendelezo wetu huuhuu tutapata nafasi ya kufunua vijisehemu vidogovidogo vya ulinzi wa siri (clandestine defense) wa nchi ya Israel, mbali na Mossad. Aidha utakuwa hauvifahamu vijishirika hivi, au basi kama wavifahamu basi si kiundani. Moja; ni ile inayoitwa ujasusi wa kiyahudi "Jewish Intelligence", ambayo hii husaidia wayahudi kuendesha ama kusimamia haki ya kisheria ya Israel kurejea kwenye ardhi wanayoamini wao kuwa ni ya mababu zao (ancients), ambapo huko hupewa uraia - lakini pia huendelea kuwalinda dhidi ya matamko, miongozo na nguvu za mataifa ama oganaizesheni kubwa za kimataifa kuligusa ama kutishia uwepo wa taifa hilo.Kijishirika kingine kidogo kilikuwapo kwa minajili rasmi ya ushirikiano wa karibu sana wa kisayansi "science liaison", ambacho husemekana kilifutwa baada ya jasusi; Jonathan Pollard kukamatwa akiwa anaipeleleza Marekani mwaka 1985. Kijishirika hiki kilifanikiwa sana kitunza siri za nguvu ya kisayansi ya Israel ikiwamo nyuklia, na taarifa zingine za kisayansi ambazo mpaka sasa hatuzijui, na ambazo mpaka sasa hazijathibitishwa na serikali ya Israel.
MEZA MATE ... HAYA, TUANZE TARATIBU...
Taifa la Israel limekuwa vitani tokea kipindi David Ben-Gurion alipotangaza utaifa wa jamii hiyo mnamo mwaka 1948. Na viongozi wa Israeli bado wanajichukulia wapo vitani kila siku. Lakini 'vita' hii siyo ile ya utaifa (1948), wala ile ya siku sita za mapambano (1967). La hasha! Jumuia zao za kijasusi zinataka kuhakikisha kwamba haitokuja kujirudia yale ya vita ya Yom Kippur, ama vita ya Ramadan (1973), ambapo shambulizi la ghafla la waarabu (Egypt na Syria), kama lipizo la vita ya siku sita (six days war), lililoigharimu nchi ya Israel, lingeweza kuzuiwa endapo kama majasusi waliopandikizwa nchini Misri wangepata kutiliwa maanani.
Kama ilivyo kazi ya taasisi ama shirika lolote la kiusalama, kazi yao ya kwanza si kupambana vita, bali ni kuzuia vita ama basi kuimaliza vita kabla ya 'kupambana vita'.

Kumuacha adui aanze kurusha kombora ni hatari sana kwani huwezi jua hilo kombora lina uwezo gani, laweza kukusambaratisha ama kukupoteza kabisa kwenye uso wa dunia. Na hapa Mossad ndio wanahangaika usiku na mchana kuhakikisha adui haanzi, bali anaanzwa na kumalizwa ikilazimika. Lengo ni ushindi tu, kuharibu ama kuchelewesha mipango ya adui bila ya kuhatarisha usalama wa wanajeshi lukuki na rasilimali ama wananchi wa Israel.HARAKATI KAZI ZA MOSSAD; MISHENI YA KWANZA. MPELELEZI NYUMA YA KINYAGO CHA CHUMA.Makazi ya watu wenye uwezo nje ya kitongoji cha Afeka kaskazini mwa Tel Aviv, yalikuwa yanatumika kumtazamia mwanaume ajulikanaye kwa jina la Rafael “Rafi” Eitan. Mwanaume mzee, mwenye uono hafifu na pia kiziwi wa sikio lake moja la kulia tangu apambane katika vita ya uhuru wa Israel.
Muonekano wake wa kimavazi ambao haupendezi machoni, huwafanya majirani zake kuamini kwamba ni mojawapo ya njia ya mwanaume huyo kuyakwepa, kiakili, yale mambo ya kikatili aliyowahi kuyafanya. Majirani hawa wanajua wazi bwana Rafi aliua watu kadhaa kwa ajili ya nchi yake (Israel), lakini si kwenye uwanja wa wazi wa vita (open battle) bali kwenye uwanja wa siri (secret battle) ambao ndio uwanja pendwa kwa Israel, uwanja wenye vita isiyokoma dhidi ya maadui zake.
