Misaada ya EU imerudi kwa masharti yaleyale, japo....

Misaada ya EU imerudi kwa masharti yaleyale, japo....

Misaada kutoka nchi za Ulaya imerudi kwa gharama. Taarifa za ndani ni kwamba nchi za Ulaya zilikataa kabisa kutoa misaada kwa Tanzania. Tukalazimika kumtumia mtu wa kati, Rais Mstaafu wa Benki ya Afrika Donald Kaberuka, kutuunganisha na nchi za Ulaya.

Misaada inarudi kwa masharti ambayo tumeridhia:
1) Kuheshimu demokrasia, pamoja na kuruhusu vyama vya siasa vifanye kazi bila vipingamizi vya serikali
2) Utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar
3) Utawala wa sheria
4) Uhuru wa maoni
5) Uhuru wa vyombo vya habari
Mbona sioni masharti hapo!!!! Haya ndio masharti?
 
Nami niweke neno kidogo. Awam ya tano iliingia ikiwa focused na kujitegemea,ni jambo jema sana. Lakini kila jambo lina hatua.Matamko ya kisiasa yalikua ni mengi bila ya kufanyika utafiti. Kwa mfano trend yetu ya makusanyo yalifahamika kwa miez mitatu ya kwanza kuwa ni Tsh 1.12 hadi1.3+Tn/- kwa mwezi. Hii trend tayari kwa mtu makini angejua tu hatuna hela za kutosha kuendesha nchi kwa 100%.Hivyo ilitakiwa kuchunga maneno ya kuongea. Kwa maana hiyo makusanyo kwa mwaka unaona kabiasa isingeweza kufika Tsh 15.5tn/- kwa mwaka. Sasa unapopitisha bajeti ya 29tn/- huku uwezo wako wa kukusanya ni nusu tu ya bajeti yako,basi jua bado utalazimika kuwa mtumwa wa IMF,WB,ADB na misaada ya Nchi za Magharibi ambao wao kamwe hawawez kutoa misaada ukienda nje ya matakwa yao. Hili ni somo kubwa la kujifunza.
Ni kweli mkuu, nimependa hapo kwenye kuchunga maneno. Unajua kuna mambo mengine inatakiwa timing, ikiwemo silent approach.
Tukumbuke hawa watoa misaada wanatuspy sana. Hizi balozi zao zipo hapa zimekaa kimya lakini zinakusanya data sana na kuzitupia huko kwao.
 
Kweli kabisa mkuu,halafu nchi inawahitaji wawekezaji,serikali kila kukicha inawakoroga hata hawa wachache waliopo ambao wangekuwa mabalozi wetu wazuri.

Hawa vijana waliomaliza vyuo wakakosa ajira,na wale wengine ambao hawakufika vyuoni tusitarajie watakaa kimya muda wote,hao ni kama bomu tu lililotegwa kwa muda,sekunde na dakika zina hesabu tu
 
Ni kweli mkuu, nimependa hapo kwenye kuchunga maneno. Unajua kuna mambo mengine inatakiwa timing, ikiwemo silent approach.
Tukumbuke hawa watoa misaada wanatuspy sana. Hizi balozi zao zipo hapa zimekaa kimya lakini zinakusanya data sana na kuzitupia huko kwao.
Mkuu umesema kweli, balozi zao ni kama extension ya ofisi za mashirika yao ya kijasusi,wanakusanya data na kufanya analysis na kisha kuzituma kwa wakubwa wao,wanatujua nje ndani,
 
Mkuu umesema kweli, balozi zao ni kama extension ya ofisi za mashirika yao ya kijasusi,wanakusanya data na kufanya analysis na kisha kuzituma kwa wakubwa wao,wanatujua nje ndani,
Hilo la balozi kuwa ofisi za kijasusi mbona liko wazi. Hata mashirika yao ya misaada,kampuni zao pia zina maagent wa usalama.
Nakumbuka zamani kidogo kuna uzi ulianzishwa humu JF kuonyesha hata mabosi wa Symbion wengi ni Agents wa Usalama.
 
Unajua Wazungu wanaifahamu vizuri sana Afrika naweza sema kuliko waafrika tunavyoihamu Afrika. Wana kumbukumbu ya vitabu vinavyoelezea Afrika kwa kina miaka 300-400 iliyopita, lakini pia wamekuwa involved na plan zote za maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa Bara la Afrika hata baada ya kuondoka.

Wao wanachoamini ni kwamba viongozi wa kiafrika wanapatikana 'by chance". Lakini pia wanakuwa hawana uelewa wa kutosha wa changamoto kiasi gani walizonazo watu wao na nchi yao na hivyo kukosa dira ya maana ya kuziondoa. Mara nyingi wanawachukulia poa tu kwani wanajua wakiendelea kuishi kwa fikra za viongozi hao, watawaathiri wananchi zaidi. Kwahiyo hata huyu walimchukulia poa tu. Walijua akishajua ugumu wa urais na changamoto halisi za nchi yake ataanza kufikiri sawasawa.

Hakuna asiyejua usmart wa Nyerere au Mkapa. Lakini walikuwa makini sana katika kukosoa mataifa makubwa. Wengine tuliposikia yale, tukacheka tu kwani tukajua ni harakati pasipo mkakati.
"Hakuna asiyejua usmart wa nyerere au Mkapa,lakini walikuwa makini sana kukosoa mataifa makubwa....."
 
