ME NADHAN BASIC SALARY KWENYE SLIP YA MLETA MADA INASOMA 432,000.kwa hyo sio kosa lake,ila hajawah kuona salary slip nyingne zaid ya za watumish wenzie wa kada yake na ya huyo jamaa yake.
asante sana.
Unajua mnaweza kumlaumu mtu kumbe yeye hajawahi ona huo mshahara wa mamilion ya fedha, so mnachotakiwa ni kumuelimisha kuwa kuna walio zidi huo na wamo humu humu Tanzania, inawezekana yeye mshahara wake kwa mwezi ni 366,666/= kwa mwezi na hapo hajakatwa kodi, so akiona huo wa milion 1.35, anaona kama ni kumkufuru Mungu.Unajua humu Tanzania kuna wengine wanaishi kama peponi wengine wanajiuliza watapata wapi mlo mmoja kwa siku.
wakuu, hii mamlaka ya serikali inayoendeshwa kwa kodi za wavuja jasho ina unyeti sana kiasi cha watumishi wake kuenjoy pepo duniani? Cjajua Taasisi zingine kama TRA mishahara yao ikoje ila nimeijua mishahara ya SUMATRA hadi nimeshangaa. Huenda sijafahamu unyeti wa mamlaka hii ila wanaoijua watatueleza. Rafiki yangu amemaliza pale IFM akichukua Accouting, amepata ajira mwanzoni mwa mwaka huu katka mamlaka ya SUMATRA na kwa macho yangu amenionyesha Salary Slip yake daah, ni Milioni 1.53 kwa mwezi. Wakuu hii mishahara inapangwa na ofisi ya utumishi au wanajipangia wafanyakazi wenyewe wa Mamlaka?
hapo bold sasa umeanza matusi,
una uhakika gani kwamba mtoa mada ni mwanamke??
je wewe mama yako alikuwa baba?? na dada yako ni kaka??
mwanao wa kike ni mvulana na mkeo ni mume??
Wakuu, hii mamlaka ya serikali inayoendeshwa kwa kodi za wavuja jasho ina unyeti sana kiasi cha watumishi wake kuenjoy pepo duniani?
Cjajua Taasisi zingine kama TRA mishahara yao ikoje ila nimeijua mishahara ya SUMATRA hadi nimeshangaa. Huenda sijafahamu unyeti wa mamlaka hii ila wanaoijua watatueleza.
Rafiki yangu amemaliza pale IFM akichukua Accouting, amepata ajira mwanzoni mwa mwaka huu katka mamlaka ya SUMATRA na kwa macho yangu amenionyesha Salary Slip yake daah, ni Milioni 1.53 kwa mwezi.
Wakuu hii mishahara inapangwa na ofisi ya utumishi au wanajipangia wafanyakazi wenyewe wa Mamlaka?
ndugu yangu husishangae sana meli itakuacha......by the way wakala wengi wa serikali mishahara yao si haba kabisa. lakini pia kama unamuona huyo anafaidi basi kaangalie mishahara ya hawa jamaa TANROADS, TRA, BoT, TPA, EWURA, TBS, TANTRADE, hapo bado haujaenda PCCB etc.
1.53 ni mshahara wa kawaida sanaaa, na hapo am sure makato bado anaweza kuwa anaondoka na 900,000 na kitu.....TPA ukifikia ngazi ya umeneja tu kwenda juu ujue unakula above 9mil, sasa jiulize wakurugenzi watakua wanalamba ngapi...? kwahiyo huyo jamaa wa SUMATRA ujue anatakiwa alalamike mshahara mdogo
unashangaa muhasibu kulipwa hivyo,wakati kuna taasisi za serikali dereva tu analipwa 3.5.:heh:
Dereva wa benki kuu, lapf,