Hakuna jirani anayejua haswa idadi ya watu waliouawa na Rafi, aidha kwa silaha ama kwa mkono wake wenye nguvu. Yale yote aliyokuwa anasema bwana huyo (Rafi) kwa majirani zake ni kwamba;
"Punde nilipotaka kuua, nilitaka kuyaona macho yao, uweupe wa macho yao. Basi nilikuwa mtulivu sana na mwenye mwongozo, nikifikiria kile tu ninachotakiwa kufanya. Alafu nikafanya. Hivyo ndivyo ilivyokuwa."Maneno hayo alikuwa akiyaambatanisha na tabasamu, tabasamu ambalo unaweza ukalifananisha na la mtu mwenye nguvu aliyedhamiria kumtisha mdhaifu.Kwa karibu robo karne, Rafi amekuwa naibu kiongozi wa harakati za Mossad. Sio kwa kukaa nyuma ya meza akisoma ripoti na kutuma wemgine kufanya kazi. Kwa kila fursa iliyotokea, alienda kwenye uwanja wa mapambano, alikuwa mbele akiwa anaongozwa na falsafa aliyofanikiwa kuifupisha ndani ya sentensi moja isemayo; "Kama wewe si sehemu ya jibu, basi ni sehemu ya tatizo."
“If you are not part of the answer, then you are part of the problem.”
Hakukuwahi kuwapo kama yeye (Rafi) kwa ukatili usio na huruma hata punje (cold-blooded ruthlessness), mipango ya ulaghai na ushawishi, na uwezo wa haraka mno wa kuandaa jambo ghafla. Ujuzi wa kupanga, na kutochoka kwenye ufwatiliaji wa mlengwa wake. Sifa zote hizo zilikuja kwake kwenye oparasheni moja tu iliyompa umaarufu mkubwa usiokoma kwenye nyanja ya ujasusi. Oparasheni hiyo si nyingine bali ni ile ya kumteka kiongozi mkubwa wa utawala wa ki- Nazi, Adolf Eichmann, ambaye ni mojawapo wa wahusika wa maamuzi ya mwisho yaliyotolewa na Adolf Hitler ya kuwaua Jews (6 million).Kwa majirani zake (Rafi) kwenye mtaa wa Shay, Rafi ni mfano mtakatifu, mwanaume aliyelipiza kisasi cha ndugu zao waliokufa, mwanaume mpiganaji aliyepewa fursa ya kuukumbusha ulimwengu kwamba hakuna kiongozi yeyote wa Nazi aliye salama baada ya kuwaangamiza watu milioni sita.
Hawachoki (majirani) kutembelea nyumba ya Rafi na kumsikiliza tena na tena akielezea oparasheni ambayo bado inatikisa kwa uthubutu wake.Akiwa amezungukwa na vitu vya thamani, Rafi angefungua mikono yake yenye misuli na kukaa kimya kwa muda, akiwaruhusu wasikilizaji wake wazame fikirani kipindi kile taifa la Israel linazaliwa. Alafu kwa sauti yenye nguvu, pasipo kuacha kitu, alianza kuwaambia majirani zake hao namna gani alipanga kumkamata Adolf Eichmann.
Kwanza, alitengeneza mazingira mazuri mno ya kuelezea simulizi yoyote ya utekaji nyara kwa muda wowote.Baada ya vita vya pili vya dunia, zoezi la kuwafuatilia wahusika wa mauaji ya Jews lilianza kufanywa na wale walionusurika na mauaji hayo. Walijiita "Nokmin" wakimaanisha walipiza kisasi. Hawakujisumbua kufuata mfumo wowote wa kisheria, wao walikuwa wanamnyonga mhusika yeyote wa Nazi waliyemtia mikononi.Rafi Eitan hajui wala hakumbuki kama kuna mahali popote walipowahi kumuua mtu asiyestahili kufa.