Hilo la balozi kuwa ofisi za kijasusi mbona liko wazi. Hata mashirika yao ya misaada,kampuni zao pia zina maagent wa usalama.
Nakumbuka zamani kidogo kuna uzi ulianzishwa humu JF kuonyesha hata mabosi wa Symbion wengi ni Agents wa Usalama.
Eti ndio mwakyembe alienda marekani kuulizia ofisi za Richmond(baadae symbion ) zilipo,hivi kweli wewe mbunge wa kyela,mbeya uruhusiwe kuwahoji maofisa wa kampuni ya CIA?
 
Tatizo anaongea sana.

Wawe wanamwandikia hotuba itasaidia sana
Siyo kwamba hotuba haandikiwi na wasaidizi wake, tatizo huyo Ngosha anajifanya 'kidume' na hataki kusoma hotuba hizo anazoandikiwa na wasaidizi wake na badala yake ndicho hiki ambacho huwa tunakishuhudia kwa Mkulu kutema 'pumba' kwenye hotuba zake anazotoa kichwani mwake!
 
Tangu wakati ule tulisema, si tu kwamba kwa sasa hatuna ubavu wa kukwepa misaada ya wahisani lakini pia up to the next five years hatutakuwa na uwezo wa kukusanya japo TZS 3 Trillion kwa mwezi!! Lakini pia tukapigilia msumari kwamba, hata kama tutaweza kukusanya TZS 3 Trilioni kwa mwezi, kutokana na changamoto luluki tulizonazo nchi hii bado hizo trilioni 3 zitakuwa ni sawa na tone la maji kwenye bahari na hivyo suala la kutokwepa misaada kubaki pale pale!!!
 
Wewe ndiye unastahili elimu,mpaka sasa unaona ni sawa Mnyarwanda kuzunguka dunia nzima kwa nauli ya watanzania eti akituombea msamaha kwa wafadhili

Makosa yenyewe ni ya kurekebisha tu sisi wenyewe,kuruhusu mikutano ya hadhara mpaka tushauriwe? Kuruhusu demokrasia mpaka tushauriwe?

Hivi vitu vilikuwepo tangu Nyerere akiwa hai, na yeye kama baba wa taifa aliona havina tatizo,sisi wa miaka hii tunajiona wajuaji,haya sasa,hospitali hazina dawa,na hata hizo hela za wafadhili haziji ghafla,ukitangaza sasa mikutano ya hadhara ruksaaaa,inakuja mia tano,bunge laivu,mia mbili,utaongea na maalim,inakuja milioni moja,unarekebisha sheria ya mitandao,wanakupa milioni mbili, ni piece by piece,hela inatolewa kwa action plan iliyowekwa na mzungu mwenyewe
Tatizo ni nyie vijana kujifanya mnajua! Wewe upo naive kubali tukuelimishe. Negotiations za kimataifa hizo. Aidha uache roho mbaya na ukabila. Kupinga kila kitu ni utoto
 
Tatizo ni nyie vijana kujifanya mnajua! Wewe upo naive kubali tukuelimishe. Negotiations za kimataifa hizo. Aidha uache roho mbaya na ukabila. Kupinga kila kitu ni utoto
Si Mara ya kwanza Tanzania kutumia watanzania kufanya negotiatons za kimataifa,huo mpango wa kumfanya kagame mjomba wetu hatuutaki na hatuukubali
 
hapo serikali wameniangusha. msema kweli mpenzi wa mungu. kwa nini tusingeomba tafukwa marafiki zetu wa kufa na kuzikana rwanda na uganda.
 
Sio sisi ni kapuku... Washauri wake toka CCM ndo kapuku pia vilaza mpaka anachukua viraka vya ACT ah ah ncheke mieeer
Mtamuelewa tu baada ya miaka 5. Maproffessor na Madok. Wanamuelewa waache watufanyie kazi sisis kina Thomaso tuje tushuhudie Outputs/ outcomes, ndio akili itakaa sawa. Sasa bwana changamka maana kama humuelewi individually utaathirika maana kifamilia miaka mitano ni mingi. Cngamkia Fursa hakikisha- Unafanya kazi kwa bidiii kama hauna akili nzuri, unafuata uadilifu- unalipa kodi na malipo stahiki, Unatumia mitandao kwa mambo ya biashara na siyo kwa umbea na uzushi, unatafuta mianya ya kujiendeleza , asante Serekali maana sasa hivi oppourtunities kibao mafunzo ya ufundi , kilimo biashara nk- kwenye hayo mafunzo usitegemee kuwezeshwa posho bali ujuzi, Sikuliza vyombo vya habari wapi na viwanda vya aina gani vinaanzishwa uchangamkie fursa- basi mengine jazia mwenyewe!
 
Chaza, mimi sidhani kama awamu hii ilikuwa na mkakati au hata agenda ya kujitegemea. Kilichotokea ni kuwa awamu hii ilirithi nchi ikiwa na hali mbaya kimapato, madeni mengi na ahadi za uchaguzi lukuki zenye kuhitaji fedha nyingi. To add insult to injury, MCC ikafuta sehemu kubwa msaada wake huku wahisani wengine wakinuna na kulalamikia kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar. Mazingira haya ndiyo yaliyozaa ile political rhetoric kuwa nchi hii ni tajiri na inaweza kujitegemea! Good idea but certainly siyo leo wala kesho. Hivyo kila mmoja wetu alijua hayo ni maneno ya kufurahisha baraza.
 
Back
Top Bottom