Unajua Wazungu wanaifahamu vizuri sana Afrika naweza sema kuliko waafrika tunavyoihamu Afrika. Wana kumbukumbu ya vitabu vinavyoelezea Afrika kwa kina miaka 300-400 iliyopita, lakini pia wamekuwa involved na plan zote za maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa Bara la Afrika hata baada ya kuondoka.
Wao wanachoamini ni kwamba viongozi wa kiafrika wanapatikana 'by chance". Lakini pia wanakuwa hawana uelewa wa kutosha wa changamoto kiasi gani walizonazo watu wao na nchi yao na hivyo kukosa dira ya maana ya kuziondoa. Mara nyingi wanawachukulia poa tu kwani wanajua wakiendelea kuishi kwa fikra za viongozi hao, watawaathiri wananchi zaidi. Kwahiyo hata huyu walimchukulia poa tu. Walijua akishajua ugumu wa urais na changamoto halisi za nchi yake ataanza kufikiri sawasawa.
Hakuna asiyejua usmart wa Nyerere au Mkapa. Lakini walikuwa makini sana katika kukosoa mataifa makubwa. Wengine tuliposikia yale, tukacheka tu kwani tukajua ni harakati pasipo mkakati.