Lakini liwekwe rasmi kwamba, ndani ya Israel kulikuwa kuna haja hafifu sana ya kuwatafuta wahusika wa mauaji ya watu wao. Lilikuwa ni jambo la kipaumbele. Kama taifa, Israel walikuwa bado wachanga, tena wakizungukwa na mataifa adui ya kiarabu. Walikuwa na mambo mengi kwanza ya kuyazingatia kabla ya hilo, ila si kwamba walikuwa wamelipuuza. La hasha! Taifa la Israel lilikuwa mlemavu, lisilo na nguvu, na kama vile linapotea baada ya siku moja mbele.Ndani ya mwaka 1957, Mossad walipokea taarifa za kusisimua kwamba Adolf Eichmann, ameonekana nchini Argentina. Rafi, ambaye alikuwa ni nyota inayong'aa kutokana na ufanisi wa kazi zake dhidi ya waarabu, aliteuliwa kwenda kumkamata Eichmann na kumleta Israel kwa ajili ya kupewa anachostahili.Rafi aliambiwa oparasheni hiyo itakuwa na faida lukuki endapo ikitimia. Itakuwa ni hatua moja takatifu kwa watu wake kueleka kutendewa haki dhidi ya kile walichofanyiwa na wa -Nazi. Itaikumbusha ulimwengu wa kambi za vifo (death camps) na uhitaji wa kuhakikisha jambo kama lile haliji kutokea tena duniani. Lakini mwisho ni kwamba itaifanya Mossad kuwa mbele ya shirika zote za kijasusi ulimwenguni.Hakuna tumishi yoyote ya kijasusi ambayo ingethubutu kufanya oparasheni kama hiyo. Hatari yake ilikuwa ni kubwa mno. Rafi atafanya kazi maelfu ya maili toka nyumbani, atatumia dokumenti za kufoji, na kutegemea kwa kiasi kikubwa rasilimali zake mwenyewe kwenye mazingira adui. Argentina ilikuwa ni mahala salama kabisa kwa wa - Nazi, hivyo wana - Mossad wangeweza kukamatwa, kufungwa na mwishowe hata kuuawa punde tu wakigundulikana.Kwa miaka mirefu miwili, Rafi Eitani kwa uvumilivu alingojea wakati kuonekana kwa mara ya kwanza kwa Adolf Eichmann kunathibitishwa kwamba mwanaume huyo alikuwa yupo katikati ya kitongoji cha watu wa daraja la kati Buenos Aires akitumia jina la Ricardo Klement.
Pale amri ya mwisho ya kufanya tukio ilipotoka (go order), Rafi alikuwa 'barafu.' Alishafanya mafikirio yake yote juu ya nini kinaweza kikaenda kombo. Kisiasa, kidiplomasia, na kwake pia bila kusahau madhara yatakayofuata baadae.Alijiuliza nini kitatukia akimkamata Eichmann na polisi wa Argentina wakaingilia ama kumzuia?
"Niliamua nitamnyonga kwa mikono yangu mpaka afe. Kama nikikamatwa, nitasema mahakamani kwamba nimefuata maneno ya biblia; jino kwa jino." Alisema Rafi.El Al, shirika la ndege la taifa, ambalo ndege yake (hii iliyotumika) ilitoka kwenye shirika la kutengenezea ndege la Uingereza huku pesa ikitoka mfukoni mwa Mossad, ndilo lilimsafirisha Rafi kwenda Argentina. Rafi alisema;
"Tulimtuma mtu Uingereza akanunue moja. Alitoa pesa tukapewa ndege."
Lakini rasmi ndege hiyo iliyoelekea Argentina ilikuwa ni kwa ajili ya kubebelea maafisa wa ki Israel waliolenga kuwasili kwenye sherehe ya maadhimisho ya uhuru wa Argentina (115th). Hakuna afisa hata mmoja aliyekuwa anajua kwanini walikuwa wanaongoza na wao (Rafi na wenzake), na wala hawakuwa wanajua kama ndani ya ndege hiyo kulikuwa kuna chumba mahususi cha kumuhifadhia Adolf Eichmann.Rafi na timu yake walifika Buenos Aires May mosi, 1960. Walichukua nyumba moja iliyokodiwa na mkubwa wao, ambaye alipewa kificho (code) cha kiebrania "Maoz". Na mahali hapo ndipo palikuwa mahususi kama eneo la kuendeshea oparesheni yao. Walitengeneza pia mahali pengine maalum kwa ajili ya kumtunzia Adolf Eichmann baada ya kumkamata. Nyumba zingine pia zilikuwepo lakini mahususi kwa ajili ya kukabiliana na presha ya msako inayoweza kutokea toka kwa polisi wa ki Argentina. Pia magari kadhaa yakaandaliwa kwa ajili ya kazi.
