Mimi napata 6m kwa mwezi wewe unasema 1m?
ME NADHAN BASIC SALARY KWENYE SLIP YA MLETA MADA INASOMA 432,000.kwa hyo sio kosa lake,ila hajawah kuona salary slip nyingne zaid ya za watumish wenzie wa kada yake na ya huyo jamaa yake.
Mleta hoja atakuwa katika TGTS C1. Labda hoja ingekuwa muda wake wa utumishi na kias cha mshahara alichoanza nacho ukilinganisha na kada nyingine za UMMA utabaini kaanza na mshahara mkubwa kiukweli
Huo ni mshahara kwa wafanyakazi wawakuu, hii mamlaka ya serikali inayoendeshwa kwa kodi za wavuja jasho ina unyeti sana kiasi cha watumishi wake kuenjoy pepo duniani? Cjajua Taasisi zingine kama TRA mishahara yao ikoje ila nimeijua mishahara ya SUMATRA hadi nimeshangaa. Huenda sijafahamu unyeti wa mamlaka hii ila wanaoijua watatueleza. Rafiki yangu amemaliza pale IFM akichukua Accouting, amepata ajira mwanzoni mwa mwaka huu katka mamlaka ya SUMATRA na kwa macho yangu amenionyesha Salary Slip yake daah, ni Milioni 1.53 kwa mwezi. Wakuu hii mishahara inapangwa na ofisi ya utumishi au wanajipangia wafanyakazi wenyewe wa Mamlaka?
Anatakiwa aongezewewatu unamshambulia mtoa.mada ila point yake ni utofauti wa mIshahara baina ya watumishi wa umaa..wote elimu sawa ila Huyo wa Sumatra analipwa 1.53mil wakati mhasibu wa halimashauri ana TGS D 625,000 yaani hata nusu hajamfikia..hata kama tofauti ilitakiwa iwepo ila si kwa kiwango hicho..ikiwa wote wanalipwa kwa pesa ya Kodi.
hakuna aliekuuliza mshahara wako ni kiasi gani, na hiyo haituhusu. Soma uzi kwa umakini ujue lengo lake ni nini?
Naona wewe na wengi wa wachangiaji hapa mna tatizo la kukurupuka, kwa mtazamo wangu hapa jamaa anajaribu kuikosoa serikali kwa kupendelea baadhi ya taasisi kimaslahi. Inawezekana sumatra wanamaslahi mazuri zaidi ya taasisi alieko yeye, wakati wote wanaelimu sawa na mwajiri wao ni mmoja. Sidhani kama jamaa anashangaa hizo 1.53m au hata hizo chenji zako 6m.
Tujifunze kutokukurupuka tunapochangia, after all you have an ample time to think before start writing!!
Mbona mshahara mdogo sana huo.
Kuna watu nchi hii wanapokea milioni 40 kwa mwezi wameajiriwa.
Wewe angalau unaweza kuwa Great Thinker kati ya wengi waliojaribu kujitutumua huku na mishahara yao bila kujaribu kumwelewa mleta mada.
Wengi walivyo shalo na wameishia kusema Tshs 1.35M badala ya Tshs 1.53M aliyoitaja mleta mada.
Watu wanashindwa kusoma btn the line, mleta mada anasema anayepata amount hiyo ni fresh from school, na hiyo ni salary ya kuanzia, sasa mtu najiita great thinker analinganisha mshahara wake wa TZS 10m na wa novices. Hapo utakuwa great thinker kweli? Mtu anazungumzia mtumishi wa uma na si wa mashirika ya kimataifa. Kama wewe unafanya huko UN utajilinganishaje na mtumishi wa uma wa TZ anayeanza kazi? Mwenyewe ni mtumishi wa uma wa hayo mnayofikiria yanalipa sijui TANESCO, TRA, TPA na kwa taarifa tu wanaoanza kazi kwingine wanaishia kupata gross za hizo laki nane na tisa so acheni mleta mada alete hoja yake kwa SUMATRA kulipa TZS1.53 kwa anyeanza kazi.
Kwa kumuelimisha tu ni kuwa nijuavyo mimi na kama mambo hayajabadilika huko SUMMATRA, tofauti na agency na authority nyingina , SUMMATRA ajira zao ni za mikataba ya miaka 2-3 ambapo wengine ni permanent na pensionable. Hiyo yaweza kuwa moja ya sababu ya mshahara kuwa mkubwa relative to others.
Tuache kubeza watu na kutishiana na vimishahara vyenu na badala yake jibu hoja au kaa kimya
Nikupe tu tuisheni kidogo. Unaposema mshahara mkubwa lazima useme relative to wapi maana hata miashahara ya TRA umesema huijui. Leta comparison ambayo ipo relativbe na mamlaka zingine za serikali ndo utaeleweka zaidi. Mishahara ya mamlaka zote za serikali na taasisi za serikali kwa kawaida ndo huanzia range hizo. Mishahara yao ipo tofauti na Central Government. Mhasibu wa hazina anapokea mshahara mdogo zaidi ya mhasibu wa TRA. Kwa hiyo bado sijaona point ya post yako:biggrin1:wakuu, hii mamlaka ya serikali inayoendeshwa kwa kodi za wavuja jasho ina unyeti sana kiasi cha watumishi wake kuenjoy pepo duniani? Cjajua Taasisi zingine kama TRA mishahara yao ikoje ila nimeijua mishahara ya SUMATRA hadi nimeshangaa. Huenda sijafahamu unyeti wa mamlaka hii ila wanaoijua watatueleza. Rafiki yangu amemaliza pale IFM akichukua Accouting, amepata ajira mwanzoni mwa mwaka huu katka mamlaka ya SUMATRA na kwa macho yangu amenionyesha Salary Slip yake daah, ni Milioni 1.53 kwa mwezi. Wakuu hii mishahara inapangwa na ofisi ya utumishi au wanajipangia wafanyakazi wenyewe wa Mamlaka?