gillard
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 227
- 165
Kwanza nianze kwa kusema, naunga mkono juhudi za Rais wetu kutaka Tanzania ijitegemee. Ni mtazamo wa watanzania wengi tu na hata vyama vya upinzani wameliongelea sana suala hili.
Misaada ambayo Rais wetu amepokea juzi toka kwa umoja wa ulaya imerudi kwa masharti yaleyale, The Citizen linaripoti. Kwa mujibu wa gazeti hilo licha ya msimamo wa Rais kuhusu misaada toka nje, ilikuwa vigumu kwa bajeti ya 2016/2017 kutekelezeka kama mchezo wa paka na panya ungeendelea.
Ukweli ni kwamba watu kutoka serikalini walikuwa wanafanya jitihada nyuma ya pazia kuokoa jahazi kwani ilikuwa bayana kwamba misimamo wa kisiasa wa Rais wetu ulikuwa haumsaidii yeyote.
Wakati Rais Magufuli akiendelea kutuaminisha wananchi masikini kwamba wahisani hawana tena nafasi ya kutupangia masharti, inaelezwa kuwa wawakilishi wa serikali walijadiliana mpango ambao kimsingi utamfanya mkuu wa nchi aendelee kuyaishi masharti yaleyale ambayo alijinasibu huko nyuma kuwa hatoyakubali asilani.
Naishauri serikali na Rais wetu, ukimya nao una busara zake katika kufanya maamuzi na kuweka mambo sawa, "tusitukane mamba kabla hatujavuka mto", tusipende kuongea sana kwa kufurahisha genge, “twende strategically” tutafika. Kwa madhara yaliyotukuta safari hii kwa bajeti yetu ya 16/17 kupumulia mashine hili liwe fundisho kwetu sote.
Ushauri kwa wasomi wetu, acheni kujipendekeza, mwambieni Mh. Rais ukweli, ongeeni ukweli kwa faida ya Taifa letu na vizazi vijavyo. Msiongee kumpendezesha Mh. Rais ili tu muonekane.
Mwisho, shukrani za pekee kwa bosi wa zamani wa Africa Development Bank Ndg. Donald Kaberuka kwa kuongoza mazungumzo yaliyofanikisha misaada tuliyoshuhudia ikirudi wakati Rais wetu alipokutana na Balozi wa Umoja wa ulaya.
Mungu ibariki Tanzania