Kila kitu kikiwa sawa, Rafi alitulia na kuzingatia. Shaka lolote lingeweza kupelekea wao kushindwa, lilikuwa limekabiliwa na sasa msukumo mkubwa ukawa kwenye kungojea.
Kwa siku tatu, Rafi na timu yake walifanya upelelezi kumfatilia Adolf Eichmann, ambaye awali alikuwa akiendeshwa ndani ya gari refu Mercedes limousine. Sasa siku hiyo Adolf Eichmann alikuwa anasafiri kwa basi na alishuka kwenye kona ya mtaa wa Garibaldi.Usiku wa siku hiyo, May 10, 1960. Rafi alikuwa ndani ya gari akiwa na dereva mwenye mafunzo ya kutosha, pamoja pia na mmojawapo wa wanaume wenye uwezo wa kumtageti mtu wanayemtaka mtaani. Yeye (Rafi) alikuwa pembeni ya dereva tayari kusaidia lolote litakalotokea. Walipopata walichokuwa wanakihitaji waliondoka wakilenga kufanya oparesheni jioni ya kesho yake.
Kwenye majira ya saa mbili usiku May 11, gari lililobebelea timu ya Rafi liliwasili kwenye mtaa wa Garibaldi. Hakuna yeyote aliyekuwa na presha. Hakuna yeyote aliyeongea. Hakukuwa na kitu cha kuongea bali kutenda. Rafi alitazama saa yake ya mkononi, saa mbili na dakika tatu. Walisogeza gari mpaka eneo fulani pweke.Mabasi kadhaa yalikuja na kuondoka. Kwenye majira ya saa mbili na dakika tano, basi lingine likaja. Wakamuona Eichmann akishuka.
"Mtaa bado ulikuwa mtupu. Nyuma yangu nilimsikia mtaalamu wetu wa ukamataji (snatchman) akifungua mlango wa gari. Tuliendesha gari taratibu kumfuata Adolf Eichmann. Alikuwa anatembea haraka kama mtu anayewahi chakula cha usiku nyumbani. Nilimsikia mkamataji mtaalamu wetu akihema taratibu, namna alivyofundishwa mafunzoni." Alisema Rafi."Alikuwa ana sekunde kumi na mbili tu za kufanya tukio. Kutoka ndani ya gari, kukamata shingo ya Eichmann na kumvutia ndani ya gari kisha tuondoke upesi!"Gari lilisonga karibu na Eichmann, aligeuka nusu kumtazama mtaalamu wetu aliyekuwa anashuka toka kwenye gari, ambaye hakufika mbali kabla ya kudakwa na kamba ya kiatu iliyokuwa haijafungwa vizuri. Nusura imwangushe.Kwa huo muda Rafi alitamani ashuke akamalize kazi. Alitoka karibia nusu ya dunia mpaka kufika pale kwa ajili ya kumkamata mtu anayehusika na kifo cha watu milioni sita wa nchi yake, na sasa walikuwa wanaelekea kumpoteza kwa sababu ya kamba za viatu! Eichmann aliongeza mwendo, ni kama alishajua yupo kwenye mazingira hatarishi. Akianza kutupa miguu yake, Rafi aliruka toka kwenye gari."Nilimdaka shingo kwa nguvu ambayo kama ningeiongeza kidogo tu basi ningemuua. Macho yake yalitoka nje. Mtaalamu wetu alifungua mlango upesi, nikamrushia Eichmann viti vya nyuma, haraka mtaalamu naye akajitupia humo ndani na kuketi juu ya nusu ya mwili wa Eichmann. Tukio hilo lilidumu kwa sekunde tano tu!"
Toka kwenye siti ya mbele, Rafi alikuwa anasikia Eichmann akihangaika kuhema. Mtaalamu wao alikuwa amemdhibiti mwanaume huyo vema kiasi kwamba kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele, alizidi kuwa mpole zaidi. Ilifikia mahali akauliza nini ilikuwa maana ya kile anachofanyiwa.Hakuna aliyemjibu. Kwa ukimya walifika kwenye nyumba salama iliyoko umbali wa maili tatu toka eneo la tukio. Rafi alimtaka Eichmann avue nguo kisha akamkagua akitazama vipimo vya kifizikia vya mwanaume huyo kama kweli ndiye. Rafi hakushangazwa na hali ya kutokuta tattoo ya SS (Schutzstaffel) mwilini mwa mwanaume huyo kama ilivyokuwa kwa wa - Nazi wengine, ilikuwa imeondolewa. Lakini vipimo vingine vyote vilikuwa sawa kabisa. Walimfungia Eichmann kitandani kwa pingu. Kwa masaa kumi wakamwamcha mwanaume huyo gizani pasipo na sauti yoyote."Lengo lilikuwa ni kuchochea hisia za kukosa matumaini ndaniye. Mpaka asubuhi tayari Eichmann alikuwa yu mnyong'ofu kiakili. Nilimuuliza jina lake akanitajia la kihispania ... Nilisema hapana, hapana, hapana, jina lako la kijerumani, akataja jina alilotumia kukimbilia nalo huko Ujerumani, nikasema tena hapana! Nataka jina lako la ukweli, jina lako la SS. Alijinyoosha kitandani kisha akasema kwa nguvu akisikika 'Adolf Eichmann'. Sikumuuliza tena, sikuwa na hitaji hilo."Kwa siku saba zilizofuata, Eichmann alikuwa bado gizani. Alikula na kulala gizani. Hakuna yeyote aliyemuongelesha."Kumuweka kimya na gizani kilikuwa ni zaidi ya matakwa ya oparesheni. Hatukutaka kumwonyesha Eichmann namna tulivyokuwa na hofu kwani hilo lingempa matumaini. Na matumaini humfanya asiye na matumaini kuwa hatari. Nilihitaji ajisikie hana msaada wowote kama vile watu wangu walivyokuwa kabla ya kupelekwa kuteketezwa kwenye kempu za vifo." Anaeleza Rafi.
**Siku ya kumsafirisha Adolf Eichmann.**Kwanza Eichmann alivalishwa nguo za wafanyakazi wa ndege ya El Al, ambazo nguo hizo zililetwa na Rafi toka Israel. Alafu alinyeshwa chupa nzima ya Whiskey na kumwacha katika hali ya kulewa chakari.
Rafi na timu yake walivalia suti zao na kidogo wakanywa Whiskey. Walimvalisha Eichmann kofia ya shirika la ndege na kumweka kwenye viti vya nyuma.Rafi aliendesha gari mpaka kwenye kambi ya jeshi huko ambapo ndege ilikuwa inawangojea, injini tayari zikichemka. Katika geti la kambi hiyo ya jeshi, gari likasimamishwa na wanajeshi wa Argentina. Kwenye viti vya nyuma Eichmann alikuwa anakoroma.

"Gari lilikuwa linanuka kama kiwanda cha pombe. Tulijifanya kama Jews walioparamia na kushindwa kuendana na vinywaji vikali vya ki-Argentina. Wanajeshi wale walifurahishwa na hilo jambo, hawakumtazama Eichmann mara mbili." Anaeleza Rafi.Ikiwa ni saa sita kasoro tano siku ya tarehe 21, May 1960, ndege iliacha ardhi ya Argentina huku Adolf Eichmann akiendelea kukoroma, sasa akiwa katika chumba chake mahususi ndani ya ndege.Baada ya kusikikizwa kwa urefu kwa kesi yake (Adolf Eichmann), alikutwa ana makosa dhidi ya ubinadamu. Kwenye siku yake ya kunyongwa, May 31, 1962, Rafi alikuwa kwenye chumba cha unyongaji."Eichmann alinitazama na kusema 'muda wako unakuja, myahudi', nikamjibu, 'lakini sio leo, Adolf, sio leo.Shingo yake ilimezwa na kitanzi, Eichmann akatoa sauti ndogo sana ya kukabwa. Kisha kukawa kunasikika sauti ya mwili wake tu ukibembea. Sauti ya kuridhisha sana." Anasema Rafi.Jiko maalum liliandaliwa kwa ajili ya kuuchoma mwili wa Adolf Eichmann. Ndani ya masaa majivu yake yalimwagiwa baharini ndani ya eneo kubwa. Hakikutakiwa kibakie kiashiria chochote cha Adolf Eichmann juu ya uso wa dunia.
Baada ya hapo, jiko lililomchoma liliharibiwa na kutotumika tena. Jioni hiyo Rafi alisimama ufukweni na kutazama bahari, akijisikia amani kabisa."Kumaliza kazi yangu, hilo siku zote ni hisia nzuri."
Tutaendelea na visa vya MOSSAD moja baada ya moja ... karibu..
Iko muzuri sana
 
SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
5,613
2,000
Mkuu naomba nijuze kwann Israel imewaachia Iran wajenge kituo cha nyuklia wakati mataifa mengine kma Syria na Iraqi walivilipua vituo vyao au walijaribu na kushindwa?
Swala la Iran lina mitazamo kadha wa kadha. Kwa mujibu wa kiongozi wa Mossad, bwana Meir Dagan, kama ambavyo tayari nimeshainisha hapo awali, amesema kwao nyuklia ya Iran haipo kwenye kipaumbele chao. Na litakuwa swala la kijinga endapo tu wataiparamia Iran pasipo kuangaza na sababu zingine za kufanya hivyo.
"Litakuwa wazo la kijinga kuishambulia Iran kabla ya kuzingatia vitu vingine."Lakini pia kwenye miaka ya 2000, Israeli Chief of the General Staff Lieutenant General Gadi Eizenkot, naye alisema;
"Bila shaka jambo la Nyuklia kati ya Iran na magharibi ni jambo la kimageuzi kihistoria. Ni badiliko kubwa katika njia ya mwenendo ambao Iran inaelekea, na hivyo ndivyo nasi twaona vitu."
Lakini pia hakusita kusema;
"Kwenye miaka kumi na tano mbeleni, tunaiweka Iran kwenye vipaumbele vyetu vya juu kwasababu tunahitaji kujua na kuongoza Nyuklia yake. Hili ni jambo kubwa."
Kwahyo basi waweza ona kuna ushawishi wa magharibi ndaniye, lakini pia upembuzi wa Israel kwenye madhara ya jambo hilo unaweza ukawa hafifu.Upande wa pili wa shilingi, nabanwa kusema moja kwa moja juu ya uhusishwaji wa Mossad kwenye mauaji ya wanasayansi wa nyuklia wa taifa la Iran. Kwanini?Mostafa Ahmadi Roshan, naibu msimamizi wa mpango wa Uranium wa Iran huko Natanz, alikuwa kwenye gari kuelekea kazini alipolipuliwa na bomu la sumaku lililopandikizwa kwenye mlango wa gari lake kwa ustadi.Tangu mwaka 2010 mpaka sasa, wanasayansi watatu wa Iran wamekwishauawa katika mazingira yanayofanana akiwemo pia Darioush Rezaeinejad, mtaalamu wa umeme ambaye alipigwa risasi nje ya shule ya nursery alipompeleka mwanaye huko Tehran. Mpaka hapa unaweza kushawishika kwa namna moja Mossad ndio wametenda.Ila hapa sasa. Mojawapo wa wanasayansi waliouwawa ni Dr. Ardeshir Hosseinpour. Kifo chake kimeleta utata kwasababu kuna njia mbili ndaniye, wanaosema ameuawa na Mossad na wengine wanaosema ameuawa na serikali ya Iran, ikiwemo dada wa marehemu bi Mahboobeh.
Dada huyo anasema mnamo mwaka 2004, Dr Ardeshir alifuatwa na majasusi wa ki Iran (IRGC) kwa niaba ya kiongozi wa Iran muda huo bwana Ayatollah Ali Khamenei kwa malengo ya kuongea naye kuhusu mambo fulani juu ya uendelezwaji wa Uranium iijengayo nyuklia.
Kwa mujibu wa dada wa marehemu, kaka yake alikataa kufanya kazi kwenye mpango wa nyuklia wa Iran akiamini kwamba utadhuru uchumi wa nchi yao (Iran) na jumuiya za kimataifa. Kutokana na katazo hilo la Dr. Khamenei akaagiza mauaji yake january 2007.Kuungwa mkono kwa hili, kiongozi mmojawapo mkubwa katika usalama wa Israel (jina limen'toka) alisema kwamna wao hawajahusika na hili ila hawezi akatoa chozi juu ya vifo hivyo, kauli ambayo ilizizima kwa utata.
 
NYIRO

JF-Expert Member
Nov 12, 2014
248
250

Kudos mzee unachambua bila bias endelea kutushushia mavitu aisee
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom